Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #641
Nimejenga Msingi wa nyumba kwakutumia tofali za kuchoma, pia sijafunga beam. Je naweza kupandisha kozi za ukuta kwa kutumia tofali za cement na mchanga (broku) bila kuleta madhara? Hali ya udongo ni tifutifu na inch 12 chini ni mfinyanziNimepita mahali nimekuta mafundi wamelaza nondo moja moja tu kwenye mkanda (beam). Sasa wanaweza wakawa wana nia nzuri ya kubana matumizi lakini je boss anafahamu kwamba imetumika nondo moja moja?!!
Au boss ndio kapigiwa hesabu ya nondo nne nne then kwenye usukaji wa nondo kafungiwa nondo moja moja, kwa kuwa yeye hayupo, mimi sijui.
Kuna ule mfumo wa watu (maboss) kuwa wanalipia pesa hard ware then wanakuwa wanamuagiza fundi akachukue material dukani wakidhani kwamba wamewakomoa mafundi kuiba.
Kwenye suala la pesa, hata maadui wanaweza wakaungana kuipambania hiyo pesa ili wakipata wagawane, baada ya mgao uadui unaendelea kama kawaida.
Risiti sio ishu, unaweza ukaandikiwa risiti ya mifuko 20 ya cement kumbe umeuziwa mifuko 15, kinachofanyika na hawa wauzaji nikikielezea hapa itakuwa ni mbinu hata kwa wengine ambao hawana hiyo tabia wakajifunza. Kiufupi ni kwamba usiziamini risiti unazopewa ukajua kilichoandikwa pale ni kweli 100%
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Ilikuwa ufanye kinyume chake, tofali za block ziwe chini (kwenye msingi), tofali za kuchoma ziwe juu (kwenye boma)Nimejenga Msingi wa nyumba kwakutumia tofali za kuchoma, pia sijafunga beam. Je naweza kupandisha kozi za ukuta kwa kutumia tofali za cement na mchanga (broku) bila kuleta madhara? Hali ya udongo ni tifutifu na inch 12 chini ni mfinyanzi
Hapo ndg yangu ulitakiwa ufunge mikanda miwili kwenye msingi kutokana na kina cha msingi kuwa kirefu. Udongo wa msingi una uwezo wa kuusukuma ukuta hivyo unahitaji ukuta imara utakaoweza kukinzana na hiyo nguvu ya udongo (earth pressure)Hechy Essy Mkuu Kuna hii Case Inanitesa.
Nyumba imejengwa mpk juu, imejengwa kwa tofari za inchi 6, ipo enelo lenye bonde kiasi, msingi ulichukua kozi 9, then mkanda wa chini una nondo zilisukwa nne nilikuwepo, mkanda ni inchi 7. Then kwenye Kona zote za Kuta imewekwa joint ya Zege. Na ring beam juu tayari. Sasa shida naiona imekuja kuta zimeanza kuweka nyufa sehemu nyingi[emoji24][emoji24] [emoji24] hili swala wapi wamenichemsha. Inaniumiza sana.
So, hapo nyufa zitaendelea kutokea na nitakua naziba nyufa siku zote?😥 Je angeweka Yale matundu kwenye msingi ingesaidia? maana hata hayo hakuweka. Na sikua naelewa kabisa.Hapo ndg yangu ulitakiwa ufunge mikanda miwili kwenye msingi kutokana na kina cha msingi kuwa kirefu. Udongo wa msingi una uwezo wa kuusukuma ukuta hivyo unahitaji ukuta imara utakaoweza kukinzana na hiyo nguvu ya udongo (earth pressure)
Pia mlikosea kutumia udongo kama kifusi, kwa kesi kama hiyo ulitakiwa ujaze mchanga (kama ni rahisi kupatikana) au udongo wa kichanga ambao hata ukiuloweka kwenye maji haubaki na tope chini
Kutoweka matundu kwenye msingi (hasa kwa kifusi cha udongo) ni kosa lingine ambalo ukijumlisha na kosa la kufunga mkanda mmoja linaongeza ukubwa wa tatizoSo, hapo nyufa zitaendelea kutokea na nitakua naziba nyufa siku zote?[emoji26] Je angeweka Yale matundu kwenye msingi ingesaidia? maana hata hayo hakuweka. Na sikua naelewa kabisa.
Wenye mamlaka wameuhamisha huu uzi kwenye jukwaa la matangazo madogo, sijajua wametumia vigezo gani maana hata wenye matangazo yanayofanana na tangazo langu nyuzi zao bado zipo kwenye jukwaa la ujenzi. Muhimu inabidi tu musubscribe ili muendelee kupata notification ninapoweka dondoo mpyaUnajua huu uzi inafaa kusoma comments zote za Hechy Essy ukiwa na note book. Fundi akifanya kazi unaangalia na desa lako linasemaje
Tofalo za inch 6 sio tafsiri ya uimara au ubora, zipo tofali za inch 5 ni bora kuliko inch 6, inategemea na walovyofanya mixing na compression wakati wanafyatuaHechy Essy Mkuu Kuna hii Case Inanitesa.
Nyumba imejengwa mpk juu, imejengwa kwa tofari za inchi 6, ipo enelo lenye bonde kiasi, msingi ulichukua kozi 9, then mkanda wa chini una nondo zilisukwa nne nilikuwepo, mkanda ni inchi 7. Then kwenye Kona zote za Kuta imewekwa joint ya Zege. Na ring beam juu tayari. Sasa shida naiona imekuja kuta zimeanza kuweka nyufa sehemu nyingi😭😭 😭 hili swala wapi wamenichemsha. Inaniumiza sana.
Suala la zile holes kwenye msingi, logic yake ipo lakini naonaga haina mashiko kulingana na msingi umejengwa vipi. Unaweza usiweke na bado hakuna chochote kitachokua vibayaSo, hapo nyufa zitaendelea kutokea na nitakua naziba nyufa siku zote?😥 Je angeweka Yale matundu kwenye msingi ingesaidia? maana hata hayo hakuweka. Na sikua naelewa kabisa.
Hizo Kona za Kuta Kuna joint ya zenge yenye vikokoto vidogo dogo vyeusi. Na sio Nguzo ya zege.Tofalo za inch 6 sio tafsiri ya uimara au ubora, zipo tofali za inch 5 ni bora kuliko inch 6, inategemea na walovyofanya mixing na compression wakati wanafyatua
Msingi kozi 9 ilipaswa kuwepo na mikanda miwili, Kona za kuta kuna joint ya zege au nguzo za zege? Na je hizi nguzo zipo pia kwenye kona kwenye msingi?
Kuta zimeanza kuweka nyufa sehemu nyingi? Je hizi nyufa ni kwenye kuta tu au zipo na kwenye msingi? Haya maswali yatafanya kujua solution ya tatizo lako kwa urahisi
Tatizo Hilo linawezekana kutibika vizuri tu na utasahau nyufa zote
Lakini pia sehemu ya slope kama hiyo ilipaswa awepo mtu anayejua vizuri kumuongoza fundi nn cha kufanya. Kwanza ilipaswa kujua aina ya udongo
Pia sidhani kama aliweka carpet la zege kuzunguka msingi wote kabla hajaanza kujenga tofali za msingi
Maumivu everywhere..Suala la zile holes kwenye msingi, logic yake ipo lakini naonaga haina mashiko kulingana na msingi umejengwa vipi. Unaweza usiweke na bado hakuna chochote kitachokua vibaya
Nimeelewa, pole sana kwa hizo cracks.Hizo Kona za Kuta Kuna joint ya zenge yenye vikokoto vidogo dogo vyeusi. Na sio Nguzo ya zege.
Hizo joint za zege hazijaanzia kwenye kwenye msingi.
Hizi nyufa Kuna sehemu zipo kwenye msingi na kuna sehemu zipo kwenye ukuta wa boma na Kuna ufa, mwingine upo kwenye Nguzo ya tofari yenye kona Moja kwenye verandah sasa ile joint ya zege inaufa pia tena mkubwa 😥
Maumivu everywhere..
Kwahiyo huu msingi ilibiidi baada ya kozi nne niweke mkanda na nikimaliza pia pale kozi ya mwisho niweke mkanda? Jamani ngojeni nipumue
Ngoja papumzike kwanza 😥. Haraka zote zimeniishia.Nimeelewa, pole sana kwa hizo cracks.
Kwanza hizo joint za zege hazikua na haja, bora angeweka nguzo tu, ambazo pia sijaona haja yake labda urefu wa nyumba ulimtisha.
Alichotakiwa ni kuweka nguvu chini kwenye msingi, angeweza nguzo kwenye kona za msingi na angeweka mikanda miwili, wa kwanza after four course na wa pili wa juu kabla ya kupandisha kuta
Solution ipo, sasa sijui ubora wa huyo fundi upoje. Hapo ni kutumia wire mesh. Sasa jinsi ya kutumia ndio inategemea na uzuri wa fundi upoje, anapaswa kutindua nyufa zote mwanzo mpaka mwisho. Wala hakuna gharama sana kutibu hilo tatizo
Imalize tu sababu imeshafika mbali maana hayo makosa huwezi rekebisha sasa hivi ni wakati unapiga plasterNgoja papumzike kwanza 😥. Haraka zote zimeniishia.
Umeandika imalize tu as if ni kwenda tu kufanya sha Shaa. Tusubiri inyeshewe mara Moja kwanza. Imeishia Top kozi tatu.Imalize tu sababu imeshafika mbali maana hayo makosa huwezi rekebisha sasa hivi ni wakati unapiga plaster
Tafuta fundi makini na ww pia ujue mawili matatu ili uweze kumbana. Atarekebisha
😂😂 usiichungulie sana pesa, huwa siku zote haitoshi. We fumba macho imalize, hayo makosa yanarekebishika vizuri tuUmeandika imalize tu as if ni kwenda tu kufanya sha Shaa. Tusubiri inyeshewe mara Moja kwanza. Imeishia Top kozi tatu.
.Maelezo ya Mafundi ni mengi, Kuna Mmoja aliona tutashindwana nilikua injinia wa mchongo😺 huu Uzi ulinipiga brush kidogo.