Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Hujui chuki iko wapi ina maana hii ndio mada ya kwanza inayo husu Dini ndani ya hili jukwaa?

Je Sheria za jukwaa hili zimekataza members kuandika kuhusu dini zao?

Kaa utulie uliyo yapata ndio ulio yatafuta.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Chief

Wapuuzi kama hawa najua unajua kuishi nao, Mimi nimemalizana nae
 
NIMEACHANA NA NINYI,WAISLAM NAWAJUA AKILI ZENU,SIKU ZOTE MNAONA MNAONEWA AU KUWEKWA CHINI.

Endelezenj matusi yenu,ila mtu akiwa ana akili atajua tu uhalisia wenu kupitia uzi huu,dini imewafanya wengi wenu mmeacha utu,sikuona haja ya mtu kuniita kafiri,au nateseka,au eti nimemkera kisa swali dogo namna ile.
ANAYETAKA NIONGOKE AONGOKE YEYE KWANZA,MAANA UISLAM HALISI SIO HUU WA KUJIBU WATU SHIT NA KUJIFANYA HAMTAKI MASWALI.

HIVI WAKATOLIKI WAKIWEKA MADA ZAO,WALOKOLE,WAYAHUDI,WAHINDU,WASABATO,WOTE WAANDIKE MAMBO YAO HUMU,TUTAFIKA KWELI?.

MIMI NAJUA IPO SIKU KWELI ITAWAWEKA HURU,OTHERWISE MMEJIFUNGIA KWENYE VIFUNGO VYA KUTOULIZA MAMBO NA NDIO MAANA ILIM YA DINI MNAJUA YA JUU JUU NA UPOTOSHAJI.

HATA HIVYO,MKISHINDWA NENO,WAULIZENI WATU WA KITABU.
 
Amiin ukhty wangu

Hakika umefanya Jambo jema Sana la kutuzindua na kukaa tayar tayar Kwa mgeni wetu adhwim kabisa mwezi mtukufu wa Ramadhan...
Swadaqta yaa akhy

Ikiwa mfungaji anajizuia na yale ambayo ni halali kwake, kama kula, kunya n.k
Hivyo kujizuia na maovu na mambo ya kipuuzi, na yoote yasiyompendeza Allah, ni bora zaidi.

Lakini wengi hujisahau na kuona swaumu ni kujizui tu na yale yenye kufunguza, huku wakifanya mambo ambayo yanapoteza thamani ya funga au kuibatilisha kabisa.

Amesema Mtume wa Allah rehma na amani ziwe juu yake" Yule ambaye hataacha maneno ya uongo na kuyafanyia kazi, na ujinga, basi Allah hana haja na swaumu yake".

Na wanasema wanawachuoni hapo kwenye ujinga yanaingia pia maaswi.

نسأل الله السلامة و العافية.
 
Jazakallahu kheir Al akhy
 
Wakuu naomba kujua,hivi misikitini hapatoshi kufundisha na kukumbushana haya mambo mpaka tulete threads kidini za kuhusu kundi la watu fulani kwenye jamii yenye mchanganyiko kama jf?,

Maana hapa jf si kwa waislam tu,ni wakristo pia,naona haya yangefaa yawe maalum kwa watu wa imani husika,sasa hapa jukwaani yana umuhinu gani mambo haya?,
Msikitini hapatoshi neno la mungu ni vizuri likawekwa kila mahali na jf haikatazi hilo nimuhimu kueshimu tu sheria na taratibu thread hukiona upendezwi nayo unaachana nayo tu..
 
Amiin ukhty wangu

Hakika umefanya Jambo jema Sana la kutuzindua na kukaa tayar tayar Kwa mgeni wetu adhwim kabisa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ningependa kutahadharisha upande wa kuepukana na mambo yote ambayo ni ya kipuuzi wakati WA Ramadhani.

Wakati WA Ramadhani sio Mda wa kushinda unaangalia series au movies mchana kutwa ili Muda uende ufike wasaa WA magharibi ufuturu,huo ni upuuzi na unahatarisha funga yako na kukosa fadhila kubwa za mwezi huo.

Sio wakati WA kununua Karata na Domino na kucheza vijiweni eti Mda uende mfike magharibi na mfungue Swaumu,hakika Hilo sio kusudio la mwezi wa ramadhani.

Sio Mda WA kukaa vijiweni na kupiga soga na kusengenya watu,maana mtaongea ya kuongea mtajikuta mwisho wa siku mnaanza kusengenya,ni kujitafutia madhambi bure na kujikuta mnashinda na njaa bure bila malipo yoyote Yale.

Huo ni mwezi mmoja lakini Kwa wanao jua thamani yake na kujitenga na mambo yote ya kipuuzi hakika kwao ni kama mwaka kwasababu wanazinyima nafsi zao na Yale yote ambayo huwafanya wafurahi na kujipinda na kujitenga nayo Kwa kusudio moja Tu nalo ni kujikurubisha Kwa Allah Kwa kutaraji radhi zake na fadhila zake.

Ni Bora mchana WA Ramadhani ulale kwani utapitwa na mambo mengi ya kipuuzi kuliko kukaa vijiweni na kufanya mambo ya kipuuzi
Hii ingependeza kuwa ndio utaratibu au maisha ya kila siku na si mwezi mmoja tu.
 
Wakuu naomba kujua,hivi misikitini hapatoshi kufundisha na kukumbushana haya mambo mpaka tulete threads kidini za kuhusu kundi la watu fulani kwenye jamii yenye mchanganyiko kama jf?,

Maana hapa jf si kwa waislam tu,ni wakristo pia,naona haya yangefaa yawe maalum kwa watu wa imani husika,sasa hapa jukwaani yana umuhinu gani mambo haya?,
Kama halikufurahishi, unapita tu.
 
Kashike nyaya za umeme kama umeudhika sana
 
Shukrani KWA ujumbe murua,Allah karim aturahisishie tudiriki kikamilifu mwezi mtukufu wa Ramadhani.
 
Back
Top Bottom