Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Jamani ndugu zangu katika imani Assalam alykum, jana kazini kulitokea upotevu wa pesa kama Million 1 na kadhaa sasa lile balaa kulikua na machaguo mawili.
1. Ningesema ukweli mimi ndo ningeonekana muhusika na hatua zingechukuliwa
2. Ningesema uongo muhusika nisingeonekana mimi
Dah japo nasikitika lakini nilidanganya ilihali nimefunga hii imekaaje dah[emoji31] [emoji31] [emoji31] [emoji24] [emoji24]
 
Jamani ndugu zangu katika imani Assalam alykum, jana kazini kulitokea upotevu wa pesa kama Million 1 na kadhaa sasa lile balaa kulikua na machaguo mawili.
1. Ningesema ukweli mimi ndo ningeonekana muhusika na hatua zingechukuliwa
2. Ningesema uongo muhusika nisingeonekana mimi
Dah japo nasikitika lakini nilidanganya ilihali nimefunga hii imekaaje dah[emoji31] [emoji31] [emoji31] [emoji24] [emoji24]
uwongo dhambi...
 
Jamani ndugu zangu katika imani Assalam alykum, jana kazini kulitokea upotevu wa pesa kama Million 1 na kadhaa sasa lile balaa kulikua na machaguo mawili.
1. Ningesema ukweli mimi ndo ningeonekana muhusika na hatua zingechukuliwa
2. Ningesema uongo muhusika nisingeonekana mimi
Dah japo nasikitika lakini nilidanganya ilihali nimefunga hii imekaaje dah[emoji31] [emoji31] [emoji31] [emoji24] [emoji24]
kama ni wewe umechukua sio vizuri rudisha
 
*HUKMU YA MUISLAM ANAYE FUNGA LAKINI WAKATI HUO HUO HASWALI*

السؤال: ما حكم الصوم مع ترك الصلاة في رمضان؟

Swali: *Nini hukumu ya funga ya Ramadhaan ya mtu asiyeswali?*

[emoji430]فأجاب الشيخ بن عثيمين رحمه الله:

*Akajibu Shekh Ibn 'Uthaimin -Allah Amrehemu:*

"إن الذي يصوم ولا يصلي لا ينفعه صيامه

*"Hakika yule ambaye anafunga na wala haswali hainufaishi funga yake*

ولا يُقْبَل منه ولا تبرَأ به ذمَّته.

*Wala haikubaliki kwake hiyo funga na wala haimuondoi yeye kwenye dhima ya kutekeleza hiyo funga (anahesabika kuwa hajafunga)*

بل إنه ليس مطالباً به مادام لا يصلي؛

*Bali hakika ya hiyo funga yake haihitajiki maadam haswali*

لأن الذي لا يصلي مثل اليهودي والنصراني،

*Kwasababu asiyeswali ni mfano wa Myahudi na Mnaswara (mkristo)*

فما رأيكم أن يهوديًّا أو نصرانيًّا صام وهو على دينه، فهل يقبل منه؟

*Mnaonaje iwapo Myahudi au Mnaswara akifunga na hali yuko kwenye dini yake, je atakubaliwa funga yake?*

لا. إذن نقول لهذا الشخص:

*Hapana, Haiwezi kukubaliwa, kwahiyo tunasema kumwambia huyu mtu:*

تب إلى الله بالصلاة وصم،

*Tubia kwa Allah, kwa kuswali na kufunga.*

ومَن تاب تاب الله عليه.

*Na atakayetubu, Allah atamkubalia toba yake".*

Niwatakieni mfungo mwema
 
*HUKMU YA MUISLAM ANAYE FUNGA LAKINI WAKATI HUO HUO HASWALI*

السؤال: ما حكم الصوم مع ترك الصلاة في رمضان؟

Swali: *Nini hukumu ya funga ya Ramadhaan ya mtu asiyeswali?*

[emoji430]فأجاب الشيخ بن عثيمين رحمه الله:

*Akajibu Shekh Ibn 'Uthaimin -Allah Amrehemu:*

"إن الذي يصوم ولا يصلي لا ينفعه صيامه

*"Hakika yule ambaye anafunga na wala haswali hainufaishi funga yake*

ولا يُقْبَل منه ولا تبرَأ به ذمَّته.

*Wala haikubaliki kwake hiyo funga na wala haimuondoi yeye kwenye dhima ya kutekeleza hiyo funga (anahesabika kuwa hajafunga)*

بل إنه ليس مطالباً به مادام لا يصلي؛

*Bali hakika ya hiyo funga yake haihitajiki maadam haswali*

لأن الذي لا يصلي مثل اليهودي والنصراني،

*Kwasababu asiyeswali ni mfano wa Myahudi na Mnaswara (mkristo)*

فما رأيكم أن يهوديًّا أو نصرانيًّا صام وهو على دينه، فهل يقبل منه؟

*Mnaonaje iwapo Myahudi au Mnaswara akifunga na hali yuko kwenye dini yake, je atakubaliwa funga yake?*

لا. إذن نقول لهذا الشخص:

*Hapana, Haiwezi kukubaliwa, kwahiyo tunasema kumwambia huyu mtu:*

تب إلى الله بالصلاة وصم،

*Tubia kwa Allah, kwa kuswali na kufunga.*

ومَن تاب تاب الله عليه.

*Na atakayetubu, Allah atamkubalia toba yake".*

Niwatakieni mfungo mwema
Masha Allah
 
Jana nilikuwa safarini nikiwa katika mabasi yetu haya ya kwenda mikoani, safari ilikuwa nzuri japo kusema kweli nilijikuta napata wakati mgumu na hiki kinachoendelea saa hivi kwenye haya mabasi. Kwanza nikiri wazi mie si muislamu lakini naelewa wahusika wanahitaji nini na wangependa kutendewaje katika mwezi huu mtukufu na wa kuwaweka karibu zaidi na Muumba

Huwa nasikia na kuona wakikumbushana kujisitiri, kujiepusha na mabaya ambayo yanaweza kuzifadhaisha nyoyo zao na kiukweli katika hili niko nao sana. Sasa nawauliza hawa wenye vyombo vya usafiri, ni kwanini hawaheshimu mwezi huu walau kwa hizi siku 30 tu? Kwanini mnawakwaza wenzetu kiasi hiki na wakati hata nyie mnaelewa ugumu wa mwezi huu, tena ajabu zaidi mnaofanya hivi wengine ni waumini na mmefunga pia.

Hivi kuwasha hivi vi video vyenu na mkaweka nyimbo za watu wakiimba nusu uchi na wengine wamevaa vibikini huku wakikata mauno ya kila aina si kuchafua mwezi huu kwa wahusika? Hivi kweli mmeshindwa kutafuta vitu vingine vyenye staha kidogo mkawaonesha abiria wenu kuliko kuwawekea huu uchafu? Binafsi nilijikuta nikiwaza peke yangu juu ya hili, nikajiuliza mbona huku mtaani watu wanazingatia na hata sie wakristu tunawajari sana hawa ndugu zetu tusiwakwaze, kwanini watu wa mabasi nao wasizingatie uhitaji huu wa ki utukufu kwa abiria wao?

Na je, ni vipi endapo mtazamaji akafanya jambo baya kwa kutokana na kumtizamisha huu uchafu? Kwanini msiwawekee muvi na nyimbo zingine zisizokuwa na mavazi ya aibu hivi ya kughafirisha nafsi za watu. Si lazima taarabu na si lazima kaswida lakini vipo vingi vya kuwawekea abiria wenu kipindi hili. Wekeni hata mikanda ya wanyama na mbuga Zetu mbona iko mingitu?

Mie kwa leo hili nimeliona, nimelifikisha na huyooooo... Nawatakia mfungo mwema ndugu zetu waislamu!
 
Kuna siku dereva alichomeka ki flash chake, kumbe kilikuwa na X nilikuwa nimekaa jirani na maza...nilinyanyuka taratibu nikaenda kumwambia dereva nishushe japo ndio safari ilikuwa inaanza yani tupo mikese tunaelekea dar, nikashuka nikapanda bus ingine, madereva wengi busara ni ndogo sana
 
Mfungo ni pamoja na kuzishinda hivyo vishawishi.

Ramadhan haimaanishi kuacha dhambi kipindi cha Mwezi Mtukufu Pekee, La Haula!.

Kama u msafi kuwa msafi kwa miezi yote na ujue ni kwa namna gani utajiepushia na vishawishi vyote kama hivyo.

Haileti maana uache kuangalia kwa mwezi huu kisha ikiisha unashabikia huo Upupu. Unajidanganya bure kabisa.
 
Naomba niongee juu ya usengenyaji

Kusengenya manake ni Kungumza maneno ambayo ikiwa atasikia au kuyaona mwenyew atakasirike hapo unakuwa umeingia kwenye kusengenyenya. Na tukumbuke adhabu ya usengenyaji ni kubwa sana kulko hata uongo japo usiombe adhabu ya mola wako.

Tujiepushe na kusengenya kwa hali yeyote ile ukisengenya huna funga kabisa utakuwa umeshinda njaaa.

epuka kusema lolote litakwenda kinyume funga mdomo wako kabisa

Aina za usegenyaji zipo tafaut katika makundi
Muonekano
mavazi
Tabia
Maisha ya kidunia

Ndugu zangu tuepuke kuwazungumzia watu wengine kama mtu anatabia inakukera yakupasa kumuendee na kumwambia kama humuwez wagize watu wake wa karibu ....
 
Unachukia watu waovu lakini wewe ni mmoja wao, unaogopa kufa kutokana na wingi wa madhambi, ukipata maradhi unabaki kulalamika, ukiwa mzima unafanya mambo ya kipuuzi, huwa unajiona bora pale unapokuwa mzima, unakata tamaa pale unapopewa mtihani, ukipewa mtihani unaomba kwa huzuni, ukipewa raha unajisahau kwa starehe, nafsi inakushinda kwa mambo ya dhana na huwezi kuishinda kwa mambo ya uhakika.(Imam Ally a.s katika Nahjulbalagha hikma no 150)
 
Asalaam Aleikum!
Tule futari kwa kiasi jamani
Japokuwa Mtume (saw) anasema kufuturu ni furaha kwa mfungaji,ila pia anatufundisha wakati wa kula tuligawe tumbo sehem 3 chakula,maji na hewa(usishindwe kupumua)
Na haswa watoto wetu hizi ndizo hadithi za kuwafundisha kipindi hiki, tusisahau tumbo ndio mama wa maradhi.
Pia baada ya adhana ni vizuri kufuturu kwa tende badala ya maji baridi,juice n.k kuna faida nyingi za kiafya unapofuturu kwanza kwa tende
View attachment 516076
View attachment 516077
2b2a45063a1b0311394d9b986ea27b1e.jpg
 
✳✅ Nikweli nabii Suleiman alikuwa na wanawake 1000..❤ 700 wake wa ndoa na 300 masuria. ..wanawake masuria (women slaves ).. ni wanawake wanaopatikana kwa vita vya jihad (holy war vita vitakatifu ).... *( kama nyara.....⏩.tazama quran.sura 70 :30. .women slaves...wanawake hawa masuria hufungi nao ndoa ...wao ni nyara na hamna idadi ya mwisho kuwamiliki na wanasilimu yaani wanakuwa waumini.....wakikataa kusilimu .yaani kuamini wanakuwa watumwa.na itabidi walipe kodi kwa nchi ya kiislam. Au nchi yawaumini . ( taifa lililokombolewa.kwa vita vitakatifu). .... Hata maswahaba walikuwa nao wanawake hawa. .ila maswahaba waliwaaacha huru .... ....mitume na manabii wa m/mwenyezi wanakuwa wana sifa nyingi tofaut na sisi. ..mfano .wanakuwa na nguvu sana.akikushika na mkono wake huwezi kujichomoa. ...wana nguvu za kiume zisizopungua wanauwezo wa kufanya kitendo cha ndoa 24 hrs continously bila kupumzika * non stop ).... Hata kidogo....wakitembea ugenini hawapotei njia. ..✳ wakipigana vita na yoyote hushinda ..mfano nabii daudi kumuua jitu kubwa sana * hefty and a giant goliath * David and goliath.... mitume wanaweza kaa bila kula kwa masiku mengi. .mfano nabii issa mathayo 4 :2 akafunga siku 40 mchana na usiku ..N .B ▶ manabii hawalali usingizi ...wanapumzisha mwili ( repose the body)...hawalali maanake huwa wanaongea na mola usingizin kwa kuoteshwa ..♎ mitume na manabii wanaweza tembea mwendo mrefu bila kuchoka. ....♦sauti yao hufika mbali kuliko yoyote ....wao huona mbali ( keen sight) kuliko yoyote ↘ mioyo yao huwa haina chuki kinyongo. .siwachoyo. .siwabahili. ..hawafanyi uovu au kuasi amri ya Allah. ...✡ hawali mpaka wasikie njaa na wakila☕ hawali wakashiba......hawapigi miayo. ....hawacheki wao hutabasamu tu. .......miili yao hunukia perfume. .♐...mitume na manabii shetani hawezi kuwapoteza wala kuwapandikiza fikra potofu. Tazama mathayo 4 5. .na quran 72 :27 na 28. ......N.B hakuna nabii wala mtume wa m/mungu alieoa mke mmoja ..aliyeoa wake wachache ni nabii Ibrahim alioa 3. .na nabii Ayub 3...na mitume Muhammad s.a.w.alioa wanawake 11. ......haya waigeni manabii oeni mitaala acheni ku-divert.(michepuko).
Daaruul ilmu Naafia...Marangu. kilimanjaro
 
منهج الأنبياء:

[emoji257]DUA YA QUNUUT[emoji257]

Qunuut kwa maelezo ya Fuqahaa (wanachuoni wa fiqh), ni du'aa inayosomwa katika Swalah katika sehemu maalum wakati mtu anapokuwa amesimama baada ya kurukuu (au kabla kwenye kauli nyingine). Na inatumika katika Swalah ya witr kwenye raka'ah ya mwisho baada ya kurukuu kwa kauli yenye nguvu.

Qunuut ni du'aa itumikayo wakati wa matatizo, majanga na maafa yanapowafika Waislam. Na wakati huo ndipo du'aa hii huombwa na huwa inaombwa katika kila Swalah na si Swalah ya alfajiri tu kamailivyozoeleka na baadhi ya watu kwa kutumia baadhi ya hadiyth ambazo hazijasihi kuhusiana na Qunuut ya kudumu (katika Swalah ya Alfajir). Du'aa hii si fardhi bali ni Mustahab, na Swalah ya mtu ni sahihi kabisa hata kama hajasoma Qunuut, na wala usiposoma Qunuut huhitaji kufanya sijdatus-sahw (sijida za kusahau) kama wanavyodhani wengine. Inapendezwa kufanywa wakati ikifikia dharura kamatulivyotaja juu. Na vilevile wakati mwingine wa kuisoma Qunuut ni wakati wa Swalah ya Witr.

Ni kinyume na Sunnah kuisoma Qunuut kwenye Swalah za asubuhi na kudumu nayo kama inavyofanywa kwani hilo halijathibiti katika hadiyth sahihi kutoka kwa Mtume (Swallah Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam).

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma du'aa hiyo wakati Maswahaba zake sabini wajuzi wa Qur-aan walipouliwa kwenye sehemu iitwayo Bi-ir Ma'uunah na Makabila ya Bani Sulaym ya Ri'il, Dhakwaan, Ussayah wakati alipowatuma kwenda kuwafundisha diniyao. Aliisoma du'aa ya Qunuut kwa muda wa mwezi mzima dhidi ya hao Wauaji. (Hadiyth ya Anas iliyopo kwenye Al Bukhaariy na Muslim).

Pia kwenye Hadiyth nyingine iliyopokelewa na Abu Hurayrah, inaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kuwaombea baadhi ya Maswahaba waliokuwa wamepotea kwa maadui, na aliomba kiasi cha mwezi kisha akaacha, na Abu Hurayrah alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwanini ameacha kuwaombea, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu,''Je,huoni kuwa washarejea?" (Al Bukhaariy na Muslim)

Hivyo, inaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma Qunuut hiyo ambayo inaitwa Qunuut an Nawaazil kwa muda ambao yale aliyokuwa akiyaomba, yamejibiwa ndipo akaacha.

Vilevile imethibiti kuwa alikuwa akiwaombea wale waliokuwa dhaifu, wananyanyaswa na maadui na kuwa chini ya wavamizi kama hali tuliyonayo leo huko Iraq, Afghanistan, Palestina, Chechnya na kwengineko.

Imepokewa pia kuwa Abu Maalik Al-Ash'ariy alisema: "Nilimuuliza baba yangu, 'Ee baba yangu, uliswali nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nyuma ya Abu Bakr, 'Umar, 'Uthmaan na 'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhum ajma'iyn). Je, walikuwa wakisoma Qunuut katika Swalah ya alfajiri?' Akajibu, Ee mwanangu, hili ni jambo jipya lililozushwa,'" (Imesimuliwa na wapokezi wote (watano) isipokuwa Abu Daawuud). Hakika muongozo mzuri na bora ni ule wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Na Qunuut inaposomwa, basi ni vizuri kusoma kwa ile shida inayoombewa kwa wakati huo; kama ni njaa au udhaifu au manyanyaso n.k., iombwe kutokana na masuala hayo, na si kusoma du'aa ile iliyozoeleka kwenye Qunuut 'Allahumma ihdiyna fiyman hadayta, wa'afina fiyman 'afayta...' Du'aa hii inawezwa kusomwa kwenye Qunuut ya witr na si kwenye Qunuut ya Nawaazil.

Na endapo utaswali nyuma ya Imaam anayesoma Qunuut katika Swalah ya Alfajiri, basi unatakiwa umfuate na Swalah yako ni sahihi, kwani kumfuata Imam ni wajibu, na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:

"Imaam amechaguliwa ili afuatwe" na akasema: "Msitofautiane na Maimaam wenu",

na pia katika Swahiyh Al-Bukhaariy amesema:

"Wanawaongoza katika Swalah; ikiwa wamepatia, (ujira) ni wenu na wao, na wakikosea, (ujira) ni wenu na (dhambi) ni zao."

Wa Allaahu A'alam

☘[emoji257]☘☘[emoji257]☘[emoji257]☘☘[emoji257]
 
Back
Top Bottom