Hii napata kwa bei gani mkuu?Ramani ya vyumba viwili (vyote self), sebule, jiko, dining na choo cha jumuiya
+255(0)624068809View attachment 2969197
Haya sasa mashikolo mageniii 🤣🤣🤣🤣 mambo ya tenaile forces sie tuliokimbia physics hapa bila bilaKatika slab huwa kuna force mbili, tension force na compression force. Zege ni nzuri zaidi katika kuzuia compression forces, huku nondo yenyewe ikiwa nzuri zaidi katika kuzuia tension forces (japo kuna muda zege ikishindwa kuzuia compression forces, huwa tunaiwekea/kuiongezea nondo pia)
Tension force inaact zaidi chini ya slab, na compression force inaact zaidi juu ya slab
Upande wa juu wa slab, kipande cha 1/3L cha kati tensile stress huwa ni ndogo kiasi kwamba huwa tunaweza tukaachana nayo (ndio maana nondo za juu katika hili eneo huwa tunazikata), lakini compression force ni kubwa ambapo yenyewe itakuwa inabebwa na zege
Upande wa chini wa slab, kipande cha 1/3L cha kati tensile stress huwa ni kubwa (ambapo maximum tensile stress hutokea kati kati ya slab) hivyo lazima nondo ziwekwe na ikibidi spacing ya nondo iwe ndogo kuliko spacing ya vipande vya 1/3L vya pembeni (kushoto na kulia)
NB. "L" ni urefu/upana wa slab kutokea katika nyuso za mkanda (beam)
Sasa hizi open kitchen plan za misasa sii ndio majanga mwanawaneNimekuwa nikipokea ramani kutoka kwa watu mbali mbali kwa lengo la kuzifanyia makadirio, kitu ambacho huwa kinanishangaza ni kuona kitchen inakuwa na uwazi unaoangaliana na dining room mbali na milango inayotumika kuingia ama kutoka jikoni (mpaka hapo privacy kwa mpishi jikoni inakuwa hamna, watu wakiwa wamekaa dining wanamuona mtu akiwa yupo jikoni)
Hebu tuangalie kiusalama madhara ya hii design ni nini. Tukuchukulie kwamba una familia yenye watoto (watoto wa primary/secondary etc) na wewe huwa unatoka kwenda zako kazini. Watoto wamerudi kutoka shuleni, na wana access ya kuingia jikoni sehemu ambayo hatari ya moto inaweza kutokea muda wowote pindi uzembe utakapofanyika.
Kama mnavyojua akili za watoto, mtoto anaweza akawasha jiko baada ya muda akajisahau akapitiwa na usingizi au akaenda kucheza na wenzake nje, usalama wa nyumba yako mpaka hapo tayari unakuwa ni wa mashaka, ni Mungu tu ndio anakuwa anatulinda lakini siku yoyote linaweza likatokea la kutokea ukajikuta unapoteza nyumba hivi hivi japo hatuombei iwe hivyo. Kama mtu mzima tu na akili yake timamu anaweza akafanya uzembe kama huu kwa kupitiwa, vipi kwa watoto ambao akili zao bado hazijakomaa?
Jiko kama jiko linatakiwa liwe na milango ambayo ikifungwa hiyo milango kusiwe na access nyingine yoyote ya kuweza kuingia jikoni mpaka ufunguliwe mlango mmoja wapo, chakula kikiiva weka hotpot Dining mezani watoto wakirudi shule watakula bila kuingia jikoni. Fuatilia matukio mengi ya nyumba kuungua moto, utagundua matukio mengi yamesababishwa na uzembe jikoni hasa kwa watu wanaotumia majiko ya gesi na majiko ya umeme.
Mimi mtazamo wangu katika designing ni huo (safety first) na huwa namshauri mtu anapokuja na idea yake jinsi inavyotakiwa iwe (akitaka nidesign kama anavyotaka yeye, mimi huwa nadesign hivyo hivyo lakini najua tayari nimeshamshauri)
Umbali kati ya chemba na ukuta wa nyumba unatakiwa usipungue mita ngapi?Katika ujenzi wa chemba za vyoo, hakikisha kuta zote nne za chemba zinajitegemea (usitumie ukuta wa nyumba kama moja ya kuta za chemba hata kama chemba ipo karibu na nyumba). Utafanya kuta zako ziloane kutokana na maji yanayopita kila mara katika chemba na kupelekea rangi/plaster kubanduka (ukuta kuoza)
Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
Mie nilijuaga ni urembo tuuu🤣🤣🤣🤣Kipindi cha upepo mkali kama hichi, nyumba nyingi bati zake huezuliwa na upepo. Kama nyumba yako hujaweka fascia board, nyumba yako itakuwa katika risk kubwa ya kuezuliwa paa na upepo.
Fascia board ni zile mbao za 1×6,1x8, au 1×10 ambazo huwa zinapigiliwa kuzunguka paa la bati (ambapo mkingio wa maji (gutter) hupigiliwa)
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Ewaaah! Hii ndio nilikuwa naisaka sana.Kumekuwa na matukio mbali mbali ya slab za makaro ya vyoo/visima kushuka/kuporomoka baada ya muda flani.
Ukiona slab ya karo/kisima imeshatengeneza kitu kama sahani kati kati, basi ujue hapo slab yako imeundergo deflection na inaweza ikashuka muda wowote.
Kutokana na ufinyu/udogo wa eneo, watu wengi huwa wanaweka mabanda ya mifugo au parking ya magari juu ya haya makaro kitu ambacho ni hatari kama slab itakuwa ipo katika risk ya kushuka
1. Unene wa zege la slab hautakiwi kuwa mkubwa sana kwa sababu unene unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo uzito wa slab unavyozidi kuongezeka. Unene wa nchi 5 mpaka 6 unatosha, sasa wengine slab wanaweka mpaka nchi 8
2. Nafasi kati ya nondo na nondo (spacing) isiwe kubwa sana. Weka spacing ya 15cm mpaka 20cm tu, mafundi wengine wanaweka spacing mpaka 30cm ili wabaki na pesa nyingine ya nondo wagawane (hivi vitu kama huna ujuzi navyo, mafundi wanaweza wakawa wanavifanya mbele yako huku wewe mwenyewe unaona)
3. Usiweke mfuniko wa karo kati kati ya slab kwa sababu kati kati ya slab ndipo maximum deflection ya slab hutokea, hivyo nondo hazitakiwi kukatwa ili kuacha huo uwazi wa mfuniko, uwazi wa mfuniko wa karo weka pembeni kabisa
Ili kuepuka hiyo hali, ni vizuri ukaweka cross beams ambapo utakuwa salama zaidi
Mfano kama karo lako ni la duara, mkanda mmoja unajenga kutokea kaskazini kwenda kusini na mkanda mwingine unajenga kutokea mashariki kwenda magharibi ambapo zinakuja kukutana kati kati kutengeneza alama ya jumlisha (+). Hizi ndio tunaita cross beams, ambapo slab inakuja kulala juu yake
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
So mchanga amaluf ndio unamwaga zege la blainding?Huwa tunaanza kumwaga mchanga kabla ya kulaza tofali za msingi ili kutengeneza tabaka (layer) kati ya udongo na tofali lakini pia inaleta urahisi katika zoezi la kuset tofali (kulikandamiza tofali katika mchanga ili likae level ni rahisi kuliko kulikandamiza kwenye udongo)
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Hizi kwenye masuala ya kiyoyozi i akuwaje? Ubaridi haupotei kwa haraka?
Kibalaza mwisho tank la litre ngapi i aweza beba? Au na ye yewe upige cross beams ili kubeba uzito zaidi?Ili kuepuka gharama za kujenga mnara wa tank la maji, kibaraza cha mbele au cha nyuma juu weka zege badala ya bati ili upate nafasi ya kuweka tank juu
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Okay kumbe ni kama maofisini tuu huku, sometimes unaenda kula chakula cha mama ntilie na mlinzi pale alafu unamnunulia glass ya mtindi na ndizi asugumie ubwabwa.Ili mafundi wafanye kazi kwa moyo wote, siku moja moja jaribu kufanya majukumu ambayo wenyewe wanajua kabisa sio majukumu yako kuyafanya.
Mfano siku moja unaweza ukawaagizia chakula, pesa ya chakula ukawalipia wewe. Siku nyingine unaweza ukawanunulia hata matunda ukawapelekea site.
NB: Usifanye hivi mwanzoni, kwa sababu wataweka akilini kwamba suala la chakula kwao ni jukumu lako kuwanunulia, kwa hivyo siku ukiacha kuwanunulia utakuwa umewadisappoint na kuwavunja moyo. Acha kwanza wajinunulie chakula wenyewe siku za mwanzoni ili wajue kwamba suala la chakula ni jukumu lao, uwe unawanunulia tu siku moja moja (iwe kama surprise kwao)
Hii katika Construction Management tunaita Motivation
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Yah, siku moja moja unawapelekea hata matunda. Ukiwathamini, watafanya kazi yako kwa moyo wote lakini wakiona hauwathamini, wanaweza wakakuharibia kazi yako makusudi hata kama unawalipaOkay kumbe ni kama maofisini tuu huku, sometimes unaenda kula chakula cha mama ntilie na mlinzi pale alafu unamnunulia glass ya mtindi na ndizi asugumie ubwabwa.
Kwa mahesabu uliyotupa na nondo hizi hakomolewi mtu hapa. Wanamwaga zege la columns tayari najua kabisa mifunko mingapi inahitajika, mchanga kiasi gani na kokoto kiasi ganiUkishinda site kinachofata ni kukukomoa, mahali ambapo panahitajika mifuko mitatu ya cement, wenyewe watachanganya mifuko mitano. Lengo lao hasa ni kukutia hasara zaidi baada ya wewe kuamua kuwabana kupita kiasi
Kumbeee hapa ndio ninalpfeliiii.Usiogope kujenga nyumba ya ndoto yako kwa sababu ya uchumi mdogo
Unachotakiwa kufanya ni kujenga msingi wote kwanza, kisha huku juu unakuwa unainunua boma kidogo kidogo kwa kuacha matoleo ya tofali sehemu zote ambazo zitahitaji kuunganisha kuta baadae.
Ukifanya hivi, utajikuta unakamilisha ujenzi ndani ya muda mfupi (miaka miwili, mitatu n.k) kwa sababu utakuwa unajenga kwa malengo tofauti na kusubiri upate pesa yote mara moja kwa mkupuo ndipo uanze ujenzi
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Umepigaje hapo kwenye round colum 4 imerokea wapi tena jamani hesabu hizi wenhine tulikimbiaJe wajua nguzo ya duara ambayo kipenyo chake kinalingana na upana wa nguzo ya mraba inatumia zege kidogo ukilinganisha na kiasi cha zege kitakachotumika katika nguzo ya mraba
Nguzo ya mraba (230mmx230mmx3m)
Ujazo, Volume (m³)= 0.23mx0.23mx3m = 0.15m³
Nguzo ya duara (230mm diameter, 3m height)
Ujazo, Volume (m³) = (3.14x0.23²)/4×3m = 0.125m³
Tofauti = 0.15m³ - 0.125m³ = 0.025m³
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Alooh! Lazima uchoke mwanawane. Pumua kwanza🤣🤣🤣🤣Hizo Kona za Kuta Kuna joint ya zenge yenye vikokoto vidogo dogo vyeusi. Na sio Nguzo ya zege.
Hizo joint za zege hazijaanzia kwenye kwenye msingi.
Hizi nyufa Kuna sehemu zipo kwenye msingi na kuna sehemu zipo kwenye ukuta wa boma na Kuna ufa, mwingine upo kwenye Nguzo ya tofari yenye kona Moja kwenye verandah sasa ile joint ya zege inaufa pia tena mkubwa 😥
Maumivu everywhere..
Kwahiyo huu msingi ilibiidi baada ya kozi nne niweke mkanda na nikimaliza pia pale kozi ya mwisho niweke mkanda? Jamani ngojeni nipumue
Kuna hotel moja ipo kigoma aisee jamaa alivyo manuva ile slope na kutoa kitu hatari sana.😂😂 usiichungulie sana pesa, huwa siku zote haitoshi. We fumba macho imalize, hayo makosa yanarekebishika vizuri tu
Mm huwa napenda plot ambayo Ina slope kubwa kama yako huwa ndio zina aesthetic views, na tena hapo kwenye msingi wa kozi tisa, ungefanya manuva vizuri na kuongeza kidogo ungetengeneza basement moja kali tu, angalia pia hata garden zinazokua kwenye slope plots jinsi zinavyovutia
Hiyo imetoka hapaUmepigaje hapo kwenye round colum 4 imerokea wapi tena jamani hesabu hizi wenhine tulikimbia
Mweeh! Hapo bado bila bila mwanawane.Hiyo imetoka hapa A= πR².....eqn (1), where R= D/2
A= π(D/2)²
A= πd²/4
Fundi wetu hawa .entality yao ni kumaliza na kusepa hawana jingineKutokujua tu na pia fundi huwa wanatakiwa kujiongeza, fundi mzuri asingejenga hivyo
Hii ya kifusi then mawe then mchanga then zege ni kwa majengo yote au ghorofa tuuKabla ya kumwaga zege la jamvi chini, hakikisha unamwaga mchanga wa kutosha. Usiruhusu zege yako igusane moja kwa moja na udongo maana huwezi jua udongo una madini gani ambayo yanaweza kupambana na cement na kuua au kupunguza nguvu yake
Hata kama utakuwa umeweka mawe, mchanga pia inabidi umwage juu ya mawe ili uende kuziba nafasi iliyopo kati ya jiwe moja na jiwe lingine (wakati mwingine zege inashindwa kupita katika hizi nafasi hivyo usipomwaga mchanga, chini kutabaki matundu mengi)
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane