Ramadhani Lenny aliwezaje kucheza mpira ligi kuu akiwa na miaka 50 na yale matege?

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Huyu mchezaji alikuwa classmate wa mzee fulani mtaani,huyo mzee sasa ni mzee kweli hakosi miaka 70 shule ya msingi, Jamaa alikuwa na matege fulani hivi yanastaajabisha.

Kama ungeambiwa ni namba sita bora kuwahi kutokea hapa nchini huwezi kuamini.

Alimudu hiyo namba kwa kiwango cha juu sana akiwa Simba Sports Club na timu fulani ya uarabuni.

Kinachonishangaza ni kumudu kucheza kwa umri mrefu,miaka zaidi ya 50
 
Lenny michuano yake ya mwisho ni wakati Simba inatinga fainali ya CAF mwaka 93, mwaka 93 mpaka Sasa ni miaka 30. Inawezaje kusema Lenny alicheza akiwa na miaka 50? Pia nafasi alivyokuwa anachezea ni kiungo was Kati, kiungo maestro anazunguka uwanja mzima, Kama angekuwa na miaka 50 umri wake ungeonekana uwanjani.
 
Kazuyoshi Miura ana 51 bado anakichafua.

Some people are built different.
 
Ndio hivyo,mwamba alikuwa mtu mzima sana wakati anacheza,alikuwa na mvi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…