Kipindi nipo mdogo wakati nasoma madrasa miaka ya 90 nakumbuka ustadh wangu alinifundisha wakati wa kutia udhu kuna dua ya kusoma katika katika kila kitendo, baada ya kutia nia,
Unapoanza kuosha viganja unasema:
اللهم سبت قدمي يوم تضل فيه الأقدام
Unapotia maji kinywaji na kupandisha puani unasema:
اللهم ارحني راءهة الجني
Unapoosha uso unasema:
اللهم بيض وجواح يوم تبيض وجواح و تسود وجواح
Unapoosha mkono wa kulia unasema:
اللهم اعطني كتابي بيميني وحاسبني حساب يسيرا
Unapoosha mkono wa kushoto unasema:
اللهم لآ تجعل كتابي بشمالي وجعلني وراء ضحره
Unapotia maji kichwani unasema:
اللهم حرم الشعري وبشري علي النار
Unapoosha masikio mawili unasema:
اللهم جعلني ممن يستمعوان الكول فيتبعوان احسني
Unapoosha miguu miwili unasema:
اللهم حرم الرجليني من معاصيك كله.
Ama baada ya kutia/kuchukua udhu unasema:
اشهد ان لا اله الا الله واشهدوا ان محمد عبدهو ورسوله، اللهم جعلني من التوابين وجعلني من المتطهرين وجعلني من عبادك الصالحين.
Kufuatana na mlolongo huu. Je kuna usahihi na kama kuna usahihi je kutaja jina la Allah maliwatoni hakuna tatizo??
[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769]
Mkuu waalimu wetu walikuwa na nia nzuri sana kutufundisha mambo mengi ambayo yana sura ya uzuri na nia ya kutufanya kuwa wema zaidi.
Lakini wakati mwingine kidogo kunakuwa jitihada zenye kwenda kinyume na mafundisho ya bwana Mtume wa Allah sala na salamu ziwe juu yake.
Hizo dua zote ukiangalia hazina uthibitisho na usahihi kuwa alizifundisha mtume,ni jitihada za waalimu wetu wabora Allah awabaariki.
Yaliyothibiti hasa ni kukosha viungo kama ulivyosema,hizo dua zingine hazina mafundisho kutoka kwa Mtume wa Allah.
Kuna dua ambazo zimethibiti tuu baada ya udhu wenyewe,na sio baada ya kiungo fulani kila ukimaliza kutia basi kuna duna.
Lau ikiwa hivyo manake kunakuwa na uzito tunauongeza katika mafundisho ya Allah na Mtume na yeye kasema kuwa..
"وما جععل عليكم في الدين من حرج"
"Na wala Allah hakujaalia katika dini mambo mazito mazito"
Na Allah akasema tena "يريد الله بكم اليسرى ولا يريد بكم العسرى"
"Allah anawatakieni wepesi na wala hawatakii mazito"
Lakini pia tunaamrishwa na Qurani kuwa " Alichokupeni mtume kichukueni,na alichokukatazeni kiwacheni"
Ikiwa kile alichotupa mtume tukichukue,je ambacho hakutupa tutakifanyeje ?
Ikiwa tutakichukua na tutaitakidi kuwa ni kizuri na ni katika ibada basi mtume Anasema...
ما تركت شيء يقربكم الى الله إلا أمرتكم به
Sikuacha jambo ambalo litawakaribisha nyie na Allah isipokuwa nimeriamrisha jambo hilo kwenu.
Basi je kuna jambo ambalo Mtume hakufundisha na likawa linatukaribisha sisi na Allah na likawa zuri ?
Nafkiri kiufupi hizo dua hazijathibiti kutoka kwa Mtume na sio sahihi kuzisoma.
Ila tu kuna ikhtilaafu za maulamaa kuwa wengine wanasema ni waajibu kusema bismillahi wakati wa kutia udhu na wengine wanasema sio waajibu.
Sasa ikiwa wewe unaona ni waajibu kusema bismillah basi unapotia udhu chooni LAZIMA useme bismillah kwa sababu usiposema hivyo udhu unakuwa haujatimia.
Kuhusu kusema bismillah chooni ama kutaja jina la Allah chooni hilo jambo ni kweli ni makruhu (karaha,linachukizw,halipendezi)
Ila makruhu na wajibu basi wajibu hutangulizwa kwanza kuliko makruhu.
Yani hatuachi uwajibu kwa kuogopa makruhu.tunafanya uwajibu kwanza makuruhu inakuja baadae.
Hivyo utasema bismillah chooni kama unaitakidi ni wajibu kisha utatia udhu.
Kama kuna sehemu sijafahamika naam....