Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Ramadhan Kareem.
IMG-20180517-WA0000.jpg
 
Assalamu alaykum warahmatullah wabarakatu

Bila shaka mpo vyema, sitozungumzia kuhusu Ramadhan ila kuna jambo moja nimeliona baada ya kupitia baadhi ya nyuzi. Jambo hilo ni kurushiana maneno makali kati ya waislamu na ndugu zetu munasaba wa Adam(wasio waislam).

Nafahamu baadhi ya majibu yao yanaleta jazba hebu tujikumbushe maisha aliyoishi mtume na watu wa kaliba hiyo. Tukitizama sira ya mtume tunaona kwamba mtume alikuwa ni mwenye subira, mkarimu tena mpole na hata akiamiliana na wasiokuwa waislamu hata kama wakimjibu kwa lugha mbaya bado mtume aliwajibu kwa kauli laini zenye hekima. Kwani kwa kuwajibu kauli mbaya wanaweza wakamtusi Mungu wa kweli pamoja na mtume pia.

Vilevile tumeitwa umma bora katika Qur'an sababu ni kukatazana mabaya na kuamrishana mema, katika hilo mtume amesema tumfikishie ijapokuwa hata aya 1kwani ndio kazi aliyopewa na Allah. Kwa hiyo kwenye baadhi ya nyuzi kama zinatumika kuelimishana kuhusu mambo ya Mungu na Mtume wake basi tusitumie lugha za maudhi kwao hata kama wakikutusi wewe wajibu kwa kauli yenye amani. Tukumbuke nabii Mussa alipotumwa kwa Fi'raouwn ambaye aliyejiita Mungu, tuangalie Allah alimwambiaje Mussa kuhusu Fi'raouwn. Alimwambia aamiliane kwa kauli laini tena yenye hekima. Sasa kwama kwa huyu kiumbe aliyejiita Mungu nabii Mussa anaambiwa atumie maneno laini tena yenye hekima. Vipi hawa wengine tusitumie maneno laini tena yenye hekima?

Mwisho kabisa Sheikh Othman Maalim alisema "Tusiwadharau wala kuwakebehi au kuwatolea maneno makali wanaokosea au wanaokujibu mbaya. Bali tuwahurumie kwani masikini ya Mungu hawajui walitendalo na tusichoke kuwapa mawaidha. Kama wakiyapa mgongo wayape kwa kukautaa kwao na Allah anatosha kuwa shahidi juu ya hilo"

Samahanini kwa maelezo marefu. Ramadhan Mubaraka.
 
Back
Top Bottom