Katika makubaliano ya gharama za kazi na fundi, jitahidi makubaliano yasiwe juu juu (ile kazi husika iwekee na vipengele vyake ili mwisho wa siku fundi asije akakuruka).
Mfano unaweza ukakubaliana na fundi kazi ya kukata miti katika eneo lako la ujenzi, sasa usishangae kuona mafundi wanakuja kukudai pesa yao baada ya kukata hiyo miti maana ukiwaambia mbona hamjaitoa watakuambia sisi tumekubaliana kazi ya kukata miti sio kuikata na kuitoa. Mpaka hapo itakulazimu uingie tena gharama zingine, maana itabidi mfanye tena makubaliano ya kazi ya kuhamisha miti
Sasa kwa mfano huu wa miti, itatakiwa uwaambie kwamba hiyo kazi itainclude kukata miti yote, kuihamisha eneo la ujenzi (na ikibidi waoneshe mahali ambapo unataka yakae hayo magogo, wasije wakayaweka tu pembeni baadae ukaingia tena gharama ya kutafuta watu wayasogeze pembeni zaidi), na malipo yote ni baada ya kazi kukamilika/kuisha. Ukijichanganya kuwalipa malipo kwa kazi waliyofanya, kesho wanaweza wasirudi hasa pale kazi inapokuwa ni ngumu, lakini kama hujawalipa kabisa au umewalipa kidogo hawawezi kukutoroka kesho wasije site.
Ramani, Makadirio na Ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane +255(0)624068809