Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Mkuu naomba kufahamu yafatayo;
1. Unapoweka Jamvi unakuwa huna haja ya kuweka mkanda?
2. Kipi naweza kuskip katika namna ya kupunguza gharama lakini nikawa nimelinda ubora ktk haya;
a/kuweka Jamvi
b/ kuweka mkanda
c/ kuweka lenta 2, nikaweka moja tu ile ya juu.
1. Hapana, hapo kila kimoja kina kazi yake...ukiweka vyote inakuwa bora zaidi ila ukishindwa kuweka vyote kutokana na hali ya uchumi, weka mkanda

2. Inategemea na uimara wa tofali pamoja na aina ya udongo. Kuna tofali flani zilikuaga zinatumika sana miaka ya nyuma (zilikuwa zinatengenezwa kwa kutumia saruji, mchanga na vikokoto vidogo vidogo).

Enzi hizo gari la tofali likifika site, tofali zilikuwa zinamwagwa tu kama mchanga na hazivunjiki (baada ya hapo ndio zinaanza kupangwa)

Hizi tofali zilikuwa imara sana tofauti na hizi za sasa ambazo zinatengenezwa kibiashara zaidi (cement kidogo, mchanga mwingi). Watu wengi wakitumia hizi tofali kwenye msingi, huwa wanaskip kuweka mkanda kwa sababu uimara wake unakaribiana na uimara wa zege yenyewe, kama utatumia hizi tofali za kileo nakushauri uweke mkanda hata wa nondo 3 ili kujiweka salama zaidi

Upande wa kuweka jamvi, kama udongo wako uko vizuri na uchumi wako hauruhusu unaweza ukajaza kifusi chenye mawe mawe na kukishindilia vizuri, baada ya hapo ukamwaga zege nyembamba
 
Shukrani Sana mkuu Kwa Ushauri wako huu mzuri, vipi kwasisi tunaotumia msingi wa mawe kipi kitafaa zaidi? Hapa umeshauri zaidi Kwa wanaoutumia msingi wa tofali. Asante sana
 
Shukrani Sana mkuu Kwa Ushauri wako huu mzuri, vipi kwasisi tunaotumia msingi wa mawe kipi kitafaa zaidi? Hapa umeshauri zaidi Kwa wanaoutumia msingi wa tofali. Asante sana
Kiufupi ni muhimu sana kuweka mikanda yote miwili katika aina yoyote ya msingi utakayotumia, lakini ikiwa mfuko hauruhusu weka mkanda wa juu (hapa pia uwe tayari kwa matokeo). Chini ni heri ukajipinda ukaweka hata mkanda wa nondo 2 kuliko kutoweka kabisa
 
Aina ya msimamizi au mafundi utakaowatumia inaweza ikachangia kuongezeka kwa gharama za ujenzi. Unaweza ukapata msimamizi ambaye hana mbinu zozote za kupunguza gharama ukajikuta pesa uliyopanga kuitumia kujenga jengo lako isitimize lengo (ukaishia njiani)

Ukishaona fundi au msimamizi anakuambia mnunue mbao kwa ajili ya kuset msingi wakati tofali zipo site, ujue hapo kumaliza ujenzi ni 50/50...pesa nyingi zitatumika katika vitu ambavyo havina ulazima wa kuvinunua

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Mkuu vipi kuhusu namna ya kukadria gharama ya ufundi hasa Kwa ujenzi wa msingi, Boma n.k ni namna gani hasa ya ukadiriaji wa gharama sahihi ambao utasaidia kuepusha upigaji wa mafundi??
 
Mkuu vipi kuhusu namna ya kukadria gharama ya ufundi hasa Kwa ujenzi wa msingi, Boma n.k ni namna gani hasa ya ukadiriaji wa gharama sahihi ambao utasaidia kuepusha upigaji wa mafundi??
Gharama za ufundi huwa ni around 20% mpaka 25% ya gharama za material katika hatua husika. Mfano kama material ya upauaji gharama yake ni milion 4, basi ufundi ni kati ya laki 8 mpaka milion 1.

Lakini kuna baadhi ya hatua, labour charge inakuwa haifiki hata 5% au hamna kabisa mfano ukienda kununua madirisha (iwe ni aluminium au grill), watengenezaji huwa wanakuja kukuwekea wenyewe site kwako kwa hivyo kama ulitumia let say milion 5 katika ununuzi wa hayo madirisha, gharama ya ufundi haiwezi kuwa 20-25% (milion 1) tena kama ilivyo huko juu

Na pia kuna hatua zingine huwezi ukatumia hayo mambo ya percent maana material cost yake inakuwa ni ndogo sana. Mfano upande wa plaster, skimming, rangi,tiles n.k huku tunatumia SQM eg Tsh 3500 to 4500/SQM kwa plaster, Tsh 4000 - 5000/SQM kwa tiles n.k kutegemeana na fundi
 
Kama viwanja vipo vingi, chagua kiwanja ambacho kipo kwenye kona. Hii itakupa options zaidi ya moja ya kuielekeza nyumba yako kutokana na uwepo wa bara bara pande mbili za kiwanja

Nyumba huwa ina mapana na marefu, sasa wakati mwingine nyumba inagoma kuelekea upande flani kutokana na mapana au marefu ya kiwanja kuwa madogo, kwa hivyo kama kiwanja ni kidogo na barabara ipo upande mmoja tu itabidi design ifanyike kwa kufuata pattern ya kiwanja, upande wa mbele wa nyumba unatakiwa uwe unaangalia barabara (ikishindikana kabisa, upande wa mbele uelekezee ubavuni).

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika ujazaji wa kifusi katika msingi, jaza kifusi kwa matabaka (layers)....mfano unaweza ukajaza kina cha futi moja ukashindilia, unajaza tena kifusi kingine unashindilia hivyo hivyo mpaka unafika juu ya msingi.

Usijaze kifusi chote kwa pamoja then ukaja kushindilia juu, unaweza ukasababisha nyufa katika kuta

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ni bora plaster ikawa ni nyembamba lakini yenye ratio (uwiano wa saruji na mchanga) kali kuliko kuwa na plaster nene yenye ratio dhaifu

Unene wa plaster unatakiwa usizidi nusu nchi, na baada ya kuapply tabaka la kwanza (first coat) inatakiwa iachwe kwa muda kabla ya kufuta na ubao (rati)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kwanini tiles huwa zinabanduka baada ya muda mfupi?
Kuna aina flani ya tiles huwa zinanyonya maji kwa kiasi kikubwa, hivyo punde tu baada ya kuzibandika huwa zinaanza kufyonza maji ya kwenye udongo (mortar) na kufanya hydration reaction kupungua kasi yake ama kusimama kabisa

Kabla ya kuanza kubandika tiles zako, inabidi ujue tiles zako ni za aina gani (tiles za kuloweka au lah)

Utajuaje?

Chukua kipande kimoja cha tile, geuza nyuma (katika uso ambao unaenda kukutana na udongo), weka matone kadhaa ya maji. Ukiona maji yamechukua muda mfupi kupotea (kufyozwa), basi ujue tiles zako inabidi uziloweke kwanza kwenye pipa/beseni la maji (Dakika 20 mpaka 30) kabla hujaanza kuzibandika.

Kama maji yatakaa muda mrefu bila kupotea, basi tiles zako hazitokuwa na haja ya kuziloweka kwenye maji.

Lengo la kuziloweka ni kuzifanya tiles zishibe maji ili zitakapobadikwa zisifyozwe maji ya kwenye udongo na kuathiri hydration reaction (reaction kati ya saruji na maji)

Mbali na hivyo, kuna sababu zingine zinazopelekea tiles kubanduka (hii ni moja wapo tu kati ya nyingi)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane

Huduma ya site visit (kutembelea site) pia ipo
 
Ukienda kununua tofali, chukua kwanza tofali moja liachie chini bila kutumia nguvu. Kama litapasuka mapande mengi mengi basi ujue hapo hamna tofali, kama litakatika kati kati na kutengeneza mapande mawili basi hilo tofali litakuwa ni imara

Katika tofali, sehemu ya kati kati ndio sehemu dhaifu zaidi na ndipo ambapo huwa panaanza kukatika kama tofali litaelemewa mzigo

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ili kuepuka gharama za kujenga mnara wa tank la maji, kibaraza cha mbele au cha nyuma juu weka zege badala ya bati ili upate nafasi ya kuweka tank juu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Je wajua, bati lina upande dume na upande jike?

Sasa katika upigiliaji, upande jike unatakiwa uwe juu ya upande dume. Ukifanya vice versa, mtu akipita nje atakuwa anaona bati zote zilipoanzia na zinapoishia (inapoteza mvuto, inakua kama umetandika mikeka) na kingine hata upepo ukipita juu ya bati, upepo utakuwa unakwama kwama kwenye maungio ya bati moja na lingine ambapo itakuwa rahisi kuezua bati

Ramani, Makadirio na Ushauri tuwasiliane
 
Ili mafundi wafanye kazi kwa moyo wote, siku moja moja jaribu kufanya majukumu ambayo wenyewe wanajua kabisa sio majukumu yako kuyafanya.

Mfano siku moja unaweza ukawaagizia chakula, pesa ya chakula ukawalipia wewe. Siku nyingine unaweza ukawanunulia hata matunda ukawapelekea site.

NB: Usifanye hivi mwanzoni, kwa sababu wataweka akilini kwamba suala la chakula kwao ni jukumu lako kuwanunulia, kwa hivyo siku ukiacha kuwanunulia utakuwa umewadisappoint na kuwavunja moyo. Acha kwanza wajinunulie chakula wenyewe siku za mwanzoni ili wajue kwamba suala la chakula ni jukumu lao, uwe unawanunulia tu siku moja moja (iwe kama surprise kwao)

Hii katika Construction Management tunaita Motivation

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ukiweka dirisha la aluminium la futi 4, basi hapo ni sawa na umeweka dirisha la wavu la futi 2 kwa sababu dirisha la aluminium huwa linafunguka nusu,na kujiziba nusu.

Kama nyumba yako ipo katika maeneo ya joto, hizi dirisha zitakutesa sana na joto vinginevyo itakulazimu kuweka madirisha mengi ili kupata hewa ya kutosha

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Back
Top Bottom