Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ni vyema katika chumba ukaweka two way switch karibu na kitanda ili mtu akitaka kuzima/kuwasha taa asilazimike kuamka kitandani na kwenda kuwasha/kuzima taa katika switch ya mlangoni, mtu awe anaweza kuzima/kuwasha taa akiwa hapo hapo kitandani.
 
Usiuamini sana mlango wa mbao, kwa kuwa hata hicho kitasa mtu akitaka kuiba anaweza kuja na screw driver (star) yake akafungua hizo screw. Milango yote ya kuingilia ndani (sebleni na jikoni) jitahidi uweke na milango ya grill (mageti) ambapo ukitoka utaweza kufunga komeo kwa ndani kwa kufuli. Jiongezee usalama mwenyewe, maana siku wakikuotea hasara yake watakayokuingiza ni kubwa kuliko hiyo gharama ya kujiongezea usalama
 
Ni muhimu sana kuacha matundu katika kuta za msingi ili kuruhusu ardhi ipumue na kuzuia nyufa zitokanazo na joto kali lililopo chini ya ardhi. Matundu yasiwekwe katika usawa mmoja, weka katika level mbili yaani chini na juu katika kila umbali wa mita moja mpaka mita moja na nusu kati ya tundu na tundu kuzunguka kuta. Kwa kuwa joto huwa linaongezeka zaidi kadri unavyoenda chini, basi weka matundu mawili chini, tundu moja juu kwa kufatana kuzunguka kuta
Ungeweka picha mkuu ingesaidia sana.
 
Kabisa kabisa, hiyo ni kwa sababu ya zile kemikali za sabuni, body wash n.k....maji ya bafuni inatakiwa yaelekezwe moja kwa moja ktk shimo la duara (soak way pit) bila kupitia ktk shimo la mstatili (septic tank)
Je inewezekana uka-interchange, kazi ya soak way pit ikafanywa na septic tank? au kwanini yanamaumbo tofauti kitaalanu? yakiwa duara yote au mstatili yote uchakataji utakuaje?
 
Bro,
Nje ya mada, naweza kufahamu wewe halisi ulivyo? Yaani hua nakusomaga mpaka Facebook uko kwa username ya jina hili hili, unatema madini sana.

Naweza kukukadiria kua ukiacha Ufundi-kipaji pia una Ufundi-elimu. Na hua unajibu very technical na in details kiasi cha kwamba unaelewa unachojibu.

Wewe ni aina ya watu ambao ki uhalisia walipaswa kua Walimu sababu hufundisha na kuelezea zile key points ambazo unajua mtu akizielewa hizo basi anakua ameelewa swala husika.

Wewe unaelezea kitu na technicalities zake, kwamba hata anaekusoma au kufundishwa na wewe anakua anaelewa haraka zaidi. Kuna vitu viko hivyo vilivyo sababu ya vitu vingine, vyote hivi wewe huelezea.

Maua yako chukua Mkuu, uko vizur sana kwenye kuelewa, na kuelewesha pia.
Jamaa hana tofauti na Chief-Mkwawa
 
Je inewezekana uka-interchange, kazi ya soak way pit ikafanywa na septic tank? au kwanini yanamaumbo tofauti kitaalanu? yakiwa duara yote au mstatili yote uchakataji utakuaje?
Soak way pit tunaliweka ktk umbo la duara ili kufanya pressure ya maji katika point yoyote katika kuta iwe sawa (urefu kutoka kati kati (center) kwenda kwenye point yoyote katika kuta ni sawa (radius)) hivyo inafanya pressure iwe distributed equally from the center.
 
Namna nzuri ya kuweka box zako za switch/socket kabla ya kupiga plaster ni kuanza kuweka timanzi kwanza, baada ya hapo unafunga kamba katika misumari kwa kufuata timanzi ambapo box zako zitakuwa zinafuata hiyo kamba (baadae ukija kupiga plaster, plaster inaflash vizuri kabisa na box zako). Ukiona hilo zoezi ni gumu, basi toa nje box zako japo kwa sentimita moja kutokea ukutani

Wengine huwa wanaanza kupiga plaster kwanza then ndio wanachana kuta ili kuweka bomba na hizo box ili kupata kazi inayovutia zaidi, na hata ukija kufunga switch/socket zako switch/socket zako zinakaza vizuri kwenye hizo box

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane +255(0)624068809
 
Soak way pit tunaliweka ktk umbo la duara ili kufanya pressure ya maji katika point yoyote katika kuta iwe sawa (urefu kutoka kati kati (center) kwenda kwenye point yoyote katika kuta ni sawa (radius)) hivyo inafanya pressure iwe distributed equally from the center.
Pressure ikiwa sawa inasaidia nini? yakiwa yote ya duara, au mraba kutakua na madhara gani?
 
Kama huna ujuzi na mambo ya ujenzi, ni vizuri ukamshirikisha mtaalam katika kila hatua ya ujenzi unayoiendea.

Hii inatakiwa uifanye kuanzia mwanzoni kabisa, watu wengi wanauziwa viwanja vidogo kwa sababu hawana ujuzi na mambo ya vipimo. Unakuta mtu ana malengo ya kutaka kujenga nyumba ya vyumba vinne lakini kiwanja alichonunua unakuta ni futi 40 kwa futi 40

Hapo nimezungumzia upande wa vipimo, lakini kuna vitu vingine vya kuangalia kabla ya kununua hicho kiwanja mfano aina ya udongo n.k

Hatua kama hizi ni vyema ukatafuta mtaalam ukaambatana nae kwenda site ambapo inaweza ikakusaidia kwa kiasi kikubwa. Katika uuzaji wa viwanja, wauzaji wengi wanapenda kutumia kizio cha futi badala ya mita kwa sababu upande wa futi inaonekana kama kiwanja ni kikubwa (kwa asiyejua). Mfano kiwanja cha futi 40 kwa futi 40 ni sawa na kiwanja cha mita 12 kwa mita 12

Karibuni kwa ramani, makadirio na ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaaaan

Yaaan nilifanya makosa mengi sana katika ujenzi, Mungu akinijalia uzima na pesa nyingine basi nyumba ya pili nitajitahidi Sana kushirikiana wataalam.
 
Yaaaan

Yaaan nilifanya makosa mengi sana katika ujenzi, Mungu akinijalia uzima na pesa nyingine basi nyumba ya pili nitajitahidi Sana kushirikiana wataalam.
Watu wanafikri kumtumia mtaalam ni mpaka mtaalam afike eneo la tukio, hapo ndio watu wanapoogopa gharama. We nunua ramani kwa mtu ambaye ni mtaalam wa mambo ya ujenzi ili kutengeneza ujamaa wa kumtumia kama mshauri ktk kipindi chako chote cha ujenzi
 
Katika ufungaji wa bomba za umeme, sio lazima njia zote zitokeee juu ya distribution board, njia zingine mfano njia za socket unaweza ukazitolea chini ili kupunguza idadi ya bomba
 
Kila mafundi wana namna yao ya kuiba material, ambapo kama mtu sio mtaalam wa mambo ya ujenzi huwezi kuelewa kama umeibiwa. Mfano mafundi umeme wengi hupendelea kuweka main switch karibu na jikoni ili watumie waya kidogo ktk circuit ya cooker, utakaobaki wanaondoka nao(sio wote lakini)..kwenye quotation unaweza ukaandikiwa waya wa mita 10 au na zaidi, lakini kwenye matumizi ukatumika waya mita 3 tu.

Kwenye circuit ya cooker, huwa tunatumia waya wa 4mm² ambao ni ghali na huwa inanunuliwa kwa mita, waya mwingine ambao ni ghali ni ule unaotoka kwenye main switch kwenda kwenye bracket ya tanesco, hapa unatumika waya wa 10mm² ambao mita moja ni around 9,000..ukinunua mita 10 tu, tayari inagonga laki moja kasoro

Kama hamtaki kutumia washauri, mtaendelea kupoteza pesa nyingi ambazo zinazidi hata ile ambayo ungemlipa mshauri
 
Hakikisha round box zako unazifunga vizuri mifuniko yake ili hata Panya wasiweze kula nyaya na kusababisha shoti ambayo inaweza kupelekea hata moto kutokea.
 
Plaster nzuri ni ile ambayo ukimwagia ukuta maji, ukuta unakauka bila kuchora alama za matofali. Kiujumla michoro ya tofali katika ukuta uliopigwa plaster hutokea pale ratio ya udongo uliotumika kujengea tofali ni kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kupigia plaster

Kitaalam udongo wa kujengea tofali tunatumia ratio ya 1:6 na udongo wa kupigia plaster tunatumia ratio ya 1:4 na 1:5 (ratio ya 1:4 inatumika kwenye kuta upande wa nje, na 1:5 upande wa ndani)

Ratio ya plaster inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kujengea

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
Yan Ratio inayoshikilia tofauti iwe ndogo kuliko ratio ya plasta....?kweli
 
Yan Ratio inayoshikilia tofauti iwe ndogo kuliko ratio ya plasta....?kweli
Bro unahangaika sana kutafuta umaarufu, na kwa bahati mbaya nyuzi zako zinakosa attention kwa wasomaji. Unaanzisha nyuzi kila lisaa na bado watu hawakuzingatii, lengo lako hasa ni kutafuta umaarufu

Najua umekuja na humu baada ya kuona humu kuna views nyingi, sasa mimi sio mtu wa ligi...we kwa akili ya kawaida, kati ya plaster na hiyo mortar inayounga tofali ni kipi kinamfunika mwenzake?

Na kama ratio ya mortar ya kujengea tofali inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya plaster, hiyo plaster unapiga ya kazi gani? Yani ni sawa na kumuweka Paka ili amlinde Simba

20240331_200408.jpg
 
nimeuliza swali moja tu ambalo nilihitaji ufafanuzi simple coz hamna mtu anayejua kila kitu, and unaongelea vitu ambavyo hata havihusiani duh...

Napost kila napokuwa na mda ,coz yapo mengi ya kuwajuza watu....

Kumbe wanifuatilia,sasa si tayari nishapata umaarufu au...
Anyway bro mimi huwa siyo mtu wa hivyo am doing out of passion,kama umekwazika aya.
 
Bro unahangaika sana kutafuta umaarufu, na kwa bahati mbaya nyuzi zako zinakosa attention kwa wasomaji. Unaanzisha nyuzi kila lisaa na bado watu hawakuzingatii, lengo lako hasa ni kutafuta umaarufu

Najua umekuja na humu baada ya kuona humu kuna views nyingi, sasa mimi sio mtu wa ligi...we kwa akili ya kawaida, kati ya plaster na hiyo mortar inayounga tofali ni kipi kinamfunika mwenzake?

Na kama ratio ya mortar ya kujengea tofali inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya plaster, hiyo plaster unapiga ya kazi gani? Yani ni sawa na kumuweka Paka ili amlinde Simba

View attachment 2950235
Aya turudi kwenye swali la msingi...
Fafanua vizuri ratio ya mortar kuwa kali kuliko plaster inaathiri vipi na kwa namna gani hiyo process hutokea?

Weka hata na ushahidi wa kitabu hata kimoja,,
Usiogope challenge,embrace it.
 
Back
Top Bottom