Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Asalaam Aleykum ndugu zangu wote katika imani,

Kuelekea mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan, waislamu wote ninawaomba tukutane humu ili tuelimishane mawili matatu kuhusu mwezi huu.

Lengo kuu ni kuweza kufahamu yale yote aliyotufunza kipenzi chetu mtume Muhammad S.A.W kuhusu mwezi huu.

Vitu gani tukifanya vitaharibu swaumu zetu, vitu gani tukifanya vitaongeza thawabu zinazopatikana katika kufunga, ipi hukumu kwa wale wasiofunga na yapi malipo anayopewa mja ambaye anafunga swaumu kikamilifu.

Pia tuweze kujifunza neema zinazopatikana kwenye usiku wa lailatul qadr, usiku ambao umebarikiwa kuliko siku elfu moja.

Kwa haya machache ninapenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa muumba wa mbingu na ardhi ambaye si mwingine bali ni Allah S.W. T na kipenzi chake, Mtume Muhammad S.A.W.

Karibuni.
 
Pedezhee kumbe nawe yakhe!
Hadi mwezi mtukufu ndipo tutambue dini yako!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] muumini wa kweli hufanya ibada bila kumbugudhi mtu wala kujionesha onesha hovyo kama ni mcha Mungu .

Hiyo ndo tabia yangu ukiniona utadhani ni mtu nisiyejua chochote kuhusu dini.
 
Screenshot_2017-05-22-19-54-32_1.jpg
 
Assalam aleykm warahmatullah wabatakatul! Naomba kujuzwa juu ya ulaj/ kutokula daku.Je nikiacha kula daku funga yangu itaswih?
Walykum salam dada.

Jibu ni ndio, swaumu yako iko sahihi hata kama hujala daku.

but daku ni sunnah tu na hasa ukichelewsha kula but isiingia alfajir...allah hututakia wepesi ili tusiwe wadhoofu sana kwenye funga ndio maana kutuhusu daku dada, na si lazima ule wali au kitu chakushibisha. Unaweza kunywa ata maji, tende, chungwa, au chochote, kama huwezi kula usiku, ili kupa fadhila za sunnah ya daku

Allah ni mjuzi zaid hakika...
 
Hivi ndivyo binadamu tunatakiwa kua,kukumbushana mambo ya kheri,unaweza kufanya jambo dogo tu kama la mleta uzi Kumbe kwa MOLA ni jambo kubwa,tumuombe ALLAH atujaalie tuwe ni wenye kukumbushana mara kwa mara mpaka mauti zitapotufika.
 
Back
Top Bottom