Tutaulizwa Juu ya Neema Tulizopewa
Tukiwa ktk mfungo wa Ramadhani tunakumbashana maswala mbali mbali Juu ya dini yetu
Hakika tutaulizwa juu ya neema ya Uhai, Afya, familia ,kuona, kusikia na neema nyingine mbali mbali je tulimshukuru Allah? Je tulimuabudu?kama sehemu ya kuonyesha shukrani yetu kwake?
Sikia tukio hili katika hadith iliyopokelewa na Abu hurairah,,, siku moja mchana au usiku Mtume rehma na amani ziwe juu yake alitoka nje ya nyumba yake na kuwakuta Umar na Abubakar (radhiallahu anhuma ) wamekaa nje.
Akawauliza nini kilichowafanya muwe nje mda huu? Wakajibu ni njaa, Rasul nae akasema nami kilicho nitoa nje ni hicho hicho
Basi wote watatu wakaongoza wakaenda kwa ansar mmoja, hawakumkuta bali walimkuta mkewe, akawaambia huyu bwana ameenda kutuchotea maji,,, mara kidogo yule bwana akarudi akaweka ndoo yake chini na kusema, hakika hakuna jambo zuri kwa mtumwa wa Allah kama kutembelewa na Mtume wa Allah.
Basi akawaletea tende pale na kisha akaenda kuwachinjia kondoo au mbuzi, Mtume akamwambia usimchinje anayekamuliwa maziwa.
Basi wakatayarishiwa na kula chakula kile mpaka wakashiba.
Kisha Mtume rehma na amani ziwe juu yake akasema hakika mtakuja kuulizwa juu ya neema hii "kuwa mlitoka makwenu mkiwa na njaa kisha mkatayarishiwa Chakula hamkuondoka mpaka mkala na kushiba,je mlishukuru?
Ndugu zangu ebu chukua dakika kadhaa kidogo kutafakari ni neema ngapi umejaaliwa na Allah Mpaka mda huu,je unashikamana na ibada ya swala kama kuonyesha shukrani kwa Allah? Je unatoa sadaka? Je unawasaidia wenye uhitaji kama maskini na mayatima?
Ndugu katika imani Tumshukuru Allah kwa kufanya amali njema ambazo zitatuokoa siku ya kiama