Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

*بسم الله الرحمن الرحيم*

*MADA YA KUMI NA NNE*

*FADHILA ZA KISIMAMO CHA USIKU*

Miongoni mwa jihadi kubwa ya nafsi ni kusimama usiku kufanya ibada na ibada hiyo ina fadhila kubwa moja kati ya hizo ni bora kuliko dunia na vilivomo ndani yake, miongoni mwa fadhila za kusimama usiku ni:

1. Kusamehewa dhambi zilizopita

2. Wakati wa usiku kuna muda lau kama Muislamu atamuomba Allah jambo la dunia na akhera, Allah atampa.

3. Kisimamo cha usiku ni katika amali za Mitume.

4. Ni miongoni mwa sababu ya kuingia Peponi

5. Ni miongoni mwa sababu za kukingwa na Moto

6. Ni miongoni mwa sababu za kuwashinda Mashetani na Maadui

Ni vyema katika mwezi huu wa Ramadhani Muislamu akajitahidi kusimama usiku kufanya ibada na zipo sababu zenye kumsaidia mtu kusimama usiku ambazo tutakuja kuzitaja katika mada zijazo, in shaa Allah.

Tunamuomba Allah atujalie nasi tuwe katika waja wake anao waacha huru na moto na kuwatakabalia dua zao na anaowasamehe madhambi yao . Aamiyn
 
*﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾*

*☪ LEO KATIKA FUNGA ☪*
*( 20 )*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{ ﺷَﻬْﺮُ ﺭَﻣَﻀَﺎﻥَ ﺍﻟَّﺬِﻱَ ﺃُﻧﺰِﻝَ ﻓِﻴﻪِ ﺍﻟْﻘُﺮْﺁﻥُ }*
*Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani.*
ﺳﻮﺭﺓ ﺍﻟﺒﻘﺮﺓ، ﺁﻳﺔ : .185
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""

*TUKIWA NDANI YA MWEZI HUU WENYE KHERI NA FADHILA NYINGI KABISA, NA LEO TUKIWA TUNAKAMILISHA SIKU YA 20 KWA UWEZO WAKE ALLAH MTUKUFU, IN SHA ALLAH DARSA YETU YA FUNGA SIKU YA LEO ITAKUA NA MAUDHUI FUPI KUHUSU.*

*☆ ﻟَﻴْﻠَﺔُ ﺍﻟْﻘَﺪْﺭِ:*
*☆ USIKU WA CHEO:*

*☆ ﻟﻠﻴﻠﺔ ﺍﻟﻘﺪﺭ ﻣﻜﺎﻧﺔ ﻋﻈﻴﻤﺔ ﻭﻓﻀﻞ ﻋﻈﻴﻢ ﻋﻨﺪ ﺍﻟﻤﺴﻠﻴﻦ، ﻭﻫﻮ ﺃﻣﺮ ﻭﺭﺩ ﻓﻲ ﺍﻟﺤﺪﻳﺚ ﺍﻟﺸّﺮﻳﻒ ﻋﻦ ﺍﻟﺮّﺳﻮﻝ ﻋﻠﻴﻪ ﺍﻟﺴّﻼﻡ:*
*LAYLATUL QADRI NI SEHEMU YENYE NAFASI TUKUFU KABISA NA UBORA MKUBWA KABISA KWA WAISILAMU. NALO NI JAMBO AMBALO IMEPOKELEWA KATIKA HADITHI TUKUFU KUTOKA KWA RASULI(ﷺ) PALE ALIPOSEMA:*

*" ﻣَﻦْ ﻗَﺎﻡَ ﻟﻴﻠﺔَ ﺍﻟﻘَﺪﺭِ ﺇِﻳﻤَﺎﻧًﺎ ﻭَﺍﺣْﺘِﺴَﺎﺑًﺎ ﻏُﻔِﺮَ ﻟَﻪُ ﻣَﺎ ﺗَﻘَﺪَّﻡَ ﻣِﻦْ ﺫَﻧْﺒِﻪِ"*

*[emoji840] MAANA YAKE.*

*"Atakae simama LAYLATUL QADRI kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia."*

*HAPA RASULI (ﷺ) ATUBAINISHIA KWAMBA: WATU WATAKAO KUTWA WAKIFANYA IBADA MBALIMBALI KATIKA USIKU HUO WA CHEO, BASI HAO NDIO WATAKAO STAHIKI MSAMAHA KUTOKA KWA ALLAH MTUKUFU, NA WALA SIO WALE WATAKAOKUTWA HALI WAMELALA.*

*من ﻓﻀﺎﺋﻞ ﻟﻴﻠﺔ ﺍﻟﻘﺪﺭ:*
*MIONGONI MWA FADHILA ZA LAYLATUL QADRI:*

*● ﻓﻀّﻞ ﺍﻟﻠﻪ ﺗﻌﺎﻟﻰ ﻫﺬﻩ ﺍﻟﻠﻴﻠﺔ ﺑﺄﻥ ﺃﻧﺰﻝ ﺍﻟﻘﺮﺁﻥ ﺍﻟﻜﺮﻳﻢ ﻓﻴﻬﺎ، ﻭﻫﻮ ﺍﻷﻣﺮ ﺍﻟﻮﺍﺭﺩ ﻓﻲ ﺍﻟﻘﺮﺁﻥ ﺍﻟﻜﺮﻳﻢ ﻧﻔﺴﻪ ﺣﻴﻦ ﻗﺎﻝ ﺗﻌﺎﻟﻰ : ‏{ ﺷَﻬْﺮُ ﺭَﻣَﻀَﺎﻥَ ﺍﻟَّﺬِﻱَ ﺃُﻧﺰِﻝَ ﻓِﻴﻪِ ﺍﻟْﻘُﺮْﺁﻥُ ‏}*
*■ ALLAH MTUKUFU AMEUFADHILISHA USIKU HUU KWA KUITEREMSHA QUR'AAN TUKUFU NDANI YAKE, NALO NI JAMBO LILILOPOKELEWA NDANI YA QUR'AAN YENYEWE, PALE ALLAH ALIPOSEMA:*

```Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani```
ﺳﻮﺭﺓ ﺍﻟﺒﻘﺮﺓ، ﺁﻳﺔ : .185

*● ﺗﻔﻮﻕ ﻫﺬﻩ ﺍﻟﻠﻴﻠﺔ ﺑﺄﻫﻤﻴّﺘﻬﺎ ﻋﻠﻰ ﺃﻟﻒ ﺷﻬﺮ، ﻓﻴﺮﺗﻔﻊ ﻓﻀﻠﻬﺎ، ﻭﻳﺘﻀﺎﻋﻒ ﺍﻷﺟﺮ ﻓﻴﻬﺎ ﻭﻫﻮ ﻣﺎ ﻭﺭﺩ ﻓﻲ ﺍﻟﻘﺮﺁﻥ ﺍﻟﻜﺮﻳﻢ ﺣﻴﻦ ﻗﺎﻝ ﺗﻌﺎﻟﻰ : ‏{ ﻟَﻴْﻠَﺔُ ﺍﻟْﻘَﺪْﺭِ ﺧَﻴْﺮٌ ﻣِﻦْ ﺃَﻟْﻒِ ﺷَﻬْﺮٍ ‏}*
*■ HUWA ZAIDI (MALIPO YAKE) KWA UMUHIMU WA USIKU HUU ZAIDI YA MIEZI ELFUMOJA (KWA MTU ALIEFANYA IBADA) HUWA JUU ZAIDI FADHILA ZAKE NA HUONGEZEKA MALIPO YAKE, NAYO KAMA ILIVYO POKELEWA NA KUELEZWA NDANI YA QUR'AAN PALE ALLAH MTUKUFU ALIPOSEMA:*

```Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.```
ﺳﻮﺭﺓ ﺍﻟﻘﺪﺭ ، ﺁﻳﺔ : .3

*● ﺗﺘﻨﺰّﻝ ﺍﻟﻤﻼﺋﻜﺔ ﻓﻲ ﻫﺬﻩ ﺍﻟﻠﻴﻠﺔ ﻟﺘﺤﻒّ ﺍﻟﻤﺴﻠﻤﻴﻦ، ﻗﺎﻝ ﺗﻌﺎﻟﻰ ﻓﻲ ﺍﻟﻘﺮﺁﻥ ﺍﻟﻜﺮﻳﻢ : ‏{ ﺗَﻨَﺰَّﻝُ ﺍﻟْﻤَﻼﺋِﻜَﺔُ ﻭَﺍﻟﺮُّﻭﺡُ ﻓِﻴﻬَﺎ ﺑِﺈِﺫْﻥِ ﺭَﺑِّﻬِﻢْ ﻣِﻦْ ﻛُﻞِّ ﺃَﻣْﺮٍ ‏}*
*■ HUSHUKA MALAIKA KATIKA USIKU HUU KWA AJILI YA KUWAFUNIKA WAISILAMU (KWA REHEMA ZAKE ALLAH MTUKUFU) AMESEMA ALLAH MTUKUFU:*

```Huteremka Malaika na Roho (Jibriliu) katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.```
ﺳﻮﺭﺓ ﺍﻟﻘﺪﺭ، ﺁﻳﺔ : 4

*● ﺗﺨﻠﻮ ﻫﺬﻩ ﺍﻟﻠﻴﻠﺔ ﻣﻦ ﺍﻟﺸﺮﻭﺭ، ﻓﻴﻌﻢّ ﺍﻟﺴﻼﻡ ﻭﺍﻟﻄﻤﺄﻧﻴﻨﺔ ﻭﺍﻟﺮّﺍﺣﺔ، ﻭﻫﻲ ﻛﻤﺎ ﻭﺭﺩ ﻓﻲ ﺍﻵﻳﺔ ﺍﻟﻜﺮﻳﻤﺔ : ‏{ ﺳَﻠَﺎﻡٌ ﻫِﻲَ ﺣَﺘَّﻰٰ ﻣَﻄْﻠَﻊِ ﺍﻟْﻔَﺠْﺮِ ‏}*
*■ HUEPUKANA USIKU HUU KUTOKANA NA SHARI, BASI HUENEA AMANI NA UTULIVU NA RAHA, NAYO KAMA ILIVYO POKELEWA NA KUELEZWA NDANI YA QUR'AAN:*
```Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.```
ﺳﻮﺭﺓ ﺍﻟﻘﺪﺭ، ﺁﻳﺔ : 5

*NDUGU YANGU KATIKA IMANI, HIZI NI BAADHI YA FADHILA ZINAZOPATIKANA NDANI YA LAYLATUL QADRI, BALI ZIPO FADHILA NYINGI AMBAZO HATUWEZI ZIELEZEA KWA UKAMILIFU WAKE, KUBWA ZAIDI NA MUHIMU: HAKIKISHA UNASIMAMA IMARA NDANI YA HIZI SIKU ZOTE ZILIZOBAKIA KATIKA MWEZI HUU WA RAMADHANI ILI UWEZE KUZIPATA FADHILA HIZO NA KHERI ZA LAYLATUL QADRI, KWANI UKILALA NA UKAFANYA UZEMBE, UTAKUA UMEPEATA KHASARA ISIYO NA MFANO.*

☪☪☪☪☪☪☪☪

*[emoji257] ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*

Ameen

*الدعوة اﻹسلامية.*
 
KCWW MASWALI YA RAMADHANI XVI

Tarehe 20 Ramadhani, 1438, sawa na 15 Juni, 2017.‎
SEHEMU YA KUMI NA SITA

Nimeulizwa, NANUKUU:-‎

Salam alaykum Shareef Abdulqadir. Hakika tunaelimika sana kutoka kwako ‎juu ya Dini yetu! Mwenyezi Mungu akulipe kheri duniani na akhera. ‎Naomba kuelimishwa zaidi, Alhabib.‎
‎ ‎
Je, inajuzu kwa wafanya kazi wa viwanda vya kufua vyuma, kama chuma ‎cha pua, au migodi ya kuyeyusha madini, ambako wanafanya kazi karibu na ‎matanuri ya moto mkali sana, unaowaka masaa 24, siku nenda siku rudi, bila ‎ya kusita, na hivyo inakuwa shida kubwa sana kwao kufunga Ramadhani. ‎

Je, wanaweza kufidia kwa kulisha masikini, badala ya kufunga? Maana likizo ‎yao ni kama wiki mbili au tatu tu, katika mwaka mzima, hivyo hawana muda ‎wa kutosha kuja kulipa, Ramadhani yote. Nini hukumu yao? Wanaweza ‎kutoa fidia, tu, badala ya kufunga? ‎

JIBU

BISMILLAH

Haijuzu! Wenye kufanya kazi za sulubu, sulubu yoyte ile, yenye mazingira ‎magumu kama hayo uliyoyataja , ambao wanafanya kazi karibu na matanuri ‎ya moto mkali -au vibarua na mafundi wa ujenzi wa barabara, majumba na ‎kadhalika, chini ya Jua laki, na khasa katika mataifa yenye joto kali- ‎haiwajuzii kuacha kufunga Mwezi wa Ramadhani kwa hoja ya kwamba ‎mazingira ya kazi zao ni magumu sana, na hivyo watoe fidia ya kulisha ‎masikini. Haijuzu. Sharia ya kufunga inawahusu kama inavyo mhusu mtu ‎yeyote mwengine. Hivyo, haiwezekani kutolewa fatwa ya jumla jamala ‎kwamba wenye kufanya kazi za sulubu, mchana wa Ramadhani, wanaweza ‎kuacha kufunga, na badala yake watoe fidia ya kulisha masikini mmoja kwa ‎kila siku moja. Haiwezekani. ‎

Sharia, kama wanavyo sema- ni msumeno. Na Sharia za Mwenyezi Mungu ‎nazo vile vile ni msumeno, tena wenye makali pande zote mbili. Mwenyezi ‎Mungu amesema: ‎فمن شهد منكم الشهر فاليصمه!‏‎ : Ataye shuhudia kuingia mwezi ‎afunge!” Yaani atayekuwepo aishipo unapoingia mwezi wa Ramadhani, basi ‎afunge. ‎
Hivyo basi, ni wajibu wa kila aliyekuwepo hai kufunga isipokuwa wale ‎wachache tu, walioruhusiwa kutokufunga na baadala yake ama kulipa baada ‎ya Ramadhani, au kutoa fidia kutokana na ugonjwa usiotazamiwa kupona au ‎wazee wasiomudu kufunga kabisa. Wengine wote, lazima wafunge, na kama ‎kuna udhuru wa muda, basi ataruhusiwa kutokufunga, lakini LAZIMA alipe ‎baadae, baada ya kuondoka udhuru huo, kama maradhi ya muda.‎

Wafanya kazi za sulubu hawamo humo. Na hivyo, ni suala la mtu mmoja ‎mmoja na jinsi ya kukabiliana na kazi hiyo, siku hadi siku. Hakuna leseni ya ‎jumla jamala, kwa sababu zifuatazo.‎

‎1.‎ Kila mfanya kazi ana uwezo wake wa kuhimili uzito; hawawiani kwa ‎nguvu wala uzima. Kila mmoja na uwezo wake na uzima wake.‎
‎2.‎ Kila mfanya kazi, anaweza - akidhamiria kikweli- kuomba doria\shifti ‎ya usiku, katika Ramadhani, badala ya mchana. Lilio muhimu ni ‎kujipanga itakikanavo, ili aweze kufanikiwa.‎
‎3.‎ Kila mmoja ana likizo katika mwaka. Kama hawezi kufunga katika hali ‎kama hiyo, aombe kuchukua likizo yake katika Mwezi wa Ramadhani ‎ili afunge.‎
‎4.‎ Kila mtu, anapaswa kuamka kwa nia ya kufunga, na afunge kama ‎kawaida. Endapo itamtokea baadaye, katika siku hiyo hiyo, kushindwa ‎kuendelea na swaumu, basi inamjuzia WAKATI HUO, kufungua na ‎kulipa siku nyengine baadae. Lazima alipe baadae kwa sababu udhuru ‎wake ni wa muda; hivyo haingii katika wasioweza kufunga maisha ‎yao. ‎
Kwa maneno mengine, wafanya kazi za sulubu, kama wafanyakazi za ‎viwanda vya kufua vyuma, madini, wachoma mikate kwenye matanuri, ‎wahunzi, wajenzi wa barabara, wamwa-zege na kadhalika, wote hao ‎LAZIMA WAAMKIE NA NIA YA KUFUNGA, na WAFUNGE, kikomo ‎cha uwezo wao. Inapofikia kutoweza kuendelea na swaumu, katika siku ‎maalumu, basi HAPO ndipo MWENYE tatizo hilo ndiye anaye ruhusiwa ‎kufungua na anapaswa kulipa siku nyengine, nje ya Ramadhani. Lakini ‎KAMAWE haingii katika kuacha kufunga na hivyo kufanya mbadala wa ‎kulisha masikini. ‎

Hivyo, hata akifikia hali hiyo, na akajikuta anapaswa kufungua, basi siku ya ‎pili LAZIMA anuwie kufunga na aamke akiwa amefunga, na aendelee na ‎kufunga kikomo cha uwezo wake, kwa mtindo huo huo, hadi mwisho wa ‎Ramadhani. Siku atayohemewa, kikomo cha kuhemewa, basi afungue siku ‎hiyo, na alipe siku nyengine baada ya Ramadhani. Hakuna kutoa fidia. ‎

Ndiyo maana, hata madereva wa mabasi ya abira ya masafa marefu; kutoka ‎mji mmoja hadi mji mwengine, wanawajibika kuamka wakiwa wamefunga; ‎maana wao SI WASAFIRI, bali wamo kazini. Na hakuna basi au teksi ‎inayosafiri, masaa 12 mfululizo, pasi na kutoweza kusimama katika miji ‎mbali mbali. Hata mafuta ya gari hilo yataisha, na kupaswa kusimama kujaza ‎mafuta. ‎
Hivyo, madereva wa mabasi ya abiria hawamo safarini, wamo kazini. Na ‎kama ilivyokuwa wafanya kazi kwenye migodi ya kufua vyuma na madini, ‎wamo kazini, basi na madereva wa mabasi ya abiria, au treni, au ndege, au ‎meli, na kadhalika, na wao wamo kazini. Si wasafiri. Wanasafiri ama na ‎vyakula vyao, ndni ya vyombo hivyo, au wanajuwa wasimame wapi kupata ‎chakula na wapi pa kupumzikia na kadhalika. Hivyo, lazima waamke na nia ‎ya kufunga, na wafunge kikomo cha uwezo wao. Na hivyo, kufungua au ‎kutokufungua ni kwa mujibu wa siku hadi siku, na kwa mujibu wa mtu na ‎mtu mwengine; siyo kwa kuamua kuwa mwezi mzima hatofunga, na hivyo ‎atowe fidia. Hapana. ‎

Mfano wao ni zima-moto. Wafanyakazi wa kuzima moto, wanapaswa ‎kuamka wakiwa wamefunga. Iktokea ajali ya moto, wakapaswa kwenda ‎kuuzima moto huo, na mmoja wao akajikuta anapaswa kuvaa mavazi ‎maalumu na kujitoma kwenye ndimi za moto, ili kwenda kumuokoa mtu ‎ndani ya jumba linalowaka moto na kuweko moshi mkubwa, basi huyo ‎anaweza kufungua ili akatekeleze wajibu huo, kwa wakti huo, kwa ajali hiyo, ‎na atalipa siku nyengine. Lakini kama ataweza kuifanya kazi hiyo pasi na ‎kufungua, basi aifanye na swaumu yake. ‎
Maswahaba wa Mtume ‎ﷺ‎ na yeye mwenyewe, walipigana vita vya vikli vya ‎Badr huku wakiwa wamefunga, hawajui hata watafuturia nini. Hivyo, ‎unafunga kikomo cha uwezo wako, na unafungua unapokaribia kufika ‎kikomoni. Katika hali kama hiyo, hakuna junaha kufungua na kulipa swaumu ‎siku nyengine, nje ya Ramadhani. SI kulisha masiiini, kama mbadala wa ‎kufunga.‎
‎ ‎
Fidia ni kwa mgonjwa asiyetazamiwa kupona ugonjwa wake, au mzee, ‎kikongwe, hawezi kabisa kufunga, na hana rajwa ya kurudia ujana, hadi kufa ‎kwake. HAO, peke yao, ndio wanaoruhusiwa kutoa fidia ya kumlisha ‎masikini kwa kila siku moja, badala ya kufunga. Akifariki, kati kati ya ‎Ramadhani, basi fidia yake ni kwa siku alizokuwa hai tu, siku zinazo fuata ‎kifo chake, hawajibiki, na hivyo halipiwi. Maana hana deni kwa siku hizo. ‎

Kwa ufupi, kila mwenye kumuanini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, ‎anapaswa kuamka, katika Ramadhani akiwa amefunga, isipokuwa wale ‎waliopewa ruhusa kuamka pasi na kufunga. Hawa, peke yao, ndio inawajuzia ‎kuamka bila ya kufunga, na badala yake kulisha masikini kwa kila siku moja ‎inayo wapita, katika Ramadnani. Wengine wote, lazima waamke na nia ya ‎kufunga, na wafunge kuanzia alfajiri hadi kuchwa Jua. Atakaye tokewa na ‎udhuru wa kisheria, kati kati ya mchana wa Ramadhani, basi anaruhusiwa ‎kufungua siku hiyo, na alipe baadae. Vile atayeharibu swaumu yake, ‎makusudi, kwa tendo la ndoa, mchana wa Ramadhani anapaswa siyo kulipa ‎siku hiyo tu, bali na kutoa KAFARA yaa kuhuaribu swaumu yake kwa ‎makusudi. ‎
‎******** ‎

‎2. Habib Abdulgadir! Assalamu alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh. ‎Naomba msaada wako kunifafanulia jambo moja geni kabisa nimelikuta ‎ughaibuni nilipokuja kufanya kazi. Niko mataifa ya joto kali (nchi imetajwa ‎jina). Na nimekuta kuwa ni kawaida kwa watu wa nchi hii, mwenendo wao ‎katika mwezi wa Ramadhani, ni kwamba mchana kwao ni kama usiku na ‎usiku ni kama mchana. Kulingana na shughuli zao za kila siku. Yaani mchana ‎wanalala kwa muda mrefu sana, na kama wanaenda kazini, basi kwa masaa ‎machache sana. Wakitoka makazini wanarudi majumbani na wanalala hadi ‎magharibi. Mchana mzima barabara ni tupu, na maduka karibu yote ‎yanafungwa, hata yasiyokuwa ya kuuza vyakul. Lakini, ikiingia magharibi, ‎wanaamka, wanafungua kinywa kwa kitu kidogo tu, kisha wanaanza kwenda ‎mabarazani kwa mazungumzo, au kwenda madukani, hadi usiku wa manane. ‎Kisha wanarudi majumbani mwao au kwenda kwenye makaramu na huko ‎wanakula kila aina ya vyakula, mpaka ikiingia alfajiri, wanaaza kufunga kama ‎jana. Wengine hata hawaendi msikitini. Yaani mchana wa Ramadhani kwao ‎ni usiku, na usiku wa Ramadhani kwao ni mchana. Je, nini hukumu yao?‎

JIBU

BISMILLAH
Ni kweli, zipo badhi ya jamii zenye watu kama hao, na wanafanya hayo ‎uliyoyasema na zaidi ya hayo. Na watu kama hao wapo siyo tu hapo ulipo, ‎bali hata nje ya eneo ulipo. Ila si wote. Bado wapo waja wema wanaofunga ‎Ramadhani kama itakikanavyo, na yumkini hao ndio wengi. Ila, kama ‎kawaida, wapo vile vile wanaofanya munkari huo, hadharani, na kama ‎utamaduni unaokubalika na kuzoweleka katika jamii husika, licha ya ‎wanazuoni mbali mbali kukemea tabia hiyo. Hao ni miongoni mwa wenye ‎kujidanganya na kuvuruga thawabu za swaumu yao. Ila swaumu zao ni ‎swahihi. Kulala hakubatilishi swaumu, isipokuwa kwa kuzimia mchana ‎kutwa. Hapo ni kuzimia na kutokwa na fahamu mcahan kutwa ndiko kunako ‎batilisha swaumu. Ama kulala hakubatilishi swaumu, kwa sababu hakuna ‎anayelala fofoforo mchana kutwa, pasi na kuzindukana hata kama ni sekunde ‎chache. ‎

Hivyo, kimsingi, usingizi haubatilishi swaumu. Na ni makuruhu sana, kulala ‎mchana wa Ramadhani kwa makusudi kwa muda mrefu, hata kama kulala ‎hakufunguzi swamu. Bali kunaweza kuwa ni haramu, iwapo vipindi vya ‎swala vitampita bila ya kuamka na kuswali swala za faradhi za machana. ‎Ataingia katika dhambi za kupuuza swala, na dhambi za kupuuuza swala ni ‎kubwa.‎

Hivyo, ni vibaya sana, tena sana, kwa Mwislamu kugeuza mchana wake wa ‎Ramadhani kuwa ndio usiku, na usiku wake wa Ramadhani kuwa ndio ‎mchana, wake. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa ibada, kuomba maghfira, ‎kutenda amali njema, kukithirisha kuswali, kusoma Qur’ani, kutoa sadaka na ‎kadhalika. Si mwezi wa kualal, wala si mwezi wa kufakamia na kula kila aina ‎ya vyakula; utadhani mtu ametangaza vita vya vyakula aina kwa aina.‎
‎. ‎
Naam, kama mtu ni mgonjwa, na ugonjwa wake hauhitaji kula dawa ‎mchana, bali unahitaji kupumzika, kikamilifu, au kwa muda mrefu, basi ‎hakuna junaha kwa mtu kama huyo kulala mchana wa Ramadhani, pasi na ‎kupuuza kuswali swala za faradhi utapo wadia wakati wake. Na endapo ‎itamwia shida kufunga na ugonjwa huo, basi anaruhusiwa kufungua na ‎kulipa siku nyengine, nje ya Ramadhani. ‎
‎****** ‎

‎3. Alhabib, Sayyid Abdulqadir. Nina suali. Baba yangu mzazi amefariki ‎katikati ya Ramadhani. Je inajuzu nimlipie Ramadhani yote, au siku anazo ‎daiwa tu? Na je inajuzu nimlipie kwa kumtolea fidia tu ya kulisha masikini? ‎

JIBU

BISMILLAH

Endapo amefariki katikati ya Ramadhani, pasi na kuwa na deni la swaumu, ‎basi hakuna cha kumlipia kitu; maana hawajibiki kufunga baada ya kifo ‎chake. Lakini endapo amepitisha siku kadhaa, katika Ramadhani, bila ya ‎kufunga, kutokana na udhuru wa kisheria, basi unaweza kumfungia, baada ya ‎Ramadhani, kwa siku anazodaiwa, tu. Mtume ‎ﷺ‎ ameseam: ‎من مات وعليه صم صام ‏عنه وليه (متفق عليه)‏
‎“Ataye fariki, akiwa na deni la swaumu, basi anaweza kufungiwa na walii ‎wake.” Muttafaq ‘Alayhi. ‎
Hivyo, anaweza kulipiwa deni lake, tu, si asichodaiwa. Na kama hakuna wa ‎kumfungia, hasa miononi mwa watoto wake au jamaa zake, basi inajuzu ‎kumlipia fidia kutokana na mali aliyo acha, au kama hakuwacha mali, basi ‎anaweza kulipiwa na jamaa wengine, hata watoto wake. Ila atatolewa fidia ‎kwa siku anazodaiwa tu. ‎

والله أعلم

وبالله التوفيق

السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم‎ ‎

Imejbiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza ‎chchote, na kuweka kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na kwenye ‎Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

kcwajawema@gmail.com
 
Mwadau mwadau ya ramadaan*2

Mwadau mwadau ya ramadaan *2..
Mwez unatuacha kaa chin jiulize nn umevuna ..km bdo kumi la mwisho hili jipinde inshaallah...
 
☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆
Mahojiano baina ya TV ya Israel na Profesa wa Kiyahudi (Malhum Akhnof) mtungaji wa fikra: "PAZIA LA TAALUMA"!
★★★★★★★★★★
[emoji298]Swali la kwanza: Unajihisi vipi leo ukiwa umefanikiwa kutimiza ndoto yako ya "Pazia la Taaluma" ndani ya nchi za Kiislamu? Akajibu:
Furaha yangu haielezeki, lakini imetumia muda wetu mwingi mpaka tukaweza kufikia lengo letu hili.

[emoji298]Akamuuliza: Unakusudia nini unaposema umetumia muda mwingi? Akasema: Tumetumia miaka mingi hadi tukaweza kujiingiza katika nchi za magharibi, kisha katika nchi za Kiarabu,na tulikuwa tukijua kuwa mpango wetu utakuwa na mafanikio makubwa katika maendeleo ya Dola la Israel.

[emoji298]Akamuuliza: Kwa nini mulikua na uhakika wa kufanikisha fikra hii? Akasema: Kwa sababu tunajua Waislamu wa leo wako mbali na Dini yao, na wakati huo huo vijana wa Kiislamu wameanza kushikamana na Uislamu, na kama hali itaendelea hivyo,wataimaliza dola yetu.

[emoji298]Akamuuliza: Kwa nini mkasisitiza "Pazia la taaluma" ndiyo njia ya kuwafika Waislamu? Akasema: Kwa sababu tunataka wawe mbali na Dini yao.

[emoji298]Akamuuliza: Muna mipango gani ya kuuhujumu Uislamu baada ya "Pazia la taaluma"? Akasema kwa ushindani na ubaya, tunapanga kuwapiga vita (vya kifikra) wanawake wa Kiislamu!!

[emoji298]Kwa nini wanawake wa Kiislamu siyo wanaume? Akajibu: Kwa sababu tunajua mwanamke akipotoka,umma mzima utapotoka nyuma yake.

[emoji298]Akamuuliza tena: Unaelezaje vita yenu dhidi ya mwanamke wa Kiislamu? Akasema: Sisi tunakazania kumpiga vita Muislamu mwanamke na kumharibu kiakili, kifikra na kimwili kuliko kutengeneza vifaru na ndege za kivita!! Na tunasaidiwa sana na wao ktk kujishughulisha kwao na vifaa kama Blackberry na mambo mengine kama hayo na hiyo ni sehemu ya mpango wetu.

[emoji298]Akaulizwa: Je, munao mkono katika mpango wa taaluma ambao unatekelezwa sasa Lebanon? Akajibu: Hakika, sisi tunawachangia kila siku pesa nyingi na uko chini ya usimamizi wetu endelevu!!
Kwa kumalizia mahojiano yetu unawaambia nini watu wa Israel? Nawaambia: Watumie vizuri usingizi wa umma wa Kiislamu..kwani wakiamka watarejesha waliyoyakosa kwa karne kadhaa...!
'Hasbuna llaah wani'ma lwakiil'.
★★★★★★★★★★
Eneza ujumbe huu ili umma wa Muhammad (s.a.w) uamke kutoka ktk usingizi mzito na waelewe yanayowazunguka,
Mwenyezi Mungu ambariki anayesoma haya na kuueneza ujumbe huu kwa ajili ya Dini yake, in Shaa Allah.
[emoji287]TUAMRISHANE[emoji287]
[emoji287]MEMA[emoji287]
 
Asalaam Aleykum ndugu zangu wote katika imani,

Kuelekea mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan, waislamu wote nawaomba tukutane humu ili tuelimishane mawili matatu kuhusu mwezi huu.

Lengo kuu ni kuweza kufahamu yale yote aliyotufunza kipenzi chetu mtume Muhammad S.A.W kuhusu mwezi huu.

Vitu gani tukifanya vitaharibu swaumu zetu, vitu gani tukifanya vitaongeza thawabu zinazopatikana katika kufunga, ipi hukumu kwa wale wasiofunga na yapi malipo anayopewa mja ambaye anafunga swaumu kikamilifu

Pia tuweze kujifunza neema zinazopatikana kwenye usiku wa lailatul qadr, usiku ambao umebarikiwa kuliko siku elfu moja.

Kwa haya machache napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa muumba wa mbingu na ardhi ambaye si mwingine bali ni Allah S.W. na kipenzi chake, Mtume Muhammad S.A.W.

Karibuni.
Hivi nduguzo ni Waislam tu?

Kwanini usiku wa Lailatul qadr ni wa muhimu kuliko siku elfu 1 ?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] muumini wa kweli hufanya ibada bila kumbugudhi mtu wala kujionesha onesha hovyo kama ni mcha Mungu .

Hiyo ndo tabia yangu ukiniona utadhani ni mtu nisiyejua chochote kuhusu dini.
Wewe ni nafuu kuliko wale wabwabwajaji koko

Sisi tumeandikiwa katika BIBLIA TAKATIFU kuwa:

"ajikwezae atashushwa na ajishushae atakwezwa"

Pia imeandikwa katika BIBLIA TAKATIFU kuwa:

"Angalieni msiwe Wanafiki kama Mafarisayo kwakuwa wao wapenda kuonekana wakamilifu mbele za watu ila mioyo yao imejaa unafiki"

Hao wamefananishwa na makaburi ambayo kwa nje kuna maua yang'aao ila kwa ndani kuna mifupa mitupu.
 
Assalam aleykm warahmatullah wabatakatul! Naomba kujuzwa juu ya ulaj/ kutokula daku.Je nikiacha kula daku funga yangu itaswih?
Ukiacha kula daku ndio utakuwa umefunga mfungo wa kweli

Ukiamka kula daku utakuwa umebadilisha masaa ya kula tu na sio kufunga huko.

Pia jitahid ufunge ule mfungo sita (6) na usijikweze kuwa umefunga na wala usijioneshe kuwa mnyonge mnyonge na kusema eti "swaumu kali" ili tu watu wajue kuwa umefunga.

Funga kimya kimya ukimwomba Mungu wako huku ukijiepusha na madhambi ya dunia hii.

Na huo ndio mfungo wa kweli....zingine mbwembwe.
 
Ukiacha kula daku ndio utakuwa umefunga mfungo wa kweli

Ukiamka kula daku utakuwa umebadilisha masaa ya kula tu na sio kufunga huko.

Pia jitahid ufunge ule mfungo sita (6) na usijikweze kuwa umefunga na wala usijioneshe kuwa mnyonge mnyonge na kusema eti "swaumu kali" ili tu watu wajue kuwa umefunga.

Funga kimya kimya ukimwomba Mungu wako huku ukijiepusha na madhambi ya dunia hii.

Na huo ndio mfungo wa kweli....zingine mbwembwe.
Dini sio maoni ya mtu, wala logic, au nadhani, nafikiri ....la hasha dini inaongozwa na taratibu za mafundisho yaliyopo kwenye vitabu. Kitabu cha Allah na sunna yaani hadith....Suala la kula daku ni sunna na kuna fadhla kubwa sana kwa mtu kulala kisha kuamka na kula daku lake. Na wala si kama unavyodhani au unavyofikiri kuwa kula daku ni kubadili masaa ya kula. Jambo lingine nikuonezee ni kwamba funga sio kuacha kula na kunywa tu Bali ni kuacha au kujizuia kula kunywa na matamanio ya halali tangu kuchomoza kwa jua mpaka kuchwa kwake. Ndani ya usiku Yale yote ya mchana ya halali unaweza kuyafanya. Hivyo basi umempotosha muulizaji juu ya suala alilouliza. Na tusijibu vitu tusivyokua na ilmu navyo. Wallahu aalam
 
Dini sio maoni ya mtu, wala logic, au nadhani, nafikiri ....la hasha dini inaongozwa na taratibu za mafundisho yaliyopo kwenye vitabu. Kitabu cha Allah na sunna yaani hadith....Suala la kula daku ni sunna na kuna fadhla kubwa sana kwa mtu kulala kisha kuamka na kula daku lake. Na wala si kama unavyodhani au unavyofikiri kuwa kula daku ni kubadili masaa ya kula. Jambo lingine nikuonezee ni kwamba funga sio kuacha kula na kunywa tu Bali ni kuacha au kujizuia kula kunywa na matamanio ya halali tangu kuchomoza kwa jua mpaka kuchwa kwake. Ndani ya usiku Yale yote ya mchana ya halali unaweza kuyafanya. Hivyo basi umempotosha muulizaji juu ya suala alilouliza. Na tusijibu vitu tusivyokua na ilmu navyo. Wallahu aalam
Msijibu wewe na nani?

Hayo mamlaka ya kukataza kujibu umeyatoa wapi?
 
Ninakuusieni Kumcha Allah, na kuiacha dunia japo Dunia itawataka, musisikitike juu ya kitu chochote ambacho kitazuwia kufika kwenu japo ni haki yenu, semeni ukweli na fanyeni matendo kwa ajili ya malipo, kuweni maadui juu ya wenye kudhulumu na kuwasaidia wenye kudhulumiwa. ( Wasia wa Imam Ally a.s no 47 katika nahjulbalagha)
 
TUNAKUMBUSHA HUU UZI NI KWA AJILI YA WAISLAMU HATUPO HAPA KWA MALUMBANO TUPO KWA AJILI YA KUELIMISHANA KAMA HAUKUHUSU TAFADHALI PITA KIMYA KIMYA TUTAKUHESHIMU ZAIDI KWA HILO
 
Habari ndugu zangu tunakumbushana ukiwa unafunga epuka kumsema mtu yeyote kwa jambo ambalo mwenyew akilisikia litamkera, epuka kusema uongo, kutazama wanawake wanaopita inamisha macho yako baada ya mtazamo wa kwanza, husivae nguo ambayo ulinunua kwa pesa haramu yan pesa hiyo kama ulidhulmu au uliiba au ulipata kwa njia ambayo sio halali utakuwa huna funga, husile vitu ambavyo vimepatikana kwa njia ya haramu yan futari yake isiwe imepatikana kwa njia ambayo sio halali, kama kwa pesa ya kuuza pombe,guest,hotel au hata kupatikana kwa kuuza nguo za kike za uchi kwa wenye maduka......

Ndugu waislam binadamu tunapaswa kuish kwa njia ya haki kila pumz yetu.

Tumia muda wako mwingi kusoma Quran ikiwa ujui waweza mtaja mwenyezi mungu kwa wingi utapata dhawabu pia.......

Tumia ramadan hii kufanya toba na kujutia uloyatenda.....
Swadakta mkuu tuchunge funga zetu kwa kuepuka kula vya haramu, riba, kamari ni mfano tu wa vingi vya haramu alivyotukataza Mungu sasa dunia inatulazimisha tuvione vya kawaida

Mtume (saw) "kisha akataja mtu aliesafiri safari ndefu, kachafuka na kajaa mavumbi na huku ananyanyua mikono yake mbinguni akisema "Ewe Mola!Ewe Mola!nipe kadhaa na nikinge na kadhaa,wakati chakula chake ni cha haramu,kinywaji chake cha haramu,kivazi chake cha haramu na anashibishwa na haramu,Je vipi atajibiwa(dua zake)? (Al bukhari na muslim)
 
Huu uzi hadi leo ramadhani 22 bado tu haujafika hata 1k?,
Tuache uvivu.


Ramadhani Kareem
 
Back
Top Bottom