Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Ndugu zangu katika imani matendo ya kiibada ambayo yanapokelewa na Allah ni yale ambayo yamefanywa tu kwa kutaka radhi zake

Je swaumu yako umeifunga kwa kuwa hapo nyumbani wote wamefunga ndio maana umefunga au umefunga kwa ajili ya Allah?

Je umefunga kwakuwa wafanyakazi wenzako wote wamefunga ndio maana nawe umefunga kwa kukwepa aibu?

Je umefunga kwakuwa mume kafunga nawe umefunga au kwakuwa mke kafunga ndio nawe kwa aibu umefunga?

Ndugu yangu katika imani ikiwa umefunga kwa ajili ya watu au mazingira uliyopo basi tambua hakika unashinda na njaa tu,hutalipwa na Allah

Hakika Allah hukubali tu matendo yanayofanywa kwa ajili yake tu

Takasa nia yako kwa kila ibada iwe ni kutoa sadaka,swala,funga au amali nyingine yoyote ile hakikisha ni kwa ajili ya kupata radhi za Allah tu

Tumche Allah ukweli wa kumcha
 
Ndugu zangu katika imani matendo ya kiibada ambayo yanapokelewa na Allah ni yale ambayo yamefanywa tu kwa kutaka radhi zake

Je swaumu yako umeifunga kwa kuwa hapo nyumbani wote wamefunga ndio maana umefunga au umefunga kwa ajili ya Allah?

Je umefunga kwakuwa wafanyakazi wenzako wote wamefunga ndio maana nawe umefunga kwa kukwepa aibu?

Je umefunga kwakuwa mume kafunga nawe umefunga au kwakuwa mke kafunga ndio nawe kwa aibu umefunga?

Ndugu yangu katika imani ikiwa umefunga kwa ajili ya watu au mazingira uliyopo basi tambua hakika unashinda na njaa tu,hutalipwa na Allah

Hakika Allah hukubali tu matendo yanayofanywa kwa ajili yake tu

Takasa nia yako kwa kila ibada iwe ni kutoa sadaka,swala,funga au amali nyingine yoyote ile hakikisha ni kwa ajili ya kupata radhi za Allah tu

Tumche Allah ukweli wa kumcha
Ukumbusho mzuri sana
 
Wenzetu maswahaba walipokuwa wanaagana baada ya mazungumzo yao,walikuwa wanapeana nasaha kwa kusomeana suratil al asir ndio kisha wanaagana

Sura hii inazungumzia kwamba hakika wanadamu wote haijalishi waislamu au wasio waislamu,kuanzia baba yetu Adamu mpaka Mtume wa mwisho Muhammad swalla lahhu alaihy wa salaam, wote wapo katika hasara

Isipokuwa wale waliomwamini Allah kwa maana Mungu mmoja, kisha wakafanya mambo mema kwa maana matendo mema,kisha wakahusiana kuhusu mambo ya haki,kwa maana haki ya kumjua Allah, kukijua kitabu cha Allah na kujua mafundisho sahihi ya mtume Muhammad

Kisha wakahusiana juu ya kusubiri,hakika subira ni ibada kubwa sana,maana uwe na subira ya kuacha maovu uliyoyazoea na uwe na subira na kudumu kufanya mambo mema,maana hakika kudumu kufanya ibada za Allah ni mtihani mkubwa sana

Hawa ndio ambao hawapo katika hasara yani wamesamilika

Je sisi tupo upande upi? Tujitathimini na kufanya yale yenye kutupa mwisho mwema
Ukumbumsho mzuri Allah akulipe, nakukubali sana maalim wewe na kaka adriz Allah awahifadhi
 
Siku ya jana nikiwa pale mloganzila nimempeleka mzee wangu katika clinic yake,katika korido za pale hospitalini nikamsikia muislamu mwenzangu anaongea na simu huku akisema " tutamuoshea hapa hapa na kumswalia kabisa huku huku"

Naam huyo ni ndugu yetu katika imani ameondoka jana katika mgongo wa ardhi,na huenda yeye na wengine kama yeye waliazima kumaliza mfungo salama lkn hakika umri wao wa kuishi duniani umefikia mwisho


Je mimi na wewe ambao tupo hai hadi leo tunajitahidi vipi kuchuma zaidi ndani ya mwezi huu,je tutafanikiwa kumaliza salama mfungo au nasi huenda ikatufika safar ya kwenda kwa mola wetu?

Tutumie kila dakika na sekunde ya uhai wetu katika mwezi huu kuchuma thawabu nyingi zaidi kwani huenda,tusiimalize ramadhani hii au ama tusikutane na ramadhani nyengine

Tumche Allah sana
Allahu akbar ukumbusho huu umenipa hamasa zaidi
 
Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake,anasema akitaka mtu daftar lake la matendo limfurahishe siku ya kiama au siku ya hesabu basi apende sana kuomba msamaha kwa kusema astaghfirullah mara kwa mara

Na ndio maana dua bora sana kudumu nayo na ambayo pia ni dhikri nzur kuifanya mwezi huu wa ramadhani ni "Allahuma innaka afuwun tuhibulah afwa fafuana"

Ewe mola wangu hakika wewe ni msamehevu na unapenda kusamehe basi nisamehe

Tumche Allah ukweli wa kumcha
Kuomba msamaha "Toba na Istighfar" ni muhimu mno ndio maana katika mambo ya kufanya mtu wakati wa kuomba dua na mtu akitaka Dua yake ikubalike kwa wepesi basi kabla ya kuomba Dua atangulize na Istighfar kwanza kwani madhambi ni kiwazo Cha mambo mengi na chanzo Cha mabalaa.

Kutilia mkazo swala hilo Mtume Mwenyewe Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake ) licha ya kusamehewa madhambi yake yote yaliyopita na yajayo lakini alikuwa akiomba Msamaha kwa Allaah zaidi ya mara 100 kwa siku , halafu sisi ambao tunakosea kila siku huenda mtu ikampita miezi hajawahi kukakaa kitako kutafakari kusuhu madhambi yake na kutubia na kuomba msamaha.

Na kuomba msamaha na kutubia ni miongoni mwa vitu anavyovioenda mno Allaah ('Azza wa Jalla) kwa mja wake kwani yeye mwenyewe amejifu kuwa msamehevu sana , mwenye huruma , mwenye Kukubali Toba kwa waja nk.

Na inapaswa tuwe tunaopa msamaha na Toba kila mara tunapokosea bila kujali ukubwa wa madhambi yetu , tumerudia mara ngapi dhambi hiyo nk .

Na iwe utaratibu wetu mara kwa mara sio tu muda ambao tunahisi tumekosea ,hapana iwe ni ada yetu sababu Inapendeza Allaah na kuonyesha Utiifu na unyenyekevu kwake Allaah subhanahu wa taa'la na huenda tukifanya madhambi bila kujua na ikawa ninkheri kwetu.
 
Screenshot_2025_0315_064254.jpg
 
Miongoni mwa mambo muhimu sana katika mwezi huu ni kuomba dua,hakika dua katika mwezi huu ni zenye kupokelewa ikiwa utaomba kwa imani na unyenyekevu mkubwa

Inasemwa hakika kipenzi cha umma Muhammad swala na salamu zimfikie alikuwa anaomba dua zake kwa unyenyekevu sana katika ramadhani

Tunapotaka msaada kwa binadamu wenzetu huwa tunaonyesha uhitaji mkubwa sana na kujieleza vizur ili wapate kushawishika kutusaidia

Je inakuwaje tunapomuomba Allah hatuonyeshi unyenyekevu mkubwa na uhitaji wa hali ya juu,yaani mtu hata kunyanyua mikono yake mbele ya Allah kuomba dua anaona uvivu,wenzetu inasemwa walikuwa wananyanyua mikono mpaka baadhi yao makwapa yanaonekana kwa kule kunyanyua mikono yao kwa kuonyesha uhitaji wao

Sisemi nawe ufanye hivyo laa,bali walau nyanyua viganja vyako vya mikono kuonyesha adabu ya kuomba dua,jidhalilishe kwa Allah na nyenyekea kwake kwani yeye ndio mfalme wa wafalme

Na kuomba dua kwa Allah ni lazima kwani inaonyesha jinsi ulivyo kiumbe dhaifu kwake na mhitaji kwani hakika yeye ndio mpaji

Hakika ni dhambi na kosa kubwa sana kwa mtu kutomuomba Allah kwani hiyo ni kibri au kiburi mbele ya Allah

Hakika Allah huchukia mno pale mja wake anapokuwa haombi dua,na anatoa ahadi ya adhabu kwa mtu ambaye anajivuna na ibada hii ya kuomuomba yeye

Kinyume na wanadamu ambao hukasirika pale wanapoombwa au kuliliwa shida mara kwa mara lkn kinyume chake Allah hupenda mno kuombwa na mja wake tena sana,na hii ni ibada kubwa sana

Mtu akiwa tajir anajitoshereza kwakuwa hela ya kula anayo,anaweza kujitibu na anapata chochote anachotaka basi hujiona hamuhitaji Allah kwa chochote,je ni wangapi wana hela na wamelala vitandani mwao,ni wangapi wana uwezo wa kula chochote lkn Allah amewapa mtihani wa maradhi na hawawezi kula chochote wanachotaka ingawa uwezo huo wanao

Hakika ibada ya kumuomba Allah ni ibada muhumu sana kwani vyote tulivyo navyo ni kwa neema yake yeye na si kwa ujanja wetu
 
Inasemwa kuna kipindi watu walimuuliza Muhammad je mola wako yupo mbali au karibu,ili tujue kama yupo mbali tuombe dua kwa sauti kubwa au kama yupo karibu basi tuombe kwa sauti ndogo

Wakati mtume Muhammad swala na salamu zimfie anatafakari swali hilo,hapo hapo Allah akamtuma Jibril alayh salaam kushusha aya hii

" Wakuulizapo waja wangu kuhusu mimi waambie nipo karibu yao,naitikia maombi yao wanaponiomba,basi waniamini,waniitikie na wawe na subira"

Kwahiyo hapo tumeona kwanza Allah amesema anasikia maombi yetu au dua zetu na anajibu,lkn akatupa masharti,kwanza tumuamini yani omba ukiwa unaamini utajibiwa na hakuna lenye kumshinda Allah,pili tumuitikie kwa maana nasi tufuate maamrisho yake anayotaka tuyafuate na sharti la tatu tuwe na subira

Cha kufurahisha zaidi ni kwamba aya hii imeshushwa au ipo sambamba na aya za swaumu,kwa mujibu wa wanazuoni ni kwamba,hii inaonyesha hakika kwamba dua hukubaliwa zaidi wakati wa swaumu au kufunga,na wakati huu ndio waja humuitikia sana Allah kwa maamrisho yake,hatusemi uongo,hatu zini,hatusengenyi na tunajiepusha na madhambi mengi sana,kwahiyo sharti la kumuitikia Allah tunalifanya

Na dua hujibiwa kwa namna tatu,kwanza Allah huenda akakujibu haraka na kupata utakacho,au akakuhifadhia hitaji lako na kukupa kipindi ambacho utakuwa na uhitaji mkubwa sana au badala ya kupata utakacho badala yake ukaepushwa na balaa kubwa sana ambalo lilikuwa likupate,utasikia mtu anasema dah nusura leo nigongwe na gari na huenda nisingekuwq hai,kumbe uliomba gari lkn Allah kwa hekima zake akajibu kwa kukuepusha na ajali mbaya

Na huenda Allah asikupe hapa duniani lkn akaja kukulipa huko akhera,kwahiyo hapo unaona kabisa Allah hapuuzi dua yako tatizo ni sisi hatujui hekima ya Allah pale tunapomuomba mambo yetu

Kikubwa tambua Allah yupo karibu yetu sana kuliko mshipa wa shingo yako,ebu jiulize mshipa upo shingoni mwako lkn yeye yupo karibu zaidi na wewe na huo mshipa upo mbali

Tumche Allah ukweli wa kumcha
 
7:55 - Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi warukao mipaka.
 
.7:56 - Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema.
 
Back
Top Bottom