Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #401
Ungeweka picha mkuu ingesaidia sana.Ni muhimu sana kuacha matundu katika kuta za msingi ili kuruhusu ardhi ipumue na kuzuia nyufa zitokanazo na joto kali lililopo chini ya ardhi. Matundu yasiwekwe katika usawa mmoja, weka katika level mbili yaani chini na juu katika kila umbali wa mita moja mpaka mita moja na nusu kati ya tundu na tundu kuzunguka kuta. Kwa kuwa joto huwa linaongezeka zaidi kadri unavyoenda chini, basi weka matundu mawili chini, tundu moja juu kwa kufatana kuzunguka kuta
Je inewezekana uka-interchange, kazi ya soak way pit ikafanywa na septic tank? au kwanini yanamaumbo tofauti kitaalanu? yakiwa duara yote au mstatili yote uchakataji utakuaje?Kabisa kabisa, hiyo ni kwa sababu ya zile kemikali za sabuni, body wash n.k....maji ya bafuni inatakiwa yaelekezwe moja kwa moja ktk shimo la duara (soak way pit) bila kupitia ktk shimo la mstatili (septic tank)
Jamaa hana tofauti na Chief-MkwawaBro,
Nje ya mada, naweza kufahamu wewe halisi ulivyo? Yaani hua nakusomaga mpaka Facebook uko kwa username ya jina hili hili, unatema madini sana.
Naweza kukukadiria kua ukiacha Ufundi-kipaji pia una Ufundi-elimu. Na hua unajibu very technical na in details kiasi cha kwamba unaelewa unachojibu.
Wewe ni aina ya watu ambao ki uhalisia walipaswa kua Walimu sababu hufundisha na kuelezea zile key points ambazo unajua mtu akizielewa hizo basi anakua ameelewa swala husika.
Wewe unaelezea kitu na technicalities zake, kwamba hata anaekusoma au kufundishwa na wewe anakua anaelewa haraka zaidi. Kuna vitu viko hivyo vilivyo sababu ya vitu vingine, vyote hivi wewe huelezea.
Maua yako chukua Mkuu, uko vizur sana kwenye kuelewa, na kuelewesha pia.
Soak way pit tunaliweka ktk umbo la duara ili kufanya pressure ya maji katika point yoyote katika kuta iwe sawa (urefu kutoka kati kati (center) kwenda kwenye point yoyote katika kuta ni sawa (radius)) hivyo inafanya pressure iwe distributed equally from the center.Je inewezekana uka-interchange, kazi ya soak way pit ikafanywa na septic tank? au kwanini yanamaumbo tofauti kitaalanu? yakiwa duara yote au mstatili yote uchakataji utakuaje?
Pressure ikiwa sawa inasaidia nini? yakiwa yote ya duara, au mraba kutakua na madhara gani?Soak way pit tunaliweka ktk umbo la duara ili kufanya pressure ya maji katika point yoyote katika kuta iwe sawa (urefu kutoka kati kati (center) kwenda kwenye point yoyote katika kuta ni sawa (radius)) hivyo inafanya pressure iwe distributed equally from the center.
Tuwasiliane ndgNahitaji ramani ya 2 apartments under 1 roof
Kila apartment itakuwa na room 2 self + dinning+ living room+ kitchen+ a public toilet
: Roofing= Bati la kuficha
YaaaanKama huna ujuzi na mambo ya ujenzi, ni vizuri ukamshirikisha mtaalam katika kila hatua ya ujenzi unayoiendea.
Hii inatakiwa uifanye kuanzia mwanzoni kabisa, watu wengi wanauziwa viwanja vidogo kwa sababu hawana ujuzi na mambo ya vipimo. Unakuta mtu ana malengo ya kutaka kujenga nyumba ya vyumba vinne lakini kiwanja alichonunua unakuta ni futi 40 kwa futi 40
Hapo nimezungumzia upande wa vipimo, lakini kuna vitu vingine vya kuangalia kabla ya kununua hicho kiwanja mfano aina ya udongo n.k
Hatua kama hizi ni vyema ukatafuta mtaalam ukaambatana nae kwenda site ambapo inaweza ikakusaidia kwa kiasi kikubwa. Katika uuzaji wa viwanja, wauzaji wengi wanapenda kutumia kizio cha futi badala ya mita kwa sababu upande wa futi inaonekana kama kiwanja ni kikubwa (kwa asiyejua). Mfano kiwanja cha futi 40 kwa futi 40 ni sawa na kiwanja cha mita 12 kwa mita 12
Karibuni kwa ramani, makadirio na ushauri
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaaan nilifanya makosa mengi sana katika ujenzi, Mungu akinijalia uzima na pesa nyingine basi nyumba ya pili nitajitahidi Sana kushirikiana wataalam.Kama huna ujuzi na mambo ya ujenzi, ni vizuri ukamshirikisha mtaalam katika kila hatua ya ujenzi unayoiendea.
Hii inatakiwa uifanye kuanzia mwanzoni kabisa, watu wengi wanauziwa viwanja vidogo kwa sababu hawana ujuzi na mambo ya vipimo. Unakuta mtu ana malengo ya kutaka kujenga nyumba ya vyumba vinne lakini kiwanja alichonunua unakuta ni futi 40 kwa futi 40
Hapo nimezungumzia upande wa vipimo, lakini kuna vitu vingine vya kuangalia kabla ya kununua hicho kiwanja mfano aina ya udongo n.k
Hatua kama hizi ni vyema ukatafuta mtaalam ukaambatana nae kwenda site ambapo inaweza ikakusaidia kwa kiasi kikubwa. Katika uuzaji wa viwanja, wauzaji wengi wanapenda kutumia kizio cha futi badala ya mita kwa sababu upande wa futi inaonekana kama kiwanja ni kikubwa (kwa asiyejua). Mfano kiwanja cha futi 40 kwa futi 40 ni sawa na kiwanja cha mita 12 kwa mita 12
Karibuni kwa ramani, makadirio na ushauri
Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wanafikri kumtumia mtaalam ni mpaka mtaalam afike eneo la tukio, hapo ndio watu wanapoogopa gharama. We nunua ramani kwa mtu ambaye ni mtaalam wa mambo ya ujenzi ili kutengeneza ujamaa wa kumtumia kama mshauri ktk kipindi chako chote cha ujenziYaaaan
Yaaan nilifanya makosa mengi sana katika ujenzi, Mungu akinijalia uzima na pesa nyingine basi nyumba ya pili nitajitahidi Sana kushirikiana wataalam.
Yan Ratio inayoshikilia tofauti iwe ndogo kuliko ratio ya plasta....?kweliPlaster nzuri ni ile ambayo ukimwagia ukuta maji, ukuta unakauka bila kuchora alama za matofali. Kiujumla michoro ya tofali katika ukuta uliopigwa plaster hutokea pale ratio ya udongo uliotumika kujengea tofali ni kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kupigia plaster
Kitaalam udongo wa kujengea tofali tunatumia ratio ya 1:6 na udongo wa kupigia plaster tunatumia ratio ya 1:4 na 1:5 (ratio ya 1:4 inatumika kwenye kuta upande wa nje, na 1:5 upande wa ndani)
Ratio ya plaster inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kujengea
Kwa mahitaji ya ramani, makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
Bro unahangaika sana kutafuta umaarufu, na kwa bahati mbaya nyuzi zako zinakosa attention kwa wasomaji. Unaanzisha nyuzi kila lisaa na bado watu hawakuzingatii, lengo lako hasa ni kutafuta umaarufuYan Ratio inayoshikilia tofauti iwe ndogo kuliko ratio ya plasta....?kweli
Aya turudi kwenye swali la msingi...Bro unahangaika sana kutafuta umaarufu, na kwa bahati mbaya nyuzi zako zinakosa attention kwa wasomaji. Unaanzisha nyuzi kila lisaa na bado watu hawakuzingatii, lengo lako hasa ni kutafuta umaarufu
Najua umekuja na humu baada ya kuona humu kuna views nyingi, sasa mimi sio mtu wa ligi...we kwa akili ya kawaida, kati ya plaster na hiyo mortar inayounga tofali ni kipi kinamfunika mwenzake?
Na kama ratio ya mortar ya kujengea tofali inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya plaster, hiyo plaster unapiga ya kazi gani? Yani ni sawa na kumuweka Paka ili amlinde Simba
View attachment 2950235