Ramadhan Special Thread

Ni kweli hata Mimi Jana nilijiuliza maswali mengi kama tupo masaa sawa na Saudia kwa nini kila siku watangilie wao

Ikabidi nianze Ku Google kuhusu mwenendo wa mwezi nimeona kitu hicho hicho tarehe 23 mwezi mpya ulikuwepo ila ulikuwa unazama kabla ya jua kuzama hivyo huwezi kuuona kwa macho

Hawa Saudia hili jambo wasipo liacha litawatesa sana na ndio maana mahakama kuu ya Saudi Arabia ndio ilitoa amri mwezi utafutwe na utangazwe maana ingekuwa kituko wamekamilisha 30 bila ya mwezi kuonekana

Pia nimeona mwezi mpya utaandama tarehe 22 May saa 2:38 asubuhi ina maana hu mwezi utazama mida ya saa 2 usiku kwa hiyo kuna uwezo kano mkubwa tukala idi pamoja wao itakuwa 30 sisi 29

Sent using Jamii Forums mobile app
 
swadakta
 
Acha Uongo wewe....

Ukiambiwa lete ushahidi wa Saudia kuomba Radhi....ninahakika hutoleta

Hizo zilikuwa ni habari za Mitandao tu,na si uhalisi...

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kujipa uhakika bila kujua anaeongea amejipanga vipi. Acha kabisa, hata mwezi wa muandamo kwa juzi haukuwepo, ubaya ni kwamba tayari walikuwa wako ndani ya Shaaban 30 sasahapo utaona ni jindi gani wametangaza mwezi kuepusha madhara na kwa vile hakuna Shaaban 31, miezi yote ya kiislam muandamo wake ni kuanzia 29 hadi 30. Bado unataka ushahidi? Na vile vile mwezi wa muandano kiusahihi ni ule ambao utaonekana kwa macho ya kawaida na sio kwa kifaa kama telescope. Saudi Arabia wametumia twlescope hatima yake sawa wameuona lakini jinsi ulivyokuwa katika ukuaji wake ulikuwa ndio kwaknza upo katika asilimia 0.2 ya ukuaji wake kitu ambacho ni vigumu kuonekana. Kwa sisi ambao tumeanza kufunga leo tar 25 ambapo tar 24 ndio tumetizama mwezi, mwezi ulikuwa kwenye asilimia 3.5 ya ukuaji wake kitu ambacho unaweza kuonekana kwa macho ya kawaida. Saudi wanasababisha Controversy. IN SHAA ALLAH atujaalie tuwepo hadi mwisho wa Ramadhan ili tuje kushuhudia itakavyokuwa.

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
جزاك الله خيرا
 
Niliandika kwenye uzi huu huu, lakini bado kuna wengine wamepinga, hivi mwezi ukiwa katika 0.4% ya ukuaji wake utaonekana wapi. Kwasisi ambao tuliangalia mwezi tar 24 tayari ulikuwa katika 2.5% ya ukuaji wake hivyo ni rahisi kuonekana, ila wengine wana ubishi wa kiadili kwa vile tu Saudi Arabia katangaza kuuona.

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
Nimefurahi sana Ramadhan ya mwaka huu naskia wanyamwezi wote wamerudi kwao. Zanzibar hotel zote za kitalii zimefungwa kwaio kutokuwepo kwa hawa majamaa wa kibara kumeifanya zanziba kuwa shuari kabisa i wish ningekueko Zenji ramadhani ya mwaka huu
[emoji848][emoji848][emoji848]

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
Jazzakhallàh khàigr

Ahsante kwa ukumbusho Mwenyez Mungu atufanyie wekepes katik hili
In shaa Allah
السلام عليكم

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 


Mkuu kwanza tambua kuwa ukiwa mwezi thelathini hata kama hukuuona mwezi basi kesho yake ni mwezi mosi ya mwezi unaokuja

Unatakiwa ujue kuwa kuingia mwezi mosi ni eidha uonekane mwezi au itimie mwezi thelathini.

Kiislamu hakuna mwezi 28 kama ulivyosema,sijui umeetoa wapi mwezi 28 kiislamu jamaa ?

Mwaka 93 kama sikosei mwezi ulionekana tarehe 29 ya waliotangulia huku bakwata ikiwa ni tarwhe 28,mufti akatangaza watu wasali iddi na wailipe siku ile.

Lau kama ingekuwa kuna siku 28 za mwezi kiislamu basi mufti asingetangaza watu walipe.

Kwa hiyo mkuu hata kama saudia wasingeuona mwezi hiyo juzi bado kesho yake lazima ingekuwa ramadhani kwa sababu ilishatimia tarehe 30 shaabani tayari kwa hiyo hapo unatoa madai ambayo kimsingi yanaonesha kwamba wewe unadhani kuwa kama hukuuona mwezi basi uende hata tarehe 32 huko jambo ambalo sio sawa.

Unaposema mwezi sahihi ni ule unaoonekana kwa macho ya kawaida unamaanisha kuwa wanaotumia telescope kuangalia mwezi wanatumia macho yasiyo ya kawaida sio ?

Sasa kama unakataa telescope kuutafuta mwezi kwa madai ya kuwa ati mwezi utafutwe kwa macho ya kawaida basi hata simu usipige kumpigia mtu wa zanzibar wewe ulieko dar kumuulizia mwezi kwa sababu..

Unapopiga simu kumpigia mtu wa zanzibar unatumia kifaa kumsikia mtu wa zanzibar akikupa taarifa za mwezi wakati ambao kwa macho ya kawaida huwezi kumsikia kabisa bila simu mtu aliyeko zanzibar.

Kwa hiyo hata simu tusitumie kuwapigia watu kuwauliza taarifa za mwezi kwa sababu kutumia simu sio njia locally ambayo inahusisha masikio peke yake kama ambavyo kutumia telescope sio njia locally inayohusisha macho peke yake.

Ukipinga telescope kuangalia mwezi pia unatakiwa upinge kutumia simu na tv kusikiliza habari zamwezi.

Ukiikubali simu itumike basi unataka kuingiza vifaa ambavyo havikutumika enzi hizo kuutafuta mwezi kabisa.

Alafu jee ukitumia telescope kuangalia mwezi siku ya 25 utauona japo kwa 0.1% kwa kutumia hiyo telescope ?

Kwani telescope inauona mwezi kwa kuwa inauwezo huo wa kuona au telescope inauona mwezi kwa kuwa siku za mwezi kuonekana zimefika ?
 
Kuhusu 28 nakiri nilikosea na nimesharekebisha.

Kaka haya maswali yako yote nakujibu kiurahisi kama ifuatavyo:
Kuangalia na kutafuta mwezi wa mwandamo katika eneo la magharibi wakati wa jioni wakati Jua linapozama, ndio msingi wa kuamua mwanzo na mwisho wa mwezi wowote wa Hijri katika Uislamu.

Ni kama amri nyingine yoyote katika Uislam, hii ndio njia iliyoelezewa na Mwenyezi Mungu katika Quran na kwa nabii Muhammad ﷺ katika Hadith. Ni Sharee'ah ambayo Mwenyezi Mungu alimtumia Nabii wetu Muhammad ﷺ (Rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Ni ya ulimwengu na ya milele, mpaka Siku ya Kiyama. Ni halali kwa kila wakati na mahali, ikiwa sayansi za ulimwengu ni za hali ya juu au vinginevyo, ikiwa kuna darubini au la.

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
Ila kiukweli ugumu wa kwenye kufunga kwa pamoja tunauleta sisi wenyewe waislam, ndani yake kuna mambo ya kisiasa. Kuanzia leo nikisikia mwezi umeonekana kokote kule nafunga, hayo ndio maagizo kutoka kwenye Quran na hata hadith, waislam tunatakiwa tushikamane na wala tusifarikiane. Akiuona mwezi muislam yoyote yule duniani inatakiwa iwe ni sawa na tumeuona waislam wote.

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 

Mkuu nimekuuliza maswali hujajibu kila swali kama nilivyouliza hapo juu.

Unasema msingi wa uislamu ni kuangalia mwezi magharibi pale unapoandama ili kupata tarehe hijri katika uislamu.

Kama ni hivyo Sasa saudia hizo telescope wanatumia adhuhuri kutizama mwezi au wanatumia muda wa magharibi ule ule kutizama mwezi ?

Alafu kama unakubali kuwa hakuna mwezi 28 katika uislamu jee umewahi kusikia saudia wanaangalia mwezi siku ya 28 au 27 au 26,alafu wakauona mwezi kwa hizo teleescope ?

Kama hawajawahi huoni kuwa wanatizama mwezi katika masiku ambayo kisheria ndo inatakiwa mwezi utizamwe ?

Na kama unakataa mwezi ambao unaonekana kwenye telescope mwezi ambao ni kweli mwezi na umeanza kuchomoza kwa hizo 2% na masiku ya kuangaliwa ni yale yale ya kishwria yaani 29 na 30 ila tu unaukataa kwa kuwa tu kinatumika kifaa cha kisayansi kusaidia kuuona

Kama ni hivyo mbona usizikatae simu ambazo zinatumika kutafuta taarifa za mwezi kutoka kwa mtu wa mbali.

Tena sauti unayoisikia hiwezi kuisikia katika hali ya kawaidia,yaani mtu wa kigoma na dar hawawezi kupeana taarifa za mwezi kwa kuongea bila simu kwa sababu ni maeneo mbali mbali,sasa ili iwe rahisi kwao kuwasiliana kikatumika hiki chombo cha kisayansi yaani simj kurahisisha mawasiliano ambayo locally hayawezi kufanyika na kuwezekana.

Kama pia ni hivi kwa nini unakataza saudia kutumia telescope ya kisayansi kutizama mwezi alafu wewe unatumia na kuhalalisha simu ambazo nazo ni za kisayansi zinatumika kufanya mawasiliano kuipata sauti ambayo huweI kuisikia localy ?

Sasa hapa nataka uninibu kila nukta niliyouliza mkuu ili na sisi tupate faida katika majawabu yako.

والله أعلم
 
Allah akulipe shekh ,aiseee nimekupenda sana kwa ajili ya Allah.Nimejifunza kutoka kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nataka kujibu hoja yako moja badala ya nyingine lakini kila nikiedit inapotea..

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
Nawakumbusha pia ndugu zangu katika dini

katiika kufuturu tuache israfu tule kwa kiasi, kula chakula kwa saizi yako

Allah sw hawapendi wanaofanya israfu( hili lipo na ushahidi hata ndani ya quran na hadithi)

isije kuwa tunafunga funga zetu vizuri kisha tunakuja kuziharibu kwenye kufuturu
 
Yawezekaka isiwe 30 kama walikosea mahesabu ya mwezi wa shaabani

Mimi binafsi sijawahi kuona mwezi 30 usionekane kwa macho ya kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…