Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Katika wakati ambao nimeona Moderator ni watu wa ajabu ni hiki kitendo cha kuhamisha huu uzi Jukwaa la Matangazo. Maxence Melo angalia upya kama huyo Mod anakufaa, otherwise mfunge Jukwaa la Ujenzi tujue moja. Haihitaji D mbili kujua huu uzi unatakiwa kuwa wapi.

Hatuhitaji benefit of doubts kujua sababu, labda tuamini mnaona tunafaidi sana mjadala. Kuweni wastaarabu.

Mod aliyefanya hiki kitendo amenikumbusha siku mlipohamisha uzi wa NBAA jukwaa la elimu na kupeleka jukwaa la michezo.
Kinachonishangaza hasa ni kwamba watu wenye nyuzi zinazofanana na zangu (kuuza ramani) wote post zao zimeachwa jukwaa la ujenzi isipokuwa uzi huu tu, na ukiangalia mimi nimebase sana katika kutoa elimu kuliko hata kutangaza hizo ramani

Kama wangefanya hivi kwa nyuzi zote, nisingeshangaa. Ni watu wengi walikuwa wakifatilia hizi dondoo, wale ambao hawakusubscribe watakuwa wanapata shida kuutafuta kwenye jukwaa la ujenzi
 
😂😂 usiichungulie sana pesa, huwa siku zote haitoshi. We fumba macho imalize, hayo makosa yanarekebishika vizuri tu

Mm huwa napenda plot ambayo Ina slope kubwa kama yako huwa ndio zina aesthetic views, na tena hapo kwenye msingi wa kozi tisa, ungefanya manuva vizuri na kuongeza kidogo ungetengeneza basement moja kali tu, angalia pia hata garden zinazokua kwenye slope plots jinsi zinavyovutia
Kwa Hela zetu za kuunga unga ni manyanyaso tu 😂 .
 
Ndugu zanguni tutaendelea na dondoo zetu kama kawaida siku watapourudisha huu uzi kwenye jukwaa la ujenzi, mpaka sasa bado sijafahamu vigezo vilivyotumika...wengi tu wanaouza ramani matangazo yao yameachwa jukwaa la ujenzi (hakuna usawa), kama wataweka usawa kwa kuhamisha nyuzi zote zinazofanana na zangu jukwaa la matangazo, pia tutaendelea na dondoo
 
Huu ndio ukweli wenyewe kabisaa!! Haki iko wapi? Tusikilizwe wadau wa Uzi huu jf please.

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Uzi wetu umerudishwa katika jukwaa la ujenzi, Mungu awabariki wote mliosaidia hili jambo kufanikiwa. Shukrani zangu za dhati kabisa ziende kwa OKW BOBAN SUNZU ambaye amejitokeza zaidi ya mara moja kutetea hili jambo.

Pia nimshukuru ndg kawombe ambaye nae pia alijitokeza kupaza sauti, na amekuwa mdau mkubwa wa huu uzi kwa muda mrefu

Lakini pia niupongeze uongozi wa Jamii forum kwa kuwa wasikivu, kwani hawakushindwa kuuacha huu uzi kule kule walipouweka awali
 
Tunawashukuru Moderator kwa kuwa wasikivu
 
Upande wa majengo ya ghorofa, ramani moja inaweza ikajengwa sehemu mbili tofauti lakini jengo moja likakaa na jengo lingine likadondoka

Hii inasababishwa na utofauti wa uwezo wa udongo kuhimili mzigo uliopo juu yake (soil bearing capacity)

Mchoro unaweza ukaonesha kwamba nguzo flani katika jengo zinatakiwa ziwe na kitako cha urefu wa futi 4 upana wa futi 4 na kina cha 40cm kwa soil bearing capacity ya 180KN/mm² , sasa ukijenga hivi hivi kwa eneo ambalo soil bearing capacity yake ni chini ya 180KN/mm² basi ujue vitako vya nguzo havitakuwa kama hapo juu bali vitaongezeka (inaweza ikawa urefu futi 5, upana futi 4, kina 45cm kutegemeana na mahesabu yatakavyokupa majibu)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Tofalo za inch 6 sio tafsiri ya uimara au ubora, zipo tofali za inch 5 ni bora kuliko inch 6, inategemea na walovyofanya mixing na compression wakati wanafyatua

Msingi kozi 9 ilipaswa kuwepo na mikanda miwili, Kona za kuta kuna joint ya zege au nguzo za zege? Na je hizi nguzo zipo pia kwenye kona kwenye msingi?

Kuta zimeanza kuweka nyufa sehemu nyingi? Je hizi nyufa ni kwenye kuta tu au zipo na kwenye msingi? Haya maswali yatafanya kujua solution ya tatizo lako kwa urahisi

Tatizo Hilo linawezekana kutibika vizuri tu na utasahau nyufa zote

Lakini pia sehemu ya slope kama hiyo ilipaswa awepo mtu anayejua vizuri kumuongoza fundi nn cha kufanya. Kwanza ilipaswa kujua aina ya udongo
Pia sidhani kama aliweka carpet la zege kuzunguka msingi wote kabla hajaanza kujenga tofali za msingi
kwenye carpet la zege kuna wanatumia mchanga huu wakujengea wanasema et n mzuri kuliko zege kabla hujaanza msingi

sijui n kweli?
 
Kabla ya kulaza nailoni (damp proof membrane, DPM), mwaga kwanza mchanga. Hii inasaidia DPM yako isitoboke wakati unamwaga zege la jamvi kutokana na ncha za mawe chini ya DPM
Usilaze DPM juu ya mawe

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kabla ya kulaza nailoni (damp proof membrane, DPM), mwaga kwanza mchanga. Hii inasaidia DPM yako isitoboke wakati unamwaga zege la jamvi kutokana na ncha za mawe chini ya DPM
Usilaze DPM juu ya mawe

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Mkuu gharama ya kujenga boma la 14.7m kwa 12m
standard inaweza kua ngap kuanzia msingi mpaka juu pale

kuna kanambia 2.5M
mwingine 3.5M
 
Mkuu gharama ya kujenga boma la 14.7m kwa 12m
standard inaweza kua ngap kuanzia msingi mpaka juu pale

kuna kanambia 2.5M
mwingine 3.5M
Gharama huwa inategemeana na factor zingine nyingi mfano nature ya eneo (slope au flat), mzunguko mzima wa nyumba ili kujua kila kozi inaingia tofali ngapi(maana mara nyingi fundi mkuu huwa anawalipa mafundi wake kwa kuhesabiana tofali walizojenga ili kuepuka kutegeana katika kazi), aina ya nyumba (ya kawaida ama contemporary), aina ya udongo (kichanga/mfinyazi n.k)

Ukiona fundi amekutajia gharama kabla hata hajaiona site au ramani, ujue huko mbele mtasumbuana, muda wowote anaweza akadai nyongeza ya malipo. Mtu hawezi akataja gharama wakati hajajua ukubwa wa kazi upoje, vinginevyo atataja kiasi kikubwa ambacho yeye itakuwa inamlipa licha ya ukubwa wowote wa kazi atakaokutana nao

Kingine unaweza ukadondokea kwa dalali wa kazi ambaye yeye anakuwa anajuana na mafundi, mfano unaweza ukampa mtu kazi kwa milion 3, yeye akamtafuta fundi akamuuzia hiyo kazi kwa milion 2.2 so laki 8 nzima inayobaki anaweka mfukoni kitu ambacho kinaumiza sana, ni heri hiyo milion 3 yote angeipata huyo fundi aliyefanya kazi au ungeelewana na fundi mwenyewe kwa hiyo milion 2.2, laki 8 ikakusaidia katika hatua za mbele
 
uyu jamaa wa 3.5m yeye ni injinia ndo anaset nyumb maan hashiki kijiko kazi yake ni kusimamia mafundi wake na mafundi wake ni hao hao naona n kama jopo lake

uyu wa 2.5m yeye anaset na anashika kijiko nayeye kazini kama wenzake anasimamia na anashika tofali anapiga kazi
 
Hapo sasa inabidi uangalie na mfuko wako ulivyo, ukishindwa tafuta tu fundi mzoefu then mtaalam uwe unamuita siku muhimu tu kama vile siku ya kuset msingi n.k, unakuwa unamlipa per day, mpaka boma linaisha unaweza ukawa umemuita mara 3 kwa hivyo unakuwa umeokoa zaidi ya laki 7 hapo kwenye hiyo 1M iliyozidi.

Injinia mwenyewe unakuta anakuja site, anakaa dakika 10 tu anaondoka na haji siku zote, wakati mwingine mafundi wanakuwa wanafanya kazi tu wenyewe bila hata uwepo wa huyo injinia. Kwa nyumba za ghorofa uwepo wa injinia haukwepeki, lakini kwa nyumba za kawaida kama mafundi wanajua wanachokifanya suala la uwepo wa injinia inakuwa ni optional
 
Mkuu makadilio ya chini ya chumba master na sebule kwa eneo tambalale mpaka boma kukamilika, materials yanapatikana karibu ni kiasi gani?.Plan ya kwanza ilikua ni kujenga vyumba viwili kimoja master sebule na jiko ila kutokana na hali kubadilika nikaona nikimbie nyumba za kupanga kwa kuanza na hiyo chumba Master na sebule huku nikijitafuta kujenga pembeni hiyo ramani ya kwanza niliyoihitaji.
 
Hapo ndg inakuwa ni makisio sio makadirio, mana ili uweze kufanya makadirio ni lazima uwe na ramani yenye vipimo ili mtu aweze kufanya hesabu ya material kupitia hiyo ramani
 
Ni afadhali ukanunua cement ya 42.5N (extra) kuliko ukanunua cement ya 32.5N (plus) kwa sababu ya utofauti wa Tsh 500 katika bei.

Kama utatumia ratio moja katika kuchanganya udongo/zege, strength ya udongo uliotumia cement ya 42.5N haiwezi kufanana na strength ya udongo uliotumia cement ya 32.5N

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Back
Top Bottom