Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Katika ujenzi, maji utakayotumia kujengea inatakiwa uwe unaweza kuyanywa...uwepo wa madini mbali mbali kama chumvi n.k unaathiri chemical reaction ya cement na maji (hydration reaction) hivyo inapunguza nguvu ya cement katika mortar/zege
 
Ili kuzuia maji yasitambae chini ya slab, ni muhimu kuweka hako kamkato kwenye picha(kanaitwa drip groove). Mfano mzuri ukipita kwenye daraja la Kimara, angalia chini ya slab utaona wameweka huo mkato, lengo ni kufanya maji yasiwe yanatambaa chini ya slab, yadondoke chini mwanzoni mwa edge za slab

 
Aina ya mchanga utakaoutumia katika shughuli za ujenzi unaweza ukachangia kuongezesha kwa gharama za ujenzi, mchanga wenye vumbi jingi sio mzuri katika ujenzi, unafanya saruji itumike kwa kiasi kikubwa kutengeneza muunganikano mzuri. Mchanga mzuri ni ule mchanga wa mtoni, ambapo vumbi huzama chini ya maji na kuacha punje punje za mchanga zikae juu
 
Mbona kuna mafundi wengine wanajenga bila hiyo micholo na kazi zinakuwa nzuri! Huwa mkianzaga na 3D zenu, af uharisia unakuwa tofauti,ndo nachekaga. Labda ghorofa, ila nyumba ya kuishi ya kawaida!?
 
Mbona kuna mafundi wengine wanajenga bila hiyo micholo na kazi zinakuwa nzuri! Huwa mkianzaga na 3D zenu, af uharisia unakuwa tofauti,ndo nachekaga. Labda ghorofa, ila nyumba ya kuishi ya kawaida!?
Maisha yana machaguo mengi, usilazimishe chaguo lako liwe chaguo kwa watu wengine...mimi sijamlazimisha mtu anunue ramani, akiona kuna umuhimu wa kufanya hivyo atakuja na akiona hakuna umuhimu pia ni sawa. Sasa sijui concern yako hasa ni nini, maana hapa nimebase sana kwenye kutoa elimu kuliko kufanya hiyo biashara ya ramani lakini bado mnanipiga vita...wahenga walisemaga penye riziki hapakosi fitina, kamwe huwezi zuia riziki ya mtu kwa kuwa atoae riziki ni Mungu na sio huyo anayelipia ramani
 
Moja kati ya sababu nyingi zinazosababisha nyufa katika msingi ni pamoja na uwepo wa miti karibu na jengo, unaweza ukajenga msingi mzuri lakini mizizi ya miti ya jirani yako ikawa inakuathiri bila wewe mwenyewe kujua chanzo cha tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…