Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #341
Hiyo sasa inafanywa chini kabisa kabla ya kulaza tofali za msingi, linamwagwa zege (blinding) kuzunguka msingi wote ambalo linakuwa na nondo zinazosukwa kama nondo za jamvi (slab) ili kuzuia hiyo mipasuko ya chini isiathiri msingiinasaidiaje nyufa kwa maeneo yenye ardhi ya kupasuka (ardhi inachanika chanika kipindi cha jua)
Asante kwa elimu,natamani ningekufahamu mapema ungenisaidia sanaBaada ya kufunga na kumwaga mkanda wa juu, pandisha kozi tatu badala ya mbili kama wengi wanavyofanya. Kumbuka ule mlalo wa bati (overhang) utaificha kozi moja (au na zaidi) na hivyo itabaki kozi moja inayoonekana ambapo nyumba itaonekana kama imemezwa na paa. Ukiweka kozi 3, nyumba itapendeza zaidi na pia itafanya hata taa za nje zikae vizuri bila shida
Tena izo bati nyeupe za alaf tumia G28. Ziko vzr mnoo.Mkuu
Kuna apartments zinatakiwa kuezekwa
Sasa Kuna fundi kanishauri ili kuokoa gharama pamoja na ubora niezekee bati ya Alaf nyeupe halafu nipake PVA ya plascon au kiboko...kuliko kuezeka bati nyingine ya rangi
Ushauri wako wa kitalaamu tafadhali
ili liwe imara izo nondo zinatakiwa ziwe ngapi pale chiniHiyo sasa inafanywa chini kabisa kabla ya kulaza tofali za msingi, linamwagwa zege (blinding) kuzunguka msingi wote ambalo linakuwa na nondo zinazosukwa kama nondo za jamvi (slab) ili kuzuia hiyo mipasuko ya chini isiathiri msingi
Noted boss wangu asanteTena izo bati nyeupe za alaf tumia G28. Ziko vzr mnoo.
Mininum nondo 4 kwa zile ndefu ambapo utaziweka katika spacing ya 15cm or less kutegemeeana na upana wa msingi uliochimba (kawaida upana ni futi moja na nusu sawa na 45cm)ili liwe imara izo nondo zinatakiwa ziwe ngapi pale chini
Bro,Mzigo unaobebwa na mkanda huwa unatawanywa sawa sawa kutokea katikati na kuupeleka pembeni, yaani mfano kama mkanda una mita 4 basi uzito uliobebwa na nusu ya huo mkanda (mita 2) unapelekwa kushoto, na uzito wa nusu iliyobaki unapelekwa kulia.
Katika makutano yoyote ya kuta, kunakuwa na mkusanyiko wa uzito kutokea kati kati ya hizo kuta zinazounda hiyo kona kwa hivyo ni muhimu sana kuweka nguzo katika kona ili kuongeza uimara zaidi kwa sababu ndipo mahali ambapo mzigo mkubwa unapokelewa ili kuupeleka ardhini (japo wakati mwingine mkusanyiko huo wa uzito unaweza ukabebwa na tofali tu bila shida yoyote lakini ukiweka nguzo inakuwa imara zaidi)
Kozi 4 mwisho stop, wait till next day ready constructed courses will hv gained maxi strength to bear on next loaded courses. From this point hakikisha una cure hizo kozi vizuri siku Saba na zaidi guysKatika ujenzi wa kuta, kitaalam inatakiwa usizidishe kozi 6 kwa siku ili kuruhusu kozi za chini zianze kukomaa kabla kozi za juu hazijajengwa juu yake
Bado 4 ipo katika range ya 1 mpaka 6. Katika ujenzi muda ni mali sana, ndio maana hata kwenye ujenzi wa maghorofa huwezi ukakuta watu wanasubiri zege ikae siku 28 ndipo waendelee na ujenzi kwa hatua inayofata.Kozi 4 mwisho stop, wait till next day ready constructed courses will hv gained maxi strength to bear on next loaded courses. From this point hakikisha una cure hizo kozi vizuri siku Saba na zaidi guys
Nashukuru sana ndg, mimi hicho kipaji cha kufundisha mtu mpaka akaelewa ninacho tangu muda. Ilikuwa mfano kama nimekosa kipindi, basi aliyehudhuria kipindi anakuja kunifundisha mimi halafu baada ya hapo ananiomba discussion ya hicho alichonifundisha ili aelewe zaidi. Tupo pamoja mkuuBro,
Nje ya mada, naweza kufahamu wewe halisi ulivyo? Yaani hua nakusomaga mpaka Facebook uko kwa username ya jina hili hili, unatema madini sana.
Naweza kukukadiria kua ukiacha Ufundi-kipaji pia una Ufundi-elimu. Na hua unajibu very technical na in details kiasi cha kwamba unaelewa unachojibu.
Wewe ni aina ya watu ambao ki uhalisia walipaswa kua Walimu sababu hufundisha na kuelezea zile key points ambazo unajua mtu akizielewa hizo basi anakua ameelewa swala husika.
Wewe unaelezea kitu na technicalities zake, kwamba hata anaekusoma au kufundishwa na wewe anakua anaelewa haraka zaidi. Kuna vitu viko hivyo vilivyo sababu ya vitu vingine, vyote hivi wewe huelezea.
Maua yako chukua Mkuu, uko vizur sana kwenye kuelewa, na kuelewesha pia.
Naanza na hiyo nyufa ambayo haijapigwa plasterYaan mimi nyufa zangu zinaanzia juu kushuka chini
Hii ni nini shida yani kila mwezi nyufa tuuuView attachment 2924280View attachment 2924279
Mafundi wa mtaani siku hizi wanatuambia tutumie cement ku-skim.Katika kuta za nje ni vizuri ukatumia white skim wall putty badala ya gympsum powder kama wengi wanavyofanya. Wall putty unatumia maji tu kuchanganyia, lakini white cement unatumia rangi kuchanganyia
Duh!! Hii nimeipenda. Sasa kwa sisi ambao tulishamaliza nyumba na tunaishi inawezekana kupandisha tofali tukajenge huo ukuta wa hapo kibarazani?Moja ya aspects za building design ni pamoja na usalama, hakutakiwi nje kuwe na access yoyote ya kuingia ndani bila kuingilia mlangoni. Wezi mara nyingi wanaposhindwa kuingilia mlangoni, huwa wanatoboa dari la kwenye kibaraza na kutambaa juu kwa juu (kwenye dari) na kuingia ndani hivyo inashauriwa kuta za juu zinazozunguka kibaraza ziende mpaka juu kabisa kugusana na bati ili ikitokea mwizi ametoboa dari nje ashindwe kuingia ndani mpaka avunje ukuta
Ni ngumu kumzuia mwizi lakini inabidi utengeneze mazingira yatakayomfanya mwizi atumie muda mwingi zaidi kuweza kufanya tukio, hii itamfanya asitishe zoezi lake la kuiba kwa kuhofia kukamatwa
Kwa mahitaji ya ramani za kitaalam zinazozingatia aspects zote za usanifu majengo tuwasiliane
Hapo labda ufumue dari kwanza, upandishe hizo kozi halafu ndio urudishie. Jirani yetu mmoja aliibiwa kupitia njia hii, watu wamechana dari ya kwenye kibaraza wakatambaa juu kwa juu wakaiba vitu. Ilikuwa ni fremu za kupangisha, wezi wamepitia frem zote huko huko ndani kwa ndaniDuh!! Hii nimeipenda. Sasa kwa sisi ambao tulishamaliza nyumba na tunaishi inawezekana kupandisha tofali tukajenge huo ukuta wa hapo kibarazani?