Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anajaribu kututoa kwenye fact, tunamuonbea kwa Allah amjaze iiman arudi katika mstari.ni kweli naona huyo anataka tujadili tusiyotaka kuyajadili hapa
Mungu akulipe kheri*JEE WAIJUA NI IPI TOFAUTI KATI YA MAGHFIRAH (مغفرة ) NA A'FUW (عفو )?*
*MAGHFIRAH*: Ni vile Allah (s.w) kukusamehe dhambi zako juu ya makosa fulani ila bado makosa hayo yatabaki kuoredheshwa katika buku la matendo yako.
Na siku ya hukumu yatakuwemo katika rikodi yako na Allah atakuuliza juu ya makosa hayo.
-Lakini hatakuadhibu kwa sababu ya makosa hayo uliyokwisha yaombea *MAGHFIRAH*.
*A'FUW*: Ni vile Allah (s.w) kukusamehe dhambi za makosa Yako na kisha kufutwa kabisa makosa hayo katika buku la matendo yako kama vile hayo makosa hayakuwahi kutokea.
-Yatafutwa kabisa katika rikodi yako na Allah hatakuuliza kuhusu makosa hayo siku ya hukumu.
*Na kwa sababu hiyo ndio maana mtume (s.a.w) amesema, "Dua hii ni bora zaidi kuisoma siku ya Laylatul Qadr:*
Nayo ni :
*"Allahumma innaka a'fuwwun tuhibbul a'fwa faa'fu 'anniy"*
(Ahmad, Ibn Majah, na Tirmidhiy)
Maana ya maneno hayo ni:
*(Ya Allah hakika yako ni msamehevu na unapenda kusamehe na mimi nisamehe .)*
Msamaha unaoutaka hapo ni ule wa kufutiwa kabisa dhambi na makosa yako katika rikodi ya matendo yako.
-Kwa hiyo hakikisha unaisoma dua hiyo kila muda na ifanye ni miongoni mwa nyiradi zako.
*ZAWADI NYENGINE MUHIMU YA KUCHUKUA*
[emoji835] Hebu Jaalia katika fikra zako imefika siku ya hukumu na imefika zamu yako ya kuhisabiwa wala huna uhakika ya kuwa utaipata pepo ya Allah (s.w).
*Mara unakuta katika rikodi yako Ya matendo kuna milima kwa milima ya Wema (uliyozawadiwa)*
Unadhani itakuaje hapo.
Jee unajua zawadi hizo zinatoka wapi?
Ni kwa sababu katika duniya ulikithirisha kusema: *”SubhanAllah wa bihamdihi SubhanAllah al ‘Adhim”*
Mtume Muhammad (s.a.w) amesema *"Maneno mawili ni mepesi katika ulimi ila ni mazito katika mizani na anayapenda sana Al Rahman,:*
Maneno hayo ni:
سُبْحَانَ اللّهِ وَ بِحَمْدِهِ ، سُبْحَانَ
اللّهِ الْعَظِيمِ -
*SubhanAllahi wa biHamdihi, Subhan-Allahi 'l-`adhwiym.
*Ametakasika Allah na sifa njema zote ni zake. Ametakasika Allah alie mtukufu (mkubwa)*
(Bukhari &Muslim)
Je wajua ni kiasi gani cha wema utalipwa ikiwa utasambaza taarifa hii yenye ukumbusho mzuri kwa ndugu na marafiki zako na wao wakakithirisha kusema haya maneno. *(SubhanAllah wa bihamdihi SubhanAllah Al Adhwiym)*
Utalipwa sana kwa sababu umewahimiza watu kutenda wema.
*NA WEWE KUWA NI MIONGONI MWA WENYE KUHIMIZA WATU KHERI.*
Tujiadhari na moto ee ndugu zangu waislam
Mungu atulinde mkuu, motoni si sehemu nzuri cha muhimu tudumishe amali njema ili Mungu atuepushe na hayo?
Ameen yaarab. In sha Allah kwa sote.Mungu akulipe kheri
Umetuwekea ujumbe mzito,InshaAllah tutaufanyia kazi
Kufunga sio lazima, kama sjakosea unaruhusiwa kutofunga ukiwa safarini kama safari ni ndefu, ila pia unapokuwa safari hakuna excuse ya kutoswali, kuna swala za safari unaswali ukiwa hapo kwenye kiti chako, kama ni adhuhuri unachanganya na Alasiri.Naomba kuuliza kidogo,mm nasafili na kipando nilichopanda ni buss na niabilia wengi na niendapo panatumia siku nzima njiani, sasa je ni lazima nifunge na kama ntafunga funga yangu itakua salama pasipo kuswali?
Wailahuna yaqfee
Assalamualaik,Naomba kuuliza kidogo,mm nasafili na kipando nilichopanda ni buss na niabilia wengi na niendapo panatumia siku nzima njiani, sasa je ni lazima nifunge na kama ntafunga funga yangu itakua salama pasipo kuswali?
Wailahuna yaqfee
In sha Allah iwe kwa sote.
Ameen