Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Ndugu yangu sory naomba nieleweshe zaidi hii hadithi nimeisoma sijaielewa
haya yalisemwa na Imam Ali a.s karne 14 nyuma lakin ndiyo yanayoendelea katika jamii zetu sasa. maskini wanaendelea kuwa maskini kwa kuwa matajiri au wenye uwezo hawatoi haki ya maskini ktk utajir wao. Tajir anakufur kutokana na utajir wake, yaani matumizi yake yamekuwa ya Islafu- anatupa chakula, ananyanyasa wasionacho. Pia watu wamekuwa bakhili ktk kutoa, iwe zaka, khumsi au sadaka. Na mwisho Imam anasema wenye elim na wasio nayo wanafanana kwa kuwa wasio nayo hawaulizi, na wenye nayo hawakemei uovu, kwa kuwaridhisha viongozi.
 
Mashaallah, hakika waislam wanaiogopa sana ramadhani kuliko nguzo zingine za uislam , kwasababu mtu anaweza akawa na kila kitu ndani kwake ama mfukoni mwake , lakini anaogopa kula kwani allah atamuona.

Allah tunusuru na tuongoze kwani ndo yuleyule tunatakiwa kumuogopa hata katika nguzo zingine na makatazo mengine.



Ramadhani Mubarak
 
Mashaallah, hakika waislam wanaiogopa sana ramadhani kuliko nguzo zingine za uislam , kwasababu mtu anaweza akawa na kila kitu ndani kwake ama mfukoni mwake , lakini anaogopa kula kwani allah atamuona.

Allah tunusuru na tuongoze kwani ndo yuleyule tunatakiwa kumuogopa hata katika nguzo zingine na makatazo mengine.



Ramadhani Mubarak
Ni kweli mkuu
ila nasikitika kuona waislamu wenzetu wengi hawajui lengo la ramadhani
mtu kipindi cha ramadhani anajitahid kuacha maovu yote lakini mwezi ukiisha anarudia yale yale aliyoyaacha,
Huo ndiyo msiba mkubwa kwa wengi katika tunaofunga, tunashindwa kuendelea nao ule uchamungu amabo tunao kipindi hiki cha ramadhani
Mungu atusamehe na atuongoze katika kheri!
 
Luqman Al Hakim aliwapa wasia mtoto wake Alimwambia hivi;

Ukiwa uko sehemu hizi 3 hifadhi hivi:-

1.Ukiwa umealikwa kwa nyumba ya watu kama mgeni,Hifadhi macho yako

2.Ukiwa umekaa kikao na watu hifdhi ulimi wako

3.Kama uko kwenye karamu hifadhi tumbo lako

Na Akamwambia usisahau vitu viwili

1-Mkumbuke Allah kila wakati

2-Kumbuka mautii kila wakati

Na vitu viwili sahau;

1- Wema uliomtendeaa mtu sahau

2- Maovu uliofanyiwa yasahau,

Pongezi kwa atakayeisoma,

akaifahamu na akakimbilia

kuitendea kazi... na Allah amjaze kheri atakayeituma hii kwa wengine..

Alikuja mtu kwa Amiril Mu'mineen Aliy bin AbiTalib (Radhi Allahu Anahu) akasema:

'Ntakuuliza mambo manne (4) unijibu'.

La Kwanza: Ni lipi la wajib na lipi
la wajib zaidi ?

Na Lapili: Lipi la karibu na lipi
la karibu zaidi ?

Na Latatu: Lipi la ajabu na lipi la
ajabu zaidi ?

Na la INNE: Lipi jambo gumu na
lipi gumu zaidi ?

Akajibu Amirul Mu'mineen hivi:

1) La wajib ni kumtii Allah na la wajib zaidi ni kuacha dhambi.

2) La karibu ni kiyama na la karibu zaidi ni mauti.

3) La ajabu ni dunia na la ajabu
zaidi ni kuipenda dunia.

4) Ama gumu ni kaburi na gumu
zaidi ni kuliendea bila matayarisho.
Ewe Mola Mgeuzi wa nyoyo zithibitishe nyoyo zetu kwenye dini yako. Ewe Mola atakayefungua ujumbe huu Mfungulie baraka za Rizki kutoka Mbinguni na Ardhini.. na atakaye ieneza kwa watu
usininyime Pepo yako yaa Rabb!.Amin...

ALLAH Ameficha mambo 7 katika sehem 7

1. Kaficha "RADHI" zake ktk utiifu
(ZITAFUTE)

2. Kaficha "GHADHABU" zake ktk maasi (JIEPUSHE)

3.Kaficha "ISMUL A3DHWAM" katika majina yake 99 (MUOMBE)

4. Kaficha "SAA YA MAOMBI" ktk Ijumaa, (JIBIDIISHE)

5. Kaficha "LAYLATUL QADRI" ktk Usiku wa Ramadhani (UAMKE)

6. Kawaficha "WAJA WEMA" miongoni mwa viumbe (JIFANANISHE)

7. Na kaficha "UMAUTI" ktk umri wako, (JITAYARISHE)

Mkumbushe japo muislamu mmoja iwe ni SWADAQA kwa siku ya

leo,
TUELEKEZANE PEPONI
Siku ya "QIAMA" ataonekana "NDEGE" mkubwa anaitwa "HARISH" Upana kutoka masharik hadi maghrib ataulizwa unakwenda wapi.? Atajibu nakwenda uwanja wa "HUKUMU" nakwenda kuwabeba watu wa aina 5.

1.Aliyeacha swala 5.

2.Aliyekosana na wazazi wake.

3.Aliyedumu ktk pombe.

4.Aliyekula riba.

5.Aliyezuia zakka,

Nakwenda kuwatupa "JAHANNAM" maana najua hawana salama mbele ya Allah (Subhana Wataala )

In sha Allah mwenyezi Mungu atunusuru na moto wa jahannam na atujaalie tuwe miongoni mwa waja wake wema,

Aamin yarrabi laalamin.
 
Allah akbaar, jamani kuanzia Jana naona hali ya hewa imebadilika sana,swaumu inanibana kwakweli sio mchezo.

Mtu mwenyewe nipo kivulini muda wote, sijui ingekuwaje kama ningekuwa nafanya kazi ngumu na kukaa juani kwa muda mwingi.

Allah tufanyie wepesi katika swaumu zetu, tusione kama ni mateso vile.

Ramadhan kareem.
 
Allah akbaar, jamani kuanzia Jana naona hali ya hewa imebadilika sana,swaumu inanibana kwakweli sio mchezo.

Mtu mwenyewe nipo kivulini muda wote, sijui ingekuwaje kama ningekuwa nafanya kazi ngumu na kukaa juani kwa muda mwingi.

Allah tufanyie wepesi katika swaumu zetu, tusione kama ni mateso vile.

Ramadhan kareem.
pole ndugu yangu
mie ilinikamata ile siku ya kwanza ila baada ya hapo nimeenda nayo vizuri yaani nimeshazoea naona kama siku za kawaida tu, kwa hiyo usijari hiyo ni kawaida hutokea siku fulan ikakushika
ila pia ukipata wasaa lete dhikri na kusoma quran
 
Tusisahau kuwasaida wasiojiweza nyakati zote na zaidi ktk Mwezi huu wa Ramadhan. Hii picha imenisikitisha sana, kufikiria kuwa kuna watu wanashindwa kupata futari



DAw75VZWsAM4NYj.jpg:large
 
Asalam alykum warahma tullah wabarakatuh
 
Tusisahau kuwasaida wasiojiweza nyakati zote na zaidi ktk Mwezi huu wa Ramadhan. Hii picha imenisikitisha sana, kufikiria kuwa kuna watu wanashindwa kupata futari



DAw75VZWsAM4NYj.jpg:large
ni kweli mkuu na ndugu zetu wengine wakishafuturu wanapiga ndefu hakuna daku inaskitisha, cha muhimu tusiwasahau katika dua zetu kwani M/Mungu (sw) ndiye mtoaji
 
th (1).jpg
th (1).jpg

th (4).jpg
th (4).jpg

Hilo ni neno kubwa mno mbele ya M/mungu ndugu zangu tujitahidi kulitamka kila wakati
Mtume Muhamad saw anasema katika hadithi qudsi kwamba uzito wa neno hilo ni mkubwa kuliko dunia na vilivyomo, hivyo tujizoeshe kutamka mara kwa mara

Pia si sahihi, baadhi ya wanafamilia kumlazimisha mgonjwa katika "sakratul maut" kusema 'Lai Ilaha Ila Allah' hayo si mafundisho ya uislamu, bali kinachofundishwa ni wewe unayekuwa karibu na mgonjwa kutamka hayo maneno ili yeye asikie, na wala si kumlazimisha yeye atamke, kumlazimisha hakumsaidii chochote kwani kutamka hayo maneno ni ihsani yake Allah (sw)

Wallahu A'lam

Ramadhan kareem
 
*﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾*

*☪ LEO KATIKA FUNGA ☪*
*( 16 )*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}*
*Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.* (2:183)
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

*■ TUNAENDELEA NA DARSA YETU YA LEO KATIKA FUNGA, TUKIWA TUNATAZAMA BAADHI YA MAMBO AMBAYO YAMERUHUSIWA KISHERIA KUYAFANYA MFUNGAJI.*

*3- ومن الرُّخص: أنَّه يَجوز للمرأة أن تتذوَّق الطَّعام أثناء الطهْي، بشرط ألاّ يصِل إلى جوفها.*
*3- NA MIONGONI MWA RUHUSA PIA: HAKIKA YAJUZU KWA MWANAMKE KUONJA CHAKULA WAKATI ANAPIKA KWA SHARTI KILE CHAKULA KISIFIKE NDANI, (YANI KUINJA KWA MAANA YA KUTAZAMA KAMA CHUMVI NA VITU VINGNE VIPO SAWA, NA KINACHO TAMBUA YOOTE HAYO NI ULIMI, SASA BASI KUONJA HUKO CHAKULA KIISHIE KATIKA ULIMI KISHA AKITEME).*

*4- ومن الرُّخص أيضًا: أنَّه يجوز للصَّائم إنِ احتاج أن يضع الدَّواء في أذنه أو عيْنه.*
*4- PIA MIONGONI MWA RUHUSA ZA FUNGA: HAKIKA YAJUZU KWA MFUNGAJI IKIWA ATAHITAJIA KUWEKA DAWA KATIKA SIKIO LAKE AU JICHO LAKE.*

*♡ لأنَّ ذلك ليس بأكلٍ ولا شرب ولا بمعنى الأكل والشرب.*
*KWA SABABU HAKIKA HAYO SI KATIKA CHAKULA WALA KINYWAJI, WALA SI KATIKA MAANA YA KULA WALA KUNYWA.*

*DINI HII NI NYEPESI KABISA WALA HAKUNA UZITO NDANI YAKE.*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{وَجَاهِدُوا فِي اللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ }*
```Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim.```
☪☪☪☪☪☪☪☪

*[emoji257] ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*

*الدعوة اﻹسلامية*
 
Allah akbaar, jamani kuanzia Jana naona hali ya hewa imebadilika sana,swaumu inanibana kwakweli sio mchezo.

Mtu mwenyewe nipo kivulini muda wote, sijui ingekuwaje kama ningekuwa nafanya kazi ngumu na kukaa juani kwa muda mwingi.

Allah tufanyie wepesi katika swaumu zetu, tusione kama ni mateso vile.

Ramadhan kareem.
Pole sana. Jitahidi kula daku kabla salama ya alfajiri. Na kama hali inaruhusu pendelea kula tende kwa namba za witir. Na maziwa. Vinakaa sana tumboni.
 
URADI NI NINI ?
Uradi na kuleta dhikri.
Yaani kumtaja Mwenyeezi Mungu.
Kama kusema SubhanaAllah. Alhamdulillah. Lailaha ila Allah. Allahu akbar.
Au SubhanaAllah wabihamdih. SubhanaAllah laadhym.
Au kumsalia mtume.
Au kuleta istighfar. Yaani Kustaghfiru.
Na mengine kama hayo.
Shukraan
 
*﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾*

*☪ LEO KATIKA FUNGA ☪*
*( 15 )*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}*
*Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.* (2:183)
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

*■ NAAM NDUGU ZANGU KATIKA:*

*LEO KATIKA DARSA YETU FUPI YA KILA SIKU, DARSA MAALUM KWA AJILI YA IBADA YA FUNGA, KWA UWEZO WAKE ALLAH MTUKUFU TUTATAZAMA BAADHI YA MAMBO AMABYO YAMERUHUSIWA KWA MFUNGAJI.*

*♢ رابعًا: رُخص الصيام وآدابهُ:*
*SEHEMU YA NNE: RUHUSA ZA FUNGA NA ADABU ZAKE.*

*♡ هناك رُخص عديدة امتنَّ الله بها على عبادِه؛ دفعًا للحرَج ورفعًا للمشقَّة، ومنها:*
*ZIPO RUHUSA NYINGI SANA AMBAZO ALLAH MTUKUFU AMEWAPA WAJA WAKE, ILI KUONDOA UZITO NA TABU, MIONGONI MWA HIZO RUHUSA NI-*

*1- جواز الفطر في نهار رمضان للمريض وكذا للمسافر الذي يشقُّ عليه الصوم؛ لقوله تعالى:*
*1- KUJUZU (KURUHUSIKA) KULA MCHANA WA RAMADHANI KWA MTU MGONJWA PIA MSAFIRI AMBAE ATAMPA TABU NA DHIKI IKIWA ATAFUNGA HALI YUPO SAFARINI. RUHUSA HII IMEKUJA KWA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU:*

*﴿ وَمَنْ كَانَ مَرِيضاً أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ ﴾*
```Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito,``` [البقرة: 185].

*2- ومن الرخص أيضًا: المضمضةُ والاستِنْشاق بدون مبالغة، خشية أن يصِل شيءٌ من الماء إلى الحلق فيبَطُلُ صومه بذلك.*
*2- MIONGONI MWA RUHUSA PIA: NI KUSUKUTUWA MAJI MDOMONI NA PUANI BILA KUZIDISHA ZAIDI, KWA KUKHOFIA KUFIKA CHOCHOTE KATIKA MAJI HADI KWENYE KOO NA KUSABABISHA KUBATILIKA FUNGA YAKE KWA AJILI HIYO.*

*للحديث الذي رواه الترمذي والنسائي.... أنَّ النَّبيَّ - صلَّى الله عليه وسلَّم - قال:*
*HAYA NI KUTOKANA NA TIRMITHIY NA NASAI NA WENGI KATIKA WAPOKEZI..HAKIKA MTUME (ﷺ) ALISEMA:*

*"وبالِغْ في المضمَضة والاستنشاق إلاَّ أن تكون صائمًا".*
*NA FIKISHA (KATIKA KOO) UNAPOSUKUTUWA MAJI MDOMONI NA PIA KUPANDISHA MAJI PUANI (WAKATI UNATAWADHA), ILA UKIWA UMEFUNGA (USIFIKISHE).*

*● ALLAH MTUKUFU ANAWAPENDA WAJA WAKE, KWA HAKIKA MAPENZI YAKE YAPO WAZI PALE TU AMBAPO HAKUJALIA UZITO WALA UGUMU KATIKA DINI HII YA HAQQI.*

*والله أعلم.*
☪☪☪☪☪☪☪☪

*[emoji257] ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*

*الدعوة اﻹسلامية*
 
Bi.faizafoxy adimu sana?

Tina hata ukumbusho kidogo.

Unanikumbuka?, kwenye uzi wako wa faidika na darsa la faizafoxy,
Hakika maswali yangu yalikuwa na changamoto kubwa sana , lakini mashaallah ulijibu kadri allah alivyokuwezesha.

Ndo wadau wamwanzo kabisa kuwafahamu ndani ya Jf.

Ramadhani Mubarak.
 
maxresdefault.jpg

Mtume (saw) anasema laiti tungejua fadhila zilizomo ndani ya Ramadhan basi waislamu tungeomba huu mwezi uwe mwaka mzima!
Miongoni mwa fadhila hizo ni usiku wa cheo na Mtume saw anasema alionyeshwa siku hiyo ila Allah akamsahaulisha, na hapa hekima yake ni ili tufanye ibada mwezi wote wa Ramadhani na sio kungojea usiku wa cheo
Mtume (saw) "fanyeni bidii kutafuta usiku wa cheo katika siku zisizo gawanyika kwa mbili ndani ya kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhan'

Aisha (r.a ) alimuuiliza Mtume (saw) katika usiku wa cheo tuombe kitu gani?
Mtume (saw) akamuambia sema "Ewe Mola,hakika yako wewe ni mwenye kusamehe madhambi,tena mkarimu,wapenda sana kusamehe, basi nisamehe makosa yangu''

Tujitahidi sana kuamka usiku, masiku yaliobaki ndugu zangu!

Ramadhan Kareem
 
Back
Top Bottom