Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ukienda kununua kiwanja, beba futi kamba (tape measure) yako mkononi ili uhakiki vipimo. Kuna ujanja huwa unafanyika na wauzaji viwanja, tape inakatwa kipande hata cha mita mbili kisha tape inaungwa tena kwa gundi. Mnapima urefu wa kiwanja mnapata mita 18, kumbe kiuhalisia ni mita 16 (mita 2 hazipo)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Miaka ya nyuma, ilikuwa unakuta nyumba ina choo na bafu lakini miaka ya sasa vyoo vinajengwa 2 in 1 (choo kinatenganishwa sehemu mbili kwa step moja ndogo, ambapo sehemu inapokaa sink la choo inakuwa juu, na sehemu iliyobaki ambayo inakuwa chini inakuwa ni sehemu ya kuogea)

Iv kiongozi shimo la choo kikawaida inatakiwa kuwa na urefu gani na je kujenga shimo moja na mawili bora ni ipi hapo
 
Kawaida kina huwa ni futi 12, japo kuna muda mtu anaweza akachimba akakutana na maji kabla ya kufikia hicho kina (hapa itabidi uongeze marefu ya karo ili kufidia futi zitakazopelea kufikia hicho kina)

Kila shimo lina kazi yake, kama uchumi unaruhusu chimba mashimo yote mawili lakini kama uchumi hauruhusu, chimba shimo moja (shimo la pembe nne)
 
Ok shukran mbona naona watu wengi wanasema mashimo ya round ndo mazuri kuliko pembe nne unaweza ukaniambia lipi zuri kati ya round au pembe nne
 
kila moja lina kazi yake. ila la muhimu ni hilo la pembe nne. hilo hujulikana kama septic tank. Lina kuwa na mfumo ndani unaosaidia kuvunjavunja kinyesi ambapo humo ndani kuna anaerobic bacteria wanao saidia kuchakaa hicho kinyesi na maji hupita kwenye mfumo mwingee na hapo ndo umuhimu wa shimo la pili linapotokea ambalo lenyewe linatakiwa kujengwa kwa staili ya kuruhusu maji kupaculate arthini kidogo kidogo.

hilo shimo la kwanza ni la muhimu sana kama uchumi hauruhusu jenga hilo la kwanza vizuri. shimo la pili unaweza tengeneza kitu kama fench drain, ambapo ni mtaro mkubwa unao pangwa mawe au maburungutu na kufunikwa na nailoni kisha kufukiwa juu, humo ndani yanaenda maji tu kinyesi chote kinabaki kwenye mfumo wa kwanza.
 
hii ya kupanga mawe ninzuri ili kuepukana na adha ya kutumbukizwa kwenye mashimo na wezi
 
Iv kiongozi shimo la choo kikawaida inatakiwa kuwa na urefu gani na je kujenga shimo moja na mawili bora ni ipi hapo
Kama nilivyosema awali, kila shimo lina kazi yake

Kama utaweka shimo moja (la pembe nne), maana yake hilo shimo litachukua muda mfupi kujaa ukilinganisha na mtu aliyeweka mashimo yote mawili kwa sababu maji yake yatakuwa hayana mahali pa kwenda, lakini kama ukijenga mashimo yote mawili, maji yatakayojaa kwenye shimo la pembe nne yatapelekwa kwenye shimo la duara (ambapo hili shimo la duara pembeni huwa linaachwa matundu kwa ajili ya maji kupotelea ardhini)

Haya mashimo ya kisasa ujenzi wake ni kama ilivyo mashimo ya pembe nne (hawaachi matundu pembeni), lakini pia ikumbukwe tofali zake hazijengwi kwa udongo (mortar) kwa hivyo maji yake yanakuwa yanapotelea ardhini kupitia upenyo uliopo kati ya tofali na tofali japo pia huwa wanaweka na shimo lingine pembeni kwa ajili ya kupokea maji yanayotoka kwenye shimo la kwanza
 
Una maoni yoyote kuhusu shimo lenye chamber 3. Kami hili. Maji taka yanapitia chamber 3 kabla ya kwenda soakway.

1741015246403.png

1741015831818.png
 
Una maoni yoyote kuhusu shimo lenye chamber 3. Kami hili. Maji taka yanapitia chamber 3 kabla ya kwenda soakway.

View attachment 3257694

View attachment 3257716
Kwa hapo sijajua kazi ya hiyo chamber ya tatu inayofuata (labda tukiona namna ilivyojengwa huko chini, isije ikawa hiyo chamber ya tatu inatumika kama soak way pit)

Kawaida shimo la septic linakuwaga na sehemu mbili, ambapo kati kati kunakuwa na ukuta unaozuia taka yabisi (solid waste) zisiende kuingia katika chamber inayofuata na matundu yake katika huo ukuta huwa yanakuwa juu kama ilivyo hapo kwenye picha kwa sababu maji ya chooni huwa yanajitenga katika matabaka matatu (ambapo tabaka la kati ndio maji yenyewe ambayo tunataka yaende katika soak way pit)
 
Nilivyoelewa ni kwamba ukiongeza idadi ya chamber kabla ya soakway unaongeza uwezekano wa kupata maji safi mwisho wa mchakato.
 
Attachments

  • 3_Chamber-Septic-Tank.mp4
    6.2 MB
Baada ya kupanga mawe (hardcore) katika msingi, inashauriwa umwage mchanga mwingi ndipo uje umwage zege la jamvi (oversite concrete). Hii ni kwa sababu unapopanga mawe, ile nafasi iliyopo kati ya jiwe na jiwe zege inaweza isipite kwenda kuziba hizo nafasi. Kama hiyo sakafu itapata mgandamzo mkubwa (mfano gari ikapita) inaweza kusababisha hiyo sakafu kutitia kutokana na uwepo wa uwazi (matundu) uliopo chini yake

Kama unahitaji ramani za kitaalamu na makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
Yale mawe yanayojazwa kwenye msingi huwa yana kazi gani, na kuna tatizo kama utaamua kujaza mchanga pekee badala ya udongo au mawe?.
 
Nami ningependa kujua haya mawe yanaongeza nini maana naona si kila project inatandika mawe kabla ya kumwaga zege. Labda mwenye uzoefu wa miradi ya serikali anaweza kutujuza. Mawe ni lazima au hapana?
 
room ngapi apa na ina mita ngap kwa ngap
Room tatu, vyumba viwili ni self room, kimoja ni single room, sebule, jiko, na dining. Ukubwa ni mita 10 kwa 12 ila vyumba vyake ni vya wastani, nimeitengeneza kulingana na ukubwa wa kiwanja cha mteja pamoja na mahitaji yake

Tunaotumia App ya JF, hatupati kabisa notification mpaka tuchungulie kama hivi ndio mana nachelewa kujibu
 
Back
Top Bottom