Cesar Saint
JF-Expert Member
- Nov 18, 2016
- 423
- 726
Inawezekana Afrika ingekuwa ndiyo super power kama waafrika tusingekuwa wapumbavu na wapenda madaraka kama tulivyo mpaka sasa. Afrika iliyoungana ni hatari kuliko taifa lolote linalotawala dunia hii mpaka sasa. Ukijumlisha nguvu na eneo wanalotawala watu weusi na waafrika ndilo lenye rasilimali za aina zote, misitu iliyo bora, mafuta mengi, madini aina zote, mito ya kila namna, ardhi inayofaa kwa kila kitu, watu wengi wa kutosha, nk,nk,nk.
Tatizo la watu weusi dunia hii ni kugawanywa na kudanganywa kuwa ukiwa rais wa kanchi kama malawi utafanana na Trump au Xi Jingpin wa China. Naitamani siku Aftika imeungana, tunaweza kuwa na states hata mia na hamsini au mia mbili, lakini Rais mmoja. Federation ya Afrika ikiundwa leo na hawa viongozi wetu wakaiona Afrika kuwa nchi moja, utakuwa mwanzo wa Afrika kuwa Super power ndani ya miaka 50.
Tatizo la watu weusi dunia hii ni kugawanywa na kudanganywa
Haya ona sasa," Gorge Peter, Murdock" anaijua historia ya wafrika kuliko waafrika wenyewe wanavyoijua!
Sijui hicho kitabu kiliandikwa lini(1959)?; lakini mtu unaweza ukajiuliza katika wasomi wote tuliokuwa nao Afrika nzima hakuna aliyeweza hata kujitokeza na kuiandika historia hiyo?
Niseme hapa, inawezekana vipo vitabu vya aina hiyo vingi vilivyoandikwa na wazungu na/au WaAfrika, ambavyo hatujui kuwa vipo! Hiki kinaweza kuwa kimojawapo kati ya vingi? Lakini ni nani anayeifundisha historia hiyo?
Punda na sikio lake.
Nashukuru sana kwa majibu yako mazuri sana na mawazo yako."Kugawanywa na Kudanganywa".
Hebu yafikirie hayo maneno mawili tu kwanza, na hapo utaona upungufu wa hoja nzima unayoitetea.
Hii dhana ya weusi kuwa na udhaifu kila sehemu na kutakiwa waendeshwe na wengine ni jambo la kutisha sana.
Hapa kwetu sasa hivi tunasikia kelele nyingi kuhusu Lissu "kudanganywa' au 'kununuliwa' na mabeberu.
Kelele nyingi zinasikika kuhusu njama za mabeberu (watu wasiokuwa weusi), kutufanyia njama za kuturubuni na vimisaada vyao ili kuzuia maendeleo yetu (tusijitegemee wenyewe) kwa kujiletea maendeleo wenyewe! Na hali wakati huo huo, tunalalamika na kupiga kelele nyingi kuhusu Tundu Lissu anavyosaliti taifa letu kwa kwenda kutuchomea utambi kwa washirika wetu tusipate misaada!
Nadhani unaweza kuona mtiririko mzima wa dhana hii ya kusadikika uliyioweka katika mchango wako kwenye bandiko hapo juu.
Hivi hawa weusi ni viumbe wa aina gani ambao kila mara mambo yao ni lazima yaingiliwe na wengine na sio wao wenyewe kutokuwa na uwezo wa kuyasimamia?
Tusipende sana kuwa watu wa lawama kwa wengine bila ya kujipima sisi wenyewe kwanza madhaifu yetu.
Kwa maoni yangu, hali inayomkabili mtu mweusi kwa sasa hivi inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mweusi mwenyewe. Kama elimu tuliyopata tokea kuwa huru haiwezi kutusaidia kutumia vichwa vyetu vizuri na kuamua tunataka nini; na hapo hapo vichwa hivyo tuendelee kuvikodisha kwa hao waliokuwa wanatunyanyasa (wakoloni), tunataka kitu gani kitokee ili tuweze kuvitumia vichwa vyetu vizuri?
KWADO ABIMBOLA, usinielewe vibaya. Sipingi hoja yako, ila nina mtazamo tofauti tu na wa kwako.
Tulipaswa kuitazama Afrika kwa kuangalia watu wake na rasilimali zake na potential yake. Haya mambo ya utumwa natamani tungeyafuta kwenye sylabbus. Turudi karne ya 16, tuanzie statez za afrika zilivyokuwa organized, twende kwenye colonization ya afrika ambayo ndiyo imetuma nchi zilizopo sasa. Kwa maana halisi sisi bado tupo colonized, tumeaminishwa kuwa mfumo wa kutawala, elimu, kula, kuvaa, kusali, nk.nk. ni lazima ufanane na ule tulioletewa na wakoloni.Tatizo huanzia na kuwa historia ya afrika haifundishwi mashuleni mitaala ya wanaojiita wasomi hukazana na kufundisha utumwa na ukoloni bila kujua hujenga kizazi dhaifu kisichoweza kujisimamia na kujivunia
Sent using Jamii Forums mobile app
Afrika kuwa super power within 50 years.
Hapo sawa lakini ujue lazima tuuue sana katika vita itakayo anzishwa hapo Usa. Russia na China hazikuungana kilele mama. mamilioni walikufilia kwa mbali ambao hawakutaka umoja. kwa maana kwamba ni lazima ilikuwa waungane. chukulia mfano Zanzibar vile vijamaa havitaki muungano kabisa siyo wote baadhi Nyerere alifyatua kafara yadamu, ndo maana leo unaona tuna kajimuungano. lakini pia kun vijamaa havitaki hata kwa kuviangalia tu,Nashukuru sana kwa majibu yako mazuri sana na mawazo yako.
Japo sijafanya utafiti kuhusu watu weusi (waafrika) na mahusiano yao na sayari ya dunia, picha ninayoipata kwa haraka ni kuwa watu weusi mpaka tunaingia kwenye "civilization period -yaani kuanzia 16th century" walikuwa wametapakaa kwenye maeneo tajiri kuliko mahali pengine popote kwenye hii sayari. Yawezekana bado mpaka sasa, tukiingia deep tutawakuta binadamu weusi wanakalia maeneo yenye potential kuliko mahali pengine popote duniani (awezaye ajaribu). Na hapa namaanisha popote watu weusi walipo, siyo lazima Afrika peke yake.
Tatizo la waafrika weusi hasa ni nini? Binafsi nawaona waafrika weusi na aina ya mataifa na muundo tuliyoaminishwa kuwa ndio tunaotakiwa kuwa nao ni tatizo kubwa. (Muundo wenyewe ni Wa marais wanaotawala kama wafalme, wenye nguvu kama za miungu, wanaoweza kuamua chochote, na wanaotaka kufanana na wenzao wazungu kwa kila hali bila kuangalia uhalisia wa mataifa watokayo).
Waafrika tumedanganywa na kudanganyika vilivyo. Tunapaswa kufanya mapinduzi ya kiafrika ya karne ya 21. Tufute mifumo tuliyo nayo ya sasa na tufikiri mifumo mipya inayoweza kutukomboa. Hii mifumo ya wazungu ni namna tu ya kuhakikisha tupo under control na hatufikii potential yetu na hadhi yetu ya kuwa super power.
Binafsi sitakuwa na shida kuwa na mfalme/(au rais) mmoja wa Afrika atakayependekezwa na kuchaguliwa na wawakilishi wa state govermnents (au maseneta) kutoka kila state. Nchi kama Tanzania, inaweza kumezwa na kuwa state 5 mpaka 7. Tukawa na local governments zinazoweza kuwa efficient na ambazo hazitajihusisha na mambo ya nje wala jeshi. Hawa marais wetu wawe tu wawakilishi wa kupanga sera kuu za majimbo ya Afrika na kusimamia mambo makubwa makubwa ya kuifanya Afrika kuwa super power within 50 years.
Nakuelewa sana hoja yako. Msingi wa hoja yako ni viongozi wa Afrika wenyewe. Sidhani kama mtu kama akina Nkurunzinza au Kagame watapenda wawe magavana wa mikoa ya Burundi na Rwanda. Kila binadamu ameumbwa na greed. Ni pale tu atakapodhibitiwa na kuona hakuna namna nyingine ndipo binadamu atakubali kubadilika na kudhibiti kiu yake ya mamlaka, mali, fedha na ukuu dhidi ya binadamu wengine.Hapo sawa lakini ujue lazima tuuue sana katika vita itakayo anzishwa hapo Usa. Russia na China hazikuungana kilele mama. mamilioni walikufilia kwa mbali ambao hawakutaka umoja. kwa maana kwamba ni lazima ilikuwa waungane. chukulia mfano Zanzibar vile vijamaa havitaki muungano kabisa siyo wote baadhi Nyerere alifyatua kafara yadamu, ndo maana leo unaona tuna kajimuungano. lakini pia kun vijamaa havitaki hata kwa kuviangalia tu,
Hivi kweli tatizo ni viongozi tu ama tatizo ni jamii nzima ya waafrika? Inawezekanaje tukawa na viongozi wabovu katikati ya jamii ya watu waliostaaribika?
Kuna mambo mawili kuhusu Afrika sikubaliana nayo hata kidogo. Kwanza sikubaliani kwamba tupo hivi kwa kuwa tulitawaliwa na wakoloni ambao waliturithisha elimu yao inayotufanya tusiiangalie Afrika Kiafrika. Miaka zaidi ya 60 tangu nchi ya kwanza Afrika kupata Uhuru bado tu tunashindwa kubadili mitizamo yetu kisa tu tulitawaliwa na wakoloni?