Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Watu wengi hupendelea kutumia nguzo za pembe (mraba/mstatili) kuliko nguzo za duara kwa sababu zifuatazo

1. Urahisi wa kutengeneza umbo la nguzo (hapa unatumia tu mbao, vipande vya marine board n.k). Upande wa nguzo za duara, ni ngumu kutengeneza umbo lake hivyo utalazimika ukakodi maumbo ambapo napo inaongeza gharama za ziada

2. Katika nguzo za pembe, kiasi cha chini cha nondo kinachohitajika ni nondo nne nne lakini kwa upande wa nguzo za duara, kiasi cha chini cha nondo kinachohitajika ni nondo sita sita

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Je wajua nguzo ya duara ambayo kipenyo chake kinalingana na upana wa nguzo ya mraba inatumia zege kidogo ukilinganisha na kiasi cha zege kitakachotumika katika nguzo ya mraba

Nguzo ya mraba (230mmx230mmx3m)
Ujazo, Volume (m³)= 0.23mx0.23mx3m = 0.15m³

Nguzo ya duara (230mm diameter, 3m height)
Ujazo, Volume (m³) = (3.14x0.23²)/4×3m = 0.125m³

Tofauti = 0.15m³ - 0.125m³ = 0.025m³

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kipindi kizuri cha kumwaga zege ni usiku (kuanzia jioni jioni jua linapoelekea kuzama). Usiku hakuna jua hivyo upoteaji wa maji katika zege ni mdogo sana ama hakuna kabisa kutokana na uwepo wa baridi.

Upotevu wa maji katika zege kutokana na joto kali (through evaporation) husababisha zege kusinyaa na kufanya nyufa zitokee ndio maana sehemu zingine utaona zege (nguzo,mkanda ama slab) imefunikwa na viroba vya katani ili kuzuia /kupunguza upotevu wa maji

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Urefu kutoka usawa wa ardhi (ground level) mpaka dirisha la choo linapoanzia unatakiwa uwe zaidi ya futi 7 kwa sababu wastani wa urefu wa mtu ni futi 5.5 mpaka 6.5

Kama utaweka dirisha refu chooni, itakulazimu jengo lako liende juu zaidi, huwezi kuweka dirisha la 4 ikiwa urefu kutoka usawa wa ardhi mpaka mkanda wa juu ni futi 9

Ukichukua 9ft ukatoa na 4ft unabaki na 5ft (urefu kutoka usawa wa ardhi mpaka dirisha la choo linapoanzia) ambapo mtu mwenye urefu unaozidi futi 5 akipita nje anaweza kuona/kuchungulia chooni

Wengine huwa wanajenga mpaka kozi 12 kutoka mkanda wa chini mpaka mkanda wa juu, ili kuweka madirisha marefu zaidi, unakuta dirisha la choo lina futi 4, madirisha mengine yana urefu wa mpaka futi 8

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Nimepita mahali nimekuta mafundi wamelaza nondo moja moja tu kwenye mkanda (beam). Sasa wanaweza wakawa wana nia nzuri ya kubana matumizi lakini je boss anafahamu kwamba imetumika nondo moja moja?!!

Au boss ndio kapigiwa hesabu ya nondo nne nne then kwenye usukaji wa nondo kafungiwa nondo moja moja, kwa kuwa yeye hayupo, mimi sijui.

Kuna ule mfumo wa watu (maboss) kuwa wanalipia pesa hard ware then wanakuwa wanamuagiza fundi akachukue material dukani wakidhani kwamba wamewakomoa mafundi kuiba.

Kwenye suala la pesa, hata maadui wanaweza wakaungana kuipambania hiyo pesa ili wakipata wagawane, baada ya mgao uadui unaendelea kama kawaida.

Risiti sio ishu, unaweza ukaandikiwa risiti ya mifuko 20 ya cement kumbe umeuziwa mifuko 15, kinachofanyika na hawa wauzaji nikikielezea hapa itakuwa ni mbinu hata kwa wengine ambao hawana hiyo tabia wakajifunza. Kiufupi ni kwamba usiziamini risiti unazopewa ukajua kilichoandikwa pale ni kweli 100%

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Nimejenga Msingi wa nyumba kwakutumia tofali za kuchoma, pia sijafunga beam. Je naweza kupandisha kozi za ukuta kwa kutumia tofali za cement na mchanga (broku) bila kuleta madhara? Hali ya udongo ni tifutifu na inch 12 chini ni mfinyanzi
 
Ilikuwa ufanye kinyume chake, tofali za block ziwe chini (kwenye msingi), tofali za kuchoma ziwe juu (kwenye boma)

Tofali za cement na mchanga ni nzito (density yake ni kubwa) ukilinganisha na tofali za udongo japo kuwa tofali za kuchoma zinadumu kwa muda mrefu ukilinganisha na tofali za block. Ushauri wangu, tumia tofali hizo hizo za kuchoma kujengea boma
 
Hechy Essy Mkuu Kuna hii Case Inanitesa.
Nyumba imejengwa mpk juu, imejengwa kwa tofari za inchi 6, ipo enelo lenye bonde kiasi, msingi ulichukua kozi 9, then mkanda wa chini una nondo zilisukwa nne nilikuwepo, mkanda ni inchi 7. Then kwenye Kona zote za Kuta imewekwa joint ya Zege. Na ring beam juu tayari. Sasa shida naiona imekuja kuta zimeanza kuweka nyufa sehemu nyingi😭😭 😭 hili swala wapi wamenichemsha. Inaniumiza sana.
 
Hechy Essy Mkuu Kuna hii Case Inanitesa.
Nyumba imejengwa mpk juu, imejengwa kwa tofari za inchi 6, ipo enelo lenye bonde kiasi, msingi ulichukua kozi 9, then mkanda wa chini una nondo zilisukwa nne nilikuwepo, mkanda ni inchi 7. Then kwenye Kona zote za Kuta imewekwa joint ya Zege. Na ring beam juu tayari. Sasa shida naiona imekuja kuta zimeanza kuweka nyufa sehemu nyingi[emoji24][emoji24] [emoji24] hili swala wapi wamenichemsha. Inaniumiza sana.
Hapo ndg yangu ulitakiwa ufunge mikanda miwili kwenye msingi kutokana na kina cha msingi kuwa kirefu. Udongo wa msingi una uwezo wa kuusukuma ukuta hivyo unahitaji ukuta imara utakaoweza kukinzana na hiyo nguvu ya udongo (earth pressure)

Pia mlikosea kutumia udongo kama kifusi, kwa kesi kama hiyo ulitakiwa ujaze mchanga (kama ni rahisi kupatikana) au udongo wa kichanga ambao hata ukiuloweka kwenye maji haubaki na tope chini
 
So, hapo nyufa zitaendelea kutokea na nitakua naziba nyufa siku zote?😥 Je angeweka Yale matundu kwenye msingi ingesaidia? maana hata hayo hakuweka. Na sikua naelewa kabisa.
 
So, hapo nyufa zitaendelea kutokea na nitakua naziba nyufa siku zote?[emoji26] Je angeweka Yale matundu kwenye msingi ingesaidia? maana hata hayo hakuweka. Na sikua naelewa kabisa.
Kutoweka matundu kwenye msingi (hasa kwa kifusi cha udongo) ni kosa lingine ambalo ukijumlisha na kosa la kufunga mkanda mmoja linaongeza ukubwa wa tatizo
 
Unajua huu uzi inafaa kusoma comments zote za Hechy Essy ukiwa na note book. Fundi akifanya kazi unaangalia na desa lako linasemaje
Wenye mamlaka wameuhamisha huu uzi kwenye jukwaa la matangazo madogo, sijajua wametumia vigezo gani maana hata wenye matangazo yanayofanana na tangazo langu nyuzi zao bado zipo kwenye jukwaa la ujenzi. Muhimu inabidi tu musubscribe ili muendelee kupata notification ninapoweka dondoo mpya
 
Katika wakati ambao nimeona Moderator ni watu wa ajabu ni hiki kitendo cha kuhamisha huu uzi Jukwaa la Matangazo. Maxence Melo angalia upya kama huyo Mod anakufaa, otherwise mfunge Jukwaa la Ujenzi tujue moja. Haihitaji D mbili kujua huu uzi unatakiwa kuwa wapi.

Hatuhitaji benefit of doubts kujua sababu, labda tuamini mnaona tunafaidi sana mjadala. Kuweni wastaarabu.

Mod aliyefanya hiki kitendo amenikumbusha siku mlipohamisha uzi wa NBAA jukwaa la elimu na kupeleka jukwaa la michezo.
 
Hechy Essy Mkuu Kuna hii Case Inanitesa.
Nyumba imejengwa mpk juu, imejengwa kwa tofari za inchi 6, ipo enelo lenye bonde kiasi, msingi ulichukua kozi 9, then mkanda wa chini una nondo zilisukwa nne nilikuwepo, mkanda ni inchi 7. Then kwenye Kona zote za Kuta imewekwa joint ya Zege. Na ring beam juu tayari. Sasa shida naiona imekuja kuta zimeanza kuweka nyufa sehemu nyingi😭😭 😭 hili swala wapi wamenichemsha. Inaniumiza sana.
Tofalo za inch 6 sio tafsiri ya uimara au ubora, zipo tofali za inch 5 ni bora kuliko inch 6, inategemea na walovyofanya mixing na compression wakati wanafyatua

Msingi kozi 9 ilipaswa kuwepo na mikanda miwili, Kona za kuta kuna joint ya zege au nguzo za zege? Na je hizi nguzo zipo pia kwenye kona kwenye msingi?

Kuta zimeanza kuweka nyufa sehemu nyingi? Je hizi nyufa ni kwenye kuta tu au zipo na kwenye msingi? Haya maswali yatafanya kujua solution ya tatizo lako kwa urahisi

Tatizo Hilo linawezekana kutibika vizuri tu na utasahau nyufa zote

Lakini pia sehemu ya slope kama hiyo ilipaswa awepo mtu anayejua vizuri kumuongoza fundi nn cha kufanya. Kwanza ilipaswa kujua aina ya udongo
Pia sidhani kama aliweka carpet la zege kuzunguka msingi wote kabla hajaanza kujenga tofali za msingi
 
So, hapo nyufa zitaendelea kutokea na nitakua naziba nyufa siku zote?😥 Je angeweka Yale matundu kwenye msingi ingesaidia? maana hata hayo hakuweka. Na sikua naelewa kabisa.
Suala la zile holes kwenye msingi, logic yake ipo lakini naonaga haina mashiko kulingana na msingi umejengwa vipi. Unaweza usiweke na bado hakuna chochote kitachokua vibaya
 
Tofalo za inch 6 sio tafsiri ya uimara au ubora, zipo tofali za inch 5 ni bora kuliko inch 6, inategemea na walovyofanya mixing na compression wakati wanafyatua

Msingi kozi 9 ilipaswa kuwepo na mikanda miwili, Kona za kuta kuna joint ya zege au nguzo za zege? Na je hizi nguzo zipo pia kwenye kona kwenye msingi?

Kuta zimeanza kuweka nyufa sehemu nyingi? Je hizi nyufa ni kwenye kuta tu au zipo na kwenye msingi? Haya maswali yatafanya kujua solution ya tatizo lako kwa urahisi

Tatizo Hilo linawezekana kutibika vizuri tu na utasahau nyufa zote

Lakini pia sehemu ya slope kama hiyo ilipaswa awepo mtu anayejua vizuri kumuongoza fundi nn cha kufanya. Kwanza ilipaswa kujua aina ya udongo
Pia sidhani kama aliweka carpet la zege kuzunguka msingi wote kabla hajaanza kujenga tofali za msingi
Hizo Kona za Kuta Kuna joint ya zenge yenye vikokoto vidogo dogo vyeusi. Na sio Nguzo ya zege.
Hizo joint za zege hazijaanzia kwenye kwenye msingi.

Hizi nyufa Kuna sehemu zipo kwenye msingi na kuna sehemu zipo kwenye ukuta wa boma na Kuna ufa, mwingine upo kwenye Nguzo ya tofari yenye kona Moja kwenye verandah sasa ile joint ya zege inaufa pia tena mkubwa 😥
Suala la zile holes kwenye msingi, logic yake ipo lakini naonaga haina mashiko kulingana na msingi umejengwa vipi. Unaweza usiweke na bado hakuna chochote kitachokua vibaya
Maumivu everywhere..
Kwahiyo huu msingi ilibiidi baada ya kozi nne niweke mkanda na nikimaliza pia pale kozi ya mwisho niweke mkanda? Jamani ngojeni nipumue
 
Hizo Kona za Kuta Kuna joint ya zenge yenye vikokoto vidogo dogo vyeusi. Na sio Nguzo ya zege.
Hizo joint za zege hazijaanzia kwenye kwenye msingi.

Hizi nyufa Kuna sehemu zipo kwenye msingi na kuna sehemu zipo kwenye ukuta wa boma na Kuna ufa, mwingine upo kwenye Nguzo ya tofari yenye kona Moja kwenye verandah sasa ile joint ya zege inaufa pia tena mkubwa 😥

Maumivu everywhere..
Kwahiyo huu msingi ilibiidi baada ya kozi nne niweke mkanda na nikimaliza pia pale kozi ya mwisho niweke mkanda? Jamani ngojeni nipumue
Nimeelewa, pole sana kwa hizo cracks.
Kwanza hizo joint za zege hazikua na haja, bora angeweka nguzo tu, ambazo pia sijaona haja yake labda urefu wa nyumba ulimtisha.

Alichotakiwa ni kuweka nguvu chini kwenye msingi, angeweza nguzo kwenye kona za msingi na angeweka mikanda miwili, wa kwanza after four course na wa pili wa juu kabla ya kupandisha kuta

Solution ipo, sasa sijui ubora wa huyo fundi upoje. Hapo ni kutumia wire mesh. Sasa jinsi ya kutumia ndio inategemea na uzuri wa fundi upoje, anapaswa kutindua nyufa zote mwanzo mpaka mwisho. Wala hakuna gharama sana kutibu hilo tatizo
 
Ngoja papumzike kwanza 😥. Haraka zote zimeniishia.
 
Ngoja papumzike kwanza 😥. Haraka zote zimeniishia.
Imalize tu sababu imeshafika mbali maana hayo makosa huwezi rekebisha sasa hivi ni wakati unapiga plaster
Tafuta fundi makini na ww pia ujue mawili matatu ili uweze kumbana. Atarekebisha
 
Imalize tu sababu imeshafika mbali maana hayo makosa huwezi rekebisha sasa hivi ni wakati unapiga plaster
Tafuta fundi makini na ww pia ujue mawili matatu ili uweze kumbana. Atarekebisha
Umeandika imalize tu as if ni kwenda tu kufanya sha Shaa. Tusubiri inyeshewe mara Moja kwanza. Imeishia Top kozi tatu.
.Maelezo ya Mafundi ni mengi, Kuna Mmoja aliona tutashindwana nilikua injinia wa mchongo😺 huu Uzi ulinipiga brush kidogo.
 
😂😂 usiichungulie sana pesa, huwa siku zote haitoshi. We fumba macho imalize, hayo makosa yanarekebishika vizuri tu

Mm huwa napenda plot ambayo Ina slope kubwa kama yako huwa ndio zina aesthetic views, na tena hapo kwenye msingi wa kozi tisa, ungefanya manuva vizuri na kuongeza kidogo ungetengeneza basement moja kali tu, angalia pia hata garden zinazokua kwenye slope plots jinsi zinavyovutia
 
Back
Top Bottom