Dua nzuri sana[emoji261] ﷽[emoji261]
الحمد لله والصلاة والسلام على رسول الله وعلى آله وصحبه أجمعين ..
[emoji871]Ewe Mola wangu mimi hakika ni mja wako dhaaifu na wewe ni Mola wangu Latwifu.
Sina wa kumlilia zaidi yako Ya Hannan Ya Mannan.
Wewe ndio tegemeo la huzuni zangu na unyonge wangu.
Hakika ulimwengu waweza kunitupa lakini wewe daima utanienua na kunirehemu.
Mola wangu umenihifadhi tangu katika tumbo la mama yangu mzazi hadi leo kufikia kua hali nilio.
Nakuomba kwenye shari uniepushe na kwenye mazuri uniongoze.
Nikikosa unisamehe na nikipata nitosheke na kuridhika.
Mapenzi yako hakika ni makubwa kwetu Ya Rabb. Adhabu zako ni kubwa na msamaha wako ni mkubwa zaidi.
Ya Rabb twalia kwa dhambi zetu na tuko chini ya twaa yako ya Rahmaan.
Ya Rabb usipotusamehe na kutughufuria hakika tutakua katika hasara.
Itakuaje siku ya siku tutakapo simama mbele yako ya Rabb na huku tukingoja majibu yetu na kupewa vitabu vyetu.
Hakika hio itakua siku nzito kwetu.
Ya Rabb tujaaliye kufaulu duniani na akherah.
Ya Rabb tujaaliye nyoyo zenye kutubu kwa dhambi zetu, nuru katika majumba yetu, huruma kwa wenzetu , ihsaani kwa jirani na waisilamu wenzetu.
Ya Rabb tujaaliye mwisho mwema sisi na familia zetu.
Ya Rabb tusamehe dhambi zetu za siri na dhahiri.
Ya Rabb tujaaliye wema na huruma bayna yetu.
Ya Rabb tujaaliye kauli njema kwa wenzetu na maneno mazuri bayna yetu.
Kila mkosa Ya Rabb muongoze na kila mwenye matatizo mpe wepesi.
Ya Rabb tujaaliye kua mbali na fitnah na ubaya.
Ya Rabb Ya Rabb Ya Rabb tujaaliye vizazi vyema .
Ya Rabb kwako ndio tegemeo la kila mnyonge na mwenye tatizo.
Ya Rabb tupe muongozo wa dini na tujaaliye kua mbali na jahhanam.
Ya Rabb Ya Rabb Ya Rabb tujaaliye kila la kheri na tawfiq.
سبحان ربك رب العزة عما يصفون، وسلام على المرسلين، والحمد لله رب العالمين.
آمين.. آمين.. آمين