Ramadhan Special Thread

Kama unakusudia chooni inafaa hakuna ubaya mkuu.

Imethibiti kuwa mtume wa Allah kabla ya kuoga janaba akitia udhu kama ule wa sala na kisha ndo huoga.na akiyafanya hayo akiwa chooni,na udhu huo unafaa kusalia.

Kwa hiyo hakuna ubaya kutawadhia chooni maadamu maji ya udhu hayajaathiriwa na najisi.
 
Kipindi nipo mdogo wakati nasoma madrasa miaka ya 90 nakumbuka ustadh wangu alinifundisha wakati wa kutia udhu kuna dua ya kusoma katika katika kila kitendo, baada ya kutia nia,

Unapoanza kuosha viganja unasema:
اللهم سبت قدمي يوم تضل فيه الأقدام

Unapotia maji kinywaji na kupandisha puani unasema:
اللهم ارحني راءهة الجني

Unapoosha uso unasema:
اللهم بيض وجواح يوم تبيض وجواح و تسود وجواح

Unapoosha mkono wa kulia unasema:
اللهم اعطني كتابي بيميني وحاسبني حساب يسيرا

Unapoosha mkono wa kushoto unasema:
اللهم لآ تجعل كتابي بشمالي وجعلني وراء ضحره

Unapotia maji kichwani unasema:
اللهم حرم الشعري وبشري علي النار

Unapoosha masikio mawili unasema:
اللهم جعلني ممن يستمعوان الكول فيتبعوان احسني

Unapoosha miguu miwili unasema:
اللهم حرم الرجليني من معاصيك كله.

Ama baada ya kutia/kuchukua udhu unasema:
اشهد ان لا اله الا الله واشهدوا ان محمد عبدهو ورسوله، اللهم جعلني من التوابين وجعلني من المتطهرين وجعلني من عبادك الصالحين.
Kufuatana na mlolongo huu. Je kuna usahihi na kama kuna usahihi je kutaja jina la Allah maliwatoni hakuna tatizo??

[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769]
 

Mkuu waalimu wetu walikuwa na nia nzuri sana kutufundisha mambo mengi ambayo yana sura ya uzuri na nia ya kutufanya kuwa wema zaidi.

Lakini wakati mwingine kidogo kunakuwa jitihada zenye kwenda kinyume na mafundisho ya bwana Mtume wa Allah sala na salamu ziwe juu yake.

Hizo dua zote ukiangalia hazina uthibitisho na usahihi kuwa alizifundisha mtume,ni jitihada za waalimu wetu wabora Allah awabaariki.

Yaliyothibiti hasa ni kukosha viungo kama ulivyosema,hizo dua zingine hazina mafundisho kutoka kwa Mtume wa Allah.

Kuna dua ambazo zimethibiti tuu baada ya udhu wenyewe,na sio baada ya kiungo fulani kila ukimaliza kutia basi kuna duna.

Lau ikiwa hivyo manake kunakuwa na uzito tunauongeza katika mafundisho ya Allah na Mtume na yeye kasema kuwa..

"وما جععل عليكم في الدين من حرج"

"Na wala Allah hakujaalia katika dini mambo mazito mazito"

Na Allah akasema tena "يريد الله بكم اليسرى ولا يريد بكم العسرى"

"Allah anawatakieni wepesi na wala hawatakii mazito"

Lakini pia tunaamrishwa na Qurani kuwa " Alichokupeni mtume kichukueni,na alichokukatazeni kiwacheni"

Ikiwa kile alichotupa mtume tukichukue,je ambacho hakutupa tutakifanyeje ?

Ikiwa tutakichukua na tutaitakidi kuwa ni kizuri na ni katika ibada basi mtume Anasema...

ما تركت شيء يقربكم الى الله إلا أمرتكم به

Sikuacha jambo ambalo litawakaribisha nyie na Allah isipokuwa nimeriamrisha jambo hilo kwenu.

Basi je kuna jambo ambalo Mtume hakufundisha na likawa linatukaribisha sisi na Allah na likawa zuri ?

Nafkiri kiufupi hizo dua hazijathibiti kutoka kwa Mtume na sio sahihi kuzisoma.

Ila tu kuna ikhtilaafu za maulamaa kuwa wengine wanasema ni waajibu kusema bismillahi wakati wa kutia udhu na wengine wanasema sio waajibu.

Sasa ikiwa wewe unaona ni waajibu kusema bismillah basi unapotia udhu chooni LAZIMA useme bismillah kwa sababu usiposema hivyo udhu unakuwa haujatimia.

Kuhusu kusema bismillah chooni ama kutaja jina la Allah chooni hilo jambo ni kweli ni makruhu (karaha,linachukizw,halipendezi)

Ila makruhu na wajibu basi wajibu hutangulizwa kwanza kuliko makruhu.

Yani hatuachi uwajibu kwa kuogopa makruhu.tunafanya uwajibu kwanza makuruhu inakuja baadae.

Hivyo utasema bismillah chooni kama unaitakidi ni wajibu kisha utatia udhu.

Kama kuna sehemu sijafahamika naam....
 
Masha Allah

Allah akubaarik
Unafaa kuwa Mwalim

TANBIH
Bismillah,isemwe kimoyo iwapo chooni,usitamke kwa kutoa sauti

Ni jambo lisilofaa kisheria
Allah anajua zaidi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masha Allah

Allah akubaarik
Unafaa kuwa Mwalim

TANBIH
Bismillah,isemwe kimoyo iwapo chooni,usitamke kwa kutoa sauti

Ni jambo lisilofaa kisheria
Allah anajua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app

Atubaarik sote.

Kusema kimoyomoyo sio kusema hapo ni kuifikiria bismillah.

Kinachotakiwa ni isemwe bismillah kwa sauti ya kujiskia mwenyewe(kunong'ona)ile ya mdomo kutikisika,

mtume alikuwa akijulikanwa kuwa anasoma katika swala kwa kule kucheza ndevu zake.

Manake kama ndevu zingekuwa hazichezi isingesemwa kuwa anasoma katika sala.

Jambo la kutofaa kusema bismillah chooni ni makruhu,na kuisema katika udhu kuna wanaosema ni waajibu.

Inapokutana makruhu na waajibu basi wajibu hutangulizwa kufanywa hata kama wakati huo utakuwa una makruhu utaifanya.

Kwa sababu katika misingi ya sheria lenye madhara machache ndo hutangulizwa zaidi kuliko lenye madhara mengi
 
Hili Bro

linahitaji umakini sana,nipo na jambo hapa,in sha Allah nipatapo fursa,nitakuja na ufafanuzi mdogo,huenda tukapata njia

Shukran sana Bro
Allah akubaarik sana popote ulipo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asalam alaykum,,
Natumai mko vyema ndugu zangu! Napenda kuwashirikisha wakuu katika suala la utoaji wa zaka ya fitr! Kumekuwa na mvutano na malalamiko kuwa ni kiasi gani kinafaa kutolewa kwa kila muislam aliyefunga na makusudio yake!
.
Wadau wamekuwa wakihoji zaidi walengwa wa hii zaka kutokana na baadhi ya viongozi wetu wa dini kushindwa kufanya uadilifu na kupelekea matumizi mabaya ya hii zaka! Hali hii imepelekea hata waliofunga kudiriki kuwapatia watu ambao wao wanaona wanastahili kupewa zaka ili nao wafurahie sikukuu ya IDD,,
.
wengine wanasema zaka lazima ikabibidhiwe katika uongozi wa msikiti wa eneo husika ambapo viongozi ndio hupanga nani wampatie hiyo zaka
Napenda nikaribishe wenye elimu juu ya hili watuelimishe vizuri kwa dalili ili sote tunufaike
...
Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi mabohora jumamosi tunagonga biriani.
Ikiwa usiku tupeane mwaliko [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]

[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769]
 
The moon - Phases Calender
Pia nyingine ni Moon phases calculator

[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769]
Ndugu yang careem kwa wale walioanza kufunga ijumaa leo kwao ni yaumul shak, je kwa hizi picha inaonesha mwezi upo 0% na possibility ya kuonekana kwa macho haupo? Na pili mwezi unazama saa 12 na dk 8 jion ambapo kwa dar magharibi inakuwa haijaingia. Naomba mtizamo wako kwa hili?View attachment 1456444

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Al akhy kwa hili, kama mwezi unazama saa 12 na dakika 8 possibility ya mwezi kuonekana ni ndogo sana kwa leo hii. Ikiwa sisi tuliofata Bakwata leo tupo mwezi 28 Ramadhan na waliotangulia wapo mwezi 29 Ramadhan. Kikubwa ni kusubiri ikiwa utaonekana kheri, na ikiwa utaonekana kesho kwa waliotangulia wao watakuwa wamekamilisha mwezi 30 Ramadhan na sisi tuliofata Bakwata tutakuwa mwezi 29 Ramadhan. Yote kheri. Ila kuanzia sasa naamini tukiwa tunafutilia miandamo ya miezi kwa miezi yote mingine naamini hakuna sehemu tutakuwa na utata.

[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…