Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Ndugu zangu katika imani matendo ya kiibada ambayo yanapokelewa na Allah ni yale ambayo yamefanywa tu kwa kutaka radhi zake
Je swaumu yako umeifunga kwa kuwa hapo nyumbani wote wamefunga ndio maana umefunga au umefunga kwa ajili ya Allah?
Je umefunga kwakuwa wafanyakazi wenzako wote wamefunga ndio maana nawe umefunga kwa kukwepa aibu?
Je umefunga kwakuwa mume kafunga nawe umefunga au kwakuwa mke kafunga ndio nawe kwa aibu umefunga?
Ndugu yangu katika imani ikiwa umefunga kwa ajili ya watu au mazingira uliyopo basi tambua hakika unashinda na njaa tu,hutalipwa na Allah
Hakika Allah hukubali tu matendo yanayofanywa kwa ajili yake tu
Takasa nia yako kwa kila ibada iwe ni kutoa sadaka,swala,funga au amali nyingine yoyote ile hakikisha ni kwa ajili ya kupata radhi za Allah tu
Tumche Allah ukweli wa kumcha