Ramadhan Special Thread

Assalam aleykm warahmatullah wabatakatul! Naomba kujuzwa juu ya ulaj/ kutokula daku.Je nikiacha kula daku funga yangu itaswih?



Assalam aleykum waav rahmatullah wa barakatuhu.

Ni bora tusikilize qauli ya mtukufu mtume (saw), kasema nini juu ya kula daku. Anasemw hivi:-

"A'n Anas radhi Allahu anhu qaala, qaala rasulullahi swallallahi alaihi wa salam tasahharuu fainna fii ssuhuuri barakat"

Yaani: Imesimuliwa na Anas ra, ya kwamba mjumbe wa Allah saw, alisema : kuleni daku, maana kuna baraka katika kula daku"

Kutoka katika Bukhari.
 
Sie ni j4 sio

Taarifa kwa waislam. (Ofisi ya mufti wa tanzania) kamati ya kitaifa ya masuala ya mwezi inawajulisha waislamu wote kuwa Leo tarehe 5/5/19 kuonekana kwa mwezi hakujathibiti mbele ya mh mufti wa tanzania shk abubakar zuber mbwana.wala mbele ya kadhi mkuu tanzania bara shk abdallah mnyasi.wala hakujathibiti mbele ya mufti wa zanzibar shk swaleh kaab.wala mbele ya kadhi wa znz shk haji khamis. Wala hata jirani zetu kwa kauli ya kadhi wa kenya.hivyo mnatangaziwa rasmi kuwa huu ni usiku wa wa mwezi 30 shaaban. Kesh tunatimiza shaaban 30.hivyo basi ramadhan tutaanza rasmi siku ya jumanne 7/5/2019.ofisi ya mufti ya wa tanzania na mufti wa zanzibar.inawatakia waislam wote ramadhan mubaarak. (Shk alhad mussa salum)katibu wa kamati ya kitaifa ya mwezi muandamo na shk wa mkoa wa dsm)والسلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Baada ya hii taarifa, hakuna taarifa yoyote iliyotufikia kama mwezi ushaonekana.

Hivyo mimi na wengine tutafunga j4 insha Allah, na kuna baadhi ya wengine wanafunga kesho.
 
Shukran
 
Kilichokuwa bora Mama Debora
Ni kutoharibu uzi,na vitu hususan Picha za ajabu ajabu katika uzi huu

Tunakuomba na kukusihi sana
Nataraji utakuwa muelewa Ndg
Nachoshangaa mbona wanawake hatukeugaki kuwatazama wanaume kwa tamaa!!
 
Muhimu ni usahihi wa Hadithi

Ikiwa Hadithi ni sahihi,Basi itakuwa Dua bora sana

Na kama si sahihi
Lililokuwa zuri,ni kuachana nayo,na kutafuta sahihi na kushikamana nayo
Hata hii nayo pia inatumika
اللهم اني لكسمت، وبك امنت، وعلا رزكك افطرت، وعليك توكلت.
 
Kwann unasema nzuri sana Chief?!!!
 
Muhimu ni usahihi wa Hadithi

Ikiwa Hadithi ni sahihi,Basi itakuwa Dua bora sana

Na kama si sahihi
Lililokuwa zuri,ni kuachana nayo,na kutafuta sahihi na kushikamana nayo

We Kaka kama mtu nina tatizo LA kiafya (mfano matatizo ya tumbo) yanayonilazimu kutopitisha Massa kadhaa bila kula, je mwezi wa ramadhani natakiwa nifanyeje.

Kuna mtu kaniambia eti lazima kufunga hivohivo sababu swaumu ni nguzo ya dini.

Natakiwa nifanyeje! Nisaidie.
 
Wew sio muislamu kwenye ule uzi Jana si uliandika hivi nanukuu maandishi yako "Waislamu mna kazi kweli" Aburr Dharr usimjibu huyu kiumbe asikuchoshe na funga yako.
 
Kwa wenye matatizo ya kiafya au walio safarini wameruhusiwa kula ila matatizo yao yatakapoondoka wanatakiwa walipe funga zao. Je wewe ulieuliza hili swali utafunga?!
 
Ikiwa mtu ana tatizo la kiafya,na Madaktari wamethibitisha kuwa hawezi kufunga

Basi
Sheria itamtaka atoe Kibaba,
Yaani Kilo Moja na Nusu ya Chakula(Kipendwacho hapo mji anamoishi)
Kwa kumpa Maskini kila siku ndani ya Mwezi wa Ramadhan

Allah akufanyie wepesi popote ulipo,na akuondolee kila aina ya tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…