Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

"Fungeni kwa kuuona mwezi na mfungue kwa kuuona pia", ukifuatilia hadithi mbali mbali za mtume utagundua kwamba katika hayo mafundisho yake kuna kitu kuuona, mtume ametuachia Sunna ambapo ni kufunga kwa kusikia ikiwa mwezi umeonekana kokote kule ulimwenguni. Lakini swala linalokuja ni kwamba sisi na Saudia tupo katika longitude moja (Zone C) kwa hiyo kuna ufanano wa masaa na kitu kama hicho, lakini linapokuja swala la mwezi Saudia wanakuwa wa kwanza kuuona, kwa vile wanatumia vifaa vya kutizamia mwezi kitu ambacho mimi sikubaliani nacho moja kwa moja kwani kwa siku ya jana mwezi ulikuwa ndio umekuwa kwa 0.2% ambapo sio wa kuonekana
View attachment 1428992
na siku ya leo utakuwa umekuwa kwa 3.5% ambapo ni wenye kuonekana.
View attachment 1428994
Kumbuka pia hata mwaka jana Saudia hao hao waliomba radhi kwa kuwalisha watu mchana wa Ramadhan na wakalipa fidia.

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
Acha Uongo wewe....

Ukiambiwa lete ushahidi wa Saudia kuomba Radhi....ninahakika hutoleta

Hizo zilikuwa ni habari za Mitandao tu,na si uhalisi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
careem amekujibu kisayansi zaid inabidi ukubali yupo sahih

mwakani usifate wa saudia
Sheria ya Dini
Haijengeki Kisayansi...Bali inajengwa kwa Hoja ndani ya Kitabu cha Allah na Sunna Sahihi za Bwana Mtume Sala na Salamu ziwe juu yake kwa ufahamu wa Wema waliotangulia

Hii ndio Dini
Na si kinyume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu hana haja na kundi la WAISLAMU kwani waweza kuwa muislamu kisha ukawa mlevi, mchawi, mzinifu, mwizi nk

Haya maneno yako ndugu yangu

Ni Mabaya sana

Fahamu tu
Huwezi kuwa Mcha Mungu,mpaka Uwe Muislam

Huwezi kuuwa Mu-umin,mpaka uwe Muislam

Uislam ndio nguzo Mama katika zote
Ukipanda juu zaidi,ni utakutana na Daraja la

IMAAN na IHSAAN

Ukishuka Chini ya Uislam,utakutana na Daraja la

UNAFIKI
UKAFIRI

TANBIH

Tusiseme kama hatujui,Ukimya wako huwezi jutia,Bali neno lako laweza kukutia hatiani

بارك الله فيكم

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sifa njema zote Anastahiki Allaah Mola wa viumbe vyote na Swalah na salamu zimfikie Mtume wetu na kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na aali zake na sahaba zake wote.



Ama kwa hakika katika mwezi wa Ramadhwaan kuna fadhila nyingi ambazo mimi nitazitaja kwa uchache namuomba Allaah Aniwafiqishe 'asaa yawe na manufaa katika Duniya na Akhera.



1) NI MWEZI WA QUR-AAN

Kama Alivyosema Allaah Mtukufu:

"Mwezi wa Ramadhwaan ni mwezi ambao imeteremshwa Qur-aan ili iwe uongozi kwa watu na hoja na upambanuzi (Baina ya haki na batil)” [Qur-aan 2:185]



Vilevile kama ilivyopokewa na Ibn 'Abbaas (radhiya Allaahu 'anhu) kuwa makusudiyo yake kwa hakika kuteremshiwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Qur-aan mwanzo ni katika mwezi wa Ramadhwaan na vilevile Qur-aan mwanzo wa kuteremka ni usiku wa Laylatul-Qadir na Laylatul-Qadir iko katika mwezi wa Ramadhwaan.



Hivyo basi ni juu yetu kufanya juhudi katika mwezi huu kukithirisha sana kusoma Qur-aan. Walikua Salafus-Swaalih (Wema Waliotangulia) wakikilinda kitabu cha Allaah kwa kukisoma na kuyafanyia kazi yaliyokuwemo kwa mazingatiyo. Pia Tunaambiwa kuwa Sayyidnaa Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) akimfundisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Qur-aan katika mwezi wa Ramadhwaan, na alikuwa 'Uthmaan bin 'Afaan (Radhiya Allaahu 'anhu) kila siku akisoma Qur-aan yote yaani anakhitimisha mara moja kwa siku, kwa maana, msahafu mzima anausoma kwa siku moja. Na walikuwa baadhi yao katika wema wakisoma Qur-aan yote kwa siku tatu, wengine kwa wiki moja na wengine kwa siku kumi. Walikuwa wakisoma Qur-aan ndani ya Swalah na nje ya Swalah.



Allaah Atuwafiqishe mimi na wewe tuisome Qur-aan na kwa mazingatio khasa katika mwezi huu tufanye juhudi sana ili tuweze kupata fadhila za mwezi huu mtukufu.



2) NI MWEZI WA SUBIRA

Subira ni katika jambo gumu na halipati ila kwa mtu mchaji Allaah na mnyenyekevu kwa Allaah. Na katika kufunga kunatakiwa subira pale mtu anapojizuilia kutokana na kutokula, kunywa, matamanio na mengineyo. Imekua Swawm ni nusu ya subira na subira malipo yake ni pepo kama alivyosema Allaah Mtukufu:

"Kwa hakika (Allaah) Atawapa wenye kusubiri malipo bila ya hisabu" [Qur-aan 39:10]



3) MILANGO YA MOTO INAFUNGWA, MILANGO YA PEPO INAFUNGULIWA NA MASHETANI WANAFUNGWA

Kama ilivyokuja katika Hadiyth iliyopokelewa na Maimamu wawili:

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema, "Pindi inapokuja Ramadhwaan inafunguliwa milango ya pepo, na hufungwa milango ya moto, na mashetani wanafungwa kwa Minyororo." [mesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]



Kwa hakika utaona katika mwezi huu watu wengi wanajitahidi kujiepusha na maasi, watu wanajaa misikitini kwa kufanya ibada ya mwezi huu hii ni kwa sababu mashetani wamefungwa na shetani juu ya uasi wake lakini anauogopa mwezi wa Ramadhwaan na vitimbi vyake vinakuwa dhaifu ndio mana wengi nyoyo zinabadilika wanaswali na kujitahidi kufanya kheri. Lakini ikimalizika Ramadhwaan tu basi Swalah imekwisha kama vile Allaah yupo Ramadhwaan tu. Huu ni msiba ndugu zangu Waislamu Allaah Asitujaalie katika hao.



4) LAYLATUL QADR

Katika mwezi huu kuna siku ya Laylatul-Qadr siku ambayo ni bora kuliko miezi elfu kama Alivyosema Allaah:

"Huo ni usiku wa hishima ni bora kuliko miezi elfu.

Huteremka Malaika na roho (za viumbe watakatifu) katika (usiku) huo

kwa idhini ya Mola kwa kila jambo.

Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri"

[Qur-aan 97:3-5]



Imehisabiwa mtu atakapofanya ibada katika usiku huo mmoja ni kama amefanya ibada sawa na miaka 83 na hii ni katika fadhila kubwa kabisa. Na katika kitabu Muwatwaa, Imamu Maalik amesema.



Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameona umri wa ummah za mwanzo ni mrefu, na umri wa ummah wake ni mfupi akapewa usiku wa Laylatul-Qadr uwe ni bora kuliko miezi elfu.

[Muwatwaa, 1/321]



Hakuna siku tukufu na kubwa kama siku hii ni wajibu kwetu kuutafuta usiku huu katika kumi la mwisho kufanya ibada ili tupate fadhila hizo. Ninamuomba Allaah atuwezeshe kwa hilo, Aamiyn.



5) DU'AA NI ZENYE KUKUBALIWA

Katika hadiyth iliyopokewa na Imaam Ahmad:

Kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwa isnadi iliyo nzuri

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Amesema: "Kila Muislam du'aa zake ni zenye kukubaliwa atapomuomba katika mwezi wa Ramadhwaan"

Na imepokewa katika Hadiyth kuwa du'aa ya mwenye kufunga pia ni yenye kukubaliwa. Basi mtu ajipinde katika kumuelekea Allaah kumuomba mambo ya kheri ya dunia na akhera aombe pepo ya Jannaatul Firdaus na alete maombi mengine, Allaah Atayapokea maombi yetu, AAMIYN.



La mwisho ambalo nitakua nimekamilisha maudhui yangu:



6) MWEZI HUU NI MWEZI WA KUTOA

Na alikua Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akizidisha kheri nyingi katika mwezi wa Ramadhwaan.



Imepokewa na At-Tirmidhiy kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu 'anhu) Kasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) "Bora ya (wakati wa) kutoa sadaqa ni kutoa katika mwezi wa Ramadhwaa.n"



Na imepokewa na Zayd bin Aslam kutoka kwa babake, amesema nimemsikia 'Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu 'anhu) anasema, "Ametuamrisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) tutoe sadaqa nikatoa mali yangu nikasema leo nimemtangulia Abu Bakr nimekwenda na nusu ya mali, akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kuniambia, "Umewabakishia nini watu wako?" Nikasema, nusu kama hii, na akaja Abu Bakr na kila mali yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamuuliza, "Umewabakishia nini watu wako? Akasema, nimewabakishia Allaah na Mtume wake. Nikasema huyu Abu Bakr hapitiki na kitu chochote abadan"



Kuonyesha wema waliotangulia walikua wakishindana katika kheri lakini tofauti kubwa katika zama zetu hizi watu wanashindana katika mambo ya kidunia na kujifakharisha nayo.

Tunamuomba Allaah Atuonyeshe mema tuyafuate na mabaya tuyawache na tushindane katika kila kheri ili tuwe ni wenye kufuzu na kupata daraja ya juu ya Pepo.

Aamiyn.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu hana haja na kundi la WAISLAMU kwani waweza kuwa muislamu kisha ukawa mlevi, mchawi, mzinifu, mwizi nk

Haya maneno yako ndugu yangu

Ni Mabaya sana

Fahamu tu
Huwezi kuwa Mcha Mungu,mpaka Uwe Muislam

Huwezi kuuwa Mu-umin,mpaka uwe Muislam

Uislam ndio nguzo Mama katika zote
Ukipanda juu zaidi,ni utakutana na Daraja la

IMAAN na IHSAAN

Ukishuka Chini ya Uislam,utakutana na Daraja la

UNAFIKI
UKAFIRI

TANBIH

Tusiseme kama hatujui,Ukimya wako huwezi jutia,Bali neno lako laweza kukutia hatiani

بارك الله فيكم

Sent using Jamii Forums mobile app
itakuwa umenielewa vibaya mwalimu

mimi pia ni muislamu na najivunia kuwa muislamu na na dini ya haki mbele ya Mungu bila ya chembe ya shaka ni UISLAMU

ila kuwa tu muislamu haitoshi inatakiwa baada ya kuwa muislamu ufanye juhudi la kwenda kwenye daraja hillo la IMAAN na IHSAAN

pepo ni kwa ajili ya WACHAMUNGU

UISLAMU ni njia tu unayopaswa kuipitia kuelekea katika UCHAMUNGU
 
N
Wasafiri watakaopenda kuswali waje kuswalia hapo Msata Hotel halafu mnawauzia futari kwa sh. 3000,

Kama sijaelewa nieleweshe.

Corona Virus: Stay Home the only Medicine found.
Ndiyo hivyo,hapa Kuna eneo ambalo tumelitenga kwa ajiri ya swala hasa watu was Mombasa hulitumia kuswali.futari tunauza elfu 3
 
Nimefurahi sana Ramadhan ya mwaka huu naskia wanyamwezi wote wamerudi kwao. Zanzibar hotel zote za kitalii zimefungwa kwaio kutokuwepo kwa hawa majamaa wa kibara kumeifanya zanziba kuwa shuari kabisa i wish ningekueko Zenji ramadhani ya mwaka huu
 
aliposema Mtume saw itafuteni elimu hata ikiwa china alimaanisha pia tujifunze sayansi, ukiijua sayansi ndo utamjua na kumuelewa Mungu vizuri zaidi, japokuwa quran tukufu ndo msingi wa elimu zote


Kwa hiyo sayansi ambayo imetumika kutengeneza telescope ambayo inatumiwa kuuona mwezi ukiwa bado mdogo huikubali sayansi hii ?

Kama Qurani inaendana na sayansi huoni kwamba ni sahihi sana kutumia kifaa cha kisayansi (telescope) kuutafuta mwezi ambao utatufanya tutekeleze amri ile ile ya Qurani ?

Na jee ukitumia hiko kifaa kuutafuta mwezi shaaban 20 utauona huo mwezi ati kwa kuwa umetumia kifaa ?
 
careem amekujibu kisayansi zaid inabidi ukubali yupo sahih

mwakani usifate wa saudia

Sasa huoni kama saudia wanaitumia sayansi hiyo hiyo kwa kutumia kifaa cha kisayansi kuutafuta mwezi ?

Au watumie sayansi kupinga tuu na sio kuitumia katika kusapoti mkuu.

Inakuwaje sayansi ya kutumia simu kuwasiliana na ndugu yako wa kigoma ukiwa dar mkasikiana unaikubali sayansi hii ilhali kwa masikio ya kawaida huwezi kumsikia hata kidogo baina ya kigoma na dar,hii umeikubali.

Mbona sayansi ile ya kutumia vifaa vya kisayansi kuona mwezi ambao hauonrkani kikawaida unaikataa ?
 
Sasa huoni kama saudia wanaitumia sayansi hiyo hiyo kwa kutumia kifaa cha kisayansi kuutafuta mwezi ?

Au watumie sayansi kupinga tuu na sio kuitumia katika kusapoti mkuu.

Inakuwaje sayansi ya kutumia simu kuwasiliana na ndugu yako wa kigoma ukiwa dar mkasikiana unaikubali sayansi hii ilhali kwa masikio ya kawaida huwezi kumsikia hata kidogo baina ya kigoma na dar,hii umeikubali.

Mbona sayansi ile ya kutumia vifaa vya kisayansi kuona mwezi ambao hauonrkani kikawaida unaikataa ?
nimekuelewa mkuu
 
nimekuelewa mkuu

Haina noma mkuu.

Muhimu haya mas'ala ni khilaafiyyah..

Wanachuoni wametofautiana mnoo juu ya mambo ya mwezi.

Kwa hyo haitakiwi kukinzana na kugombana.

Watu wa fiqhi wanasema..

لا ينكر في ما يختلف فيه ، لاكن ينكر في ما يجمع عليه.

Hapakatazwi kufanya moja kati ya yale ambayo wametofautiana ulamaa,lakini panakatazwa kwenda kinyume na waliyokubaliana maulamaa.
 
Haina noma mkuu.

Muhimu haya mas'ala ni khilaafiyyah..

Wanachuoni wametofautiana mnoo juu ya mambo ya mwezi.

Kwa hyo haitakiwi kukinzana na kugombana.

Watu wa fiqhi wanasema..

لا ينكر في ما يختلف فيه ، لاكن ينكر في ما يجمع عليه.

Hapakatazwi kufanya moja kati ya yale ambayo wametofautiana ulamaa,lakini panakatazwa kwenda kinyume na waliyokubaliana maulamaa.


[emoji1317]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
S
Sio sio kweli kwamba wanaangalia mwezi kwa vifaa na wanawazuoni pia wanakataa kuuungalia mwezi kwa vifaa na tunazo fatuaa za wanazuoni wa kisaudia wanakataa kuangalia mwezi kwa vifaa na hilo la kulipa fidia pia sio la kweli nakutumia na uthibitisho na hivyo vifaa unavyosema ni vifaa gani
SAUDIA ARABIA MWEZI WALIUTAFUTA KWA DARUBINI

tarehe 23 kulikuwa hakuna uwezokano wa kuuona mwezi kwa macho ya kawaida japo ni kweli mwezi ulikuwa umeandama

Tarehe 23 mwezi umeandama sa 11:25 asubuhi

Kwakuwa mwezi mpya umechomoza sa 11:25 asubuhi ina maana hu mwezi utazama saa 11 jioni kabla jua halijazama hivyo ukisubiri jua lizame hauwezi kuuona ila ukitumia darubini kuutafuta mida ya mchana utauona ndicho walichofanya Saudi Arabia

Kwa hiyo hata sisi hapa Tanzania tarehe 23 mida ya mchana mwezi ulikuwepo katika anga letu kama tungetumia darubini kuutafuta kabla ya saa 11 jioni tungeweza kuuona

Sasa kama kuutafuta mwezi kwa njia hii inaswihi au haishihi mimi sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefurahi sana Ramadhan ya mwaka huu naskia wanyamwezi wote wamerudi kwao. Zanzibar hotel zote za kitalii zimefungwa kwaio kutokuwepo kwa hawa majamaa wa kibara kumeifanya zanziba kuwa shuari kabisa i wish ningekueko Zenji ramadhani ya mwaka huu
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom