Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

nilisoma mara 5 sielewi 🤣 ikabidi niulize tu

nilijua ukuta wa fence si ndo unasimama wenyewe
images (3).jpeg

Hapana, fikiria huo ukuta kati ya dirisha na mlango. Mtaalamu anasema urefu usipungue 45cm. Chini ya hapo bora kumwaga zege
 
View attachment 3236419
Hapana, fikiria huo ukuta kati ya dirisha na mlango. Mtaalamu anasema urefu usipungue 45cm. Chini ya hapo bora kumwaga zege
Ubarikiwe sana ndg kwa kunisaidia kuweka picha, nina imani wengi pia walikuwa hawajaelewa lakini kupitia hii picha watakuwa wameelewa

Hapo ujenzi wake wa huo ukuta unatakiwa uwe kama unavyoonekana kwenye hivyo picha (tofali zima, juu yake nusu vipande, tofali zima mpaka maisho).

Wengine huwa wanakosea, wanajenga tofali zima zima kuanzia chini mpaka juu
 
Kama eneo lako udongo wake ni mfinyanzi, basi jitahidi sana chini umwage mchanga mwingi lakini pia itakuwa vizuri katika ile zege ya chini (blinding concrete) ukaweka na nondo au BRC (BRC ni kama ilivyo wire mesh, ila yenyewe nondo zake ni kubwa ukilinganisha na vile viwaya vya wire mesh)

Lakini pia katika kujaza kifusi, usitumie udongo uliochimba katika msingi kama kifusi (tafuta kifusi kingine chenye asili ya kichanga)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ili kupunguza gharama za ujenzi, jaribu pia kushirikiana na sites za jirani kuazimana vitu mbali mbali kama vile mbao, mpira wa maji, ngazi, mapipa ya maji, machepe n.k

Sio kila kitu inabidi ununue hardware, kuna vitu vingine mnaweza mkaazimana tu na mkajikuta wote mmeokoa kiasi kikubwa cha pesa

Faida nyingine utakayopata mbali na kuokoa pesa ni kutengeneza mahusiano mazuri na jirani zako mapema kabla hata hujahamia katika nyumba, kama mtashindwa hata kuazimana vitu wakati wa ujenzi basi hata ujirani wenu utakuwa ni wa mashaka pindi mtakapohamia katika nyumba zenu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika vyumba vya kulala, imezoeleka kwamba switch za kuwashia taa huwa zinakuwa ndani ya chumba

Sasa wengine huwa wanafanya hivi hivi hata kwenye vyoo kitu ambacho sio sahihi. Switch za kuwashia taa za vyooni zinabidi ziwe kwa nje pembeni kidogo ya mlango ili mtu awe anawasha taa kabla hajaingia, na kama ni kuzima basi azime taa baada ya kutoka chooni

Switch za kuwashia taa za vyooni zikikaa ndani ya choo, kuna uwezekano pia maji yakaingia kwenye hizo switch na ikasababisha madhara

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ukienda hardware kununua tank la maji, unaweza ukakuta kuna tank fupi na tank refu lakini ujazo kwa matank yote unakuta ni ule ule mmoja mfano 1000Ltrs au 3000Ltrs

Tank refu huwa lina kitako kidogo, lakini tank fupi huna lina kitako kikubwa

Kama matank yote mawili yatakuwa na maji yanayofanana ujazo, halafu ukasema ukinge maji kwa kutumia ndoo mbili zinazofanana ujazo katika kila tank, tank refu litawahi kujaza ndoo kabla ya tank ya fupi

Tank fupi huwa linatumika zaidi sehemu ambayo kuna eneo la kutosha, na tank refu linatumika zaidi sehemu ambayo kuna ufinyu wa eneo la kuweka

Lakini pia siku hizi maghorofani huwa wanaweka matank ambayo hayaonekani, yanafichwa na paa la nyumba hivyo kwa case kama hii matank mafupi ndio huwa yanatumika zaidi


Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Engineer!

Huu mfano wa tank fupi na refu uliutoa hapa lengo ukiwalenga wale watakaotaka kuyaweka maghorofani au ulikuwa unataka kusema kuna ambalo ni bora zaidi?
 
Mkuu Hechy Essy Samahani naomba kuelimishwa. Kwa kawaida choo cha public cha ndani ya nyumba ambacho sio kikubwa sana wala kidogo sana kinatakiwa kuwa na ukubwa gani (urefu na upana)?
 
Kama ilivyo kawaida, tunaendelea kupeana dondoo mbali mbali kuhusu mambo ya ujenzi

Wapo watu ambao wanapenda kufanya mambo yao kwa siri sana (kimya kimya bila watu kujua) kiasi kwamba hata watu wa familia zao hawataki pia wajue. Sasa hii ina faida zake lakini pia ina hasara zake kwa upande mwingine

Ukienda kununua kiwanja, jitahidi sana usiende peke yako..tafuta hata ndugu yako yoyote au rafiki yako akusindikize mana huwezi jua dunia ya sasa imebadilika sana

Vuta picha unaenda sehemu kuangalia kiwanja, hakuna hata makazi ya watu au nyumba zipo mbali na eneo unalotaka kununua na upo peke yako, huku upande wa wauzaji unakuta wapo hata watatu (Unajiamini kiasi gani!!?). Hii ni risk kubwa sana, mana wanaweza hata wakakuua huko huko na watu wasijue

Kama hutaki ndugu zako wajue, basi mshirikishe hata rafiki yako mmoja unayemuamini. Hata haya magofu/mapagale mnayoyaona yamekaa miaka kwa miaka bila kumaliziwa, kuna magofu mengine wamiliki wameshafariki muda tu lakini unakuta hata ndugu zao hawajui kama ndugu yao aliwahi kujenga mahali na hakuna mtu yoyote anayefahamu kama mmiliki ameshafariki (moja ya hasara za usiri uliopitiliza)
 
Naombeni ushauri kesho naenda kukutana na fundi ili anipigie gharama za kuanza msingi kwanza

Je kuna ulazima wa kuwa na vyoo viwili vya ndani kimoja master na kimoja cha public, nyumba ya vyumba viwili tu

Au nikiweka choo kimoja tu hicho cha public itakuwa good

Kibaraza cha jikoni hicho kina umuhimu wa kukaa hapo au nikiondoe

Na naomba mnisaidie kwenye upande wa ukubwa sebule inakuwa na ukubwa gani standard urefu na upanda(futi na meter)

Chumba cha master kinakuwa na ukubwa gani pia,chumba cha kawaida kinakuwa na ukubwa gani, choo kinakuwa na ukubwa gani na jiko la kawaida linakuwa na ukubwa gani.

Sitaki nyumba kubwa inisumbue kwenye kuimalizia, nataka iliyotulia standard isinitese kwenye vifaa vinavyoanzia na english huko
 

Attachments

  • IMG_20250214_110953.jpg
    IMG_20250214_110953.jpg
    549.1 KB · Views: 3
Hakikisha circuit breaker zako unazikagua mara kwa mara kujua kama bado zipo active ili kujihakikishia usalama wa nyumba yako pale kunapotokea hutilafu za umeme kama umeme mwingi, short circuit n.k

Ni sawa na kumtegemea mlinzi anayelinda getini kwako kumbe na yeye mwenyewe kalala
Mtaalam,hizi zinakaguliwaje kwa ambaye hana analolijua kwenye masuala ya umeme?
 
Mtaalam,hizi zinakaguliwaje kwa ambaye hana analolijua kwenye masuala ya umeme?
Kwanza inabidi uwe makini sana, maana umeme ni hatari kiasi kwamba inaweza ikasababisha hata kifo hivyo ni vyema ukamtumia fundi umeme, yeye ndiye ataweza kupima sehemu yoyote anayotaka kushika kabla hajapagusa ili kujua kama kuna umeme au lah

Ukifungua distribution board yako, utakuta hiki kifaa. Ukiibonyeza hiyo button nyeupe iliyoandikwa herufi "T", kama MCB yako inafanya kazi utaona hiyo switch ya rangi ya kijivu ina-trip (yani inakata umeme yenyewe, mfano kama kulikuwa na taa zinawaka zitajizima zenyewe bila hata kugusa switch zake), na kama ndio mara yako ya kwanza kutest unaweza hata ukastuka ukadondoka mana kuna kamlio flan huwa kanatoka
20250221_210157.jpg
 
Kuna baadhi ya hatua za ujenzi fundi akikosea, marekebisho yake unaweza ukatumia gharama kubwa pengine hata kuzidi nusu ya gharama za awali.

Wengi wamekuwa wakiwashirikisha wataalam baada ya tatizo kutokea wakati kama angefanya hivyo kabla, angeweza kuepukana na hayo matatizo

Mfano unakuta nyumba hata kupauliwa tu bado, lakini nyumba imeshapiga nyufa kila mahali mpaka mtu anatamani avunje boma lote aanze upya

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kuna nyumba zingine ukienda, ndani hukuti jiko (kitchen room). Jiko limetengwa nje ya nyumba

Hii inapunguza joto ndani ya nyumba hasa kwa vyumba vinavyolizunguka jiko lakini pia hata ikitokea ajali ya moto jikoni, inafanya nyumba isalimike mana hitilafu nyingi za kuungua kwa nyumba kwa asilimia kubwa huwa zinaanzia jikoni

Kutakuwa na offer ya punguzo la bei za ramani na makadirio kwa muda wa wiki moja kuanzia leo jumanne mpaka jumanne ijayo
 
Back
Top Bottom