yello masai
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 3,927
- 4,199
Mkuu Mungu akubariki sana. Nimeelewa vizuri sana.Kitaalam hapo kwenye kibaraza ilitakiwa pawe chini kwa kozi moja ukilinganisha na level ya msingi wa nyumba ili mtu akiingia hapo mlangoni (sebuleni) apande step moja. Hizo kozi 5 zinazoonekana kwenye kibaraza ilitakiwa ziwe kozi 4 badala ya 5
Upande wa nguzo, nondo zilizotokeza juu kwa ajili ya kuungana na nondo za juu zina urefu mdogo (angalau zingekuwa zimefika urefu wa futi mbili ili zifungwe ringi 4 kwa nafasi ya sentimita 15)
Kingine cha kuwasisitiza mafundi wako waambie wajitahidi kutumia kobilo pande mbili za tofali maana ukiangalia vizuri hizo kuta utaona kuna tofali nyingi zimeinama. Upande mmoja wa tofali ni kwa ajili ya kuliset tofali likae wima, na upande mwingine ni kwa ajili ya kuliset tofali likae mlalo ulionyooka (horizontal)
Unaweza ukanunua hayo material uliyotaja na kuyaweka humo bila shida yoyote lakini je kiusalama hali inaruhusu?, wanaweza wakawa wanakuibia usiku kwa kusombelea na kuhamisha kidogo kidogo mpaka wakamaliza material yote
View attachment 3129227
1. Kutengeneza step moja inayolingana na unene wa kozi moja kwa kutumia hiyo rough floor ni gharama sana, cement na kokoto zitamezwa nyingiMkuu Mungu akubariki sana. Nimeelewa vizuri sana.
Kuhusu kozi moja ya kibalaza hapo nifanyeje mkuu. Au niongeze kifusi ndani nipandishe level ya flour ya mpaka mlangoni kwa urefu sawa na kozi moja?
Pia hii ya kutotumia kobilo na tofali kuingia ndani inaweza kuwa na madhara gani huko mbeleni? Hasa kwenye uimara wa jengo.
Natanguliza shukrani mkuu.
Sidhani kama kuna huo uhusiano wa strength ya tofali na usafirishaji, cha kuzingatia hapo ni ratio tuStrength ya tofali zilizosafirishwa
Nimekuwa na plan ya kupiga tofali za msingi wa ghorofa eneo tofauti na ilipo site kwa sababu ya changamoto ya maji. Plan ni tofali za ratio ya 25 kwa mfuko.
Engineer anasema nipigie palepale site kwa sababu za kusafirisha strength inapungua. Safari ni ya kama kilomita 5 tu hivi
Yana ukweli haya?
Mkuu ni kama umeikia changamoto yangu. Post yangu ya juu kuhusu tofali kupigia mbali na site ilikuwa ni kwa sababu ya kukosa chombo cha kutunzia maji, tofauti na bomba la mamlaka.Kama eneo lako la ujenzi lipo ndani sana (pembezoni mwa mji au mbali na makazi ya watu), usije ukajaribu kununua tank la maji na kuliacha nje ukitegemea kwamba wezi hawatoweza kulibeba
Kwa kesi kama hii, huwa tunachimba shimo na kuliingiza tank kwenye hilo shimo ambapo wezi ili waliibe hilo tank inabidi wachote maji yote na kuyamwaga na kufanya kazi nyingine ya kulifukua
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Ndio unaweza ukafanya hivyo kwa sababu za kiusalama kwamba lisiibiwe, ila kwa kesi yako ukifanya hivi, zoezi la umwagiliaji tofali litakuwa gumu sana maana itabidi mtu awe anachota na ndoo na kwenda kumwagilia tofali moja moja vinginevyo utaingia gharama ya kutafuta pump ya maji.Mkuu ni kama umeikia changamoto yangu. Post yangu ya juu kuhusu tofali kupigia mbali na site ilikuwa ni kwa sababu ya kukosa chombo cha kutunzia maji, tofauti na bomba la mamlaka.
Hapa umenipa akili, kwamba naweza kuchimbia (kwa muda) tenk.
Inaukubwa ganiPLN 0001 2BR
Ramani ya Vyumba Viwili
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana
- Living room (Sebule)
- 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
- 1 Single bedroom
- Kitchen (Jiko)
- Public toilet (Choo cha jumuiya)
Bei: Tsh. 100,000/=
Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Ina mita 9.5 kwa mita 11 ndg, lakini inaweza ikapunguzwa kidogo au kuongezwa kulingana na vipimo vya kiwanja vilivyoInaukubwa gani
Hapo kwa kupaangalia inaonekana ni padogo sana japo sijajua kipimo chake halisi kikoje, upana wa kibaraza ambacho unakusudia kuweka tank la maji juu angalau uzidi futi 8, maana utakapopaua ile overhang ya bati itapunguza ukubwa wa kibaraza kwa angalau futi 1 (mapana na marefu), hivyo utabakiwa na kama futi 7, kati ya bati na tank unaacha tena nafasi japo futi moja, inabaki futi 6 ambayo inatosha kuweka tank la ukubwa wa wastaniHabari mkuu Hechy Essy
Haba nilipozungushia nyekundu ni sehemu ya vyoo. Vipi hizo kuta za nyuma nikiweka nguzo za zege na juu nikamwaga zege kwa ajili ya kiwekea tenk la maji itakuwa sawa kweli?
Mkuu hiyo sehemu iliyotoka nje ni futi 5 kwa maana hstatosha tank la lita 2000Hapo kwa kupaangalia inaonekana ni padogo sana japo sijajua kipimo chake halisi kikoje, upana wa kibaraza ambacho unakusudia kuweka tank la maji juu angalau uzidi futi 8, maana utakapopaua ile overhang ya bati itapunguza ukubwa wa kibaraza kwa angalau futi 1 (mapana na marefu), hivyo utabakiwa na kama futi 7, kati ya bati na tank unaacha tena nafasi japo futi moja, inabaki futi 6 ambayo inatosha kuweka tank la ukubwa wa wastani
Haitoshi ndg, mana hata tank la lita 1000 tu kipenyo chake kinazidi futi 4, na pia inabidi kuachwe nafasi kati ya tank na mwisho wa slab inapoishia, tank lisiwe pembeni sana, itafanya uzito wa tank uegemee upande mmojaMkuu hiyo sehemu iliyotoka nje ni futi 5 kwa maana hstatosha tank la lita 2000