Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kuna aina mbili za mikato ya pembeni mwa tofali, kuna tofali zinazotengeneza herufi "V" na kuna zile zinazotengeneza herufi "U"

Tofali zenye mkato wa herufi "U" ni rahisi kubebeka tofauti na tofali zenye mkato wa herufi "V"

Tofali zenye mkato wa "U" ni nzuri zaidi kwa sababu mkato wake unakupa nafasi ya kutosha ya kupiligia msumari kati kati ya tofali bila tofali kumeguka. Hili zoezi lipo katika hatua ya kupigilia mbao za sahani kwa ajili ya mkanda wa juu sehemu za madirisha na milango

Muda wa offer ya punguzo la bei unaelekea ukingoni, imebaki wiki moja tu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ulishawahi kupita mahali ukaona mafundi wanatindua kuta ambazo zimeshapigwa plaster ili waweke bomba za maji na umeme?

Swali la haraka litakalokujia kichwani ni kwanini hawakuweka hizo bomba kabla ya kupiga plaster

Kuweka kabla au baada vyote ni sawa japo ipo namna nzuri zaidi kuliko hizo njia zote mbili (kabla na baada)

Ukiweka bomba za maji na umeme kabla ya plaster, kuna muda inatokea fittings zako (box za umeme, point za maji kwa ajili ya kuweka koki za maji n.k) zinakuwa zimefukiwa na plaster kiasi kwamba zoezi la kuweka switch, koki n.k linakuwa ni gumu ndio maana wengine hupendelea kuweka bomba baada ya kupiga plaster ambapo hizo fittings zote zinakuwa zinafuata level ya plaster ilipoishia na kuleta muonekano mzuri zaidi

Njia nzuri zaidi katika hili zoezi, ni kuchora michoro yako yote katika kuta (mfumo wa maji na umeme), baada ya hapo piga plaster pote isipokuwa sehemu ambazo umechora michoro yako. Baada ya hapo anza kuweka bomba katika michoro yako ambapo hata zoezi la kutindua kuta litakuwa jepesi zaidi kuliko kutindua kuta zikiwa zimeshapigwa plaster, ukimaliza chapia udongo bomba zako kufuata level ya plaster ilipo. Pia ni vizuri ukatumia grinder kuchana ukuta kabla ya kuanza kutindua ili usisababishe nyufa katika kuta

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika kupitapita nimekuta Quara wakijadili uwezekano wa nyumba ghorofa kutokuwa na idadi sawa ya columns kwa juu na chini. Kwamba kama load ya upper floor itakuwa ndogo basi unaweza kuweka idadi pungufu ya columns ukilinganisha na chini

Ukweli upoje hapa wakuu
 
Yah kuna nguzo zingine huwa zinaishia floor ya kwanza (hasa hasa nguzo za kati), au wengine hupunguza idadi ya nondo mfano kama kwenye ground floor nguzo zilikuwa na nondo sita sita, katika floor ya kwanza wanaweka nondo nne nne

Yote kwa yote ni vyema kabla ya kufanya hivi ukajiridhisha kwanza kwa kufanya analysis ya jengo lenyewe kwamba ikiwekwa hivyo haitaleta shida yoyote
 
Wakati wa kuweka sink la choo, inatakiwa uache nafasi ya kutosha hata nchi nne mpaka sita kati ya ukuta na sink.
Hiyo nafasi ni kwa ajili ya kuweka bomba linalotoa maji kutoka katika flash tank kwenda kwenye sink. Lakini pia inamfanya mtu awe comfortable kuliko sink kuwa karibu zaidi na ukuta

Bomba linalotumika hapo ni bomba la size ya nchi 1.5

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Offer itaanza muda si mrefu kabla ya mwezi december, ili kila mmoja aanze mwaka mpya na ramani yake mkononi, mvua zikikata tu watu waanze kuotesha misingi
Hivi ramani unaweza chora ata kama process ya kubadilisha hati i aendelea?
 
Unaweza ukachagua kibaraza kimoja wapo (kati ya kibaraza cha mbele sebleni, au kibaraza cha nyuma jikoni) kuweka zege juu ili usiingie gharama ya kujenga mnara wa tank la maji, lakini kingine utakuwa ume-save eneo kwa ajili ya matumizi mengine.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Ili hiki kibaraza kiweze kubeba tank la litre 5000 itabidi zitumike nondo za mm ngapi?
 
Katika kazi za usukaji wa nondo (iwe ni slab, nguzo, au chochote) , ni vizuri ukawa na document inayoitwa Bar Bending Schedule

Hii document inakuwa inaonesha urefu wa vipande vyote vya nondo pamoja na idadi zake, shape ya nondo, size n.k ambapo inakuwa inamuongoza fundi kufanya kazi yake kirahisi zaidi lakini pia inasaidia sana kupunguza mabaki yasiyotumika (wastage) kutokana na nondo kuwa zinakatwa kwa mpangilio maalum

Kupitia hii document, fundi ataweza kugundua kwamba wastage ya sehemu moja inaweza ikatumika sehemu nyingine hivyo hatoweza kutumia nondo nyingine nzima wakati kuna wastage inayoweza kutumika mahali hapo

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Hawa fundis wetu watawrza mweli kusoma maana hiyo nayo changamoto
 
Hili dude lilinipitaje? Asante kwa elimu
 
Hivi ramani unaweza chora ata kama process ya kubadilisha hati i aendelea?
Ramani unaweza ukachorewa muda wowote tu, kitu cha muhimu ni kujua vipimo vya hicho kiwanja pamoja na sketch yake (mpangilio wa barabara za mitaa) ili anayechora ajue namna ya kupangilia ramani yake katika hicho kiwanja (site layout)
 
Na kibali cha ujenzi nacho napata pia?
 
Ili hiki kibaraza kiweze kubeba tank la litre 5000 itabidi zitumike nondo za mm ngapi?
Hapo ndugu yangu kwa usalama zaidi ni heri ukajenga mnara wa tank pembeni kwa sababu hizo lita 5000 ni nyingi, kiuzito ni sawa na tani 5 na ukiangalia mkanda wa juu ambapo uzito wa slab ya kibaraza unaegemea, umelala kwenye tofali za nchi 5 na kingine mkanda wa juu mara nyingi depth yake inakuaga ni nchi 6 mpaka 8. Kwenye vibaraza sana sana huwaga zinawekwa tank za lita 2000

Kama hiyo haitoshi bado chini ya huo mkanda unakuta kuna uwazi chini (mlango na arch za varanda) na sio pande zote zinakuwa na nguzo

Hapo inabidi ujenge mnara, tofali zake uzilaze ili mkanda unaobeba slab ya kubeba tank uwe na upana wa nchi 9.
 
Watu wengi katika Ujenzi wamekuwa wakitumia tu maji ya aina yoyote ili mradi kwao iwe kuna uwepesi wa kuyapata. Sasa kitaalam unaambiwa, maji ambayo unayatumia katika ujenzi inatakiwa uwe unaweza kuyanywa bila kukuletea shida kiafya.

Uwepo wa kemikali na impurities zingine katika maji ya kujengea kama vile chumvi, magadi n.k huathiri kwa kiasi kikubwa nguvu ya saruji katika udongo wa kujengea (mortar) na zege pia ambapo baadae inaweza kukusumbua mfano rangi/plaster kubanduka katika kuta.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Offer yetu ya punguzo la bei inaisha leo saa sita usiku.
Mungu atuvushe salama tuweze kuuona mwaka mpya tukiwa na afya na uzima
 
Kuna aina mbili za mikato ya pembeni mwa tofali, kuna tofali zinazotengeneza herufi "V" na kuna zile zinazotengeneza herufi "U"

Tofali zenye mkato wa herufi "U" ni rahisi kubebeka tofauti na tofali zenye mkato wa herufi "V"

Tofali zenye mkato wa "U" ni nzuri zaidi kwa sababu mkato wake unakupa nafasi ya kutosha ya kupiligia msumari kati kati ya tofali bila tofali kumeguka. Hili zoezi lipo katika hatua ya kupigilia mbao za sahani kwa ajili ya mkanda wa juu sehemu za madirisha na milango

Muda wa offer ya punguzo la bei unaelekea ukingoni, imebaki wiki moja tu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
WEKA PICHA MKUU.

MIMI SIJAELEWA.
 
Mkuu Hechy Essy Heri ya mwaka mpya.

Nafurahia sana maelekezo yako kwenye uzi huu tangu umeanza kutupa elimu hii bure humu ndani.

Mungu azidi kukufanikishia, na pia namuomba sana Mungu aniwezeshe nami pia angalau ofa yako ya mwaka huu itakapotokea niwe ni mmoja wa watakaoitumia hata kama ni kuchorewa tu mpangilio wa ukuta wa kuzungushia kiwanja, lakini lazima nifaidike na ofa yako kwa namna yoyote kwa mwaka huu.
 
Amin amin, nashukuru ndg kwa maombi yako mazuri. Wiki hizi mbili za mwezi wa kwanza, offer itaendelea mpaka tarehe 15 January maana wengi walikuwa walikuwa na sikukuu, pengine imeshindikana kwao kujigawa kiuchumi. Karibuni sana
 
Back
Top Bottom