Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Katika majengo ya ghorofa, nguzo (columns) ndio kama miguu kwa binadamu, . Nondo ya size ya chini kabisa kutumika katika nguzo ni milimita 16

Nondo za slab kikawaida tunatumia size ya milimita 12, sasa itakuwa ni ajabu kama slab inasukwa kwa nondo za milimita 12 halafu na nondo za guzo nazo zisukwe kwa kutumia size hiyo hiyo ya 12mm.

Watu wanakwepa kutumia nondo za milimita 16 kwa sababu ya gharama, bei ya nondo ya milimita 16 ukienda hard ware unapata nondo mbili za milimita 12 (kama itaongezeka, basi ni kidogo sana)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Naomba makadilio yako katika usimamizi wa nyumba ya kawaida ya vyumba 3 ya sq 130,kwenye ujenzi wa msingi,upandishaji kuta na upauaji.
 
Katika kazi za usukaji wa nondo (iwe ni slab, nguzo, au chochote) , ni vizuri ukawa na document inayoitwa Bar Bending Schedule

Hii document inakuwa inaonesha urefu wa vipande vyote vya nondo pamoja na idadi zake, shape ya nondo, size n.k ambapo inakuwa inamuongoza fundi kufanya kazi yake kirahisi zaidi lakini pia inasaidia sana kupunguza mabaki yasiyotumika (wastage) kutokana na nondo kuwa zinakatwa kwa mpangilio maalum

Kupitia hii document, fundi ataweza kugundua kwamba wastage ya sehemu moja inaweza ikatumika sehemu nyingine hivyo hatoweza kutumia nondo nyingine nzima wakati kuna wastage inayoweza kutumika mahali hapo

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kutoka chini kwenye sakafu (floor) mpaka kwenye switch za kuwashia taa/feni panatakiwa pawe na urefu wa futi 5 sawa na mita moja na nusu lakini switch sockets (sehemu za kuchajia) zinatakiwa ziwepo katika umbali wa futi moja na nusu mpaka futi mbili kutokea level ya sakafu


Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Umahiri wa fundi huanza kuonekana mapema kabisa katika zoezi la kuset jengo

Siku ya kwanza huwa inabeba activities tatu, kuset msingi, kuchimba msingi wote na kuset kozi ya kwanza (in case kama blinding haitokuwepo) ili kesho yake asubuhi watu wanaamka na kazi ya kupandisha kuta, tofauti na hapo msingi utachimbwa siku mbili nzima kwa sababu ya kuchelewa kuset msingi

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika zoezi la uwekaji wa tiles, hakikisha mtu akitaka kuingia chooni/bafuni mlangoni kuwe na step ndogo ya kushuka, na pia mtu akitaka kuingia kwenye chumba mlangani kuwe na step ya ndogo ya kupanda

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Wiki iliyopita kuna mahali tulienda na boss kutembelea kiwanja chake

Kama ilivyo kawaida nikienda mahali kutembelea plot, huwa nabeba na futi kamba yangu kwa ajili ya kuhakiki vipimo kabla zoezi la kudesign ramani halijaanza

Kwenye document ya mauziano, ilikuwa inaonesha vipimo vilivyotumika ilikuwa ni mita lakini kiuhalisia (kwa mujibu wa boss) ni kwamba walitumia hatua (miguu) ambapo muuzaji alimuaminisha boss kwamba hatua moja ni sawa sawa na mita moja.

Baada ya kuhakiki vipimo kwa kutumia futi kamba, kiwanja kikaonekana ni kidogo kulinganisha na vipimo vilivyoandikwa kwenye document ya mauziano.

Uzuri maeneo ya pembeni yote yalikuwa ni ya huyo muuzaji, ikabidi tumtafute tuhakiki wote na baada ya hapo muuzaji akasogeza mipaka ya kile kiwanja ili iendane na maandishi

Point to Note
Hatua moja ya binadamu ni nadra sana kufikia umbali wa mita moja kwa sababu

Mguu wa mtu mzima (namaanisha unyayo), urefu wake unaanzia sentimita 20 mpaka sentimita 30 japo wachache wanavuka

Urefu wa hatua moja itakuwa ni sawa sawa na nusu ya urefu wa unyayo wa mguu wa mbele JUMLISHA nusu ya urefu wa unyayo wa mguu wa nyuma JUMLISHA umbali kati ya kisigino cha mguu wa mbele na kidole gumba cha mguu wa nyuma

Katika mita 1 ambayo ni sawa na sentimita 100, ukitoa 20cm/2 + 20cm/2 unapata sentimita 80

Hiyo 80cm iliyobaki ni zaidi ya futi 2 na nusu, ambayo hata mtu mwenye miguu mirefu pengine anaweza asiifikie

Kinachofanyika katika upimaji kwa njia ya hatua ni kwamba mpimaji anakuwa anapiga hatua ndogo na kubwa, ndogo na kubwa kitu ambacho kinahitaji umakini kukigundua, pia huwa wanakuwa na mtu wao maalum katika hilo zoezi (huyu anakuwa na urefu wa wastani tu lakini pia anakuwa amevaa suruali inayobana ili asiweze kupiga hatua kubwa zaidi)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ukiweka madirisha ya grill, usiruhusu dirisha zako zikalala/kugusa ukuta moja kwa moja. Weka hata kipande kidogo cha ubao chenye unene hata wa nusu/robo nchi ili kuacha nafasi ya dirisha kutanuka na kusinyaa pindi kunapotokea mabadiliko ya joto bila kusababisha nyufa katika kuta.

Uwazi uliopo utauziba wakati unatengeneza kopro za madirisha

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
1. Urefu wa dirisha unatakiwa uzidi upana wake, vinginevyo dirisha litakuwa linaonekana kama TV. Usitumie 5x5, sijui 4x4 au 6x6 n.k kiufupi dirisha lako liwe la umbo la mstatili na sio mraba

2. Urefu wa dirisha unatakiwa uzidi nusu ya urefu kati ya mkanda wa chini na mkanda wa juu jumlisha 1ft (H/2+1ft), mfano kama urefu kati ya mkanda wa chini na mkanda wa juu ni mita 2.7 ambayo ni sawa na futi 9, basi dirisha lako linatakiwa lizidi 9ft/2+1ft ambayo ni 5.5ft, hapo unaweza ukatumia dirisha la urefu wa futi 6 na kuendelea ambapo kutokea kwenye mkanda wa chini mpaka dirisha linapoanzia kutakuwa na urefu wa futi 3

Ukitaka madirisha marefu zaidi, ongeza urefu kati ya mkanda wa chini na mkanda wa juu, wengine wanaweka mpaka kozi 12 mkanda hadi mkanda ili atumie dirisha za urefu wa futi 8

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ukienda hardware kununua tank la maji, unaweza ukakuta kuna tank fupi na tank refu lakini ujazo kwa matank yote unakuta ni ule ule mmoja mfano 1000Ltrs au 3000Ltrs

Tank refu huwa lina kitako kidogo, lakini tank fupi huna lina kitako kikubwa

Kama matank yote mawili yatakuwa na maji yanayofanana ujazo, halafu ukasema ukinge maji kwa kutumia ndoo mbili zinazofanana ujazo katika kila tank, tank refu litawahi kujaza ndoo kabla ya tank ya fupi

Tank fupi huwa linatumika zaidi sehemu ambayo kuna eneo la kutosha, na tank refu linatumika zaidi sehemu ambayo kuna ufinyu wa eneo la kuweka

Lakini pia siku hizi maghorofani huwa wanaweka matank ambayo hayaonekani, yanafichwa na paa la nyumba hivyo kwa case kama hii matank mafupi ndio huwa yanatumika zaidi


Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Faida yake hapo ni ipi mkuu?

-Kaveli-
Maji yasiweze kuingia chumbani mfano mtu akiwa anadeki koridoni, lakini pia maji ya chooni/bafuni yasiweze kutoka nje ya choo na kuingia ndani ya vyumba/korido
 
Maji yasiweze kuingia chumbani mfano mtu akiwa anadeki koridoni, lakini pia maji ya chooni/bafuni yasiweze kutoka nje ya choo na kuingia ndani ya vyumba/korido
mkuu vip kuhusu kutumia tofali za nch 5 kweny ukuta wa nyumba
vs. kutumia nch 6, kuna utofaut gan wakitaalam
 
mkuu vip kuhusu kutumia tofali za nch 5 kweny ukuta wa nyumba
vs. kutumia nch 6, kuna utofaut gan wakitaalam
Ukitumia tofali za nchi 6, kuta zako baada ya kupigwa plaster (ndani na nje) zitakuwa na upana wa almost nchi 7

Dirisha la grill huwa linatengenezwa kwa kutumia square pipe za nchi 1, na huwa linaflash na nyuso za kuta za ndani

Dirisha la Aluminium, profile zake huwa zinatofautiana upana, zipo za nchi 3, 4 na zipo zingine pana zaidi. Hizi nazo zinaflash na nyuso za kuta za nje.

Ukichukua hiyo nchi 7 ukatoa nchi 1 ya grill na nchi 3 ya aluminium profile utabakiwa na space ya nchi 3 (ambapo kwa hii case utaweza kutumia hata grill za 1¼ square pipe au ukatumia dirisha lenye profile za nchi 4 na bado nafasi kati grill na aluminium window ikabaki)

Kwa upande wa milango, upana wa fremu kawaida huwaga ni kuanzia nchi 4, kama utaweka geti la grill kwa kutumia square pipe za nchi 1 maana yake mpaka hapo una jumla ya inchi 5, nafasi kati ya geti na mlango itakuwa nchi 2

Kuna sehemu zingine unakuta wametengeneza kingo za plaster kwa nje kuzunguka madirisha ili dirisha za aluminium ziweze kukaa kwa sababu upana wa kuta ni mdogo, na profile ni pana

Kiufupi ukuta wako ukiwa mpana, utaweza kuweka milango ya mbao na mageti ya grill au dirisha za grill na aluminium zake za upana unaohitaji bila kuweka hizo kingo nilizosema hapo juu vinginevyo itabidi utumie material yatakayoendana na upana wa kuta zako

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Sio kila mchanga unafaa kwa ujenzi, kuna mchanga mwingine huwa haushikani na cement. Kama unajengea kuta, ukipiga pasi na konobao utaona unapukutika chini
Mchanga mzuri ni ule ambao ukichanganywa na cement, mchanganyiko wake unakuwa unanata kama udongo wa mfinyanzi

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Hizo kazi yake ni kuruhusu mzunguko wa hewa ambapo kama usipoweka, lile joto la hewa iliyopo kati ya paa na dari kipindi jua linawaka inasababisha hewa kuwa na pressure ambayo inaenda kusukuma mikanda ya pembeni ya dari na gympsum board na kusababisha mipasuko ktk maungio
Kwako Imalamawazo hoja imejibiwa kwa hoja!!!
 
Mkuu Hechy Essy binafsi nilikuwa sijaona uzi wako huu. Nimetumia saa nzima kusoma mwanzo mwisho na nimenufaika.
Sasa mkuu naomba unisaidie kuchek hapa kwenye hili jengo kuna makosa gani ya kiufundi yanayoonekana mpaka hatua hiyo.

Pia nikuulize mkuu, vipi nikiwa nanunua material kama mchanga, kokoto na tofali nahifadhi ndani ya hilo jengo hapo likishafungwa linta inaweza kuwa na madhara au kuathiri jengo kwa namna yoyote?
 

Attachments

  • IMG_20240821_114916.jpg
    IMG_20240821_114916.jpg
    1.4 MB · Views: 11
  • IMG_20240718_131125.jpg
    IMG_20240718_131125.jpg
    657.5 KB · Views: 12
  • IMG_20240718_155418.jpg
    IMG_20240718_155418.jpg
    638.6 KB · Views: 13
Mkuu Hechy Essy binafsi nilikuwa sijaona uzi wako huu. Nimetumia saa nzima kusoma mwanzo mwisho na nimenufaika.
Sasa mkuu naomba unisaidie kuchek hapa kwenye hili jengo kuna makosa gani ya kiufundi yanayoonekana mpaka hatua hiyo.

Pia nikuulize mkuu, vipi nikiwa nanunua material kama mchanga, kokoto na tofali nahifadhi ndani ya hilo jengo hapo likishafungwa linta inaweza kuwa na madhara au kuathiri jengo kwa namna yoyote?
Kitaalam hapo kwenye kibaraza ilitakiwa pawe chini kwa kozi moja ukilinganisha na level ya msingi wa nyumba ili mtu akiingia hapo mlangoni (sebuleni) apande step moja. Hizo kozi 5 zinazoonekana kwenye kibaraza ilitakiwa ziwe kozi 4 badala ya 5

Upande wa nguzo, nondo zilizotokeza juu kwa ajili ya kuungana na nondo za juu zina urefu mdogo (angalau zingekuwa zimefika urefu wa futi mbili ili zifungwe ringi 4 kwa nafasi ya sentimita 15)


Kingine cha kuwasisitiza mafundi wako waambie wajitahidi kutumia kobilo pande mbili za tofali maana ukiangalia vizuri hizo kuta utaona kuna tofali nyingi zimeinama. Upande mmoja wa tofali ni kwa ajili ya kuliset tofali likae wima, na upande mwingine ni kwa ajili ya kuliset tofali likae mlalo ulionyooka (horizontal)


Unaweza ukanunua hayo material uliyotaja na kuyaweka humo bila shida yoyote lakini je kiusalama hali inaruhusu?, wanaweza wakawa wanakuibia usiku kwa kusombelea na kuhamisha kidogo kidogo mpaka wakamaliza material yote
View attachment 3129227
 
Back
Top Bottom