Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kama store haipo, na kuna uwezekano wa kuongeza ukubwa wa jiko, ukiongeza ikafika angalau futi 10 kwa 10 ambayo ni sawa na mita 3 kwa 3 itakuwa vyema zaidi

Upande wa vyumba, kama itawezekana weka futi 11 kwa 11, ikishindikana kabisa weka futi 10 kwa 10. Ukiweka size ya futi 11 kwa 11, utaweza kuweka hata vitanda viwili vya futi 4 kwa 6 na kati kati ya vitanda pakabaki nafasi ya futi 3 kama njia, nafasi itakayobaki upande wa pili utaweza kuweka meza ndogo ya kusomea au hata kabati la nguo
Asante sana kiongozi
 
It's a new year 🎊 🎊 🕛 🕛 Tuko pamoja kiongozi.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Kama ikitokea mfuko wako hauruhusu kuweka tiles katika kuta za vyoo/bafu, basi una option nyingine ya kupaka NILU (Cement paste) ukutani.

Nilu ni mchanganyiko wa saruji (cement) na maji, ambapo mchanganyiko huo unatengeneza uji uji mzito. Nilu katika kuta hutengeneza kitu kama kioo hivyo inasaidia kuzuia kuta zisifyonze maji na pia hufanya kuta zisafishike kirahisi

Nilu pia hutumika kwenye sakafu ambayo haijawekwa tiles, ambapo hata mafuta yakimwagika sakafuni, utaweza kusafisha kwa kufuta tu bila kuacha doa
 
Mafundi wengi hawawezi kutumia mchoro wa boma (floor plan) kusetia msingi, huwa wanadhani kwamba center lines za kuta za boma na center lines za kuta za msingi zote ni sawa kitu ambacho sio sahihi

Sio kuta zote za boma zitapita kati kati ya kuta za msingi, kuna kuta zingine inabidi zikae pembeni ya kuta za msingi mfano kuta zote za nje lakini pia hata baadhi ya kuta za ndani ambazo zimeungana na kuta za nje nazo inabidi ziwe pembeni

Faida na hasara ya kutumia center lines za mchoro wa boma kama center lines ya kuta za msingi ni kwamba kuna baadhi ya vyumba vitaongezeka ukubwa na kuna vingine vitapungua ukubwa kutokana na kuhama hama kwa kuta za boma
 
Boma la nyumba ya paa lakusimana inaweza kugeuzwa paa lakuficha baada ya kujengwa
 
Boma la nyumba ya paa lakusimana inaweza kugeuzwa paa lakuficha baada ya kujengwa
Hapana ndg, hizi nyumba mifumo yake katika ujenzi ni tofauti
Nyumba za paa la kuficha zinakuwa na kozi nyingi kutoka mkanda wa chini mpaka mkanda wa juu ili kuongeza height ya nyumba maana bati lake linakuaga karibu sana na dari, lakini kwa nyumba za paa la kuonekana zinakuwa na kozi chache

Na pia kwenye nyumba za paa la kuficha, juu ya mkanda wa juu napo kunakuwa na kozi nyingi tofauti na nyumba za paa la kuonekana

Katika nyumba za paa la kuficha, inatakiwa mtu ajue maji ya kwenye bati yatakuwa yanadondokea wapi ili aone ni ukuta gani utabeba mfereji wa maji kule juu, hii ni tofauti na nyumba za paa la kuonekana ambapo mtu anajenga tu vyovyote
 
Matundu katika kuta za msingi yanatakiwa yawekwe katika namna ambayo mtu akichora mstari wa kuunganisha hayo matundu, maumbo ya pembe tatu yatengenezeke kupitia hiyo mistari kwa maana ya kwamba matundu mengine yawe chini, na matundu mengine yawe juu kwa kupishana (yasifuatane kwa wima) ambapo mstari wa chini ndio utakuwa na matundu mengi kuliko mstari wa juu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ili kupunguza errors wakati wa kuset jengo, ni vizuri ukatumia misumari midogo (nchi mbili na nusu), lakini pia kamba ziwe nyembamba sana (usitumie kamba za kuanikia nguo). Na pia kama utatumia mbao kusetia, nunua mbao ndefu za futi 18 au zaidi
 
Ukipita site nyingi, utaona nondo za nguzo (column) zinachomekwa tu kwenye udongo bila kumwaga zege la kitako kitu ambacho sio sahihi

Nguzo zinabeba mzigo, achilia mbali uzito wake wenyewe hivyo inatakiwa ziegemee sehemu ambayo ni imara ili zisititie kwenda chini na kusababisha nyufa kati ya nguzo na kuta

Tofali za msingi zinazoenda kushikana na nguzo zinatakiwa zilale juu ya zege la kitako cha nguzo, na sio kwenye udongo
 
images.jpeg

Wakuu naomba ufahamu. Hii wing ya kulia gutter yake imebebwa na nini kwenye ukuta wa upande ulioungana na ghorofa (palipowekwa rangi)? Je, kuna kuta mbili upande huo, kuta iliyopiliza upper floor na kuta iliyopepa gutter?
c.c Hechy Essy
conductor
 
View attachment 3226860
Wakuu naomba ufahamu. Hii wing ya kulia gutter yake imebebwa na nini kwenye ukuta wa upande ulioungana na ghorofa (palipowekwa rangi)? Je, kuna kuta mbili upande huo, kuta iliyopiliza upper floor na kuta iliyopepa gutter?
c.c Hechy Essy
conductor
Kama majengo yameungana, hapo ukuta utakuwa ni mmoja tu ambao ni huo mrefu unaoenda mpaka juu, lakini kama majengo hayajaungana basi kila jengo litakuwa na ukuta wake (ilitakiwa picha ipigwe ubavuni ili kuona vizuri namna ilivyokaa)

Kwa jinsi paa lilivyokaa, kuna uwezekano hii nyumba ya chini ikawa ina ukuta wake maeneo hayo (kila jengo lina ukuta wake) au chini kutakuwa na ukuta mmoja lakini juu ukuta wa jengo la ghorofa ukawa umeingia kidogo ndani (kwenye slab) ili kupata nafasi ya kuweka gutter kwa jengo la chini
 
chini kutakuwa na ukuta mmoja lakini juu ukuta wa jengo la ghorofa ukawa umeingia kidogo ndani (kwenye slab) ili kupata nafasi ya kuweka gutter kwa jengo la chini
Hapa umeniongezea kitu kingine. Asante mtaalamu
 
Hapa umeniongezea kitu kingine. Asante mtaalamu
Majengo ya half-storey, paa la chini ambalo linaenda kuchora mstari wa mlalo (180°) katika kuta linatakiwa litengeneze angle zaidi ya 90 (Obtuse angle) na ukuta ambao paa linaenda kuangukia (angle ya nje)

Hii picha inaonesha upande wa paa unaoenda kugusa ukutani unatengeneza angle ambayo haizidi wala haifiki angle 90 kwa hivyo paa la chini haliwezi kwenda kugusa ukuta vinginevyo itakuwa imetengeneza mfereji katika maungio ya bati na kuta
 
Ukienda kununua kiwanja, tafuta kiwanja ambacho marefu na mapana yake yanawiana kiasi flani mfano 20m x 25m, 30m x 30m n.k (kiwanja kisiwe chembamba mfano 10m x 20m n.k)

Maeneo mawili yanaweza kufanana square meters lakini yakatofautiana mzunguko (circumference). Sasa eneo zuri katika hayo mawili ni lile ambalo linakuwa na mzingo mdogo

Mfano
Kiwanja "A" (20m x 30m)
Eneo= 20m x 30m = 600m²
Mzingo = (20m + 30m)×2 = 100m

Kiwanja "B" (40m x 15m)
Eneo = 40m x 15m = 600m²
Mzingo = (40m + 15m)×2 = 110m

Kiwanja "A" kina mzingo wa mita 100, wakati kiwanja "B" kina mzingo wa mita 110 kwa hivyo kama ungekuta hivi viwanja ndio vimebaki huko site, basi kiwanja kizuri ni kiwanja "A", pia hata ukijenga uzio (fence), kiwanja "A" kitatumia tofali chache kulinganisha na kiwanja "B" lisha ya vyote kuwa na SQM zinazofanana

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Minimum distance kwa ukuta ambao unasimama wenyewe ni sentimita 45 ambayo ni sawa na urefu wa tofali moja zima, kama distance ya mahali ambapo ukuta unatakiwa ujengwe ni chini ya 45cm (mfano 20cm, 30cm n.k) basi ni bora sehemu hiyo ukatumia nguzo ya zege badala ya tofali

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Minimum distance kwa ukuta ambao unasimama wenyewe ni sentimita 45 ambayo ni sawa na urefu wa tofali moja zima, kama distance ya mahali ambapo ukuta unatakiwa ujengwe ni chini ya 45cm (mfano 20cm, 30cm n.k) basi ni bora sehemu hiyo ukatumia nguzo ya zege badala ya tofali

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
fafanua zaid sijaelewa
distance kutoka wapi kwenda wapi
 
Back
Top Bottom