Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Usinunue ramani kwa mtu ambaye mkishamalizana tu kwenye malipo, anafuta namba yako jumla (ukimpigia simu baada ya siku mbili, anakuuliza nani mwenzangu). Utaingia gharama tena kutafuta mtu wa kukushauri kwenye ujenzi wakati ulishamuungisha mtu kununua ramani kwake
 
Offer ya msimu huu wa sikukuu na mwaka mpya, gharama ya site visit (kutembelea site) ni Tsh 20,000/= tu ambapo utapata muda wa kutosha kupata ushauri, lakini pia kama huna uhakika na vipimo vya kiwanja chako tutahakikisha kwa kutumia futi kamba kufuata mipaka ya hicho kiwanja.
Offer hii ni ya muda mfupi, kwa sababu kazi nyingi zimesimama kwa muda ili watu wapate muda wa maandalizi ya sikukuu na kujichanga kwa ajili ya mwakani panapo majaaliwa
 
Slope ya paa ni moja ya factors zinazopelekea bati kuoza haraka, slope ya paa inapokuwa ndogo kupitiliza itafanya bati lichukue muda mrefu kukauka pindi mvua inaponyesha

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kwa hiyo slope inatakiwa minimum angle degrees ngapi?
 
Uzito wa paa huwa unabebwa na mbao za tie beam kabla ya kupokewa na mbao za wall plate na kwenda kwenye kuta, kama mfuko unaruhusu mbao za tie beam tumia mbao za 2×6 badala ya 2×4

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Moja ya kazi za p-trap pamoja na gelly trap ni kuzuia gesi/harufu isiweze kurudi ndani kutokea kwenye karo. Kama choo chako kinarudisha harufu ndani, basi inawezekana kuna leakage kati ya maungio ya trap na bomba au trap haikusetiwa vizuri.

Alternatively, unaweza ukaweka bomba kwa nje (vent pipe) ambalo utalielekeza juu kwa kuunga na T-elbow katika kipande cha bomba kinachounganisha trap na chemba. Juu ya hilo bomba weka ule mfuniko wenye matundu pembeni ili maji ya mvua yasiwe yanaingia

Ramani, Makadirio, Ushauri tuwasiliane
 
Matundu utakayoyaacha kwenye msingi kwa ajili ya udongo/kifusi kupumua usisahau kuweka wavu wa waya wenye vitundu vidogo vidogo kama yale machujio ya kuchujia tui la nazi ili wadudu kama nyoka, tandu, Nge n.k wasipageuze kuwa makazi

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Unaweza ukapata msimamizi wa ujenzi ambaye hana mbinu zozote za kupunguza gharama za ujenzi ambazo zinaweza kuepukika ukajikuta unaingia gharama zaidi

Nilikuwa site moja, boss alikuwa tayari ameshamuagiza mtu wa kwenda kununua gympsum powder kwa ajili ya kusetia jengo, eneo lile lilikuwa lina udongo mweusi kama udongo wa mbugani na tayari mchanga ulikuwa umeshaletwa na ni ule mchanga mweupe kama wa mtoni (kama chumvi), nikamuambia boss ampigie simu huyo fundi aliyemuagiza arudi kama bado atakuwa hajafika.

Baada ya kufanya setting out, nikaawambia mafundi watumie mchanga ule ule kuweka mark za msingi (Boss akacheka sana, akasema kumbe unaweza ukawa una silaha kiunoni na usijue namna ya kuitumia)
 
Wapo wanaokwepa hatua ya skimming wakidhani kwamba wanapunguza gharama, mtu amemaliza kupiga ripu (plaster) halafu anapiga rangi. Ukuta ambao haujafanyiwa skimming, ukipaka rangi juu yake rangi nyingi inafyozwa na ukuta na hautakuwa na muonekano mzuri ukilinganisha na ukuta uliofanyiwa skimming kisha ukapakwa rangi
 
Mkuu nimejenga eneo ambalo lina magadi sana sasa baada ya kupiga plasta unyevu ma magadi unapanda sana na unapelekea rangi kubanduka
Nifanye nini kudhibiti hili?
 
Mkuu nimejenga eneo ambalo lina magadi sana sasa baada ya kupiga plasta unyevu ma magadi unapanda sana na unapelekea rangi kubanduka
Nifanye nini kudhibiti hili?
Bila shaka hukuweka ile nailoni (DPC na DPM) kabla ya kumwaga jamvi, hili pia limechangia kuongezeka kwa hilo tatizo

Kwa sehemu zenye asili ya maji maji kama hizo huwa tunashauri utumie mawe magumu ktk ujenzi wa msingi kwa sababu mawe huwa hayaathiriwi na maji/chumvi (hayana tabia ya kufyonza maji kama ilivyo kwa tofali)

Ulitumia rangi gani, ya kawaida au wheather gurad?
 
Back
Top Bottom