Ramadhan Special Thread

[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Hivi Ramadhan waislamu wanafunga au wanabadili muda wa kula? Na je mnaposema Ramadhan ni mwezi wa kutenda mema je miezi mingine ni ya kutenda mambaya? Asalam Allykum
Inaonekana zile funga zenu 40 we hugusi hata moja zaidi ya kujiona upo tu duniani, huamini kingine chochote zaidi ya kujijua wewe tu.
Kumbuka dini ni mfumo wa maisha kwa wenye imani yao. لا إكراه في دين قد تبيين رشدي مينل غي
 
Ndugu zangu Waislamu huu uzi upo mahususi kwa ajili ya kuelimishana sisi kwa sisi lakini pia kama kuna wa upande wa pili ameomba kuelimishwa jambo ni vema kumuelimisha kwa upole na wema, huenda akasikia na kufanya mabadiliko,
lakini kwa wale wenzetu wa kuvuruga naomba tusiwajibu chochote, mtu akikashifu na kutoa lugha mbaya, tusimjibu tumpuuze ili tusiharibu huu uzi na tusijikute tunaharibu funga zetu.

Shukrani.
 
Historia ya Funga na Maana Yake


Maana ya kufunga (Swawm) ni kujizuilia. Neno Swawm kwa maana ya kujizuilia linaweza kutumika katika kujizuia kufanya jambo lolote la kawaida mtu alilozoea kulifanya. Katika Qur-aan tunafahamishwa kuwa Bibi Maryam baada ya kumzaa Nabii ‘Iysaa (‘Alayhis Salaam) alijizuia (alifunga) ili asiseme na mtu neno lolote juu ya mtoto wake.
“...Na kama ukimwona mtu yoyote (akauliza habari za mtoto huyu) sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehema ya kufunga, kwa hiyo leo sitasema na mtu.” (19: 26).
Katika Uislamu kufunga (Swawm) ni kujizuilia kula, kunywa, kuvuta sigara, kuingiza kitu chochote katika matundu mengine mawili kama vile pua na masikio, kujizuia na kujamii, kujitoa manii kwa makusudi au kwa matamanio na kujizuia kujitapisha kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), kwa kipindi cha kati ya Al-fajri ya kweli mpaka kuingia magharibi. Hii ndio maana ya nje ya Swawm katika Uislamu.
Kufunga katika Uislamu kuna maana ya ndani zaidi, ambayo kama haikufikiwa, kuzuilia kufanya vitendo hivyo vilivyoelezwa hakutakuwa na maana yoyote kwa mfungaji.
Kufunga kwa maana ya ndani ni pamoja kujizuilia kutenda maovu yote yaliyokatazwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Ili Swawm ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu- pamoja na fikra na hisia zake na matendo aliyokataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).
Funga ya macho ni kujizuilia na kuangalia aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala); Funga ya ulimi ni kujizuilia na mazungumzo yote aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kama vile kusengenya, kusema uwongo, kugombana na kadhalika, funga ya masikio ni kujizuia kufanya yale yote aliyoyaharamisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala); funga ya miguu ni kujizuilia na kuendea yale yote aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) funga ya fikra na hisia ni kujizuia na fikra na dhana mbaya ambazo zinampelekea kuvunja amri na makatazo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Ni katika maana hii Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)anasema katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurayrah amesimulia kuwa Mtume wa Allaah amesema:
“Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allaah hana haja na kuona kuwa anaacha chakula chake na kinywaji chake (yaani Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hana haja na funga yake.” (Al-Bukhaariy).
Abu Hurayrah ameeleza kuwa Mtume wa Allaah amesema:
“Ni wangapi wanaofunga lakini hawana funga ila kukaa na kiu tu ni wangapi wanao swali usiku ambao hawana Swalah ila huambulia kupoteza usingizi tu.” (Ad-Daarimiy).
Hadithi hizi zinatuthibitishia kuwa ufungaji usioambatana na kujizuia na mambo maovu na machafu, haumpatii mfungaji faida yoyote.
 
Umuhimu Wa Funga Katika Uislamu
Funga ya Ramadhaan ni miongoni mwa nguzo za Uislamu na ni faradhi kwa Waislamu kama inavyobainika katika aya ifuatayo:
“Enyi mlioamini! Mmeamrishwa kufunga (Swawm) kama walivyofaradhishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.” (2: 183)
Kama ilivyo katika nguzo nyingine za Uislamu, mtu atakapoivunja makusudi nguzo hii hatabakia kuwa Muislamu japo atajiita Muislamu na watu wakaendelea kumwita hivyo. Katika Hadithi iliyopokelewa na Ibn ‘Abbaas, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Kuna viungo vitatu vinavyomuunganisha Muislamu na dini ya Uislamu na yeyote yule atakayevunja kiungo kimoja katika hivi atakuwa amekana Uislamu na kuuawa kwani ni halali. Viungo hivi ni: Kushuhudia kuwa hapana Mola ila Allaah, Kusimamisha Swalah tano na kufunga mwezi wa Ramadhaan.”
Katika Hadiyth nyingine Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote yule atakaye acha makusudi kufunga siku moja ya mwezi wa Ramadhaan, hawezi kuifidia siku hiyo hata akifunga kila siku katika umri wake wote (uliobakia).” (Abu Daawuud)
 
Funga ni ibada maalum iliyo muhimu sana katika kumuandaa mja kuwa mcha Mungu kwa kule kukataa kwake matamanio ya kimwili. Hivyo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa ukaribu wake ameahidi malipo makubwa kwa wenye kutekeleza ibada hii ili iwe motisha kwao ya kuwawezesha kutekeleza ibada hii kwa hima kubwa na kwa ukamilifu unaotakikana kama tunavyojifunza katika Hadiyth zifuatazo:
Abu Hurayrah ameeleza kuwa Mtume wa Allaah amesema:
“Mwenye kufunga Ramadhaan akiwa na imani na akawa na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allaah dhambi zake zote zilizopita husamehewa, Na mwenye kusimama kwa Swalah (tarawehe) katika mwezi wa Ramadhaan akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo (kutoka kwa Allaah), dhambi zake zote zilizopita zitasamehewa. Na yule atakayesimama (kwa Swalah) katika usiku uliobarikiwa (Lailatul-Qadri) akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) dhambi zake zote zilizotangulia zitasamehewa.” (Al-Bukhaariy na Muslim).
Pia Abu Hurayrah ameeleza kuwa Mtume wa Allaah amesema:
“Kila amali njema anayoifanya mwanaadamu italipwa mara kumi (Al-Qur-aan 6:160) mpaka kufikia mara mia saba (Al-Qur-aan 2:261). Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) amesema: Ila kufunga kwa sababu funga ni kwa ajili Yangu, na ni mimi mwenyewe nitakayeilipa. Mwenye kufunga anakata matamanio yake ya kimwili na anaacha chakula kwa ajili yangu. Kwa mwenye kufunga kuna furaha mbili, furaha moja anaipata wakati wa kufuturu na nyingine wakati atakapokutana na Mola wake. Na hakika harufu ya mdomo wa mwenye kufunga ni bora mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kuliko harufu ya miski. Na funga ni ngao. Kwa hiyo atakayefunga miongoni mwenu hataongea maneno ya upuuzi wala hatagombana. Kama itatokea achokozwe na yeyote, au mtu atakakupigana naye, na aseme: Nimefunga .” (Al-Bukhaariy na Muslim).
 
Historia Ya Kufunga
Funga, kama ilivyo katika ibada nyingine kama tulivyoona katika kusimamisha Swalah na kutoa zakat, imetekelezwa na Mitume wote pamoja na umma zao. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ametukumbusha hili wakati alipotupa amri ya kutekeleza ibada hii maalum, kama tunavyorejea katika Qur-aan:
Enyi mlioamini! Mmeandikiwa (mmefaradhishiwa) kufunga kama walivyofaridhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu . (2:183)
Katika historia tunajifunza kuwa, kila Mtume alipoondoka, baada ya kipindi kupita, watu waliacha mafundisho yake na kuingia katika ushirikina. Lakini bado tunakuta funga, japo si katika madhumuni na asili yake iliyoachwa na Mitume wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), imebakia katika jamii za kishirikina kwa kipindi chote cha historia. Hebu tuangalie mifano michache ya dini za ushirikina ambapo funga, kwa maana ya kushinda na njaa na kiu, imekuwa miongoni mwa ibada muhimu za dini hizo.
Jamii Ya Nabii Ibraahiym
Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) aliinuliwa katika jamii ya washirikina. Walikuwa wakiabudu jua, mwezi, nyota na masanamu chungu nzima waliyoyachonga wenyewe. Pamoja na ushirikina wao huo walikuwa wakifunga siku 30 mfululizo katika kila mwaka kwa heshima ya mwezi.
Wahindu (Hinduism)
Dini ya Kihindu ni miongoni mwa dini za kishirikina katika bara la India. Katika dini hii funga, ni kitendo kilichosisitizwa sana japo si lazima, katika siku maalum kama vile kupatwa kwa jua, kumbumbuku ya kuzaliwa mwanzilishi wa dini yao na kadhalika. Funga kwao ni kujizulia na kula na kunywa kuanzia alfajiri mpaka saa tisa mchana.
Mayahudi (Judaism)
Dini ya Kiyahudi ni dini waliyoibuni Mayahudi baada ya Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) ambapo walimfanya Uzairi mwana wa Mungu. Pamoja na hivyo wachaji wa Kiyahudi walikuwa wakifunga Alhamisi na Jumatatu kama kumbukumbu ya kwenda na kurudi kwa Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) katika safari yake ya Sinai kwenda kuchukua Taurati. Kutokana na kumbukumbu ya historia, Nabii Musa alikwenda kwenye mlima Sinai siku ya Alhamisi na kurejea siku ya Jumatatu baada ya siku arobaini kupita.
Pia Mayahudi hufunga kwa saa 24 katika kila mwezi 10 Muharamu, kwa kumbukumbu ya siku Wanaisraili (Mayahudi) walipookolewa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kutokana na udhalimu wa Fir’awn. Siku hii ambayo hata Waislamu wamesuniwa kufunga huitwa siku ya ‘Ashuuraa.
Pamoja na funga hizi, pia Mayahudi wana tabia ya kufunga mara kwa mara kulingana na haja. Kwa mfano mtu anaweza kuamua kufunga siku kadhaa kama kumbukumbu ya matukio fulani katika maisha yake, au anaweza kufunga funga kama kitubio cha madhambi yake, au anaweza kufunga wakati akiwa na matatizo ili kupata huruma ya Mungu.
Ukiacha siku ya ‘Ashuuraa ambapo funga huchukua saa 24, funga za Mayahudi huanza alfajiri na huishia pale inapojitokeza nyota ya kwanza usiku.
Wakristo
Dini ya Ukristo imebuniwa baada ya Nabii ‘Iysaa (‘Alayhis Salaam). Katika dini hii Nabii ‘Iysaa (‘Alayhis Salaam) amefanywa mwana wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kwamba yeye ndiye mkombozi wa Wakristo. Pamoja na hivyo, Wakristo wanakiri kuwa kufunga ni kitendo cha uchaji - katika dini yao. Wakristo wa mwanzo walikuwa wakifunga siku 40 mfululizo kasoro siku za Jumapili kama kumbukumbu ya siku zile alizofunga Yesu (Nabii ‘Iysaa ‘Alayhis Salaam) kama inavyobainishwa katika Biblia.
Historia inatuonyesha vile vile kuwa funga hizi za Washirikina zimetofautiana sana katika mfumo na funga ya Kiislamu aliyoiamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Ambapo Waislamu wakifunga hujizuia kula, kunywa na kujamii mchana kutwa kuanzia alfajiri mpaka kuchwa kwa jua, funga za washirikina zilichukua mifumo mbalimbali. Wengine walijizuilia kula na kunywa tu lakini waliendelea kujamii, wengine walijizulia kunywa na kula kuanzia alfajiri mpaka saa 9 alasiri, wengine walijizulia kula aina fulani tu ya chakula kama vile nyama, wengine walijizulia kwa kunywa tu maji yaliyochanganywa na chumvi au maji ya ndimu, na kadhalika.
 
Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kutupa umri tukiwa katika Uislamu na Iymaan hadi kutufikisha tena kukaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhaan. Na hii ni fursa nyingine Anayotupa Allaah Ta’aala katika maisha yetu kushuhudia mwezi huu na kupata fadhila zake.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
)) ﻳَﺎ ﺃَﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﺁﻣَﻨُﻮﺍْ ﻛُﺘِﺐَ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢُ ﺍﻟﺼِّﻴَﺎﻡُ ﻛَﻤَﺎ ﻛُﺘِﺐَ ﻋَﻠَﻰ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻣِﻦ ﻗَﺒْﻠِﻜُﻢْ ﻟَﻌَﻠَّﻜُﻢْ ﺗَﺘَّﻘُﻮﻥَ (( )) ﺃَﻳَّﺎﻣًﺎ ﻣَّﻌْﺪُﻭﺩَﺍﺕٍ ...
((Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa Swawm, kama waliyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah)) (([Mfunge] siku maalumu za kuhisabika…. [Al-Baqarah: 183-184]
Hii ni neema ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)Ambaye Ametujaalia kuwa na miezi iliyo bora kuliko miezi mingine au siku bora au masaa bora kuliko mengine, ambazo thawabu zake za mema yanayotendeka humo huwa ni zaidi ya nyakati nyingine. Mfano wake ni kama kunapokuwa na mauzo yaliyopunguzwa bei dukani ( sale ), ambayo kawaida yake huwekwa kwa muda mdogo tu maalum. Na muda huu mtu huweza kununua vitu vingi kwa malipo kidogo tu. Hali kadhalika Ramadhaan, ni mwezi mmoja tu, lakini malipo yake huwa ni mengi kuliko hata malipo ya miezi yote mingine. Ikiwa mtu atatimiza Swawm yake inavyopaswa na kufanya mema mengi, na akawa katika Twa'a (utiifu) kamili na kuomba maghfira, basi hutoka katika mwezi huu akiwa ameghufuriwa madhambi yake.
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
)) ﻣﻦ ﺻﺎﻡ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﺇﻳﻤﺎﻧﺎً ﻭﺍﺣﺘﺴﺎﺑﺎً، ﻏﻔﺮ ﻟﻪ ﻣﺎ ﺗﻘﺪﻡ ﻣﻦ ﺫﻧﺒﻪ (( ﺃﺧﺮﺟﻪ ﺍﻟﺒﺨﺎﺭﻱ ﻭﻣﺴﻠﻢ
((Atakayefunga Ramadhaan kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Ramadhaan ni mwezi ambao tunatimiza Fardhi mojawapo ya Kiislamu. Ni mwezi uliojaa baraka, kheri na Rahma za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Kila Muislamu inampasa aukaribishe mwezi huu kwa furaha na matumaini kamili.
 
Namna Ya Kuukaribisha Mwezi wa Ramadhani

1- Du'aa
Anza kwa kuomba Du'aa kwamba mwezi huu ukufikie wakati umo katika hali ya siha nzuri na usalama hata uweze kufunga na kufanya ibada zako kwa hamu kubwa na wepesi.
2-Mazoezi katika mwezi wa Sha'abaan
Funga Sunnah nyingi katika mwezi wa Sha'abaan, soma Qur-aan Juzuu moja kila siku au chini yake, amka usiku uswali japo Raka'ah mbili, kisha zidisha kidogo kidogo hadi inapoingia Ramadhaan uwe tayari umeshapata mazoezi mazuri.
3- Shukurani Na Furaha
Mshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Kukupa uhai na siha hata uifikie Ramadhaan nyingine. Imaam An-Nawawy alisema, kwamba shukurani inapasa kwa kila jambo jema unalojaaliwa kubwa au dogo na vile vile shukurani inapasa kwa kila jambo baya Analokuepusha nalo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Kwa hivyo fanya 'Sajdatush-Shukr' [Sajda ya kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)] kwa neema hii tukufu.
Furahia kukufikia mwezi wa Ramadhaan kama unavyomfurahikia mgeni mpenzi anapokuja kwako na kumuandalia mazuri yote. Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum), walikuwa wakiamkiana unapoingia mwezi wa Ramadhaan na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema hivi anapowapa habari nzuri za mwezi wa Ramadhaan:
)) ﺟﺎﺀﻛﻢ ﺷﻬﺮ ﻣﺒﺎﺭﻙ ﺍﻓﺘﺮﺽ ﻋﻠﻴﻜﻢ ﺻﻴﺎﻣﻪ ﺗﻔﺘﺢ ﻓﻴﻪ ﺃﺑﻮﺍﺏ ﺍﻟﺠﻨﺔ ﻭﺗﻐﻠﻖ ﻓﻴﻪ ﺃﺑﻮﺍﺏ
ﺍﻟﺠﺤﻴﻢ ﻭﺗﻐﻞ ﻓﻴﻪ ﺍﻟﺸﻴﺎﻃﻴﻦ ﻓﻴﻪ ﻟﻴﻠﺔ ﺧﻴﺮ ﻣﻦ ﺃﻟﻒ ﺷﻬﺮ ﻣﻦ ﺣﺮﻡ ﺧﻴﺮﻫﺎ ﻓﻘﺪ ﺣﺮﻡ (( ﺭﻭﺍﻩ ﺃﺣﻤﺪ
((Umekujieni mwezi wa Ramadhaan, ni mwezi wa Baraka. Imefanywa Swawm kwenu kuwa ni Fardh, milango ya Pepo hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na mashaytaan hufungwa. Umo katika mwezi huu usiku ulio bora kuliko miezi alfu. Atakayenyimwa kheri zake
hakika kanyimwa [yote ya kheri] )) [Ahmad]
4- Jipangie wakati na weka maazimio
Ni jambo la kusikitisha kuona watu wengi wanafurahia
kuingia mwezi wa Ramadhaan
kwa kujiandaa kupanga mambo ya kidunia badala ya mambo ya Akhera. Wengi hukimbilia kwenda sokoni kununua nguo za 'Iyd, na kufurahikia vipindi vya Ramadhaan katika televisheni ambavyo sio vya dini kama ' misalsal ' (maonyesho ya sinema yanayoendelea [ series]),
na pia kuanza kukusanya video za filamu, mipira, na mambo ya kupotezea muda usiku wa Ramadhaan. Pia wengine kunua karata, dhumna, meza ya mchezo wa
keram kwa maandalizi ya vipumbazo na vipoteza muda katika mchana wa Ramadhaan ili wasiihisi Swawm au kuupeleka muda haraka kama wanavyoamini wao. Badala ya kufanya maandalizi ya kununua misahafu ya ziada, kanda za mawaidha, Qur-aan, kukusanya video za mawaidha na mafunzo mbalimbali ya Dini, vitabu vya Dini kwa lugha wanayoifahamu kwa wepesi na
kadhalika.
Huu ni mwezi wa kufanya ibada na fursa ya kujichumia mema mengi yamfaayo mtu Akhera. Kwa hiyo ndugu Waislamu, tujitahidi kuutumia wakati wetu wote bila ya kupoteza hata dakika moja, na muhimu sana kujipangia mapema wakati wako kama ifuatavyo:
Ni bora kujipan zote za mwezi mzima vipi utatumia muda wako wa mchana na usiku. Weka maazimio ya dhati kuchukua fursa kamili ya wakati wote wa mwezi huu.
Weka mpango kazi zako hata uweze kuswali kwa wakati kila kipindi, kusoma Qur-aan, kula daku na mengineyo kama tutakavyotaja hapa chini.
Kama kama unakuwa ukisoma usiku, lala mapema, kisha uamke uswali Qiyaamul-Llayl na usome masomo yako baada ya hapo.
Anza mpango wako kwa siku chache na kama unahitaji kurekebisha kuboresha nidhaam yako fanya hivyo uweze kujua nidhaam ipi itakayowafikiana na hali yako.
 
5- Tawbah na Maghfirah
Omba Tawbatun-Nasuuha kwa Mola wako na waombe msamaha wale uliowakosea. Kufanya hivi kutanufaisha zaidi Swawm na Swalah zako na pia kukupa imani kuwa huna haki ya mtu.
6- Jifunze Fiqhi ya Swawm
Jifunze elimu ya mambo yanayohusu Swawm (Fiqhi ya funga), hiyo ni muhimu ili usije kufanya jambo la kuharibu Swawm yako. Jifunze Swawm kama aliyokuwa akifunga Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndio mfano bora kabisa wa kuufuata.
Swawm haifunguliwi kwa kula na kunywa tu, bali pia ni kujiepusha na maneno mabaya na kufanya mambo mabaya kama kusengenya, kutukana, kugombana. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
)) ﻣﻦ ﻟﻢ ﻳﺪﻉ ﻗﻮﻝ ﺍﻟﺰﻭﺭ ﻭﺍﻟﻌﻤﻞ ﺑﻪ ﻭﺍﻟﺠﻬﻞ ﻓﻠﻴﺲ ﻟﻠﻪ ﺣﺎﺟﺔ ﻓﻲ ﺃﻥ ﻳﺪﻉ ﻃﻌﺎﻣﻪ ﻭﺷﺮﺍﺑﻪ (( ﺍﻟﺒﺨﺎﺭﻱ
((Yeyote asiyeacha kusema maneno mabaya? Na vitendo vibaya basi hana haja kuacha chakula chake na maji)) [Al-Bukhaariy]
7- Jitayarishe kuchuma mema mengi
Mwezi mwezi wa ukarimu, huruma, rahma na mapenzi.
Panga kiwango fulani cha kutoa Sadaka na kutoa kwa maskini, anzia kwanza kwa ndugu na jamaa. Zakah, na umependa iwe katika mwezi wa Ramadhaan fanya hima uitimize Fardhi hii pia.
Weka 'azma ya kuf kwa kualika ndugu, jamaa, jirani na marafiki kwani kumfuturisha mtu ni thawabu.
)) ﻗﺎﻝ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ : ﻣﻦ ﻓﻄﺮ ﺻﺎﺋﻤﺎً ﻛﺎﻥ ﻟﻪ ﻣﺜﻞ ﺃﺟﺮﻩ ﻏﻴﺮ ﺃﻧﻪ ﻻ ﻳﻨﻘﺺ ﻣﻦ ﺃﺟﺮ ﺍﻟﺼﺎﺋﻢ ﺷﻲﺀ (( ﺃﺧﺮﺟﻪ ﺃﺣﻤﺪ ﻭﺍﻟﻨﺴﺎﺋﻲ ﻭﺻﺤﺤﻪ ﺍﻷﻟﺒﺎﻥﻱ
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alahyi wa aalihi wa sallam) ((Atakayemfutarisha aliyefunga, atapata ujira kama ujira wake bila ya kupungua chochote katika ujira wa yule aliyefunga)) [Ahmad, An-Nasaaiy na kasahihisha Imaam Al-Albaaniy]
Kam Muislamu, mjulishe kuhusu Ramadhaan, faida na Fadhila zake. Hii ni njia na fursa mojawapo ya kufanya da'awah kwa jirani yako.
8- Hitimisha Qur-aan, Hifadhi na jifunzeTarjama
Jipangie wakati uweze kuhitimisha Qur-aan kwani Ramadhaan ndio mwezi ulioteremshwa Qur-aan na hii ni Sunnah aliyokuwa akifanya Jibriyl (‘alayhis-salaam) kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kusoma naye Qur-aan yote:
ﻋﻦ ﺍﺑﻦ ﻋﺒﺎﺱ ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻬﻤﺎ ﻗﺎﻝ : " ﻛﺎﻥ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ ﺃﺟﻮﺩ ﺍﻟﻨﺎﺱ، ﻭﻛﺎﻥ ﺃﺟﻮﺩ ﻣﺎ ﻳﻜﻮﻥ ﻓﻲ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﺣﻴﻦ ﻳﻠﻘﺎﻩ ﺟﺒﺮﻳﻞ، ﻭﻛﺎﻥ ﻳﻠﻘﺎﻩ ﻓﻲ ﻛﻞ ﻟﻴﻠﺔ ﻣﻦ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﻓﻴﺪﺍﺭﺳﻪ ﺍﻟﻘﺮﺁﻥ؛ ﺭﻭﺍﻩ ﺍﻟﺒﺨﺎﺭﻱ
Kutoka kwa Ibn 'Abbaas
(Radhiya-Allaahu ‘anhumaa)
kwamba: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) alikuwa ni mbora (mwenye matendo mema) wa watu, lakini alikuwa mbora zaidi katika Ramadhaan kwa sababu Jibriyl alikuwa akimjia kila usiku wa Ramadhaan akimfundisha Qur-aan)) [Al-Bukhaariy]
Hadiyth hii inatufundisha yafuatayo: Ramadhaan;
Kukutana kwa ajili hiyo;
Kupima hifdh yako yaan kwa kukaa na Mwalimu au mwenye elimu nzuri ya Qur-aan kwa kukusikiliza au kukufundisha;
Kuongeza juhudi za kus Qur-aan zaidi katika mwezi wa Ramadhaan:
Katika muda wa masaa 24 weka saa moja au mbili khaswa iwe ya Qur-aan kusoma na kujifunza maana ya maneno ya Mola wako uonje ladha ya Qur-aan. Vile vile jitahidi kujiwekea wakati wa kuhifadhi japo sura ndogo ili ukitoka katika Ramadhaan uwe una surah zaidi za kusoma katika Swalah zako.
9- Mdhukuru (Mkumbuke) Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Kila Mara
Usiache ulimi wako na moyo wako kuwa mtupu bila ya kumdhukuru Mola Mtukufu kila wakati kila mahali. Huku unafanya kazi zako za jikoni, fanya Adkhaar za Tasbiyh (Subhaana Allaah), Tahliyl (Laa ilaaha illa-Allaah), Tahmiyd (AlhamduliLLaah), Takbiyr (Allaahu Akbar). Kufanya hivi utajichumia thawabu maradufu, kwa kutimiza wajib wako na kuongezea kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na juu ya hivyo kuongeza baraka katika kazi zako:
10- Darsa
Hudhuria Darsa katika mwezi huu au soma vitabu vya dini, au sikiliza mawaidha. Jambo hili ni muhimu sana kwani kusikiliza mawaidha ni njia muhimu na bora kabisa katika kuzidisha imani yako. Kwa hakika unahitaji saa tu kuweza kutimiza jambo hili muhimu kila siku.



Itaendelea......
 


Tupe dalili ya maneno yko anasema sheikh Uthamyn Allah amrehemu kwenye kuacha swala bila dharura amekufuru sasa vp mtu aliekufuru akawa anamalibo ya swiam???
 
Hivi Ramadhan waislamu wanafunga au wanabadili muda wa kula? Na je mnaposema Ramadhan ni mwezi wa kutenda mema je miezi mingine ni ya kutenda mambaya? Asalam Allykum
hayo maswali yenu zipo thread humu jf hizo mada zimejibiwa naomba mzitafute
ningewajibu ila najua mnataka ligi so mtaharibu malengo ya huu uzi
bundle ni za kwenu siwapingii cha kupost ila tunawaomba wakuu kwa ihsani yenu
 
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:


Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: 183]

Allaah Anajulisha katika Aliyoyafadhilisha kwa waja Wake kwamba Amewajibisha Swawm kama Alivyowajibisha ummah zilizopita kwa sababu ni shariy’ah (hukmu) na amri zinazomnufaisha binaadamu katika kila zama.

Nayo ni changamoto ya kumhuisha mtu nafsi yake kwani inapasa kushindana na wengine katika mambo ya kheri ili mkamilishe amali zenu na mkimbilie (kuchuma) sifa njema na hakika hayo si katika mambo mazito mliyohusishwa nayo.
 
Ramadhwaan Ni Katika Neema Za Allaah Kwa Waja wake



Hakuna shaka kwamba katika neema za Allaah kwa waja Wake ni kuwafanyia ihsaan kwa kuwajaalia mwezi huu mtukufu ambao Amejaalia kuwa ni musimu wa khayraat, na wenye chumo kutokana na ‘amal njema, na Amewaneemesha humo kwa neema za wa waliotangulia, na neemah za kuendelea daima. Basi katika mwezi huu Allaah Ameteremsha Qur-aan ambayo ni Mwongozo kwa Watu na hoja za uongofu na pambanuo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…