Naomba kuuliza kufunga swaumu bila kuswali ni sawa na kushinda na njaa?
Naam ndugu
Kizinga mpemba sala ni katika nguzo za kusihi amali zote,ni funguo ya kusihi amali zote.baada ya shahada ni sala kisha saumu zinakuja mbele.
Mtu akifunga hali ya kuwa hasali basi saumu yake haimfai chochote kwa sababu ameacha ufunguo wa ibada(sala)wapo wanaosema inasihi saumu lakini kauli ya sawa ni kwamba saumu yake haisihi mpaka atakapoanza kusali.
Anasema Mtume wa Allah salama na sala ziwe juu yakee.
أول ما يحاسب عليه العبد يوم القيامة الصلاة،فلإن صلحة صلحة سائر عمله.وإن فسدت فسدت سائر عمله
"jambo la mwanzo ambalo atahesabiwa mja siku ya kiama ni SALA ikiwa sala itatengenea basi yatatengenea matendo mengine yaliyobakia,na ikiwa sala ikawa imefisidika(imeharibika)basi yataharibika matendo yaliyobakia"
Mtume kasema ikifisidika au kuharibika sala basi yanaharibika na matendo mengi,je ikiwa mtu jakusali kabisa tutasema kaiharibu sala ama hakusali kabisa?
Ikiwa yule ambaye alisali lakini akaiharibu yanafisidika matendo yaliyobaki,vipi kwa yule ambae hakusali kabisa je matendo Mengine yatahesabiwa kweli?
Hivyo kwa mtu ambae hasali basi tunahofia saumu yake kutokubaliwa na kutoandikiwa thawabu.
والعلم عند الله