Hechy Essy
Kuhusu kulaza au kusimamisha matofali kwenye ujenzi wa nyumba ya kawaida ghorofa 1 kipi ni sahihi?
Maana kuna wanaosema kuwa ukitumia nondo 4 za mm16 kwenye nguzo tofali unaweza kusimamisha na wala hamna shida.
Then kuna wanasema ukitumia nondo 6 za mm12 basi tofali ndo utazilaza, na wakati huohuo bado kuna wanaotumia nondo hizo 6 za mm 12 na bado tofali zinasimamishwa.
Nimeona ujenzi wa nyumba Uganda, Nigeria, Kenya mara nyingi tofali hawalazi tena basi za kwao ni hollow blocks, sasa najuliza kipi ni sahihi kiutaalamu.
Then kwa sasa kuna ujenzi ule wa pre casted slab ambapo unakuta kwenye slab wanapanga tu hollow blocks, then kuna mapande marefu ya zege wanayapanga, then kuna wire mesh inatandikwa au wanaweka tu kichanja cha nondo chache then wanamwaga zege, najiuliza ujenzi huo ni sahihi?
Niseme yoyote kwa yote binafsi naamini/nahisi ujenzi huo wooote nilioutaja hapo juu nia yao ni kupunguza gharama sasa je huo ujenzi kiutaalam ni sahihi au ndo baada ya miaka kadhaa kupita tutegemee majanga?