Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Dua'a Ya Qunut


اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فـيمَنْ تَوَلَّـيْت ، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت، فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك ، إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، [ وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت ]، تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت.


“Ewe Mwenyezi Mungu niongoze pamoja na uliowaongoza, na unipe afya njema pamoja na uliowapa afaya njema, na nifanye kuwa ni mpenzi wako pamoja na uliowafanya wapenzi na nibariki katika ulichonipa na nikinge na shari ya ulilolihukumu kwani Wewe unahukumu wala huhukumiwi. Hakika hadhaliliki uliemfanya mpenzi (wala hatukuki uliemfanya adui ) Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka


اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ سَخَطِـك، وَبِمُعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك



“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako na kwa msamaha wako kutokana na adhabu yako, na najilinda kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa zako, Wewe ni kama ulivyojisifu Mwenyewe”


اللّهُـمَّ إِيّـاكَ نعْـبُدْ، وَلَـكَ نُصَلّـي وَنَسْـجُد، وَإِلَـيْكَ نَسْـعى وَنَحْـفِد، نَـرْجو رَحْمَـتَك، وَنَخْشـى عَـذابَك، إِنَّ عَـذابَكَ بالكـافرين ملْحَـق. اللّهُـمَّ إِنّا نَسْتَعـينُكَ وَنَسْتَـغْفِرُك، وَنُثْـنـي عَلَـيْك الخَـيْرَ، وَلا نَكْـفُرُك، وَنُـؤْمِنُ بِك، وَنَخْـضَعُ لَكَ وَنَخْـلَعُ مَنْ يَكْـفرُك



“Ewe Mwenyezi Mungu , Wewe tu ndie tunaekuabudu, na kwako tunasali na tunasujudu, na kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema yako na tunaogopa adhabu yako, kwani adhabu yako hakuna shaka kuwa makafiri itawifikia. Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakutaka msaada na tunakutaka msamaha na tunakusifu kwa kheri na wala hatukukufurishi na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anaekukufuru”
Allahuma Aamin
 
Hakika Allah (swt) amewaekea wazi njia ya haki na akaiangaza ima ushikamane na maovu au ushikamane na mema, chukueni zawadi kutoka katika masiku yenye kumalizika kwa ajili ya masiku yasiokwisha, kwani nyinyi ni kama wasafiri waliosimama hawajui muda gani wataamrishwa kutembea, anafanya nini duniani yule alieumbwa kwa ajili ya akhera, anaifanyia nini mali yule ambae anajua muda mfupi atanyanganywa.(Imam Ally a.s katika Nahjulbalagh hutba no 157)
 
Jana magharibi ilinikuta Sinza, basi swala na futari hadi narudi kwangu Kigamboni inakaribia saa nne usiku. Hivyo nimegundua ile futari ninayowaalika itakuwa mzigo(takliifu) kwa wengi. Hivyo nimeiondoa na nashauri kwa mwenye wasaa tuandae kwa mitaa yetu, Futari isichukue muda mwingi ili tuwahi ibada zingine
 
[emoji253]DAARUL MUSTAFA[emoji253]
[emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267]
TAFADHALI SOMA UJUMBE HUU NI MUHIMU SANA KWAKO

*IBADA MUHIMU ZA KUZIDISHA KTK MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN*

*BISMILLAHI RAHMAN RAHYM*

A.ALYKUM.
ALHAMDULILLAAH
WA S.A.W.

Ndg zng tumshukuru Sana ALLAH S.W. kwa kutufikisha salama ktk Ramadhan.

Hakika ktk mafundisho ya Uislaam tumesisitizwa sana kuzidisha ibada MBALIMBALI ili kupata rehma na barka zilizopo ktk RAMADHAN.

miongoni mwa ibada hizo ni kufanya sana DHIKRI na kuomba dua kwa wingi.

Hakika MWEZI MTUKUFU wa RAMADHAN umegawanyika ktk makumi matatu..

Kumi la kwanza ni kumi la *REHMA*

KUMI LA pili ni kumi la *MSAMAHA*

kumi la tatu ni kumi la kuokolewa ktk moto wa *JAHANNAM*

*NYIRADI ZA KUZIDISHA KTK KUMI LA KWANZA*

Kwa kua kumi la mwanzo ni kumi la*REHEMA* basi Imependekezwa sana ktk kumi hilo kujitahidi sana kusoma uradi
*(YAA ARHAMAR RAHIMINA)*

*IDADI YA URADI*
Idadi ya uradi huo ni Mara 1000 kila siku.

*NIYA YA URADI*
Utatia Niya ya uradi huo kabla ya kuanza kufanya uradi huo... utasema hv BISMILLAHI RAHMANI RAHIM . ALLAHUMMA SWALLI WA SALLIM WA BAARIK ALAA SAYYIDNAA MUHAMMAD WA ALAA AALIHI WA SALLIM.

*EWE ALLAH ULIE TUKUKA HAKIKA NIMETIA NIA YA KUSOMA URADI HUU ILI NIPATE RADHI ZAKO NA UNIJAZE REHEMA ZILIOZOPO KTK KUMI HILI LA MWANZO KTK RAMADHAN. NAKUOMBA UNIKUBALIE IBADA YANGU HII KWAKO.*

Baada ya hapo utaanza kusoma uradi mpaka utakapo maliza idadi kamili..

Ukimaliza uradi utanyanyua mikono yako kisha utaomba duaa ya shida zako mbalimbali
Usiwache kumsalia mtume S.a.w. kila baada ya maombi yako ni muhimu sana.

Ukimaliza kumi la mwanzo utakua umefanya uradi huo mara 10,000.

*MUDA WA KUSOMA URADI HUO*
Inaruhusiwa kusoma uradi ktk muda wowote utakaopanga mwenyewe lkn muda utakaochagua utautumia muda huo huo mpaka masiku 10 yaishe..

Lkn muda mzuri wa kuvuta uradi huo ni lisaa limoja kabla ya kutoka adhana ya maghribi.. Kwani muda huo ni muda mzuri unaokubaliwa duaa nyingi ktk RAMADHAN.

UKIJITAHIDI kufata utaratibu huu mpaka ukamaliza kumi LA mwanzo basi Insha ALLAH UTAPATA REHEMA Zilizomo ktk kumi hilo la mwanzo..

*NYIRADI YA KUSOMA KTK KUMI LA PILI KTK RAMADHAN*

kumi la pili ni kumi la KUSAMEHEWA MADHAMBI YOTE YALIOPITA.

Ktk kumi la pili utasoma *ASTAGHFIRULLAAH LA'ADHIM WA ATUUBU ILAIHI* mara 1000 kila siku.

Utatumia Utaratibu kama ulivotumia utaratibu wa mwanzo isipokua ktk NIYA.

*NIYA YAKE NI KAMA IFATAVYO*......
*EWE ALLAH ULIE TUKUKA HAKIKA NIMETIA NIA YA KUSOMA URADI HUU ILI NIPATE RADHI ZAKO NA UNISAMEHE MADHAMBI YANGU YOTE NILIOFANYA KWA MAKUSUDI AU KWA BAHATI MBAYA NAOMBA UNIPE RADHI ZAKO NA MSAMAHA WAKO ULIOPO KTK KUMI HILI LA PILI KTK RAMADHAN. NAKUOMBA UNIKUBALIE IBADA YANGU HII KWAKO.*

kisha utavuta uradi huo na utamalizia kwa kuomba duaa zako MBALIMBALI.

Ukimaliza uradi huo ktk kumi la pili utakua umeomba msamaha kwa ALLAH mara elfu kumi.

Inshaa Allah ALLAH atatukubalia TOBA ZETU kwa baraka za kumi la pili KTK RAMADHAN.

*URADI KTK KUMI LA TATU*

Kumi la tatu ni kumi la Kuepushwa na moto wa JAHANNAM.

utafata taratibu zilzotangulia kisha utatia niya hii.[emoji116]

*EWE ALLAH ULIE TUKUKA HAKIKA NIMETIA NIA YA KUSOMA URADI HUU ILI NIPATE RADHI ZAKO NA UNIUPUSHE NA ADHABU ZA DUNIANI NA ADHABU ZA JAHANNAMU NAKUOMBA UNIKUBALIE IBADA YANGU HII KWAKO.*

Kisha utasoma URADI HUU[emoji116]
*ALLAHUMMA AJIRNAA MINA NNAARI SAALIMINA* mara 1000 kila siku.
Kisha utaomba duaa zako za matatizo MBALIMBALI.

Ukimaliza uradi huo ktk kumi la mwisho utakua umeomba uepushiwe shida za duniani na adhabu za AKHERA mara elfu kumi.

Jumla ya uradi zote utakua umesoma uradi mara elfu THAELATHINI ktk RAMADHAN yote.

*MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KTK NYIRADI HIZO NI*[emoji116]

1. Hakikisha unao UDHUU KTK URADI.

2.HAKIKISHA unaelekea KIBLA ktk uradi.

3.usikatishe uradi kwa ajili ya mazungumzo isipokua kwa dharura.

4.chagua sehemu moja maalum ya kufanya nyiradi zako zote mpaka RAMADHAN itakapoisha. Labda itokee dharura kama KAZI,SAFARI,N.K.

5.HAKIKISHA UNAMSALIA MTUME S.A.W KILA UNAPOMALIZA NYIRADI NA DUAA ZAKO

*MWISHO*

Musinisahau kuniombea msamaha ktk duaa zenu.
URADI NI NINI ?
 
somalia.jpg
 
ENYI WANAWAKE SOMENI UJUMBE HUU,NA MUMCHE ALLAH, MAASWI YATAKAYOWATIA WANAWAKE MOTONI NI HAYA HAPA:

Bibi Aishah (Radhiallahu Anha) alimuuliza bwana Mtume (S.A.W) je kuna mtu yoyote miongoni mwa wafuasi wako atayeingiaJannah bila hesabu. Ndio akajibu Mtume (S. A. W ) mtu ambaye daima analia kwa dhambi zake
Siku moja Bibi Fatma Radhi Allah An-ha alikwenda
kwa Mtume (S.W.W) akamkuta analia sana
Bibi Fatma akamuliza nini kinachokuliza ya Rasulla
Allah ??

Akajibu:

Jinsi nilivowaona Wanawake wakipewa adhabu mbali
mbali Motoni
Bibi Fatma akamuliza:
Ni Adhabu gani hizo ya Rasulla Allah ??
Mtume Muhammad (S.A.W) akajibu:-

1. Mwanamke katundikwa kwa nywele zake na huku
ubongo wake na mikono yake inatolewa kwa
nyuma ya mgongo wake na huku anamiminiwa moto wa lami.

HUYU NI MWANAMKE ANAETEMBEA KICHWA WAZI.

2. Mwanamke kafungwa mikono yake na miguu
yake juu ya utosi wake huku kaachiwa Joka na Nge
wakimdona.

HUYU NI MWANAMKE ANAETOKA BILA RUHUSA YA MUMEWE.

3. Katundikwa kwa ulimi wake umevutwa hadi
dhiraa 70 na anamiminiwa moto wa lami.

HUYU NI YULE ALIYEMUUDHI MUMEWE HADI AKAKASIRIKA.

4. Anakula mwili wake na huku kila akila nyama inajirud upya na huku anamiminiwa moto wa lami.

HUYU NI YULE ALIYEKUWA ANAJIPAMBA NA ANADHIHIRISHA PAMBO LAKE.

5. Anakata mwili wake kwa Mikasi ya moto km
anaekata kitambaa.

HUYU NI MWANAMKE ALIYEKUWA AKIPENDA KUTEMBEA HUKU AMEVAA NGUO ZA KUBANA ZINAZO ONESHA FIGER YA MWILI WAKE.

6. Mwengine uso wake mweusi sana huku anakula
tumbo lake na mikono yake.

HUYU NI YULE ALIYEKUWA ANAFITINISHA.

7. Na wengine wametiwa ndani ya masanduku ya Moto na Nge wakiwatafuna miili yao.

HAWA NI WANAWAKE WANAOWABANDIKA WAUME ZAO WATOTO WASIO KUWA WAO.

EWE MWANAMKE JIEPUSHE NA ADHABU HIZO KWA
HAKIKA NI ADHABU KALI.

Share na rafiki zako ili mawaidha yawafikie wengi....

HAKIKA UKUMBUSHO UTAWAFAA WENYE KUAMINI
 
TUOGOPE KUSENGENYA JAMANI MUNGU HAPENDI

Ndugu zangu katika imani, hakuna jambo jipya katika dini yetu hii kila kitu kilishawekwa wazi
ila ni vizuri tukumbushane kila wakati na tusichoke kwa hilo kwani :
''Hakuwa binnadamu isipokuwa ni kiumbe mwenye kusahau sahau''

Kusengenya ni miongoni mwa mambo yaliokatazwa sana na M/Mungu kiasi kwamba Amekufananisha na kula nyama ya maiti,na hii ni miongoni mwa madhambi ambayo tunayafanya kila siku kwa kujua ama kutokujua,basi nakukumbusha tena ndugu yangu tuwe makini na ndimi zetu

Kusengenya ni kumtaja mtu kwa jambo asilolipenda. Mtume mtukufu (s.a.w.) anasema: “Kusengenya ni kumtaja ndugu yako kwa jambo analolichukia. Ikiwa jambo hilo analo huko ni kusengenya na ikiwa hana basi utakuwa unasema uongo.”.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemfananisha mwenye kusengenywa na maiti kwa vile anakuwa hayupo na akaifananisha heshima yake na nyama yake na kumtaja kwa uovu ndiyo kama unakula nyama yake. hivyo kama tunaona kinyaa kula nyama ya maiti basi pia tuone kinyaa kumsengenya asiyekuwepo.

Na Mwenyezi Mungu hasamehi kusengenya mpaka asamehe aliyesengenywa
Basi ikiwa umemsengenya mtu na mauti yakakuta bila kumuomba msamaha basi ujue utakuwa na deni siku ya kiyama na viungo vyako vitakuwa shahidi siku hiyo

Na kwenye kusengenya yule anayesengenya na msikilizaji wote wana dhambi
Nawausia na kujiusia nafsi yangu tukae mbali na maasi na tuikumbuke siku ya malipo

''Yeyote yule anaefanya wema mfano wa uzito wa sisimizi siku hiyo atauona wema wake
na yeyote yule anaefanya uovu mfano wa uzito wa sisimizi siku hiyo atauona uovu wake'

 
Hivi vilema wote ni waislam kwel

Hapana, sidhani kama ni kweli vilema wote ni waislam aidha kama wataka kufaham zaidi ni vyema ukaenda kwa Kakobe au wachungaji wowote wanaowaombea vilema na viwete wakasimama uwaulize kuwa je, wale ni waislam watakupa jibu sahihi kama vilema wote ni waislam au laa.

Shukran laka jaziylah. Marhabanbik.
 
Hapana, sidhani kama ni kweli vilema wote ni waislam aidha kama wataka kufaham zaidi ni vyema ukaenda kwa Kakobe au wachungaji wowote wanaowaombea vilema na viwete wakasimama uwaulize kuwa je, wale ni waislam watakupa jibu sahihi kama vilema wote ni waislam au laa.

Shukran laka jaziylah. Marhabanbik.
mie nimeshindwa hata kumuelewa
 
ENYI WANAWAKE SOMENI UJUMBE HUU,NA MUMCHE ALLAH, MAASWI YATAKAYOWATIA WANAWAKE MOTONI NI HAYA HAPA:

Bibi Aishah (Radhiallahu Anha) alimuuliza bwana Mtume (S.A.W) je kuna mtu yoyote miongoni mwa wafuasi wako atayeingiaJannah bila hesabu. Ndio akajibu Mtume (S. A. W ) mtu ambaye daima analia kwa dhambi zake
Siku moja Bibi Fatma Radhi Allah An-ha alikwenda
kwa Mtume (S.W.W) akamkuta analia sana
Bibi Fatma akamuliza nini kinachokuliza ya Rasulla
Allah ??

Akajibu:

Jinsi nilivowaona Wanawake wakipewa adhabu mbali
mbali Motoni
Bibi Fatma akamuliza:
Ni Adhabu gani hizo ya Rasulla Allah ??
Mtume Muhammad (S.A.W) akajibu:-

1. Mwanamke katundikwa kwa nywele zake na huku
ubongo wake na mikono yake inatolewa kwa
nyuma ya mgongo wake na huku anamiminiwa moto wa lami.

HUYU NI MWANAMKE ANAETEMBEA KICHWA WAZI.

2. Mwanamke kafungwa mikono yake na miguu
yake juu ya utosi wake huku kaachiwa Joka na Nge
wakimdona.

HUYU NI MWANAMKE ANAETOKA BILA RUHUSA YA MUMEWE.

3. Katundikwa kwa ulimi wake umevutwa hadi
dhiraa 70 na anamiminiwa moto wa lami.

HUYU NI YULE ALIYEMUUDHI MUMEWE HADI AKAKASIRIKA.

4. Anakula mwili wake na huku kila akila nyama inajirud upya na huku anamiminiwa moto wa lami.

HUYU NI YULE ALIYEKUWA ANAJIPAMBA NA ANADHIHIRISHA PAMBO LAKE.

5. Anakata mwili wake kwa Mikasi ya moto km
anaekata kitambaa.

HUYU NI MWANAMKE ALIYEKUWA AKIPENDA KUTEMBEA HUKU AMEVAA NGUO ZA KUBANA ZINAZO ONESHA FIGER YA MWILI WAKE.

6. Mwengine uso wake mweusi sana huku anakula
tumbo lake na mikono yake.

HUYU NI YULE ALIYEKUWA ANAFITINISHA.

7. Na wengine wametiwa ndani ya masanduku ya Moto na Nge wakiwatafuna miili yao.

HAWA NI WANAWAKE WANAOWABANDIKA WAUME ZAO WATOTO WASIO KUWA WAO.

EWE MWANAMKE JIEPUSHE NA ADHABU HIZO KWA
HAKIKA NI ADHABU KALI.

Share na rafiki zako ili mawaidha yawafikie wengi....

HAKIKA UKUMBUSHO UTAWAFAA WENYE KUAMINI
Bihusnil khaatimah ya Allah!! Astaghfirullah
 
Back
Top Bottom