Ramadhan Special Thread

Hata ulicho pinga sielewi naona umekubali comment yangu kwenye mwenzi Mtukufu tunakumbushwa kutoa Swadaka hapo Umeandika kwenye comment yako nilijua neno Karim ni lugha chafu kama ni hivyo acha nilitumie RAMADHAN KAREEM

Huoni kwamba tamko Karimu limeabatana na tamko Ramadhan ?

Hivi kusema "Kitabu Changu" ni sawa nakusema "Kitabu" au "Changu" ?

Unatakiwa ujue kabisa kwanza hakuna Kiswahili cha "Ramadhan Kareem" sababu tamko hili limechukuliwa moja kwa moja kwa kiarabu ila kwa maandishi ya Kiswahili.
 

Umeshawahi kusoma sherehe yoyote ya hiyo hadithi ?

Pili,naomba uniambie asili ya ile ishara ya mikono miwili na maana yake. Kisha rejea katika ile hadithi utaelewa inaelezea nini.
 
Rejea hadithi ya mtume amani ya Allah iwe juu yake isemayo "Mwenye kujifananiza na kaumu fulani,basi na yeye ni miongoni mwao"
Kwa tafsiri yako hiyo unavoipeleka huoni hizi simu tunazotumia tunajifananisha na wengine wasiokuwa sisi?

Mbona waileta hadithi katika ujumla ambao hata wewe unakukamata?

Katazo la kutumia emoji kama linaingia katika hadithi hyo kwa nini kutumia kwako simu ambayo imoji ndo zimo humo isiwe katazo la kujifananisha na wasiokuwa sisi?
 
Ramadhani kareem imekatazwa katika Quran, tuanzie hapo au ni kauli mbaya
 
Umeshawahi kusoma sherehe yoyote ya hiyo hadithi ?

Pili,naomba uniambie asili ya ile ishara ya mikono miwili na maana yake. Kisha rejea katika ile hadithi utaelewa inaelezea nini.
Kwani ile hadithi Ya
"hakika matemdo hulipwa kwa nia" ina maana ipi?

Kwani yeye aliitumia hiyo ishara kwa kufuatisha maana yao au alitumia hyo ishara kwa maana aliyokusudia yeye?

Au ndo wale ambao wanakataza kuweka alama za mwezi msikitini ati kwa sababu makafiri wamesema hyo ni alama ya shetani?

Dini hii yaenda hivyo?
 
Mkuu maana ya karerm ni nini mbona wahangaika sana?

Ebu tuliza akili sio kila fatwaa wataka kuitawanya na kuitumia pasi na adillah.

Maana YA KARIM ni ipi katika lugha ya kiswahili?
 

Hapa hujaelewa mambo,usichanganye kati ya mambo ya kiada na mambo ya kiibada. Fatilia asili ya ile ishara kisha uniambie ipo katila ada au ibada.

Suala la simu haliingii katika mambo ya kiibada,hii inategemeana na matumizi yako mwenyewe,ukiitumia kwa njia nzuri utapata faida ukiitumia kwa njia mbaya unapata madhambi,kwa maana hiyo hakuna ibada ambayo kusihi kwake sharti uwe na simu. H
 
.kwani emoji ambayo kaitumia yeye amesema ni ibada au ametumia kama ada ya kuwakilisha jambo fulani?
 
Kwani yeye aliitumia hiyo ishara kwa kufuatisha maana yao au alitumia hyo ishara kwa maana aliyokusudia yeye?

Kusihi matendo baada ya nia,kuna nguzo za kusihi matendo au ibada. Nguzo hizo wapo wanazuoni wanasema ni tatu,wengine wanasema mbili na wengine wanasema nne,almuhimu zote zinarudi kwenye asili.

Ndio maana hadithi ikawa wazi mno,imezungumzia kujifanananiza kama watu fulani,basi na wewe unakuwa miongoni mwao. Iwe nia yako ni kinyume nao au kama wao,humo unahesabika umejifananiza nao.
 
Ramadhani kareem imekatazwa katika Quran, tuanzie hapo au ni kauli mbaya

Ramadhani Kareem haijathibiti,na kama wewe unasema hivyo kwa kutegemea ujira,lazima nitakuuliza tamko hili "Ramadhani Kareem" unelipata wapi ? Je umelipata kwenye Qur'aan au Hadithi au kwa maswahaba wa mtume ?

Nikisema tamko hilo halina asili namaanisha hulikuti kwenye Qur'aan,wala Hadithi walaathari za maswahaba. Je hilo litakuwa lina jema ?

Lakini je ni lipi bora kufanya lile lenye asili au kufanya lile ambalo halina asili ?
 
Mkuu KAREEM maana yake nini?
 
Ok umeshinda huwa sipendi kubishana na muislamu mwenzangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…