mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Namaanisha nahusika[emoji30]Pentagon ndio kitu gani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Namaanisha nahusika[emoji30]Pentagon ndio kitu gani?
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji85] [emoji85] [emoji85]Umepiga pentagon[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Wale wenye VIMADA na MABUZI.Pia kwa wale mnaopenda mambo ya kubet aisee mnabidi muache hii kitu maana asilimia kubwa funga zenu zitaharibika kwa ajili ya kubet ,kubet ni haramu
Jazakallah kheirUzuri Wa Kutekeleza ´Ibaadah Ya Kufunga Mwezi Wa Ramadhaan
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:
“Yeyote atakayefunga mwezi wa Ramadhaan kwa Imani na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah basi Allaah Atamsamehe madhambi yake yote yaliyopita.” [Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim, An-Nasaaiy na Ibn Maajah].
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema tena, alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:
“Allaah amesema: “Kila ‘Amali ya mwanaadam ni yake yeye mja Wangu ila Swawm. Ni yangu Mimi na mimi ndiye Nitakayemlipa mja Wangu.”
Swawm ni kinga.
Itakapofikia siku mmoja wenu amefunga ajiepushe na kufanya kitendo cha jimai na mabishano na watu. Na yeyote atakayetaka kupigana naye basi amwambie “Mimi nimefunga.” Naapa kwa jina la Allaah, Harufu inayotoka katika mdomo wa mwenye kufunga ni nzuri kwa Allaah kuliko harufu ya Misk. Kwa Mwenye kufunga ana furaha mbili: Furaha anapofungua Swawm yake na furaha pale atakapoonana na Mola Ameridhika kwa kufunga kwake.”
[Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim na An-Nasaaiy]
Sahl ibn S’ad (Radhiya Allaahu ´anhu) alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:
‘’Peponi kuna mlango unaitwa Ar-Rayyaan. Wale wenye kufunga wataingia peponi kupitia lango huu siku ya Qiyaamah na hakuna mwengine atakayepita katika mlango huu ila (wafungaji).
Itaambiwa: ‘’Wako wapi waliokuwa wakifunga?” Watasimama na watapita katika mlango huu na watakapomalizika kuingia wote (wafungaji) utafungwa na hakuna mwengine atakayepita hapo tena.“
[Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim, At-At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na An-Nasaaiy].
Probably Mei 27Hiv ramadhan inaanza lini, msaada jaman
ShukranJazakallah kheir
Lakini ligi zimeisha,labda hizo fainali za UEFA na EUROPAPia kwa wale mnaopenda mambo ya kubet aisee mnabidi muache hii kitu maana asilimia kubwa funga zenu zitaharibika kwa ajili ya kubet ,kubet ni haramu
JazzakAllahu kheirInaswihi,ila inashauriwa unywe walau maji usiku huo as daku
Amemaanisha hio stara ya fashion show sio hijab ya kisheria..wanawapotosha watu.Stara ya mwanamke isiwe kwa ajili ya Ramadan tu wanawake tunatakiwa tujistir muda wote jaman ima Kwa wale tuliohalalishiwa nao tu asalam alykum
Ni kweli mkuu hapo ndipo kuna kuwaga na mtafaruku hapoMwezi Wa Ramadhaan Unathibitishwaje Kuonekana Kwake?
Mwezi wa Ramadhaan unathibitishwa kuonekana kwake na mtu mmoja mwenye kujulikana kwa ukweli na kumcha kwake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) au kwa kutimiza siku thelathini za mwezi wa Sha’abaan.
Ibn ´Umar amesema watu walikuwa wakitafuta kuandama kwa mwezi. nikamjulisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) kuwa mimi nimeuona mwezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akafunga na akaamrisha watu wafunge.
” [Hadiyth Swahiyh. Angalia Kitaab I’rwa al-Ghaliyl na. 908 na Imeripotiwa na Abu Daawuwd].
Ikiwa mwezi haukuandama, kwa sababu ya kufunikwa na mawingu au kwa sababu nyingine basi hapo mwezi wa Sha’abaan utatimizwa kwa siku thelathini kama alivyoripoti Abu Hurayrah katika Hadiyth iliyo hapo juu.
Lakini mwezi wa Shawwaal unatangazwa kuonekana kwa mashahidi wawili.’ ´Abdur-Rahmaan bin Zayd bin Al-Khattwaab amesema:
“Nilipokuwa nikikhutubia siku ambayo ni ya shaka (kama mwezi wa Ramadhaan kama umekwisha ama la), nikasema: “Nilikaa na Maswahaba zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) nikawauliza wao. Wakaniambia mimi kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alisema:
‘’Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi na tekelezeni ´Ibaadah ya Hajj kwa haki zake. Ikiwa kuna mawingu basi timizeni siku thelathini. Na Ikiwa Waislamu wawili watachukua kiapo kwa kuonekana kwa mwezi basi fungeni na mfungue kwa kushuhudia kwao mwezi.’’
[Hadiyth Swahiyh. Angalia Kitaab cha Shaykh Al-Albaaniy, Swahiyh al-Jamiy’ Asw-Swaghiyr na. 3811. Pia Imeripotiwa na Imaam Ahmad na An-Nasaaiy bila kipande kinachosema ‘’Waislamu wawili.’’].
Mtawala wa Makkah, Al-Haarith bin Hatwiyb amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alituambia sisi tekelezeni ´Ibaadah ya Hajj kwa haki zake munapouona mwezi. Na ikiwa hamkuuona mwezi lakini mashahidi wawili wa kuaminika wakishuhudia kwa kuona mwezi tunatekeleza ´Ibaadah ya Hajj kutokana na ushahidi wao.’’
[Hadiyth Swahiyh angalia Shaykh Al-Albaaniy, Swahiyh Sunan Abiy-Daawuwd, na. 205. Imeripotiwa na Abu Daawuwd].
Tukiangalia ripoti mbili hizi,
’’Ikiwa waislamu wawili watachukua kiapo kwa kuona mwezi, basi fungeni na fungueni’’ katika Hadiyth ya Abdur-Rahmaan bin Zayd na:
‘’Na ikiwa hamkuuona mwezi lakini watu wawili wenye kujulikana kwa ukweli wakasema wameuona mwezi tunatimiza haki za ´Ibaadah ya Hajj kutokana na ushahidi wao.’’ katika Hadiyth ya Al-Haarith wanaonyesha kwa kutilia mkazo, kuwa haifai kuanza kufunga au kumaliza kufunga kutokamana na ushahidi wa mtu mmoja pekee. Juu ya hilo, tangu kuanza kwa kufunga imeondolewa uzito kutokana na ushahidi (uliotolewa hapo juu), inawacha suala la kumaliza kufunga, ambalo halina ushahidi kwamba linatoshelezwa kwa ushahidi wa mtu mmoja pekee.
Huu ni ufupi wa mjadala unaopatikana katika Kitabu ‘Tuhfah Al-Ahwadhiy’ [Mjalada wa 3, uk. 373-3749].
Tanbihi: Ikiwa mtu atauona mwezi yeye peke yake, hafungi mpaka watu wafunge na hamalizi kufunga mpaka watu wamalize kufunga kama ilivyoripotiwa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu), kwamba amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam):
‘’Swawm (kufunga) ni siku ambayo watu wanafunga. Na kumaliza kufunga ni siku ambayo watu wanamaliza kufunga. Na kuchinja ni katika siku ambayo watu wanachinja.’’
[Hadiyth Swahiyh. Angalia Swahiyh Al-Jami’ Asw-Swaghiyr, na. 3869].
Imehifadhiwa na Imaam At-At-Tirmidhiy ambaye amesema:
‘’Baadhi ya Maulamaa wanaifasiri Hadiyth hii kwa maana:
“Kuanza kufunga na kumaliza kufunga kunatekelezwa na watu wote kwa pamoja na wakati mmoja.”
Na hapo ndio taraweh zinapo kimbiwa hapoLakini ligi zimeisha,labda hizo fainali za UEFA na EUROPA
Taraweh imekua mtihani sana hasa kwa vijana.Na hapo ndio taraweh zinapo kimbiwa hapo
ni kweli kabisa na ndomana tunasisitizwa tusome ili kuijua dini yetu ,maana ukisoma hutoburuzwa wala hutofauta mkumbo,Ni kweli mkuu hapo ndipo kuna kuwaga na mtafaruku hapo
ila kikubwa hitirafu zipo zilikuwepo na zitakuwepo
Na ktk hitirafu kuna zinazo kubalika na zisizo kubalika.mf:Hitirafu isio kubalika kuna watu wana dai Mitume inaendelea ,Baada ya Muhammadi swalla allah alayhi wasallam alikuja Mwingine (Mirriza Ghuram Ahmedy) n.k. hizi hazikubaliki
Hitirafu ya Mwezi ni hitirafu inayo kubalika kikubwa yapaswa kufunga kutokana na ulivyo amina sio kwa kumuhufia mtu fulani au nyumbani wao wanaanzaga basi na mm nitaanza kwa kuhufia nyumbani.au sianzi kwa kuhufia nyumbani au mtu fulani .Siai Tunafunga kwa ajili ya Allah .
Wanafunga...Hivi Ramadhan waislamu wanafunga au wanabadili muda wa kula? Na je mnaposema Ramadhan ni mwezi wa kutenda mema je miezi mingine ni ya kutenda mambaya? Asalam Allykum