Nimekuwa nikipokea ramani kutoka kwa watu mbali mbali kwa lengo la kuzifanyia makadirio, kitu ambacho huwa kinanishangaza ni kuona kitchen inakuwa na uwazi unaoangaliana na dining room mbali na milango inayotumika kuingia ama kutoka jikoni (mpaka hapo privacy kwa mpishi jikoni inakuwa hamna, watu wakiwa wamekaa dining wanamuona mtu akiwa yupo jikoni)
Hebu tuangalie kiusalama madhara ya hii design ni nini. Tukuchukulie kwamba una familia yenye watoto (watoto wa primary/secondary etc) na wewe huwa unatoka kwenda zako kazini. Watoto wamerudi kutoka shuleni, na wana access ya kuingia jikoni sehemu ambayo hatari ya moto inaweza kutokea muda wowote pindi uzembe utakapofanyika.
Kama mnavyojua akili za watoto, mtoto anaweza akawasha jiko baada ya muda akajisahau akapitiwa na usingizi au akaenda kucheza na wenzake nje, usalama wa nyumba yako mpaka hapo tayari unakuwa ni wa mashaka, ni Mungu tu ndio anakuwa anatulinda lakini siku yoyote linaweza likatokea la kutokea ukajikuta unapoteza nyumba hivi hivi japo hatuombei iwe hivyo. Kama mtu mzima tu na akili yake timamu anaweza akafanya uzembe kama huu kwa kupitiwa, vipi kwa watoto ambao akili zao bado hazijakomaa?
Jiko kama jiko linatakiwa liwe na milango ambayo ikifungwa hiyo milango kusiwe na access nyingine yoyote ya kuweza kuingia jikoni mpaka ufunguliwe mlango mmoja wapo, chakula kikiiva weka hotpot Dining mezani watoto wakirudi shule watakula bila kuingia jikoni. Fuatilia matukio mengi ya nyumba kuungua moto, utagundua matukio mengi yamesababishwa na uzembe jikoni hasa kwa watu wanaotumia majiko ya gesi na majiko ya umeme.
Mimi mtazamo wangu katika designing ni huo (safety first) na huwa namshauri mtu anapokuja na idea yake jinsi inavyotakiwa iwe (akitaka nidesign kama anavyotaka yeye, mimi huwa nadesign hivyo hivyo lakini najua tayari nimeshamshauri)