Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Wazee wakubadili ratiba ya menu
Ndio. Hata ratiba ya matendo inabadilika. Walevi wanapungua, uzinzi unapungua. Sioni tatizo ndivyo ilivyosemwa. Tule usiku tusile mchana. We unakwazika na nini?
 
Ndugu zangu iko hivi

Kilugha kusema Ramadhan Kareem haileti maana sahihi.
Neno Ramadhan Mubaarakah.....yaani Ramadhan yenye barka....inaendana na neno Ramadhan Mukarramah....yaani ramadhan yenye upole/unyenyekevu na mfanowe

Kwahiyo ni kheri Kusema Ramadhan Mukaramah na sio Ramadhan Kareem.

Kama una hoja njoo.
 
Huyo jamaa hayupo hapa kwa ajili ya kujifunza mkuu bali kufanya mzaha na kuharibu maudhui ya mjadala.
Huu ni uzi maalum kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani lakini yeye analeta habari za kitimoto tena akijinisabu kwamba yeye ni Muislam na bado anajiuliza ima afunge au la maana atamisi hicho kitimoto chake!!.
Allah amwongoze
 
Hakuna haja juu ya hili

Kuna vitu vingi vya msingi na vyenye faida kwa wote
Ni bora tuchague yenye faida,na si mijadala mfano wa hii

Shukran ndg
Ndugu zangu iko hivi

Kilugha kusema Ramadhan Kareem haileti maana sahihi.
Neno Ramadhan Mubaarakah.....yaani Ramadhan yenye barka....inaendana na neno Ramadhan Mukarramah....yaani ramadhan yenye upole/unyenyekevu na mfanowe

Kwahiyo ni kheri Kusema Ramadhan Mukaramah na sio Ramadhan Kareem.

Kama una hoja njoo.
 
Kufuatia hiyo fatawa ya sheikh uthaymiiin rahima hu allah

Je kusema ramadan mubarak ndo kusema ramadan inaleta baraka??
Ikiwa kusema ramadhan kareem kuwa ramadhan ndio inayoleta ukareem

Hiyo fatwa imezungumzia kutofaa kusema "Ramadhan Kareem". Iko wazi isome utaelewa.
 
Maelezo mazuri sana mkuu ila labda namimi nitie neno kwanza..

Bwana Zurri hakutoa maana ya neno karimu كريم bali alitia hili na lile hakutoa maana.
Ila ndugu umefafanua vizuri lakini niseme kwamba kukataza jambo ambayo ni mubaha tu wala haliingii katika ibada basi inakuwa haifai kwa sababu ni kuharamisha aliyohalalisha Allah.

Neno karimu كريم ni kweli ni waznu wa فعيل kwa maana inakuwa kama ni kitenda hivi.

Lakini wakati huo huo neno hilo linaweza likawa na maana ya مفعول به (mtendwa).

Hasa pale ambapo neno hilo limetanguliwa na jina ambalo kiuhalisia HALITENDI BALI HUTENDWA.

Hivyo neno hili kulichambua peke yake kwa maana hiyo alafu ukasema haifai sio sawa sawa kwa sababu inakuja katika hali nyingi lakini kwa muktadha ule ule wa صيغة المبالغة ila inaweza kuja katika maana ya kuwa ni kilichoTENDWA.

Mfano wa maana ambazo zinaonyeshwa kwamba neno kariym كريم linaweza kuwa na maana ya مفعول (mtendwa,mfanyiwa)angalia aya za Allah...

قالت يا أيها الملأ إني ألقي إلي كتاب كريم

[ AN-NAML - 29 ]
(Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu.

Ukiangalia mwisho wa aya hapo neno KARIYM limetanguliwa na neno KITABU(jina)kwa maana ya hapo utafasiri kwamba kitabu ni MTENDA (فاعل)?

Hapo kitabu kinageuka kinakuwa ni mtendwa na kariym inageuka inakuwa ni mtendwa kwa maana ya hicho kitabu KIMEFANYWA KUWA KITUKUFU kwa msingi ule ule wa صيغة المبالغة (yaani kama kukitukuza kitu na kukipa ukubwa zaidi)

Aya nyingine...

أولم يروا إلى الأرض كم أنبتنا فيها من كل زوج كريم

[ ASH-SHUA'RAA - 7 ]
Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri?

Umeona neno kariym lina maana ipi hapo?
Wamefasiri maana ya uzuri yaani imefanywa kuwa nzurii.

وزروع ومقام كريم

[ ADDUKHAN - 26 ]
Na mimea na mahali pazuri

Hapo kariym inamfasiri huyo maqaam(mahali)kwa maana ya hapo neno KARIYM ni mtendwa ambaye anamuwakilisha SEHEMU kwa hvyo tafsiri ya neno kariym hapo ni kwamba SEHEMU ILIYOFANYWA KUWA NZURI na sehemu wala haiwezi kujifanya kuwa nzuri bali hufanywa.

Na aya nyingi zinaomyesha kwamba kariym anaweza akawa mtendwa..

إنه لقرآن كريم

[ AL -WAAQIA'H - 77 ]
Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu,

Hapo neno kariym limetanguliwa na neno QURANI kwa maana tafsiri yake ni "QURANI ILIYOFANYWA TUKUFU"

Kwa maana hiyo tunaweza kufupisha kwa kusema hivi.

"KARIYM IKITANGULIWA NA KITU AMBACHO HAKINA SIFA YA KUTENDA BASI NENO KARIYM LINAGEUKA LINAKUWA NI MTENDWA NA SIO MTENDA TENA".... Ndo mana hata aya zimetumia neno kariym kwa namna hiyo.


Hivyo mtu akisema "RAMADHAN KARIYM" maana yake ni ramadhani(mwezi)uliofanywa kuwa mtukufu" na wala haina maana ya kuwa eti huo mwezi ndo umetenda na kuwa mtenda.ukitafsiri hvyo maana yake mpaka aya tulizotoa zitatafsiriwa kwa makosa pia.

Na kiarabu ujanja wake wooooteee basi ikiwa kinaenda kinyume na Qurani twatakiwa tuifate Qurani imeweka msingi gani kwa sababu ndo marejeo.

Na hiyo Qurani ndo imetuonyesha kwamba neno KARIYM likitanguliwa na jina ambalo halitendi basi hilo jina hugeuka kuwa MTENDWAA..

Ramadhani kariym maana yake ni ramadhani iliyofanywa kuwa tukufu.

Zurri maana ya kariym usikariri kwa namna moja tu,huwa inakuwa na maana mbalimbali kwa mujibu wa kilichotangulia.





Neno Kareem كريم
limekuja katika uzani wa فعيل ambayo ina maana ya صيغة المبالغة na inaweza ikawa na maana ya صفة مشبهة

ama neno مبارك MUBAARAK
Limekuja katika uzani wa اسم المفعول

kwamaana ya Mtendwa( Iliyobarikiwa)

Kwamaana imefanyiwa kitendo cha Baraka

Allah anajua zaidi
 
Nikuonyeshe namna ya kuswali swala tano hakika imenishangaza comment yako nimekuuliza swali lengine unajibu tofauti mbaya zaidi unataka kuingiza topic nyingine. Mkuu wew Kusimamisha swala hujui.

Swali langu lilikuwa na maana sana,wala sikutaka nikutoe kwenye mada,bali nilitaka ufikirie kiundani ya kuwa,sio kwamba ukiona jambo halipo katika Qur'aan ukajua halijaelezewa katika msingi mwingine wa Uislamu.

Huwezi kukuta katazo la Ramadhan Kareem katika Qur'aan ila katika hadithi utakuta sababu imethibiti matumizi ya tamko Ramadhan Mubaraak na si Ramadhan Kareem. Ndio kama ilivyo huwezi kuta maelekezo ya namna ya kusali katika Qur'aan ila unakuta maelekezo katika hadithi.

Naomba uniambie Ramadhani Kareem wewe umeipata wapi ?
 
Back
Top Bottom