Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

[5/27, 10:51] ‪+968 9420 2435‬: ⃣ MAMBO MUHIMU MWENYE KUFUNGA ANAPASWA AYAJUE KUHUSU SWAWM *⃣

بسم الله الرحمن الرحيم

YANAYOBATILISHA (YANAYOHARIBU) SWAWM

[emoji654] Kula na kunywa kwa makusudi. Na si kwa kusahau au kwa kulazimishwa, katika mchana wa Swawm.

[emoji654] Kujitapisha kwa makusudi. Kuwe kujitapisha huko kwa kutia kidole mdomoni au kunusa kitu kitachopelekea kutapika.

[emoji654] Mume kumuingilia Mke wake. Na pia kumkumbatia au kumchezea hadi yakamtoka manii.

[emoji654] Kujichua (kuyatoa manii) kwa makusudi ima kwa mkono au kwa kuchezewa na Mkeo au kwa njia yoyote ile. Ama manii hayo yakitoka kwa kuota (ndoto) au kutazama (bila kukusudia) basi haiharibu Swawm.

[emoji654] Kupatwa na Hedhi au Nifasi kwa Mwanamke. Hata kukiwa kutokea huko kuwa ni wakati wa kukaribia kufuturu/kufutari.

[emoji654] Mwenye kutia Niyyah ya kula wakati amefunga, kwa sharti kuwa kaazimia tendo hilo hata kama hakulitekeleza.

[emoji654] Kudhania kuwa jua lishazama Magharibi au bado hakujapambazuka (yaani haujaanza wakati wa kufunga), kisha akala akanywa au akamuingilia mke wake.

YASIYOBATILISHA (YASIYOHARIBU) SWAWM

[emoji654] Kula au kunywa kwa kusahau, kimakosa au kulazimishwa.

[emoji654] Kuingia maji ndani ya matundu ya mwili bila kukusudia, kwa mfano wakati wa kuoga.

[emoji654] Kudungwa sindano mwilini wakati wa maradhi.

[emoji654] Dawa ya maji idondoshewayo machoni.

[emoji654] Kujipulizia dawa ya asthma mdomoni (puffer au inhaler).

[emoji654] Kuoga na kujimwagia maji mwilini wakati wa joto kali.

[emoji654] Kuonja chakula kwa mpishi kwa sharti asimeze kile akionjacho.

[emoji654] Kumbusu au kumkumbatia mkeo, kwa sharti awe mtu ana uwezo wa kujizuia na kudhibiti matamanio yake.

[emoji654] Kupiga chuku (cupping), ikiwa kupiga chuku huko hakutomfanya huyo mtu adhoofike. Ingawa kuna baadhi ya 'Ulamaa wanaona kuwa haifai.

[emoji654] Haitobatilika Swawm ya mtu atakayeamka na janaba au atakayeota mchana wa Swawm akatokwa na manii.

[emoji654] Kuingia harufu ya manukato au udi puani mwake. Ingawa baadhi ya 'Ulamaa wanasema ni vizuri kujiepusha moshi usiingie hadi kufika tumboni.

[emoji654] Kupiga mswaki, kusukutua au kusafisha pua kwa kutia maji puani bila kuzidisha.

DU'AA YA KUFUTURU/KUFUTARI

Wanachuoni wa Hadiyth wanaeleza kuwa hakuna Hadiyth yoyote iliyo sahihi katika du'aa ya kufungua.

KUFUNGUA KWA TENDE AU MAJI

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((من وجد التمر فليفطر عليه ، ومن لم يجد التمر فليفطر على الماء ، فإن الماء طهور)) رواه أحمد وأبو داود والترمذي

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Atakayepata tende afuturu kwayo, na asiyepata basi afungue kwa maji, kwani maji ni twahara)) Imesimuliwa na ma-Imaam Ahmad, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy

WATU WALIORUHUSIWA KUTOFUNGA

Kufunga Ramadhaan ni Fardh kwa kila Muislam aliye baaligh, mwenye akili timamu isipokuwa kwa wale kufunga ni shida na itawaletea madhara nao ni wenye udhuru kama huu ufuatao:

[emoji654] Walio katika safari na wagonjwa ambao kufunga kwao kutawafanya wawe wagonjwa zaidi, haipendezwi kwa watu hao kufunga, lakini wakifunga Swawm yao itakubaliwa. Wakichagua au kupenda kuwa wasifunge basi ni lazima walipe siku hizo wasizofunga baada ya Ramadhwaan.

[emoji654] Wanawake walio katika hedhi na waliotoka kuzaa ambao wako katika damu ya Nifaas hawaruhusiwi kufunga, na wakifunga katika hali hii, basi Swawm yao haitokubaliwa. Nao pia ni lazima walipe kila siku walizoacha baada ya Ramadhwaan.

[emoji654] Wanawake wajawazito na wanaonyonyesha ikiwa watakhofu kuwa Swawm itawadhuru watoto wao au wenyewe, hao si lazima kufunga. Lakini ikiwa hawatofunga Ramadhwaan basi ni lazima wafunge baada ya Ramadhwaan kulipa siku zao. Na ikiwa waliacha kufunga kwa sababu tu ya kukhofia afya ya watoto wao, basi wanapaswa kulipa na kumlisha maskini mmoja kwa kila siku moja iliyowapita katika Ramadhwaan.

[emoji654] Watu wasioweza kufunga kutokana na umri mkubwa na maradhi yasiyopona hawatakiwi kufunga. Inawatosheleza kulisha maskini mmoja kwa kila siku moja wanayoshindwa kufunga. Na kila wakiweza kulisha maskini zaidi ni bora.

⃣ Maelezo yote hapo juu ni kutoka katika mkusanyiko wa fataawa mbalimbali za 'Ulamaa. *⃣

By

Mzee Mussa

[emoji390] 0659 612669
[5/28, 10:20] ‪+255 623 967 725‬: [emoji96]HUKMU YA MUISLAM ANAYE FUNGA LAKINI WAKATI HUO HUO HASWALI

[emoji184]السؤال: ما حكم الصوم مع ترك الصلاة في رمضان؟

[emoji419]Swali: Nini hukumu ya funga ya Ramadhaan ya mtu asiyeswali?

[emoji430]فأجاب الشيخ بن عثيمين رحمه الله:

[emoji430]Akajibu Shekh Ibn 'Uthaimin -Allah Amrehemu:

"إن الذي يصوم ولا يصلي لا ينفعه صيامه

"Hakika yule ambaye anafunga na wala haswali hainufaishi funga yake

ولا يُقْبَل منه ولا تبرَأ به ذمَّته.

Wala haikubaliki kwake hiyo funga na wala haimuondoi yeye kwenye dhima ya kutekeleza hiyo funga (anahesabika kuwa hajafunga)

بل إنه ليس مطالباً به مادام لا يصلي؛

Bali hakika ya hiyo funga yake haihitajiki maadam haswali

لأن الذي لا يصلي مثل اليهودي والنصراني،

Kwasababu asiyeswali ni mfano wa Myahudi na Mnaswara (mkristo)

فما رأيكم أن يهوديًّا أو نصرانيًّا صام وهو على دينه، فهل يقبل منه؟

Mnaonaje iwapo Myahudi au Mnaswara akifunga na hali yuko kwenye dini yake, je atakubaliwa funga yake?

لا. إذن نقول لهذا الشخص:

Hapana, Haiwezi kukubaliwa, kwahiyo tunasema kumwambia huyu mtu:

تب إلى الله بالصلاة وصم،

Tubia kwa Allah, kwa kuswali na kufunga.

ومَن تاب تاب الله عليه.

Na atakayetubu, Allah atamkubalia toba yake".

(من كتاب ٤٨ سؤال في الصيام للشيخ بن عثيمين رحمه الله ج١ ص١٧[emoji432])
 
ndugu zangu usiku mwema!
wakati tukisubiri daku leo tulale na neno hili la Mtume (saw)

''Anaependa kwa ajili ya Mungu akachukia kwa ajili ya Mungu, akatoa kwa ajili ya Mungu na akazuia kwa ajili ya Mungu, imekamilika imani yake"

Basi wakati tunalala leo tuifanyie fikra hii hadithi ya Mtume (saw), kwani hadithi/aya quran japo moja ukiifanyia kazi yaweza kukufaa maisha yako yote yakajaa kheri na baraka ewe ndugu yangu Muislam!
Ramadhan Kareem!
 
mkuu hayo maneno umefanya nimkumbuke Iman Petro( Mungu amrehemu)
ipo debate moja alikuwa anawapiga jamaa zetu pentagoni,kama utahitaji video nnayo ntakurushia
[emoji15] [emoji15] [emoji30] [emoji30]
Kumbe iman petro amefariki?
 
_20170528_201337.JPG

_20170528_225215.JPG

_20170528_201057.JPG
IMG_20170528_225117.jpg
IMG_20170528_201015.jpg
IMG_20170528_201012.jpg
 
Naapa kwa yule ambae nafsi yangu iko mikononi mwake, wapinzani wenu watashinda sio kwa kuwa wameshikamana na haki, isipokuwa kwa kule kuitilia nguvu batili yao na kule kuacha kwenu kushikamana na haki yenu, kawaida raia huwa wanaogopa dhulma za viongozi wao, lakini mimi nimekuwa naogopa dhulma ya raia wangu, nimekuiteni siri na dhahiri hamujaitika, nimewapa nasaha hamjakubali. (Imam Ally a.s katika Nahjulbalagha hutba no 96)
 
Asalaam Aleikum!
Tule futari kwa kiasi jamani
Japokuwa Mtume (saw) anasema kufuturu ni furaha kwa mfungaji,ila pia anatufundisha wakati wa kula tuligawe tumbo sehem 3 chakula,maji na hewa(usishindwe kupumua)
Na haswa watoto wetu hizi ndizo hadithi za kuwafundisha kipindi hiki, tusisahau tumbo ndio mama wa maradhi.
Pia baada ya adhana ni vizuri kufuturu kwa tende badala ya maji baridi,juice n.k kuna faida nyingi za kiafya unapofuturu kwanza kwa tende
What-Should-We-Use-for-Iftar.jpg

ramadan-overating.jpeg
 
Ina maana waislam tupo kdg jf ama nn?? Hii thread leo inafikia siku ya sita tangu kuanzishwa lkn haijafijafikia 1k, kuna thread zinaanzishwa hapa hazina hata faida lkn within an hour or two zinafikia hadi 2k replies.
Hebu waislam wote tusubscribe hii thread ili kila mtu akicomment tupate kusoma na kutoa maelezo tunayoyajua hapo itakuwa tushafikia lengo la hii thread.
Tufanye hivyo kwa ajili ya Allah anza kusubscribe Sasa ili sote tupate faida na yanayoletwa hapa.
Allah aalam!!
 
Tumeanza muunganisho wa Aayat-e-Karima mara 250,000,000. "LAA ILAHA ILLAA ANTA SUBHANAKA INNY KUNTU MINADWALIMEEN" kwa ajili ya amani kila mahali duniani. Soma MARA MOJA tu na uendelee kuituma kwenye anuani zako zote za Waisilam na usiache tafadha..Allah anaweza kutuzawadia sote. In Shaa Allah
 
Msione kimya wengine tunasoma tu na kuyatilia maanani.
Ukimya haumaanishi hatusomi jamn..

Me naombeni dua ya kusoma katika sala ya tahajjud na maelekezo ya kisimamo cha usiku kama rakaa ngapi,zinaswaliwaje,kama kuna sura maalum za kusoma!
 
Ndugu zangu tusisahau kua dini hii ni ya Allah, nae kamtuma mtume wetu sala na salamu ziwe juu yake ili atufundishe sisi dini yake na akamchagulia maswahaba ili atujulishe ufahamu mzuri katika mafunzo ya mtume wake. Kwahiyo usitende katika dini jambo ambalo hakulifanya mtume wala maswahaba zake hat kama Utadhani tendo hilo ni zuri kiasi gani. Na ukifanya hvyo utasalimika katika dini yako kutokana na kuzusha ambako amepasema Allah ( Sema: “Hakika mola wangu Ameharamisha machafu yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi na ukandamizaji bila ya haki, na kumshirikisha Allaah kwa ambayo Hakukiteremshia mamlaka na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”) Aaraf 33. Yule mwenye kuleta kitu kipya katika dini bila ya shaka amemsemea Allah uongo na pia amejiona yeye ni mwenye kujua kuliko Allah, na hakika Allah ameahidi kuihifadhi dini yake. Kwahiyo usimtie Allah dosari wala mtume wake kwa kuleta kitu kipya ktka dini ambacho hawa kukifundisha. Nasi tujifananishe na watu wema kwa kusema "lau kama lingekua ni kheri basi wangetutangulia kulifany". Na amesema Allah katika surat Baqara137. Basi wakiamini kama vile mlivyoamini nyinyi (Maswahaba), basi kwa yakini watakuwa wameongoka; na wakikengeuka basi hakika wao wamo katika upinzani, basi Allaah Atakutosheleza nao, Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.
Amesema imam Shafii, "nimemuamini Allah na kile kilichotoka kwake kwa makusudio yake na nimemuamini mtume wake Allah na kile alichokuja nacho mtume kwa makusudio yake mtume.

Basi ewe muislamu unataka usalama ktka dini yako???? Usizushe katika dini....
Wabillahi tawfiiq
 
MAELEZO HAYA NIMEYATOA KUTOKA KITABU CHA “MWONGOZO WA SWALA ZA USIKU”
Toka kwa Ustadh Musa Badawi
Waweza kukitafuta ili kupata faida zaidi

Waweza ukaswali mojawapo kati ya hizi 2 ambazo ni rahisi zaidi na nyepesi kuzielewa

1.Tahajud au 2.Tasbihi

1.TAHAJUDI

Inaswaliwa usiku hasa,kuanzia saa 6 na kuendelea kabla ya alfajiri,unaweza ukaswali rakaa 2 au 4 au 6 au 8 au 10 au 12
Kadri ya nguvu na nafasi yako

Nia utasema “Nawaitu Uswaliy Rakaatain Sunnat Qiyaamul layl (au Sunnat Tahajjud) Lillaah TaalaAllahu Akbar”

Rakaa ya kwanza/pili unasoma surat fatiha na sura nyingine yeyote,baada ya kumaliza rakaa 2 unatoa salaam waweza kuendelea au ukaishia tu rakaa 2

Ukishamaliza idadi utakazojaliwa unaleta tasbihi zifuatazo
“YAA RABBI YAA RABBI LUT FUKAL KHAFIYYU YAJRIY FII AMRII” *100

Kisha utamswalia Mtume saw
“ALLAHUMMASWALLI AALAANUURI RAHMAAN WAMA ADINIL MA ARIF RABBAANIYAT SAYIDINAA WAMAWLAANA MUHAMADIN WA ALAA AALIHI WASWAHBIHI WASALLAM” *100

Ukimaliza utasoma jina hili la M/Mungu kiasi unachoweza
“ALLAHU ALLAHU”

Ukimaliza utaleta istighfaar “ASTAGHFIRULLAH”*100

Kisha omba dua yoyote upumzike

2.TASBIHI

Hii huswaliwa rakaa 4,kila baada ya rakaa 2 utatoa salaam

Rakaa ya kwanza unasoma suurat Fatiha na sura nyingine yeyote baada ya hapo utasema
“SUBHAANAALLAH WALHAMDULILLAH WALAA ILAHA ILLA LLAHU WALLAHU AKBAR” *15

Utarukuu ndani ya rukuu utaleta tasbihi hiyo *10

Utanyanyuka itdali utaleta hiyo tasbihi*10

Utasujudu na kuleta hiyo tasbihi*10

Ukitoka katika sijda utakaa kidogo na kuleta tasbihi*10

Utasujudu sijda ya pili utaleta hiyo tasbihi* 10

Kisha katika kikao kidogo kabla ya kuinuka kuendelea na rakaa ya pili utaleta tena tasbihi*10

Hapo utakuwa umeleta tasbihi *75

Yatakiwa ufanye hivyo kwenye rakaa zote 4

Ukimaliza rakaa zote 4 unweza kumtaja M/Mungu kwa tamko hili
“LAA ILAAHA ILLA LLAH*100

Kisha utamswalia Mtume saw
“ALLAHUMMA SWALLIY ALAA MUHAMMAD YAA RABBI SWALLIY ALAYHI WASALIM” kiasi cha idadi utakachoweza

Kisha utaleta dua na kupumzika

3.SUNNATUL WITRI

Swala hii ya witri ni swala inayoswaliwa mwisho wa swala zako za usiku yaani ndiyo iwe hitimisho lako la swala

Huswaliwa rakaa 1 au 2 au 3 au 5 au 7 au 9 au 11
Utaswali rakaa 1 au 2-2-1 au 2-2-2-1 au 2-2-2-2-1 au 2-2-2-2-2-1

Nia unasema
“NAWAITU USWALLIY RAKAATAIN MIN SUNNATIL WITRI LILLAAHI TAALA ALAAHU AKBAR”

Katika rakaa moja ya mwisho utanuia “NAWAITU USWALLIY WAAHIDATAL WITRI LILLAHI TAALAA ALLAHU AKBAR”

Katika swala hii rakaa ya kwanza utasoma suurat Fatha na sura nyingine yeyote pia rakaa ya pili utafanya hivyo.

Hizi swala tatu TAHAJJUD TASBIH NA WITRI unaweza kuziswali zote katika usiku mmoja.
Ukaanza na Tahajud na nyiradi zake kisha ukaswali tasbihi na kumalizia na witri,ikiwa uwezo unao

Aina nyingine za ibada za usiku ni kusoma Quran na pia kumtaja Mwenyezi Mungu sana,na kumswalia Mtume saw
 
Tumeanza muunganisho wa Aayat-e-Karima mara 250,000,000. "LAA ILAHA ILLAA ANTA SUBHANAKA INNY KUNTU MINADWALIMEEN" kwa ajili ya amani kila mahali duniani. Soma MARA MOJA tu na uendelee kuituma kwenye anuani zako zote za Waisilam na usiache tafadha..Allah anaweza kutuzawadia sote. In Shaa Allah
Jazakallahu Khairan
 
Ndugu zangu tusisahau kua dini hii ni ya Allah, nae kamtuma mtume wetu sala na salamu ziwe juu yake ili atufundishe sisi dini yake na akamchagulia maswahaba ili atujulishe ufahamu mzuri katika mafunzo ya mtume wake. Kwahiyo usitende katika dini jambo ambalo hakulifanya mtume wala maswahaba zake hat kama Utadhani tendo hilo ni zuri kiasi gani. Na ukifanya hvyo utasalimika katika dini yako kutokana na kuzusha ambako amepasema Allah ( Sema: “Hakika mola wangu Ameharamisha machafu yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi na ukandamizaji bila ya haki, na kumshirikisha Allaah kwa ambayo Hakukiteremshia mamlaka na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”) Aaraf 33. Yule mwenye kuleta kitu kipya katika dini bila ya shaka amemsemea Allah uongo na pia amejiona yeye ni mwenye kujua kuliko Allah, na hakika Allah ameahidi kuihifadhi dini yake. Kwahiyo usimtie Allah dosari wala mtume wake kwa kuleta kitu kipya ktka dini ambacho hawa kukifundisha. Nasi tujifananishe na watu wema kwa kusema "lau kama lingekua ni kheri basi wangetutangulia kulifany". Na amesema Allah katika surat Baqara137. Basi wakiamini kama vile mlivyoamini nyinyi (Maswahaba), basi kwa yakini watakuwa wameongoka; na wakikengeuka basi hakika wao wamo katika upinzani, basi Allaah Atakutosheleza nao, Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.
Amesema imam Shafii, "nimemuamini Allah na kile kilichotoka kwake kwa makusudio yake na nimemuamini mtume wake Allah na kile alichokuja nacho mtume kwa makusudio yake mtume.

Basi ewe muislamu unataka usalama ktka dini yako???? Usizushe katika dini....
Wabillahi tawfiiq
Sawa mkuu
tunafanya hivi sababu ya kutafuta radhi za M/mungu,
hivyo ikiwa unaona liko jambo lolote la kupotosha ujue hakuna alieweka kwa kufahamu ni kutojua pengine hivyo ukiona jambo lolote la kupotosha usisite kutueleza
 
Back
Top Bottom