Ramadhan Special Thread

Shukrani Sana kwa ukumbusho ,tunaomba link ya ule Uzi wa Ramdhan Threads uwekwe hapa... Tupate kujiwaidhi ..

Ramadhan Special Thread
 
Naam shukrani akhy
 
Amiin ukhty wangu

Hakika umefanya Jambo jema Sana la kutuzindua na kukaa tayar tayar Kwa mgeni wetu adhwim kabisa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ningependa kutahadharisha upande wa kuepukana na mambo yote ambayo ni ya kipuuzi wakati WA Ramadhani.

Wakati WA Ramadhani sio Mda wa kushinda unaangalia series au movies mchana kutwa ili Muda uende ufike wasaa WA magharibi ufuturu,huo ni upuuzi na unahatarisha funga yako na kukosa fadhila kubwa za mwezi huo.

Sio wakati WA kununua Karata na Domino na kucheza vijiweni eti Mda uende mfike magharibi na mfungue Swaumu,hakika Hilo sio kusudio la mwezi wa ramadhani.

Sio Mda WA kukaa vijiweni na kupiga soga na kusengenya watu,maana mtaongea ya kuongea mtajikuta mwisho wa siku mnaanza kusengenya,ni kujitafutia madhambi bure na kujikuta mnashinda na njaa bure bila malipo yoyote Yale.

Huo ni mwezi mmoja lakini Kwa wanao jua thamani yake na kujitenga na mambo yote ya kipuuzi hakika kwao ni kama mwaka kwasababu wanazinyima nafsi zao na Yale yote ambayo huwafanya wafurahi na kujipinda na kujitenga nayo Kwa kusudio moja Tu nalo ni kujikurubisha Kwa Allah Kwa kutaraji radhi zake na fadhila zake.

Ni Bora mchana WA Ramadhani ulale kwani utapitwa na mambo mengi ya kipuuzi kuliko kukaa vijiweni na kufanya mambo ya kipuuzi
 
Amiin ukhty wangu

Hakika umefanya Jambo jema Sana la kutuzindua na kukaa tayar tayar Kwa mgeni wetu adhwim kabisa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Ma shaa allah, ndio raha ya kuwaita wenye elimu, ila huku mwisho wasilalae bana wafanye ibada ni nyingi mno yani nyingi sana hata wafanye ibada ya kutafakari uumbaji wa allah,
Nimependa mno nyongeza yako
 
Ma shaa allah, ndio raha ya kuwaita wenye elimu, ila huku mwisho wasilalae bana wafanye ibada ni nyingi mno yani nyingi sana hata wafanye ibada ya kutafakari uumbaji wa allah,
Nimependa mno nyongeza yako
Naam ukhty wangu

Yaani upo sahihi kabisa hakika ni mwezi wenye fadhila nyingi na ibada nyingi mno tena zalipwa Kwa thawabu kubwa kubwa,mfano wakati WA Ramadhani swala ya Sunna inalipwa kama faradhi Mashallah,na faradhi yalipwa marudufu zaidi,Kwa kila ibada INA ujazo wake wa kutosha.

Sasa ndio imeshindikana kabisa kabisa basi mja huyu ni Bora akalala atasalimika kuliko kuelekea kwenye mabalaa yatayo haribu funga yake
 
Wakuu naomba kujua,hivi misikitini hapatoshi kufundisha na kukumbushana haya mambo mpaka tulete threads kidini za kuhusu kundi la watu fulani kwenye jamii yenye mchanganyiko kama jf?,

Maana hapa jf si kwa waislam tu,ni wakristo pia,naona haya yangefaa yawe maalum kwa watu wa imani husika,sasa hapa jukwaani yana umuhinu gani mambo haya?,
 
Chief

Kwani humu hatupo waislamu na wakristo?

Hao ambao wangekumbushana misikitini na makanisani ndio hao hao ambao tupo humu

Unateseka ukiwa wapi chief?
 
Kuna watu mnashida kweli, ulivoona neno ramadhan ukajua uhusiki huku sasa kwa ninj ukasoma? Unadhani kila mtu anaenda kanisani au msikitini? Nasaha zinatolewa msikitini au kanisani peke yake?
May the Almighty grant you guidance
 
Chief

Kwani humu hatupo waislamu na wakristo?

Hao ambao wangekumbushana misikitini na makanisani ndio hao hao ambao tupo tupo humu

Unateseka ukiwa wapi chief?
Neno kuteseka sijui lina maana gani kwako,lakini hem tafakari uone nimeandika nini.

Shida kubwa ya waislam wengi huwa hamtaki kuulizwa maswali au kujibu hoja,badala yake mtaanza kejeli.

Hivi kweli hayo mambo ni ya kuweka jf wakati misikiti ipo?,ndio swali langu tu.

Neno kuteseka linatumika na watu wasiojali utu wa watu,ramadhani imekaribia,punguza dhihaka na kutumia maneno dhalimu mkuu,haikusaidii kitu.
 
Kuna watu mnashida kweli, ulivoona neno ramadhan ukajua uhusiki huku sasa kwa ninj ukasoma? Unadhani kila mtu anaenda kanisani au msikitini? Nasaha zinatolewa msikitini au kanisani peke yake?
May the Almighty grant you guidance
Sasa hapa umenijibu kweli?,ina maana mimi kuuliza hili swali nimeonekana nina shida,haya sawa.

Wewe hauna shida mkuu.
Hongera.
 
Kuna kitu hakipo sawa kwako wallah , Mungu akujalie uongofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…