Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

*﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾*

*☪ LEO KATIKA FUNGA ☪*
*( 1 )*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}*
*Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.* (2:183)
==================

*TUNAMSHUKURU ALLAH MTUKUFU KUTUJAALIA KUFIKIWA NA MWEZI HUU WA RAMADHANI, HII NI NEEMA KUBWA KUTOKANA NA WENGI MIONGONI MWETU HAWAPO TENA HAPA DUNIANI, NA WENGINE WAPO LAKINI NI WAGONJWA.*

*ALLAH AWASAMEHE NDUGU ZETU WALIYOTANGULIA MBELE YA HAQQI, NA AWAPONYE WAGONJWA WETU, PIA ATAQABBAL FUNGA ZETU. AAMIN YAA RABBAL AALAMIN.*

*[emoji680] TUINGIE KATIKA DARSA YETU FUPI KABISA INAYO HUSU FUNGA:*

*IBADA YA FUNGA NI IBADA ADHIMU KABISA MIONGONI MWA IBADA.*
*HIVO KUNA BAADHI YA MAMBO YATUPASA KWANZA TUYAFAHAMU.*

*[emoji815] KWANZA KABISA.*

*١- كم مرَّةً ذكر الصيام في القرآن الكريم؟*
*1- MARA NGAPI IMETAJWA FUNGA NDANI YA QUR'ANI?*

*[emoji841] JAWABU LAKE.*

*ذكر الله الصيام في القرآن الكريم أربع عشرة مرَّة، سبْع مرَّات في سورة البقرة وحدها، ومرَّة في سورة النِّساء، ومرَّتين في سورة المائدة، ومرَّة في سورة مريم، ومرَّتين في سورة الأحزاب، ومرَّة في سورة المجَادَلة.*

*ALLAH MTUKUFU AMEITAJA IBADA YA FUNGA NDANI YA QUR'ANI MARA 14.*
*MARA SABA KATIKA SURATUL BAQARA PEKEE, NA MARAMOJA KATIKA SURATU NISAA, MARAMOJA KATIKA SURATUL MAAIDAH, MARAMOJA TENA KATIKA SURATU MARYAM, NA MARAMOJA KATIKA SURATUL MUJAADALAH AU MUJADILAH.*

*[emoji815] JAMBO LA PILI.*

*TUFAHAMU KWA UFUPI NENO RAMADHANI.*
*(رمضان )*
*Neno Ramadhani limejengwa kwa herufi 5 ambazo ni hizi zifuatazo.*

*♢ الراء ، والميم ، والضاد، واﻷلف، والنون.*
*1-Raau. 2-Miimu, 3- Dhadu, 4-Alifu, 5-Nuuni.*

*Baadhi ya wanachuni wamelitafsiri neno hili kwa tafsiri mbalimbali.*

*KWA UFUPI.*

*♢ ﻗﻴﻞ ﺇﻧﻤﺎ ﺳﻤﻲ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﻷﻧﻪ ﻳﺮﻣﺾ ﺍﻟﺬﻧﻮﺏ ﺃﻱ ﻳﺤﺮﻗﻬﺎ ﺑﺎﻷﻋﻤﺎﻝ ﺍﻟﺼﺎﻟﺤﺔ.*
*Yaelezewa kwamba: Hakika imeitwa Ramadhani kwa sababu huyayusha madhambi kwa maana huyaunguza kutokana na amali njema.*

*♢ رمضان إسم من الرمض أى ﺷِﺪَّﺓُ الحرِّ*
*Ramadhan ni jina lililo tokana na ramdhi kwa maana joto kali (Lenye kuunguza)*

*Ramadhani huunguza madhambi, Pia vilevile huyayusha mafuta mwilini na hua sababu ya kumkinga mfungaji juu ya vitu vyoote vyenye madhara.*

*Asema Mtume (ﷺ)*

*"الصَّوْمُ جُنَّةٌ، فَإِذَا كَانَ أَحَدُكُمْ صَائِمًا فَلاَ يَرْفُثْ وَلاَ يَجْهَلْ، وَإِنِ اِمْرُؤٌ قَاتَلَهُ أَوْ شَاتَمَهُ فَلْيَقُلْ: إِنِّي صَائِمٌ".*

*☪ MAANA YAKE.*

*“Funga ni kinga, ikiwa mmoja wenu atakuwa amefunga, basi asiseme maneno machafu, na wala asifanye mambo ya kijinga, na akitokea mtu akagombana nae, au akamtukana, aseme, “Mimi nimefunga”.*

*■ FUNGA HUMZUIA MFUNGAJI KUTOFANYA MADHAMBI*.

*■ FUNGA HUMKINGA MFUNGAJI KUTOKANA NA MARADHI MBALIMBALI...*

*■ KADHALIKA HUONDOA SUMU MBALIMBALI KATIKA MWILI WA MWANAADAMU*

*[emoji677]HII NI MAANA FUPI YA NENO RAMADHANI.*

*Tazama Video fupi ifuatayo ili uone faida ya funga kwa afya yako.*
☪☪☪☪☪☪☪☪☪

*[emoji257] ALLAH MTUKUFU: TWAKUOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*


*Ukumbi Wa Faidika Na Mawaidha.*

*الدعوة اﻹسلامية*
 
kuna hili jambo hata Hance Mtanashati aliligusia siku za nyuma
napenda kulikumbusha tena ndugu zangu waislamu hasa vijana tuache mchezo wa kubet,mikeka Mungu hapendi, kama wewe unacheza huo mchezo basi ujue upo kundi moja na walevi, waabudu masanamu na wapiga ramli

''
Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi, kamari, kuabudu masanamu na kupiga ramli, ni uchafu na ni katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni navyo ili mpate kufanikiwa'' (Q 5:90 )

Mungu (s.w) atusamehe na atusaidie tuache kabisa hayo maovu,hakuna faida hapo zaidi ya kuchezewa na shetani
 
Mashaallah, leo katika msikiti wangu wakitaa ulijaa hadi safu zamwisho, wakati tulikuwa tunaswali swafu mbili hadi tatu. Nawaombea kwa Allah awajalie waendelee na ibada hawa ndugu zetu hata baada ya ramadhani.


Ramadhani Mubarak.
Ni kweli mkuu
Hata mie leo salat maghrib nimekosa nafasi ikabidi niswali nje
Mungu atuzidishie imani na uchamungu
 
*NASAHA MUHIMU*
[emoji820]Tuhifadhi ndimi zetu na maneno machafu.

[emoji820]Kama hatuna la kusema basi tunyamaze kimya.

[emoji820]Neno tulifikirie kabla hatujalitamka mbele za watu.

[emoji820]Tujiepushe sana na kusema uwongo.

[emoji820]Sema ukweli katika kila jambo lako.

[emoji820]Usiseme uwongo hata katika maskhara.

[emoji820]Jiepushe sana na vikao vya wasemaji uwongo.

[emoji820]Kumbuka kwamba kusema kweli ni kinga hata mbele ya adui yako.

[emoji820]Ikumbukeni adhabu kali ya wasemaji uwongo.

[emoji820]Epukana sana na maneno yatakayo kukaribishia na kitendo cha zinaa.

[emoji820]Mtaje Mwenyezi Mungu unapohisi fitina itakuzonga.

[emoji820]Tumia ulimi wako sana katika kumuomba Mwenyezi Mungu kwa dua za kila aina.

[emoji820]Wacha kuwasema watu kwa ubaya kumbuka wako malaika waandikao kulia na kushoto.

[emoji820]Epukana na vikao vinavyowasema watu na vichekesho visivyo na maana.

[emoji820]Epukana sana kuyachukuwa maneno ya huyu kuyapeleka kwa yule kwa kusudi ya kuwagombanisha na wala usifuate siri za watu zisizokuhusu.

[emoji820]Wacha kuuliza sana mambo yasiyokuhusu.

[emoji820]Usijibu suala kama hulijui jawabu.

[emoji820]Usibahatishe kujibu katika sheria za ALLAH kama hujuwi hukumu yake.

[emoji820]Usione aibu kusema hujuwi utakapoulizwa.

[emoji820]Epukana sana na kuwafanyia watu maskhara.

[emoji820]Wacha kuwacheka watu waliokuwa vilema.

[emoji820]Usiwafanyie mzaha waumini.

[emoji820]Waheshimu Mashekhe na watu wote kwa jumla.

[emoji820] Jiheshimu utahishimiwa.

[emoji820] Kuwa na subira utakapochekwa na wengine.

[emoji820] Usichoke kutowa nasaha njema kwa kila aliyepotea katika njia iliyo sahihi.

[emoji820]Utumie ulimi wako kwa njia yenye kheri ili kupata malipo mema Duniani na Akhera.

[emoji820]Kila muislamu amuombee muislamu mwenzanke dua nzuri ili tuoneshe mapenzi baina yetu.
Hizi ni nasaha ambazo Muislamu huweza kumpa ndugu yake.Ndugu zangu waislamu musichoke kutowa nasaha njema,
kwani huwenda neno moja likaleta athari na faida kubwa katika sikio la msikilizaji na akanufaika na nasaha hiyo.
Kila mmoja wetu awe ni mfano mzuri kwa ndugu yake, tuwache maradhi mabaya ya kuchukiana na kusemana na kuoneana choyo.
 
"Ukiona jambo lolote baya kwa hadithi sahihi ya bwana wetu Mtume Muhammad (s.a.w) fanya yafuatayo:

1. Zuia kwa mkono.
2. Kemea
3. Chukia lakini kuchukia ni udhaifu wa Imani.

Hivyo hatuwezi kukaa kimya ili hali watu wanadhalilisha dini yetu na kumtukana Mtume wetu Muhammad (S.A.W) bila kupambana nao kwa kuwa tumefunga huo ni udhaifu wa Imani kwani kinachoandikwa na hao wapotoshaji kinasomwa na wengi tukikaa kimya waweza jua ni kweli.

Dawa ya moto ni moto Malipo ya Swaumu ni moja kwa moja kutoka kwenye Arshi ya Mwenyezi Mungu anayejua nia zetu katika mambo yote. Amina.
 
بسم الله الرحمن الرحيم

الحمد لله الذي بنعمته تتم الصالحات والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين

وبعد

التوبة
Taubah

قال العلماء
Wanasema ulamaa

: التوبة واجبة من كل ذنب،

Taubah ni wajibu kwa kila dhambi

Taubah haina dhambi ambazo ndizo wajibu na dhambi za aina fulani zikawa na nafasi kwa mtendaji asitubie

فإن كانت المعصية بين العبد وبين الله j تعالي، لا تتعلق بحق آدمي؛ فلها ثلاثة شروط.

Kama yatakuwa maswiya ni baina ya mja na Allah alie tukuka yakawa hayafungamani na mwanadamu basi Taubah itakuwa na sharti Tatu

أحدها
Moja yake

: أن يقلع عن المعصية

Ajivue katika maswiya

. والثاني:mbili

أن يندم على فعلها.

Ujutie kwa kuyafanya hayo maswiya

والثالث

Tatu

: أن يعزم أن لا يعود إليها أبداً.

Aweke azma yakutokurudia na kurudi katika maswiya

فإن فقد أحد الثلاثة لم تصح توبته.

Kama litakosekana moja ya sharti hizi Tatu Taubah haita swihi

Hiyo ni kwa makosa na madhambi ambayo mwanadamu kayatenda kwa Allah na hayana mafungamano na kiumbe mwanadamu

وإن كانت المعصية تتعلق بآدمي فشروطها أربعة

Kama maswiya hayo yatakuwa yanafungamana na mwanadamu basi Taubah hapo itakuwa na masharti manne

: هذه الثلاثة
Hizi Tatu tulizo zitaja hapo juu

، وأن يبرأ من حق صاحبها،

Na Ajivue na haki ya mwenye nacho kwa kukirejesha kama kitakuwa cha kuchukulika au namna nyingine

فإن كانت مالاً او نحوه رده إليه
Kama ikiwa Mali au mfano wake atarejesha kwake (mwenye Mali)

Kama atakuwa kamsingizia uchafu wa zinaa au mfano wa uzushi mwingine wa mambo machafu ya kitabia na kimaadili atamueleza na amtake msamaha

Kama alimsengenya ambambie maneno aliyo kuwa akiyasema wakati hayupo

ويجب أن يتوب من جميع الذنب،

Na inamlazimu mtu kutubia kwa madhambi yote

. وقد تظاهرت دلائل الكتاب والسنة وإجماع الأمة على وجوب التوبة

Kwa hakika zimeenea dalili katika kitabu na suna na ijmaa ya ulamaa juu ya ulazima wa Taubah

: قال الله تعالي

Kasema Allah alie tukuka

🙂 وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعاً أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ)

Tubieni kwa Allah nyote enyi waumini mupate kufualu

(النور: من الآية31)

وقال تعالي🙂

وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ

Mumtake maghfira mola wenu kisha mtubie kwake

) (هود: من الآية3)

وقال تعالي🙂

Na Kasema Allah

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَصُوحاً) (

Enyi mlio amini Tubieni kwa Allah Taubah ya kweli

التحريم: من الآية8) .

Hizi zote ni dalili zinazo onyesha ulazima wa Taubah na nyingine nyingi

Itaendelea.........

أخوكم في الله أبو سهيل أحمد علي محمد السلفية

كن السلفيا عل الجادة

Link ya channel ni hii
منهج الأنبياء
 
Back
Top Bottom