Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Yah, hizi scenario zipo nyingi sana..mfano mwingine unaweza ukakubaliana na mafundi kujenga msingi wote mpaka jamvi, sasa wakishamaliza kujenga kuta za msingi usishangae fundi akakuambia utafute watu wa kujaza kifusi ili baadae waje wamalizie kazi ya kumwaga jamvi (wakati huo wewe unajua pesa mliyokubaliana na fundi inajumuisha kila kitu)
Kweli mwanawane inabidi kuwa specific.
 
Kwenye kiwanja changu kulikuwa na kichuguu cha siafu nimefanikiwa kumaliza kujenga msingi

Naombeni msaada wenu nifanye nini ili wasije kunisumbua baadaye
 
Nikuibie tu siri mpenzi msomaji, kuna punguzo kubwa la bei za ramani msimu huu wa sikukuu na mwaka mpya, wahi sasa kabla muda wa offer haujaisha ujipatie ramani kwa bei ya punguzo
Mzeya ukishachora ramani na building permit wamtafutia mteja?
 
Mahali ambapo kuta mbili zinakutana kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa nyufa, hii ni endapo ukuta mmoja wapo utashuka chini na ukuta mwingine ukabaki vile vile au kuta zote zikashuka chini lakini kwa viwango tofauti (unequal settlement) so mara nyingi huwa tunapendelea kuunganisha kuta kwa kutumia nguzo...mbali na hivyo, nguzo zinasaidia sana kuongeza uimara wa jengo kwa sababu uwezo wa tofali kuhimili mzigo ni tofauti na uwezo wa zege.
Ata hizi nyumba zetu za kawaida kwenye kona tuweke nguzo ya zege?
 
Katika ununuzi wa bati, usiridhike kukagua bati za juu tu...kagua bati moja baada ya nyingine ili uone kama bati zote ni gauge ile ile uliyokusudia kulipia. Unaweza ukachanganyiwa bati za gauge 32 kati kati ya bando wakati umelipia bati za gauge 30 au gauge 28, mahali popote penye pesa ujanja ujanja huwa haukosekani
Hasa mbongo akiwepo around 🤣🤣🤣
 
Ndio, uwezekano upo inategemea na namna ya ujenzi lakini na bei pamoja na aina za material yaliyotumika maana boma pekee material cost inarange kwenye 7milion to 8M..mfano wengine mkanda wa chini hawaweki kwa hivyo kuna saving anakuwa amefanya
Huu mkanda wa chini ni lazima ukizi gatia say mie nafyatua tofali 25 kwa mfumo mmoja wa cement?
 
Chukulia mfano tofali ni 3500 (hapo tayari 3.5M), chukua cement za kujengea mifuko 70 (hiyo ni 1,225,000/=), nondo 50 mkanda wa chini na wa juu (hiyo ni 1,300,000/=) mpaka hapo ni almost 6M+...bado kokoto, mchanga na vitu vitu vingine (ukija kwenye kupaua napo kuna shughuli, bati tu kama bati unaacha 2M+, bado mbao n.k
Duh mbona hela nyingi hivyo jamani tutaje ga kweli...mbona mnatukatisha tamaa mwisho tukazime hela kwa mbususu
 
4 bedroom house
  • Master 1 yenye kibaraza chake, unaweza ukaingia ama kutokea mlango huo (ramani nzuri sana kwa wadaiwa sugu)
  • Self 1
  • Single 2
  • Jiko
  • Dining
  • Store
  • Library/Pray room
  • Public toilet 2

Chumba cha master kipo mbali sana na vyumba vingine, hata kitanda kikiwa kibovu kunakuwa hakuna shida yoyoteView attachment 2898139
Kwamba kitanda kitakia kwichikwichi wakati mama yeyoo anampa baba tamuuu🤣🤣🤣🤣
 
4 bedroom house
  • Master 1 yenye kibaraza chake, unaweza ukaingia ama kutokea mlango huo (ramani nzuri sana kwa wadaiwa sugu)
  • Self 1
  • Single 2
  • Jiko
  • Dining
  • Store
  • Library/Pray room
  • Public toilet 2

Chumba cha master kipo mbali sana na vyumba vingine, hata kitanda kikiwa kibovu kunakuwa hakuna shida yoyoteView attachment 2898139
Hili bangalow sii hatari...vyumba vinne then kuna library na public toilet 2...loh hapa gbarama sii inafika million 200
 
Mafundi wengi wanatumia pipe level kwenye kozi ya mwisho (mfano kama msingi una kozi 7, basi ile kozi ya 7 ndio wanaitafutia level). Sasa kuna muda inatokea upande mmoja unadai udongo mwingi (mortar thickness) ili kufikia level ya upande mwingine hivyo inashauriwa utumie pipe level angalau katika kozi mbili kabla ya kuifikia ile kozi ya mwisho ili in case kama kuna upande utadai udongo mwingi uweze kubalance katika hizo kozi kuliko kurundika udongo sehemu moja katika kozi ya mwisho

Ramani, Makadirio na Ushauri tuwasiliane
Kwani level haitafutwi tangu kozi ya kwanza ya maingi mzeya?
Alafu hii level, kweli mzungu hajaja nankifaa cha kidigital cha kupima **** matofali yapo level?
Maana kama mie mzabzab na akili zangu za kichwa zha panzi nimeweza waza hilo jambo basi mzungu atakuwa ameshalifanyia kazi kitambooo
 
Nasisitiza Tena, "hata kitanda kikiwa kibovu kunakuwa hakuna shida yoyote".

Sio mko kwenye shughuli zenu za "kubovusha" kitanda Watoto au family members wengine wanawasikia.
Watoto wanasimia mama yao anavyo shenyentwa 🤣🤣🤣🤣
 
Uzito wa tofali la juu ubebwe na tofali mbili za chini, na huo uzito usiegemee kati kati ya tofali kwani tofali ni rahisi kukatika sehemu ya kati kuliko sehemu ya pembeni. Kiufupi tofali la chini libebe 75% ya uzito wa tofali moja na 25% ya uzito wa tofali lingine, lisibebe 50% kwa 50% ya uzito wa kila tofali
Hapa sasa mukide👍
 
Bado 4 ipo katika range ya 1 mpaka 6. Katika ujenzi muda ni mali sana, ndio maana hata kwenye ujenzi wa maghorofa huwezi ukakuta watu wanasubiri zege ikae siku 28 ndipo waendelee na ujenzi kwa hatua inayofata.

Kwanza hakuna fundi utakayemuuzia kazi halafu umuambie ajenge sijui kozi 4 au kozi 3 kwa siku, fundi atatumia siku nyingi kumaliza kazi na mwisho wa siku itakuja kumkata yeye mwenyewe. Tuchukulie mfano hizo kozi 4 kama ndio wamemaliza kujenga saa saba mchana, ina maana mafundi wasimamishe kazi warudi tena kesho kuendelea na kazi?

Ila kama hela ipo, mnaweza mkakubaliana kwa hayo masharti na kazi ikafanyika tu bila shida. Pamoja na uharaka wa mafundi wa kumaliza kazi, lakini wao wenyewe pia wanaelewa kwamba ikishafika hatua flani huwezi kuendelea tena juu, utaona tu wanaanza kupumzika mmoja mmoja hata kama ni saa kumi jioni
So this means kwa kiwanza flat msingi nadni ya siku moja kwishney?
 
Naanza na hiyo nyufa ambayo haijapigwa plaster

Hiyo nyufa bila shaka ilitokea wakati wa umwagaji wa zege, ambapo sehemu hiyo, zege iliyowekwa ilikuwa na maji mengi kwa hivyo hiyo sehemu ya chini ambayo ilikuwa na maji mengi ikashuka chini na hiyo sehemu ya zege ambayo ilikuwa ina ukavu kiasi ikawa imebaki juu (slump). Hizi kitaalam tunaziita shrinkage cracks.

Katika uchanganyaji wa zege, maji yanatakiwa yasizidi kipimo kinachotakiwa ambacho ni nusu ya uzito wa kiasi cha cement kilichotumika, maji yakizidi yanafanya kokoto zizame chini na kufanya sehemu ya juu isiwe na kokoto kabisa au iwe na kokoto chache kwa sababu kokoto zina density kubwa kuliko maji. Hii kitaalam tunaita Segregation

Hicho kipande cha juu cha tofali kilichovunjika, kuna uwezekano mkubwa wakati wa kukata tofali kikawa kimepata nyufa hivyo fundi akaona uvivu kukata kingine akaamua kukiweka hivyo hivyo. Nyufa imeendelea kukua ikiwa hapo hapo baada ya kufyonza maji mengi. Nimeassume hivi kwa sababu juu ya hicho kipande hakuna mzigo wowote juu yake kusema labda imeshindwa kuhimili huo uzito

Kingine fundi alikosea kuweka hilo tofali juu ya uwazi, ilitakiwa liwekwe katika namna ambayo uzito wake utakuwa umebebwa na tofali mbili za chini na sio hivyo alivyoweka (hii pia inaweza kuwa sababu ya hiyo sehemu kupata ufa kwa sababu upande wa kushoto wa tofali unakosa balance (kama ratio ya udongo ingekuwa ndogo, nyufa inngekatikia hapo hapo kwenye maungio ya tofali na mortar)
Hapo kwenye cement na maji mean kwa mfano umetu.ia mfuko mmoja wa cement ambao ni 50kg kwenye zege, itabidi nitumie litre 25 za maji?
 
Bei ya mlango mmoja wa mbao pamoja na frem yake ni kati ya 400,000 mpaka 500,000 (mlango 250,000 na kuendelea, frem 150,000 na kuendelea kutokana na ukubwa wa mlango na aina ya mbao zilizotumika)

Kama nyumba yako ina milango 10, maana yake utatumia zaidi ya milion 5 kwenye milango tu

Ili kupunguza gharama, sehemu ambazo hazina ulazima wa kuwekwa mlango, milango usiweke

Mfano, kama kwenye Store ya jiko mtu hawezi kuingia mpaka afungue mlango wa jikoni, basi hakuna ulazima wa kuweka mlango wa kuingilia store

Idadi ya milango inategemea na design ya mpangiliovwa nyumba

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Eeh mbona huyu fundi ananiambia mlango complete frame na top niandae million 1 mbao mkongo.
 
Eeh mbona huyu fundi ananiambia mlango complete frame na top niandae million 1 mbao mkongo.
Itakuwa umeangukia kwa dalali au labda anakuchekecha kwanza ili ukilia ukilia udondokee pale pale kwenye bei anayotaka yeye. 1M ni too expensive hata kama ni mbao ya mninga.

Tafuta wauzaji wengine ili ufanye comparison ya bei zao
 
Bro unahangaika sana kutafuta umaarufu, na kwa bahati mbaya nyuzi zako zinakosa attention kwa wasomaji. Unaanzisha nyuzi kila lisaa na bado watu hawakuzingatii, lengo lako hasa ni kutafuta umaarufu

Najua umekuja na humu baada ya kuona humu kuna views nyingi, sasa mimi sio mtu wa ligi...we kwa akili ya kawaida, kati ya plaster na hiyo mortar inayounga tofali ni kipi kinamfunika mwenzake?

Na kama ratio ya mortar ya kujengea tofali inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya plaster, hiyo plaster unapiga ya kazi gani? Yani ni sawa na kumuweka Paka ili amlinde Simba

View attachment 2950235
Paka amlinde simba tena 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom