Kama huna ujuzi na mambo ya ujenzi, ni vizuri ukamshirikisha mtaalam katika kila hatua ya ujenzi unayoiendea.
Hii inatakiwa uifanye kuanzia mwanzoni kabisa, watu wengi wanauziwa viwanja vidogo kwa sababu hawana ujuzi na mambo ya vipimo. Unakuta mtu ana malengo ya kutaka kujenga nyumba ya vyumba vinne lakini kiwanja alichonunua unakuta ni futi 40 kwa futi 40
Hapo nimezungumzia upande wa vipimo, lakini kuna vitu vingine vya kuangalia kabla ya kununua hicho kiwanja mfano aina ya udongo n.k
Hatua kama hizi ni vyema ukatafuta mtaalam ukaambatana nae kwenda site ambapo inaweza ikakusaidia kwa kiasi kikubwa. Katika uuzaji wa viwanja, wauzaji wengi wanapenda kutumia kizio cha futi badala ya mita kwa sababu upande wa futi inaonekana kama kiwanja ni kikubwa (kwa asiyejua). Mfano kiwanja cha futi 40 kwa futi 40 ni sawa na kiwanja cha mita 12 kwa mita 12
Karibuni kwa ramani, makadirio na ushauri
Sent using
Jamii Forums mobile app