Wakati mwingine sio lazima sana kuchukua vifaa vyote vya ujenzi vikiwa ktk hali yake ya uzima mfano unapoenda kununua tiles, unanunua box za tiles ambazo ni nzima na ukifika site tiles zingine unazikata ili upate vipande vya kujazia na wakati huo huo pale hardware uliponunulia hizo tiles kuna box za tiles ambazo baadhi ya vipande vimekatika na muuzaji anauza kwa bei ya hasara hivyo kama ungechanganya box nzima na zile zilizokatika ungeokoa kiasi flani cha pesa
Hii pia unaweza ukaapply kwenye gympsum board ktk uwekaji wa dari, tofali n.k kwa lengo la lengo kupunguza gharama
Kabla ya kufanya uamuzi inabidi ufanye mahesabu ili upate makisio kwamba nyumba yako itahitaji vitu vizima vingapi, ili uweze kujua sehemu iliyobaki itahitaji kiasi gani cha material ambazo sio nzima (hapa simaanishi ubovu, namaanisha utimilifu)