Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

TANBIHI!!!!
Nakuomba Usome Ujumbe Huu Muhimu Kwa Umakini Wa Hali Ya Juu.
1.Tafadhali Usitume Ujumbe wa KIDINI Unaokutaka wewe "kutuma kwa watu 10 na utapata habari njema(Ujira) au utapata jambo baya endapo hujatuma au subiri uone atakachokufanyia ALLAH (SWT) Asubuhi" kwa sababu kuna watu wanaufanyia mchezo UISLAMU.
Muislamu wa kweli inabidi aelewe kwamba UJIRA hauji kwa kutuma UJUMBE.
Ujira unapatikana kwa wewe kuwa MWEMA&KUMUOMBA ALLAH.
Lazima tujue kua kufanya hivi ni katika shirki na daima ukumbuke kua shirki ni dhambi kubwa katika Uislamu.!!
2.Kuna TOVUTI zimeanzishwa na mayahudi kwa Lengo la kueneza taarifa Zisizo SAHIHI Juu ya QUR'AN&HADITH,
kwa hiyo ujue na umtaarifu kila mtu juu ya TOVUTI zifuatazo;
[emoji732]1.www.answering-islam.org
[emoji732]2.www.aboutislam.com
[emoji732]3.www.thequran.com
[emoji732]4.www.Allahassurance.com
Ahsante.
3.Kwa kuongezea,kuna video ya Hijja mwaka 2008 inaonesha MALAIKA anatokea Mbinguni.Zote hizi zinatengezwa na maadui wa Uislamu.Usiamini wala kusambaza meseji hizo.
Tafadhali tuma ujumbe Huu kwa waislamu wapate kufahamu.Usiposambaza Waislamu Ulimwenguni watakua na taarifa zisizo sahihi juu ya Uislamu.
Kwa hiyo tuma huu ujumbe kama ulivyokufikia wewe kupitia Jitihada za watu.
Jazakumullahu Khairan.
 
[emoji117] KUMWAGA CHAKULA

Quran: “...kuleni, na kunyweni, na wala msifanye israfu. Kwa hakika Allah hawapendi wanaofanya israfu.” [Al-A’araaf 31]

Mtume s.a.w kasema: “Rambeni mikono yenu baada ya kula kabla ya kunawa. Na kama chakula kimeanguka, basi kiokoteni mukisafishe mukile” [Sahih Bukhari]

Mtme s.a.w aliiona tende njiani, akasema: “Laitani ningelijua kuwa tende hii haitokani na zaka, basi ningeliiokota na nikaila” (Yeye haruhusiwi kuchukua zaka). [Sahih Al-Bukhaari]

Anas (radhiya Allahu anhu) kasema: “Mtume sallallahu alayhi wasallam ametukataza kubakisha mabaki ya chakula sahanini, kwa sababu huwezi kuijua sehemu ipi ya iliyobarikiwa na Allah.” [Sahih Muslim & Tirmithi]

Leo watu wanatupa vyakula kwa makusudi, eti kwa sababu hapendi kula chakula cha jana. ASTAGHFIRULLAH.

Kwanini unatia chakula kingi sahanini mwako halafu kinachobakia unakitupa!? Kwani hujui kuwa Waisilamu wenzako wanakihitaji na hawana uwezo wa kukipata!? ASTAGHFIRULLAH.

Leo kuna masikini wengi sana lakini hapana anaetaka kuwapa chakula wala kuwasaidia, tunahiari kujishindilia matumboni mwetu tu. ASTAGHFIRULLAH.

Tunapoambiwa tusaidie masikini tunawajibu “sina pesa”. Lakini pesa za kununua vyakula ukavitupa unazo. ASTAGHFIRULLAH.

Leo mtu akialikwa pahala huona aibu kula/kunywa akamaliza, lazima abakishe japo kidogo ili kimwagwe/kitupwe. ASTAGHFIRULLAH.

Laitani chakula ulichokimwaga kitakwenda kukushitaki siku ya kiama, je! Tamaa ya kuingia Peponi itakuwepo???
 
Assalaam alaykum, habari zenu ma akhy na ma ukhty zangu, mi naomba mniombee dua nizidi kumlaani Iblis[laatullah alayhi] ili nizidi kuisoma Qur ani kwani juzi siku moja pekee nilisoma juz'u tano.
Masha Allah.
Tunakuombea na wewe usiache kujiombea.
Allah atuepushe na kufanya dhambi ndogo na dhambi kubwa na tuwe wepesi katika kufata na kufanya yale yote mema aliyoyaamrisha yeye.
Ndugu zangu. Waislamu wenzangu. Kweli moto umeumbwa kwa ajili ya binaadam lakini tujitahidini tusiwe wenye kukhafilika. Tuungane na tusichoke kuamrishana mema ili siku ya malipo moto uwe mbali na kila muislam.
Nawapenda wote kwa ajili ya Allah.
Tujitahidini tuupinge huu umagharibi ndio unaotumaliza.
 
Asalaam alaykum warahmatulah wabarakatuh

Tujikumbushe Du'aa ya wakati wa kufungua Swawm

ذَهَـبَ الظَّمَـأُ، وَابْتَلَّـتِ العُـروق، وَثَبَـتَ الأجْـرُ إِنْ شـاءَ اللهُ

Dhahabadh-Dhwama-u Wabtallatil-'Uruuq,, Wathabbatal-Ajru Insha-Allaah.

“Kiu kimeondoka na mishipa imelainika, na yamethibiti malipo Mwenyezi Mungu Akipenda”

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdillaahi bin ‘Amr bin ‘Al -‘Aas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: ‘Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu “Aliyefunga wakati wa kufuturu kwake ana Du'aa isiyorudishwa”

اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ بِرَحْمَـتِكَ الّتي وَسِـعَت كُلَّ شيء، أَنْ تَغْـفِرَ لِي

Allaahumma Inniy As-aluka Birahmatikal-latiy Wasi'at Kulla Shay'in An Taghfiraliy.

“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kwa rehma Zako ambazo zimeenea kila kitu, Unisamehe”
 
Wana jf naomba mnisaidie,wanawake walioweka vifaa kwenye miili yao vya kuzuiya mimba,mfano vijiti,kuchoma sindano nk,je wanahaki ya kufunga?
 
MAMBO YANAYOHARIBU SAUMU

1. Kula na kunywa kwa kukusudia ndani ya mchana wa Ramadhani
Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ} البقرة:187}

[Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni saumu mpaka usiku] [Al-Baqarah – Aya 187]

MAS'ALA

Je yafaa mtu kula kwasababu ya kazi?
Yoyote anayefanya kazi mahali pa mapishi ya mikate hivi na mahali pa kazi ngumungumu sio ruhusa kwao kutofunga (yaani hawafai kula mchana wa Ramadhani); kwasababu wamelazimika kama watu wengine kufunga Ramadhani.

MAELEZO

- Atakaye kula au kunywa kwa kusahau basi saumu yake imeswihi (iko sawa haina tatizo lolote), na inamlazimu kujizuia na vitu vinavyoharibu saumu pindi anapokumbuka; kwa kauli ya Mtume ﷺ:

من نسي وهو صائم - فأكل أو شرب فليتمّ صومه ، فإنما أطعمه الله وسقاه] رواه مسلم]

[Aliyesahau hali ya kuwa amefunga akala na kunywa, basi akamilishe saumu yake, kwani Mwenyezi Mungu amemlisha na kumnywesha (mtu huyo)] [Imwpokewa na Muslim.].

- Kinaharibu saumu chochote kile kinachoingia tumboni kwa njia ya mdomoni au puani, na chochote kinachofahamika kuwa chakula au kinywaji, kama vile sindano za lishe/chakula. Ama sindano ambazo si za chakula, kama penicillin na mfano wake, hazifunguzi saumu, kwasababu sio chakula wala kinywaji, wala sio kwa maana ya chakula.

- Chochote kinachoingizwa mdomoni kwa ajili ya kutizama kitu na vipuliza hewa vya kutibu pumu na mfano kama huu, hakiharibu saumu.

- Wanja, na matone ya kitu majimaji kutonezwa kwenye jicho na sikio na mfano wa hivi viwili havivunji saumu, kwasababu hakuna dalili ya vitu hivi kuharibu saumu, na kwasababu jicho sio sehemu inayotegemewa kwa kuingilia chakula na kinywaji, na vile vile matone ya kitu majimaji kwenye sikio na puani, lakini ubora kwa haya matone ni kujitenga nayo, kwa jinsi alivyokataza Mtume ﷺkuhusu kupita mpaka katika kupandisha maji puani kwa aliyefunga, [Imwpokewa na Tirmidhi.] na kwasababu ni sehemu inayopitisha chakula hadi tumboni.

- Anapotumia mtu kitu ambacho hakiliwi au kinadhuru, kama vile sigara basi atakuwa amefungua, kwasababu amekitumia kupitia sehemu inayotumika kwa chakula, nayo ni mdomo, kama nayo itakavyofahamika kuwa chakula ama kinywaji.

- Hakiharibu saumu kitu ambacho kwamba huwezi kukiepuka, kama vile vumbi la njiani, na mabaki ya chakula yaliosalia kati ya meno.

Dawa inayotumika kama chakula inaharibu saumu.Sindano ya penicillin haiharibu saumu.(Hii ni sindano ya kukinga au kutibu madhara yanayosababishwa na bacteria).Vipuliza hewa vya kutibu pumu haviharibu saumu.Wanja haiharibu saumu.Sigara zinaharibu saumu.Mabaki ya chakula yaani katika meno hayaharibu saumu.
2. Kufanya Tendo la Ndoa
Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ} البقرة:187}

[Mmehalalishiwa usiku wa saumu kuingiliana na wake zenu] [Al-Baqarah – Aya 187].

Na “Ar-Rafath” ni neno la kiarabu lililotumika katika Aya hii kumaanisha kuingiliana – yaani kufanya tendo la ndoa, basi yoyote atakaye ingiliana na mkewe au mumewe hali ya kuwa amefunga, saumu yake itakuwa imeharibika, na atalazimika ailipe siku hiyo, na pamoja na kuilipa ni juu yake kutoa kafara nzito, nayo ni kuacha huru mtumwa, akiwa hatopata mtumwa wa kumuacha huru, atalazimika kufunga miezi miwili mfululizo, na akiwa hawezi kufunga atalazimika kulisha masikini sitini, kama ilivyothibiti kutoka kwa Abu Hurerah radhi za Allah ziwe juu yake Anasema:

جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه وسلم فقال: هلكت، قال: وما شأنك، قال: وقعت على امرأتي في رمضان، فقال: هل تجد ما تعتق رقبة. قال: لا، قال: فهل تستطيع أن تصوم شهرين متتابعين، قال: لا، قال: فهل تستطيع أن تطعم ستين مسكيناً، قال: لا أجد، فأتى النبي صلى الله عليه وسلم بعرق فيه تمر، فقال: خذ هذا فتصدق به، فقال: أعلى أفقر منا؟ ما بين لابتيها أفقر منا، ثم قال: خذه فأطعمه أهلك. رواه البخاري ومسلم

[Alikuja mtu mmoja kwa Mtume ﷺ akasema nimeangamia. Mtume akamuuliza: Una nini? Akajibu: Nimemuingilia mkewangu ndani ya Ramadhani. Mtume akamuuliza: Waweza kuacha mtumwa huru?. Akajibu: Siwezi.. Mtume akamuuliza: je waweza kufunga miezi miwli mfululizo? Akasema: Siwezi. Mtume akamuuliza: Basi waweza kulisha masikini sitini?. Akasema: Siwezi. Mtume akamwambia: Kaa. Akakaa. Mtume ﷺ akaleta chombo ambacho ndani yake mna tende. Akasema: Chukua (hiki chombo) wende ukatolee sadaka. Akasema yule mtu: Je kuna fakiri zaidi yetu? (yaani maskini kuliko familia yake). Mtume akacheka mpaka yakaonekana magego ya meno yake, akasema: Lisha familia yako ( hizo tende)] [Imwpokewa na Bukharin a Muslim.].

MAELEZO

Na inakuwa kafara inafuata mfumo huu, hivyo basi mtu asilishe maskini isipokuwa akiwa hawezi kufunga hiyo miezi miwili mfululizo, wala asifunge isipokuwa ikiwa hawezi kuacha huru mtumwa.

JE MWANAMKE ANALAZIMIKA KUTOA KAFARA?

Na inamlazimu mwanamke kutoa kafara ikiwa ameridhiana na mumewe kufanya tendo la ndoa, na iwapo amelazimishwa na mumewe kuingiliana basi saumu yake imeharibika na itamlazimu mwanamke huyo kuilipa saumu hiyo peke yake bila ya kutoa kafara.

JE KUJITOA MANII KWA MKONO KUNALAZIMU KAFARA?

Na ni katika maana ya jimai (tendo la ndoa) kujitoa manii kwa kukusudia, Mtu akitokwa na manii kwa kubusiana, au kwa kugusa au kwa kutumia mkono, basi saumu yake itaharibika, kwa sababu hiyo ni katika shahawa inao haribu saumu, na itakuwa ni juu yake kuilipa saumu yake wala hatolazimika kutoa kafara, kwa sababu kafara imekuja kwa tendo la ndoa peke yake.

Mtu akibusu au akigusa au akifikiria akatokwa na madhii saumu yake ni swahihi. kwa kutokuwa na dadili yakuharibu saumu kwa kutokwa na madhi

Mtu anapo lala akaota, au akatokwa na manii bila ya shahawa kama kuwa mgonjwa, saumu yake ni swahihi kwa sababu hayakutoka kwa hiyari yake.

Mtu anapo amka na janaba la tendo la ndoa kabla ya alfajiri au akaota, saumu yake ni swahihi na ni juu yake kuoga ili apate kuswali alfajiri na jamaa, imethubutu kutoka kwa bibi A’isha radhi za Allah ziwe juu yake Kwamba Mtume ﷺ:

أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كان يُصبح جُنُبًا من جماعٍ ثم يغتَسِلُ ويصوم] متفق عليه]

[Alikuwa akiingiliwa na Alfajiri na yeye akiwa na janaba la mkewe, kisha akioga na akifunga.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

3. kujitapisha kwa kusudi
Nao ni mtu kutoa kilichoko tumboni kutokana na chakula au kinywaji kwa njia ya mdomo kwa kusudi, ama akishindwa na akatoka bila ya khiyari yake haiathiri saumu yake kwa neno lake Mtume ﷺ:

من ذرعه القيء فليس عليه قضاء، ومن استقاء عمدا فليقض] رواه أبو داود والترمذي وغيرهما وصححه الحاكم]

[Mwenye kushindwa na matapishi basi hana haja ya kukidhi na mwenye kujitapisha kwa kusudi basi alipe] [Imepokewa na Abuu Daud na Tirmidhiy na kusahihishwa na Al Haakim]

4. Damu ya Heidhi na Nifasi
Wakati wowote mwanamke atakapo ona damu ya hedhi au nifasi japo kuwa ni wakati wa jioni kabla ya kutwa jua kwa mda mchache saumu yake itaharibika na atawajibika kuilipa

SUALA: JE KUUMIKA HUVUNDA SAUMU?

- Kauli yenye nguvu ni kuwa kuumika hakuvundi saumu kwa sababu Mtume ﷺ Aliumika na hali yakuwa amefunga, Amepokewa kutoka kwa said Al’khudriy radhi za Allah ziwe juu yake akisema

رخص رسول الله في القبلة للصائم والحجامة] أخرجه الدارقطني]

[Aliruhusu Mtume wa Mwenyezi Munguﷺ Kubusu kwa aliyefunga na kuumika,] [Imepokewa na Al Daarqutniy]. Lakini inachukizwa kuumika kwa ajili ya kudhofika,

سئل أنس بن مالك هل كنتم تكرهون الحجامة للصائم؟ قال : لا ، إلا من أجل الضعف] رواه البخاري]

[Aliulizwa Anas bin Maalik radhi za Allah ziwe juu yake Mulikuwa mukichukiza kuumika kwa alie funga? Akasema la ila kwa ajili ya kudhofika.] [Imepokewa na Bukhari]

- Haidhuru mtu kutokwa na damu katika jaraha, au kung’oa jino au kutokwa na damu za puwa, au kutoa damu kwa ajili ya kujipma, au kujitolea, yote haya hayaharibu saumu.
 
Shehe umefafanua vizuri sana, sasa badili hiyo avatar yako ili heshima yako iendane na hii post yako
 
d794ae5eed5a9685d463afe543aef62e.jpg
hii pia inqharibu swaumu mkuu
 
Asalaam alaykum warahmatulah wabarakatuh

Tujikumbushe Du'aa ya wakati wa kufungua Swawm

ذَهَـبَ الظَّمَـأُ، وَابْتَلَّـتِ العُـروق، وَثَبَـتَ الأجْـرُ إِنْ شـاءَ اللهُ

Dhahabadh-Dhwama-u Wabtallatil-'Uruuq,, Wathabbatal-Ajru Insha-Allaah.

“Kiu kimeondoka na mishipa imelainika, na yamethibiti malipo Mwenyezi Mungu Akipenda”

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdillaahi bin ‘Amr bin ‘Al -‘Aas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: ‘Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu “Aliyefunga wakati wa kufuturu kwake ana Du'aa isiyorudishwa”

اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ بِرَحْمَـتِكَ الّتي وَسِـعَت كُلَّ شيء، أَنْ تَغْـفِرَ لِي

Allaahumma Inniy As-aluka Birahmatikal-latiy Wasi'at Kulla Shay'in An Taghfiraliy.

“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kwa rehma Zako ambazo zimeenea kila kitu, Unisamehe”
Hata hii nayo pia inatumika
اللهم اني لكسمت، وبك امنت، وعلا رزكك افطرت، وعليك توكلت.
 
Dua nzuri sana[emoji261] ﷽[emoji261]

‎الحمد لله والصلاة والسلام على رسول الله وعلى آله وصحبه أجمعين ..

✍Ewe Mola wangu mimi hakika ni mja wako dhaaifu na wewe ni Mola wangu Latwifu.
Sina wa kumlilia zaidi yako Ya Hannan Ya Mannan.
Wewe ndio tegemeo la huzuni zangu na unyonge wangu.
Hakika ulimwengu waweza kunitupa lakini wewe daima utanienua na kunirehemu.
Mola wangu umenihifadhi tangu katika tumbo la mama yangu mzazi hadi leo kufikia kua hali nilio.
Nakuomba kwenye shari uniepushe na kwenye mazuri uniongoze.
Nikikosa unisamehe na nikipata nitosheke na kuridhika.
Mapenzi yako hakika ni makubwa kwetu Ya Rabb. Adhabu zako ni kubwa na msamaha wako ni mkubwa zaidi.
Ya Rabb twalia kwa dhambi zetu na tuko chini ya twaa yako ya Rahmaan.
Ya Rabb usipotusamehe na kutughufuria hakika tutakua katika hasara.
Itakuaje siku ya siku tutakapo simama mbele yako ya Rabb na huku tukingoja majibu yetu na kupewa vitabu vyetu.
Hakika hio itakua siku nzito kwetu.
Ya Rabb tujaaliye kufaulu duniani na akherah.
Ya Rabb tujaaliye nyoyo zenye kutubu kwa dhambi zetu, nuru katika majumba yetu, huruma kwa wenzetu , ihsaani kwa jirani na waisilamu wenzetu.
Ya Rabb tujaaliye mwisho mwema sisi na familia zetu.
Ya Rabb tusamehe dhambi zetu za siri na dhahiri.
Ya Rabb tujaaliye wema na huruma bayna yetu.
Ya Rabb tujaaliye kauli njema kwa wenzetu na maneno mazuri bayna yetu.
Kila mkosa Ya Rabb muongoze na kila mwenye matatizo mpe wepesi.
Ya Rabb tujaaliye kua mbali na fitnah na ubaya.
Ya Rabb Ya Rabb Ya Rabb tujaaliye vizazi vyema .
Ya Rabb kwako ndio tegemeo la kila mnyonge na mwenye tatizo.
Ya Rabb tupe muongozo wa dini na tujaaliye kua mbali na jahhanam.
Ya Rabb Ya Rabb Ya Rabb tujaaliye kila la kheri na tawfiq.

‎سبحان ربك رب العزة عما يصفون، وسلام على المرسلين، والحمد لله رب العالمين.
‎آمين.. آمين.. آمين
 
Aaaamin
 
Back
Top Bottom